Yesu alipopaa juu aliteka mateka, Kauli hiyo ina maana gani?

Yesu alipopaa juu aliteka mateka, Kauli hiyo ina maana gani?

SWALI: Ni mateka yapi hayo aliyoyateka..na ni vipawa gani alivyowapa wanadamu.?

Waefeso 4:8 Hivyo husema, Alipopaa juu aliteka mateka, Akawapa wanadamu vipawa. 


JIBU: Ufalme wa Mbinguni umefananishwa na ngome Fulani, yenye hazina kubwa sana ambayo hupiganiwa na watu wengi kumilikiwa.

Na Ndio maana Bwana Yesu aliyasema maneno haya; 

Mathayo 11:12 Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka. 

Umeona unafananishwa na kitu cha kutekwa, sio kitu cha kuombwa, au kubembelezwa Fulani. Inahitaji kupambania.

Hivyo Kwa  maneno hayo utaelewa kuwa hata Bwana wetu Yesu Kristo, alikuwa katika operesheni hiyo ya kuuteka huo ufalme.

Na hiyo ilikuja kutimia siku ile aliposhinda pale Kalvari Kwa kifo chake na kufufuka katika wafu aliweza kumiliki vyote vya mbinguni na vya duniani…vyote viliwekwa chini yake.

Waefeso 1:20-23 aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho;  [21]juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia;  [22]akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo  [23]ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote. 

Sasa kwasababu ameteka Kila kitu cha mbinguni, aliteka pia na ‘uweza wote wa kiungu’ na kutupa sisi wanadamu, ndio vipawa au karama za Roho Mtakatifu, alizozitoa Kwa lengo la kuujenga mwili wa Kristo, kuhubiri injili, na kuhudumu.

Ndio hapo akawafanya wengine kuwa mitume, wengine kuwa manabii, wengine wainjilisti, wengine, wachungaji na wengine waalimu.(Waefeso 4:11)

Pamoja na karama zile 9, tunazozisoma katika 1Wakorintho 12.

1 Wakorintho 12:8 Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule; [9]mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja;  [10]na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha;  [11]lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye. 

Mambo ambayo hayakuwahi kuonekana zamani, hata za manabii..lakini Sasa twaziona zikidhihirika katika kanisa la Kristo.

Hivyo kumbuka Yesu hajateka mateka tu mbinguni. ni mpaka duniani. Maana yake ni kuwa sisi tuliomwamini hatuna budi pia kuwa watekaji. Hivyo popote pale uendapo kuhubiri injili, usiogope Wala usiwe mnyonge, vamia, hubiri Kwa ujasiri na hakika watu watabadilika kwasababu nguvu hizo tumepewa katika Kristo Yesu

2 Wakorintho 10:4 (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)  tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo; 

Bwana akubariki

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Wakaldayo ni watu gani?

TUNA JUKUMU LA KWENDA KUTEKA MATEKA.

MLANGO MWINGINE WA ADUI KUTULETEA MAJARIBU.

TABIA ZA NJIA YA MUNGU KWA MKRISTO

MBINGUNI YUPO NANI SASA?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments