Kuota unapigana na mtu.

Kuota unapigana na mtu.

Ndoto ya Kuota unapigana na mtu kuna inamaanisha nini?


Ndoto hii inaweza ikawa na maana mbili, maana ya kwanza, ni kuwa upo katika mashindano, Na maana ya pili ni kuwa upo katika vita.

Tukianzana na maana ya kwanza ambayo ni mashindano.

Kwa namna ya kawaida, ikiwa kipo kitu Fulani ambacho kinathamani fulani, na wote mnakitamani au kukigombania ili mkipate, au mmoja anakizuia ili kisipatikane, ni rahisi kutokea kutokuelewa na mwisho wa siku mapigano, kwamfano wengine wanaishia kupigana kisa, fedha, wengine madini, wengine fursa, wengine wapenzi, na wengine thawabu n.k,

Na ndio maana utamwona mtu kama Yakobo katika biblia, alipiigania thawabu yake sana usiku kucha kwa kushindana mweleka na Yule malaika aliyemtembelea usiku..

Mwanzo 32:24 “Yakobo akakaa peke yake; na mtu mmoja akashindana naye mweleka hata alfajiri.

25 Naye alipoona ya kuwa hamshindi, alimgusa panapo uvungu wa paja lake; ukateguka uvungu wa paja la Yakobo alipokuwa akishindana naye.

26 Akasema, Niache, niende, maana kunapambazuka. Akasema, Sikuachi, usiponibariki.

27 Akamwuliza, Jina lako n’nani? Akasema, Yakobo.

28 Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda”.

Hivyo kama wewe umeokoka halafu ukaota, unapigana na mtu muda mrefu mpaka unachoka, ni mapambano tu, Hapo ni Mungu anakukumbusha habari ya Yakobo, kwamba unapaswa utafute thawabu zake kwa nguvu mpaka uzipate, kuliko kitu kingine chochote unachoweza kukitafuta katika hii dunia. Hiyo ndio tafsiri ya kwanza.

Tafsiri ya pili: Kuota unapigana ni ishara ya vita.

Wakati mwingine, watu wanaweza kupigana, si kwa ajili wanagombania kitu Fulani, hapana, bali ni kwa ajili ya chuki, wivu, fitna, kiburi, n.k..Lengo kuu ni kutaka kukuangamiza tu basi,

Hivyo kuota unapigana na mtu, pia inaweza ikawa  ni ishara una vita vya kiroho, na vita hivyo vinatoka upande wa ibilisi, haijalishi ni kwa kupitia wachawi,au mapepo, au watu wa kawaida, au vyovyote vile, lakini upo katika vita, Hivyo kama wewe upo ndani ya Kristo, zidisha ukaribu wako na Mungu katika maombi, na kujifunza Neno,..Kwasababu Bwana anasema..

Waamuzi 8:33 “kisha itakuwa, asubuhi, mara litakapokucha jua, wewe utaamka asubuhi na mapema, na kuushambulia mji huo; tena, angalia, hapo yeye na wale watu walio pamoja naye WATAKAPOKUTOKEA NJE KUPIGANA NAWE, ndipo utapata kuwatenda kama utakavyopata nafasi”.

Lakini kama wewe hujaokoka, ni wazi kuwa upo hatarini, hivyo tahadhari hizi zichukue,

Mpe leo Yesu maisha yako ayaokoke, haijalishi wewe ni wa dini gani,au dhehebu gani, Yesu Kristo anawaokoa watu wote. Ikiwa leo utakubali kutubu dhambi zako zote kwa kumaanisha kabisa kuziacha, atakusamehe na kukukubadilisha na kukupa Roho wake, ambaye atakaa ndani yako milele..Na ndiye atakayekulinda na mipenyo yote ya ibilisi katika maisha yako, kwasababu tayari utakuwa ndani ya ulinzi wa ki-Mungu.

Hivyo kama leo upo tayari kufanya hivyo, basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba, na maombezi>>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Kumbuka hizi ni siku za mwisho, na shetani anawinda roho za watu, kwa bidii sana ili awaangamize, kwasababu anajua wakati aliobakiwa nao ni mchache, na ndio maana unaona mapambano tu, hivyo usipuuzie wokovu ndugu yangu.

Ukiwa umefungua hapo juu na kufuata maelekezo yote, Basi Bwana akubariki sana, na Hongera kwa kuokoka.

Group la whatsapp Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi

Pia tazama masomo mengine chini ya kukusaidia kukua kiroho.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

JIEPUSHE NA UNAJISI.

NA ROHO NA BIBI-ARUSI WASEMA, NJOO!

Ibada ni nini,Na je ili ikamilike inapaswa iwe na nini na nini?

MKUMBUKE MKE WA LUTU.

CHUKIZO LA UHARIBIFU

 

HASIRA YA MUNGU KUKUWAKIA, KWA KUTOMZUNGUZIA TU MUNGU IPASAVYO.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Baya kahindi
Baya kahindi
3 years ago

We trust in GOD