Gombo ni aina ya vitabu vilivyo katika mfumo wa kuviringishwa, kwa lugha ya kiingereza “Scrolls” (tazama picha juu).
Aina ya vitabu hivi vilitumika sana katika enzi za zamani na vilikuwa mara nyingi ni vya ngozi.
Lakini katika zama zetu hizi za sasa, hatuvitumii tena kutokana na kuongezeka kwa maarifa.
Vitabu tunavyotumia sasa, vinatengenezwa kwa karatasi, na vinakuwa na kurasa..Lakini Gombo hazikuwa na kurasa, bali ni ngozi uliyokuwa na maandishi na kuviringishwa.
Mfano wa Gombo ni lile tunalolisoma katika kitabu cha Ezekieli na Ufunuo.
Katika kitabu cha Ufunuo, tunasoma Bwana Yesu akikipokea kile kitabu chenye mihuri saba. Sasa kitabu hicho hakikuwa kama vitabu vyetu hivi vyenye kurasa la!..bali kilikuwa ni gombo, yaani kitabu kilichoviringishwa, na vitabu hivi vya kuviringishwa ndivyo vilivyokuwa vinafungwa kwa mihuri.. vilikuwa vinafungwa kama vile shati linavyofungwa kwa vifungo vyake, (tazama picha chini).
Kwahivyo popote katika biblia panapotajwa neno kitabu, palimaanisha aina hiyo ya vitabu (yaani Gombo)..na haikumaanisha aina ya vitabu tulivyo navyo sisi.
Unaweza kulipata neno hilo Gombo katika biblia, kupitia mistari ifuatayo. Zaburi 40:7, Yeremia 36:2-6, Ezekieli 2:9, Ezekieli 3:3, Zekaria 5:1-2, na Waebrania 10:7.
Kwa msingi huo wa kuelewa nini maana ya Gombo, utatusaidia kuelewa vizuri juu ya juu ya MIHURI SABA ya kitabu cha ufunuo.
Kama utapenda kujua juu ya ufunuo wa Mihuri saba unaweza kufungua hapa >> Mihuri saba
Je umempokea Yesu?, je Umebatizwa ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu?, Je umepokea Roho Mtakatifu a unaishi maisha matakatifu ya kumpendeza Mungu?.
Kumbuka Bwana yupo mlangoni, na unyakuo wa kanisa ni siku yoyote.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
About the author