SIKU YA MAONYESHO MAKUU YA BWANA YESU, IPO KARIBU.

SIKU YA MAONYESHO MAKUU YA BWANA YESU, IPO KARIBU.

Leo hii dunia imekuwa na sikukuu nyingi sana za maonyesho. Na sikukuu hizo Mungu ameruhusu makusudi kabisa ziwepo ili kutupa picha halisi ya jinsi sikukuu yake kubwa ya maonyesho itakavyokuwa mbinguni.

Kwamfano kipindi hiki, kwa taifa kama la Tanzania, lipo katika sikukukuu ya maonyesho ya wafanyabiashara maarufu kama saba saba (7’7). Na mwezi ujao kutakuwa na maonyesho mengine  makubwa ya wakulima yajulikanayo kama nane nane (8’8). Kama ulishawahi kutembelea maonyesho haya, au yanayofanana na haya nadhani utakuwa unaelewa ni nini hasaa kinaendelea kule.

Kwa ufupi ni kwamba utakutana na mabanda mengi sana, na kila banda lina onyesho lake la kipekee, kiasi kwamba mpaka utakapomaliza mabanda yote, hutatoka kama ulivyo. Utakutana na mambo mengi sana usiyoyajua, ni jinsi gani vitu vinatengezwa, ni technolijia gani inafanya kitu kiwe hivi au vile n.k.

Sasa, mambo hayo na kwa Bwana Yesu pia yapo. Ipo siku kubwa sana ya maonyesho, ambayo itafanyika huko mbinguni, Sikukuu hiyo biblia inatuonyesha tumeandaliwa sisi, mahususi ili kuuona utukufu wa Yesu aliopewa na Baba yake kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, kwa ajili yetu sisi.

Yohana 17:24 “Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami po pote nilipo, WAPATE NA KUUTAZAMA UTUKUFU WANGU ULIONIPA; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi ulimwengu”.

Umeona hapo? Anasema, lengo la yeye kutaka tuwepo na yeye popote alipo ni kusudi kwamba tuutazame utukufu wake aliopewa… Ndugu hadi sasa Bwana Yesu ameshajiandaa kutuonyesha ukuu wake, huko mbinguni.. Tengeneza picha jinsi siku hiyo itakavyokuwa, tutakapotembezwa katika mabanda ya mbinguni(tukitumia lugha ya kibinadamu).. Tunatoka sehemu moja anatuonyesha nchi nzuri ya dhahabu, tukidhani ndio basi, tunatoka hapo anatupeleka kwingine anatuonyesha makasri mazuri ya kifalme, halafu anasema hayo yote ni ya kwenu, niliyokuja kuwaandalia huku kwa miaka 2000, kama nilivyowaambia katika Yohana 14

Yohana 14:1 “Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.

2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.

3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo”.

Anatoka hapo anatupeleka tena katika banda lingine, anatuonyesha viumbe wa kimbinguni, ambao hutujawahi hata kuwaona huku duniani, anakuambia hawa watawatumikia nyinyi.. Tunatoka hapo anawapeleka na kwa malaika zake wote, anatutambulisha kwa mmoja baada ya mwingine, kisha Bwana anasema hawa nao watawahudumia siku zote.. Tunatoka hapo tunakwenda kuonyeshwa vyombo vizuri za muziki, ambavyo kwa hivyo tutakuwa tunamwimbia Mungu daima. Mnaenda sehemu nyingine mahali pa mafunzo mnaambia hapa mtafundishwa jinsi ya kuwa na uwezo wa kiroho kama wa malaika, mnatoka hapo mnapelekwa tena kwingine kuonyeshwa mambo ya ajabu, ambayo kimsingi hatuwezi kuyaeleza hapa, kwasababu ni mambo ambayo jicho halijawahi kuona wala, sikio kusikia, wala halijawahi kuingia katika moyo wa mwanadamu yoyote.

1Wakorintho 2:9 “lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao”.

Siku hiyo ndiyo tutakapojua Bwana Yesu ni mkuu namna gani.  Leo hii huwezi kujua lolote, kwasababu wakati wa yeye kudhihirisha utukufu wake haujafika, lakini siku si nyingi, atatunyakua na kutupeleka huko aliko. Tukauone utukufu wake aliopewa na Baba yake.

Tutaona mambo mengi sana, kila mahali tutakapokuwa tunapelekwa tutabakia kutoa macho tu, kwasababu tutasema hiki nacho tumepewa sisi? Hata hiki? Hata kile? Na Yesu atasema NDIO niliwaandalia nyinyi haya yote..Kama hatujaelewa Tutauliza maswali, na yote yatajibiwa, tutatembea katika maonyesho hayo makuu kwa muda wa miaka saba mfululizo.

Kwakweli tukose vyote sasa lakini sio hilo. Tukose mali sasa, tukose umaarufu, tukose vya kidunia, tusikose karamu kuu ya mwanakondoo, mbinguni.  Lakini kwa bahati mbaya ni kuwa watu wengi watayakosa maonyesho hayo makuu, kwasababu kama mpaka leo hii, mtu akiambiwa aokoke kwa kumaanisha kabisa kumfuata Yesu, anaona kama analetewa habari za kilokole, unategemea vipi mtu huyo, ataingia kwenye karamu hiyo na maonyesho hayo?

Hatakwenda popote,atabaki tu hapa duniani, hata akifa leo, hiyo siku yenyewe ikifika, hatoweza kufufuliwa aende katika UNYAKUO. Ndugu huo ndio wakati ambao kutakuwa na kilio na kusaga meno kama Bwana Yesu alivyosema.. Hutalia kwasababu inaingia kwenye dhiki kuu tu, bali utalia sana kwasababu umekosa tendo hilo kuu la karamu ya Bwana Yesu, ambayo itaambatana na MAONYESHO hayo MAKUBWA SANA.

Yohana 17:24 “Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami po pote nilipo, WAPATE NA KUUTAZAMA UTUKUFU WANGU ULIONIPA; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi ulimwengu”.

Maneno hayo ni lazima yatimie. Haleluya.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

Shekina ni nini? Na Je! Utukufu wa shekina unamaana gani?

Herode aliliwa na chango, Je, chango ni nini kibiblia?

TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!

Kwa jina lake Ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa.

Je! Mfalme Abiya na Mfalme Asa walikuwa ni ndugu?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments