Kuna tofauti gani kati ya uso wa Bwana na macho ya Bwana?

Kuna tofauti gani kati ya uso wa Bwana na macho ya Bwana?

Zaburi 34:15 Macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Na masikio yake hukielekea kilio chao.  16 Uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya, Aliondoe kumbukumbu lao duniani.

JIBU: Andiko hili lilinukuliwa tena na mtume Petro katika 1Petro 3:12-13  linasema;

 “12 Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Na masikio yake husikiliza maombi yao; Bali uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya. 13  Naye ni nani atakayewadhuru, mkiwa wenye juhudi katika mema?

Kama tunavyojua Macho kazi yake ni kutazama, lakini uso, ni kueleza taswira ya mtu/ kitu fulani.

Na  kimsingi macho huona vyote, vilivyo vyema na vilivyo vibaya. Isipokuwa jicho lolote hupendelea zaidi kutazama vilivyo vyema zaidi ya vile vibaya. Ndivyo ilivyo kwa Mungu wetu pia, anaona yote, maandiko yanasema hivyo katika;

Mithali 15:3 “Macho ya Bwana yako kila mahali; Yakimchunguza mbaya na mwema”.

 lakini zaidi anaelekeza macho yake zaidi kwa walio wema ili awape mema.

Na ndio maana ya hiyo sehemu ya kwanza ya andiko hilo inayosema ‘Macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Na masikio yake hukielekea kilio chao’ Lakini haimaanishi kuwa macho yake pia hayawaoni watenda mabaya.

Vivyo hivyo katika sehemu ya pili inayoeleza juu ya Uso wa Bwana. Kama tulivyoona Uso kazi yake ni kueleza taswira ya mtu. Kwa mfano mtu akifurahi, au akiwa na huzuni au akiwa na hasira ni rahisi kumtambua kwa kuutazama uso wake. Na Vivyo hivyo, kwa Mungu wetu ukiitambua tabia yake, basi ni sawa na umeuona uso wake.

Sasa uso wake pia upo katika pande mbili; 1) Wa Rehema, 2) na wa Hasira (Nahumu 1:2-3)

Maana yake ni kuwa ukimtafuta Bwana, na kumpenda, utaona uso wake mwema, utaona upendo wake, utaona fadhili zake, utaona ukarimu wake, huruma yake, na rehema zake sikuzote. Na ndio maana maandiko yanatuasa tupende kuutafuta Uso wa Bwana. Ili tuujue uzuri wake.

Zaburi 105:4 ‘Mtakeni Bwana na nguvu zake, Utafuteni uso wake sikuzote’.

Zaburi 143:7 “Ee Bwana, unijibu hima, roho yangu imelegea; Usinifiche uso wako, Nisifanane nao washukao shimoni’

Lakini pia kinyume chake ni kweli ukiwa mwovu, ukiwa mkaidi, ukiwa mbaya, unajiandaa kuuna uso wa Mungu wenye ghadhabu,na hasira, na mapigo na matokeo yake utakumbana na adhabu kali kutoka kwake. Ndio hapo, anasema.

‘Uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya, Aliondoe kumbukumbu lao duniani’.

Hivyo kwa ufupisho ni kwamba jicho la Mungu linaona wote, waovu na wema, vilevile uso wa Bwana unawaelekea wote waovu na wema. Lakini katika vifungu hivyo, na vingine baadhi, vinapozungumzia macho ya Bwana huwa vinalenga sana sana kwa wema. Na vinaposema Uso wa Bwana, huwa vinalenga sana sana kwa  upande wa waovu.

Kwahiyo usichanganyikiwe, bali fahamu muktadha, wa habari hiyo katika sehemu husika. Ili ujue alimaanisha nini hapo, kwa msaada wa Roho wa Mungu. Kwasababu hutumika kotekote

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mada Nyinginezo:

UNAVYOZIDI KUWA MWENYE HAKI, NDIVYO KUJITAMBUA KWAKO KUNAVYOPUNGUA.

ANDALIZI LA MWISHO LA UJIO WA MPINGA KRISTO.

JIFUNZE KUDUMU UWEPONI MWA MUNGU.

Biblia inaposema Kaini akatoka mbele za uso wa Bwana, Inamaana gani?

Ni kweli hakuna mtu aliyewahi kuuona uso wa Mungu Zaidi ya Bwana Yesu?

Je Paulo na Petro walishindania nini? (Wagalatia 2:11).

TABIA ZA NJIA YA MUNGU KWA MKRISTO

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments