Swali: Yale Makonde Bwana Yesu aliyopigwa yalikuwaje?.
Jibu: Turejee..
Marko 14:65 “Wengine wakaanza kumtemea mate, wakamfunika uso, na KUMPIGA MAKONDE, na kumwambia, tabiri. Hata watumishi nao wakampiga makofi”.
“Makonde” ni kiswahili kingine cha “Ngumi”. Je umewahi kuwaza kuwa Bwana wetu YESU aliwahi kupigwa ngumi?.
Ndio!..Alipigwa mijeledi (Yohana 19:1) na alitemewa mate (Marko 15:19) lakini pia alipigwa ngumi nyingi na wale askari kwaajili ya makosa yetu sisi..
Mapigo Bwana Yesu aliyoyapata kabla na baada ya kupandishwa msalabani yalimbasilisha kabisa mwonekano wa uso wake na mwili wake wote kwa ujumla, na kumfanya kuwa mtu aiyeharibika uso na mwili kuliko watu wote waliowahi kutokea duniani.
Isaya 52:13 “Tazama, mtumishi wangu atatenda kwa busara, atatukuzwa, na kuinuliwa juu, naye atakuwa juu sana. 14 Kama vile wengi walivyokustaajabia, (USO WAKE ULIKUWA UMEHARIBIWA SANA ZAIDI YA MTU YE YOTE, NA UMBO LAKE ZAIDI YA WANADAMU)”.
Isaya 52:13 “Tazama, mtumishi wangu atatenda kwa busara, atatukuzwa, na kuinuliwa juu, naye atakuwa juu sana.
14 Kama vile wengi walivyokustaajabia, (USO WAKE ULIKUWA UMEHARIBIWA SANA ZAIDI YA MTU YE YOTE, NA UMBO LAKE ZAIDI YA WANADAMU)”.
Umeona?..Mapigo aliyoyapata Bwana Yesu ni zaidi ya yanayoigizwa katika Filamu.. ya kwenye filamu yamepunguzwa makali sana, na pia ni agenda ya shetani kuurahisisha msalaba na kuwaaminisha wanadamu kuwa jambo lililomtokea Bwana lilikuwa la kawaida tu na si zito sana.
Shetani hataki tujue kuwa tumeokolewa kwa thamani na gharama kubwa sawasawa na 1Wakorintho 6:20, Lengo lake ni ili tusijikane nafsi wala tusiuthamini msalaba.
Lakini kama tukijua kwa uhalisia gharama Bwana Yesu alizoingia pale msalabani kwaajili ya dhambi zetu, tutalia kwa machozi na hatutabaki kama tulivyo zoea kufanya mchezo na dhambi.Madhara ya kudharau kazi ya msalaba ni makubwa kuliko kitu kingine chochote.
Waebrania 10:29 “Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?”
Ikiwa bado hujaokoka, ni vyema ukafanya hivyo leo!.. Na si kwasababu tu ya kuepuka hukumu, bali kasababu ya kupata uzima wa milele.
Utajisikiaje ukiukosa uzima wa milele, hata kama tu ziwa la moto lisingekuwepo???..huoni ni hasara kubwa kufutwa kabisa kwenye kumbukumbu zakichwa cha Mungu milele??.Ni heri ukampokea Kristo leo!.
Ikiwa utahitaji kufanya hivyo basi waweza kuwasliana nasi inbox tutakusaidia.
Bwana akubariki
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho mengine:
Ni kweli hakuna mtu aliyewahi kuuona uso wa Mungu Zaidi ya Bwana Yesu?
Kuna tofauti gani kati ya uso wa Bwana na macho ya Bwana?
Biblia inaposema Kaini akatoka mbele za uso wa Bwana, Inamaana gani?
MBINGUNI YUPO NANI SASA?
Je! dhambi zote ni sawa Kuna dhambi kubwa na ndogo?
Rudi nyumbani
Print this post