Ayubu 23:10 “Lakini yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu”
Kila mmoja kaandaliwa mapito yake na Mungu, ijapokuwa hatma yetu ni moja lakini mapito kamwe hayawezi kufanana. Na anafanya hivyo kwasababu ya utofauti wa wito na huduma, aliopewa kila mmoja katika kusudi lake aliloitiwa duniani.
Hivyo unapookoka anachokifanya Mungu ni kuitazama njia yako, kisha kukupitisha katika mitihani yake ili uweze kufuzu kulitimiza kusudi lake alilokuwekea mbele yako. Hivyo hii mitihani kwa jina lingine ndio yanainaitwa majaribu. Tofauti na baadhi wanavyotafsiri kwamba majaribu ni mitego ya dhambi Mungu anayompitishia mtu. Jibu ni hapana, Kama ni hivyo basi maandiko yangekuwa yanakinzana pale yanaposema, Mungu hamjaribu mtu, bali mtu mwenyewe anajaribiwa na tamaa zake mwenyewe (Yakobo 1:13-15)
Kwahiyo sasa lengo la mitihani hii ni kukuimarisha zaidi. Kwamfano labda wewe umewekewa huduma ya uponyaji ndani yako. Wakati mwingine Mungu anaweza kuruhusu upite mapito kama ya kuumwa sana, ili utambue umuhimu wa kuwajali na kuchukuliana na wagonjwa wenye hali mbaya kama hizo, watakaokuja kwako kuhitaji msaada mbeleni.
Ndio maana ya hili andiko ‘yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu’
Kwamfano katika biblia utaona mitume walipitia vipindi vingi mbalimbali vya kuvua samaki, lakini asilimia kubwa ya hivyo hawakuwa wanapata chochote baada ya kutaabika usiku kucha, yamkini wengine walikuwa wanapata lakini wao hawapati chochote, lakini walipokutana na Yesu walipata kirahisi. Ni nini Bwana alikuwa anawafundisha? Ni uvumilivu katika kuwavua watu wake, na kwamba watakapoanza huduma watambue kuwa wokovu unatoka kwa Bwana na sio katika uweza wa nguvu zao.
Vivyo hivyo na wewe utapitishwa katika pito lako la moto, ili kujaribiwa lengo ni kuimarishwa. Wengine wanafanywa watumwa wa kuteswa sana ili watakapofanywa mabwana waweze kuwastahi watoto wa Mungu kwa upole watakaokuja chini yao, wakikumbuka mateso yaliyowakuta wao hayapaswi kwenda kwa wengine.
Mwingine katika utasa, mwingine katika vifungo, mwingine katika ujane, lakini madarasa yao yakishakamilika, basi taabu hizo zinawaacha. Na hivyo wanakuwa tayari kwa ajili ya utumishi wa Bwana.
Halikadhalika na wewe pia ikiwa umeokoka, na unajikuta katika madarasa ya Mungu, yakupasa useme kama Ayubu ‘yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu’. Na mwisho wako utakuwa ni mkuu sana kuliko mwanzo. Kwasababu siku moja utayafurahia mapito ya Mungu na kumtukuza sana (Yeremia 29:11).
Lakini kama hujaokoka, usiseme unafundishwa na Mungu, hayo ni mafundisho yako au ya ibilisi. Kwasababu Mungu hawezi kumpa mitihani mtu ambaye si mwanafunzi wake. Ni heri ukafanya uamuzi wa busara leo kwa kumkaribisha Yesu Kristo moyoni mwako. Unasubiri nini usifanye hivyo?
Ikiwa upo tayari kufanya hivyo basi bofya hapa kwa mwongozo huo >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
TABIA ZA NJIA YA MUNGU KWA MKRISTO
MAJARIBU 10 WANA WA ISRAELI WALIYOMJARIBU MUNGU.
Kupwelewa maana yake nini? (Matendo 27:26).
HEKIMA NI NINI? NA UFAHAMU UNAPATIKANA WAPI?
Kwanini biblia inaitaja mara kwa mara dhahabu ya Ofiri?
About the author