Kwanini Mungu anasema “Afanyaye malaika zake kuwa pepo”?

Kwanini Mungu anasema “Afanyaye malaika zake kuwa pepo”?

SWALI: Waebrania 1:7 “Na kwa habari za malaika asema, Afanyaye malaika zake kuwa pepo, Na watumishi wake kuwa miali ya moto”..Je Mungu anawageuza malaika zake kuwa mapepo?


JIBU: Ndio! Wale malaika walioasi mbinguni waligeuka na kuwa mapepo baada ya kutupwa duniani, ndio haya yanayowasumbua wanadamu leo. Lakini mstari huo hapo juu hauzungumzii roho za malaika walioasi(yaani mapepo)… bali unazungumzia juu ya upepo huu wa asili(yaani hewa iliyopo kwenye mwendo). Sasa sio kwamba Mungu anawageuza na kuwafanya upepo hapana bali anafananisha na upepo malaika wake. Ili kuelewa hilo Zaidi tusome mstari ambao umelizungumzia jambo hilo vizuri..ambao ndiko Mtume Paulo aliko linukuu..

Zaburi 104:1 “Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Wewe, Bwana, Mungu wangu, Umejifanya mkuu sana; Umejivika heshima na adhama.

2 Umejivika nuru kama vazi; Umezitandika mbingu kama pazia;

3 Na kuziweka nguzo za orofa zake majini. Huyafanya mawingu kuwa gari lake, Na kwenda juu ya mabawa ya upepo,

4 HUWAFANYA MALAIKA ZAKE KUWA PEPO, NA WATUMISHI WAKE KUWA MOTO WA MIALI

5 Uliiweka nchi juu ya misingi yake, Isitikisike milele”.

Katika mistari hiyo unaona Mungu anavifananisha vitu vya asili kama hifadhi yake..utaona anasema umejivika nuru kama vazi!..kiuhalisia Nuru haliwezi kuwa vazi…hali kadhalika anasema ameyafanya mawingu kuwa kama gari lake, vilevile mawingu hayawezi kuwa gari…lakini kwake yeye ni kama gari…na mbingu amezifananisha kama pazia, hizo zote ni lugha za picha tu..ni kama isemavyo kwamba kilimo ni uti wa mgongo wa Taifa…kuonyesha kilimo ni kama vile mfupa uliopo nyuma ya mngongo wa mtu unaoufanya mwili uwe wima. Pasipo huo mwili hauwezi kusimama vivyo hivyo pasipo kilimo nchi haliwezi kuwepo!

Na hapa Mungu anawafananisha Malaika wake na upepo…Upepo ndio unayoyafanya mawingu yatembeee, kama vile ulivyo wa muhimu kwa merikebu baharini, bila upepo mawingu hayawezi kutembea, wala merikebu haziweki kutembea, wanasema Upepo ndio kitu chenye nguvu kuliko vitu vyote vya asili, hata majini hayakuti….na hapo tayari Mungu kashayafananisha mawingu na gari lake ambalo linakwenda juu ya upepo. Ikifunua kuwa malaika wana sehemu kubwa katika kulitimiza kusudi la Mungu na kulisogeza mbele kusudi lake.

Lakini ukisoma hiyo Waebrania utaona, Yesu Kristo ambaye ni Mwana wa Mungu, yeye hajafananishwa na upepo kama Malaika…Yeye amefananishwa na yule aketiye juu ya kiti cha enzi mwenyewe ndio maana anaitwa (chapa ya nafsi ya Mungu)..Alipopaa alikwenda kuketi katika mkono wa kuume wa Mungu Baba, hivyo ni mfano wa Baba, yeye naye mawingu yatakuwa ni Gari lake, na Malaika ni kama upepo wa kulisukuma gari lake..Ndio maana biblia inasema hapo “amefanyika bora kuliko malaika”…Haleluya!..

Na kwakuwa yeye kafanyika bora, na wale waliomwamini na watakaomwamini..watafanyika bora kama yeye..kwasababu yeye alipo ndipo na sisi tutakapokuwepo. Na hapo ndipo malaika wanatuhudumia (Waebrania 1:14)

Atukuzwe Mungu kwa kumtoa mwanawe kwaajili yetu.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

UCHAWI WA BALAAMU.

FUKUZA TAI WOTE JUU YA SADAKA YAKO.

KWANINI UBATIZO NI WA MUHIMU.

MTANGO WA YONA.

NA YEYE ALIYEKETI JUU YA WINGU AKAUTUPA MUNDU WAKE JUU YA NCHI, NCHI IKAVUNWA.

MAJESHI YA PEPO WABAYA.

KABLA YA MAANGAMIZI, KRISTO HUWA ANAONYESHA KWANZA NJIA YA KUTOROKEA.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments