Kuoatama ni lugha ya zamani, inayomaanisha “kwenda haja kubwa”
Kumbukumbu 23:13 “nawe uwe na jembe dogo katika silaha zako; napo uotamapo nje uchimbe kwa lile jembe, na kugeuka na kukifunika kikutokacho; 14 kwa kuwa Bwana. Mungu wako, yuatembea katika kituo akuokoe, na kukutolea adui zako mbele yako; kwa hiyo na kiwe kitakatifu kituo chako; asije akaona kitu kwako kisichokuwa safi, akageuka na kukuacha”.
Kumbukumbu 23:13 “nawe uwe na jembe dogo katika silaha zako; napo uotamapo nje uchimbe kwa lile jembe, na kugeuka na kukifunika kikutokacho;
14 kwa kuwa Bwana. Mungu wako, yuatembea katika kituo akuokoe, na kukutolea adui zako mbele yako; kwa hiyo na kiwe kitakatifu kituo chako; asije akaona kitu kwako kisichokuwa safi, akageuka na kukuacha”.
Wana wa Israeli walipewa maagizo na Mungu, waweke mazingira yao yanayowazunguka katika hali ya safi!.. Kwamba watu wasafishe mazingira ya maeneo wanayoishi, wasikae katika uchafu, mtu anapokwenda haja kubwa, angalau ahakikishe uchafu wake hauachi juu, bali aufukie.
Na hiyo ni kwasababu Bwana Mungu anapita katikati ya mazingira yao, ili kuwapigania..Hivyo apitapo na kuona au kukuta uchafu (mf. Kinyesi n.k), atageuka na kuwaacha!.
Hiyo ni kuonyesha kuwa Mungu haangalii roho tu, bali pia anaangalia pia Mwili na mazingira. Kama Mungu anaweza kuwaacha tu wana wa Israeli kwasababu ya kinyesi kilichozagaa juu ya ardhi, ataachaje kumwacha binti anayevaa nusu uchi?, ataachaje kumwacha binti anayevaa vimini au nguo zinazobana na kuchora maungo yake, ataachaje kumwacha kijana aliyejichora mwili wake?.
Ndugu, mahubiri ya kusema kwamba Mungu haangalii mwili anaangalia tu roho! Ni ya kutoka kuzimu!!, jihadhari nayo, ni ya adui shetani asilimia mia. Tunawajibu wa kujitunza miili yetu, kwasababu biblia inasema miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu, na vile vile tunawajibu wa kujiweka safi katika mazingira pia ya nje, kwasababu Mungu wetu pia ni Mungu wa usafi na si uchafu. Kama anayatazama mazingira ya nje, na kutoa hukumu, hatashindwa kutazama mwili wako na kutoa hukumu.
Bwana atubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho mengine
Mada Nyinginezo:
Hanithi ni nini katika biblia? (kumbukumbu 23:17)
Nini maana ya “Siku moja nyuani mwa Bwana ni bora kuliko siku elfu”?
]https://wingulamashahidi.org/2020/11/26/lango-limebadilika/
Pambaja ni nini katika Biblia kama tunavyosoma katika kitabu cha Wimbo ulio bora 1:2?
INJILI YA MANENO LAINI ITAKUGHARIMU.
Rudi nyumbani
Print this post