Bwana alimaanisha nini kusema “atazamaye mwanamke kwa kumtamani” amezini naye?

Bwana alimaanisha nini kusema “atazamaye mwanamke kwa kumtamani” amezini naye?

Je! Kutamani kwa namna yoyote hakufai?

Mathayo 5:27  Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; 28  lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.

JIBU: Ukitafakari hapo utaona mazingira Bwana anayoyazungumzia hapo ni ya uzinzi. Uzinzi ni kitendo cha kutoka nje ya mpango wa Mungu wa ki-ndoa katika eneo la kukutanika kimwili. ambao chanzo chake ni tamaa.

Sasa Bwana anaweka wazi kuwa uzinzi huanzia ndani kwenye mawazo ya mtu, moyoni mwake, tofauti na vile inavyodhaniwa kuwa mpaka wakutane dhahiri.

Lakini swali linaloulizwa je! Hatupaswi kutamani kabisa? Na kama tukitamani tutakuwa tunafanya kosa.

Kila kitu Mungu amekiweka katika utaratibu wake. Ni sawa na kusema kwanini ulafi ni dhambi, wakati Mungu ametuwekea ndani yetu hamu ya kula. Au kwanini nisile udongo wakati, najisikia hamu ya kuula mimi kama mjamzito, Au kwanini nisinywe pombe wakati ninajiona kabisa nini kiu nayo?. Kama Mungu angekuwa hapendi kwanini ameniwekea kiu hiyo?

Lakini unajua kabisa ukizidisha kula kuna madhara mwilini, pia ukila/ukinywa kitu kisichopasa utajisababishia madhara mwenyewe.

Vivyo hivyo katika tamaa. Haijawekwa, iwe ni “kutamani-tamani”, kila kitu kinachokatiza mbele. Bali Mungu aliiumba hiyo mahususi kwa wanandoa. Hivyo ikiwa upo humo huna budi kuzielekeza kwa mkeo/mumeo tu, na kama bado hujaingia humo, unapaswa uweze kuzitawala. Na hiyo inawezekana kabisa, usipozitengenezea mazingira, haziwezi kuamka na kukusumbua. Kwasababu maandiko yanasema moto hufa kwa kukosa kuni.

Ufanyeje.

Ni kujiepusha na mazingira yote, yatakayoweza kukupelekea kulipuka tamaa. Kwamfano, mazungumzo-zungumzo yasiyokuwa na maana na mtu wa jinsia nyingine, (kuchati), na kutazama video au picha zenye maudhui ya kizinzi, kuzungumza-zungumza habari hizo na marafiki zako, kuwa katika mazingira yasiyo ya kujishughulisha, kwamfano upo tu huna kazi yoyote umekaa, ni rahisi kupelekwa kwenye mawazo hayo na adui. Lakini pia kuwa msomaji wa Neno na mwombaji. Vitakusaidia sana kuwa mtu asiyetawaliwa na tamaa.

Na hivyo hata adui akitaka kukupeleka kwenye hali ya kutamani, kujengea picha, kutafakari,  basi unaweza kuyakataa hayo mawazo haraka, na ukaendelea kuwa salama, bila ya kuzini moyoni mwako. Kwasababu umevidhibiti.

Pia kumbuka jambo hili, si la wanaume tu, bali kwa jinsia zote. Hatupaswi kuishi maisha ya tamaa.

Bwana akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mafundisho mengine:

MOTO HUFA KWA KUKOSA KUNI.HATA UASHERATI NAO

Nini Tofauti kati ya uzinzi na uasherati ?

WAANDAA MEZA MBELE YANGU, MACHONI PA WATESI WANGU

Biblia imemaanisha nini iliposema “hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu”

Bwana aliposema “sikuja kutangua torati bali kuitimiliza” alikuwa anamaanisha nini?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments