Mstari huu una maana gani? “Mathayo 23:39 Hamtaniona kamwe tangu sasa”

Mstari huu una maana gani? “Mathayo 23:39 Hamtaniona kamwe tangu sasa”

SWALI: Mathayo 23:39 “Kwa maana nawaambia, Hamtaniona kamwe tangu sasa, hata mtakaposema, AMEBARIKIWA AJAYE KWA JINA LA BWANA.”


JIBU: Ukisoma kuanzia juu utaona habari hiyo alikuwa anaizungumza Bwana Yesu alipokuwa anaingia Yerusalemu, Na kuona jinsi mji ule ulivyo mkataa, na kukataa wokovu tangu zamani za Manabii wa agano la kale hadi wakati wake, Na jinsi ulivyowaua wale wajumbe wote waliotumwa kwake,..Ndipo hapa sasa Yesu akautabiria kuwa atauacha katika hali ya ukiwa mpaka hapo watakapogeuka..

Embu tusome..

Mathayo 23:37 “Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii, na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako! Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hamkutaka!

38 Angalieni, nyumba yenu mmeachiwa hali ya ukiwa.

39 Kwa maana nawaambia, Hamtaniona kamwe tangu sasa, hata mtakaposema, Amebarikiwa ajaye kwa jina la Bwana”.

Unaona, Na historia inaonyesha kweli, Wayahudi waliachwa na Mungu, tangu huo wakati hadi sasa ni miaka 2000 imeshapita, bado hajawarudiwa na mji wa Yerusalemu nao ulikuwa ni magofu tangu zamani, ni karne za juzi juzi tu ndio umeanza kujengwa tena na kukaliwa na watu.., lakini Bwana hakuishia tu pale, bali alisema, utaendelea kuwa hivyo hivyo katika hali ya ukiwa mpaka siku hiyo watakaposema tena Amebarikiwa ajaye kwa jina la Bwana..Yaani ikiwa na maana watakapotubu na kumtambua Kristo kuwa ni yule masihi kweli..

Lakini ni kwanini aseme “hata mtakaposema, AMEBARIKIWA AJAYE KWA JINA LA BWANA.” Na si mpaka hapo mtakaposema mimi ni Masihi?

Utakumbuka tukio lililotendekea nyuma kidogo kabla hajafika Yerusalemu alikuwa anaimbiwa hayo maneno Hosana, Hosana Amebarikiwa ajaye kwa jina la Bwana…

Na ndio maaana utaona Bwana akitumia maneno hayo hayo tena kuashiria kuwa mpaka siku wayahudi watakapompokea yeye kwa namna hiyo hiyo, ndipo wokovu utageuka kwao. Na dalili zote zimeshaanza kuonekana sasa, Israeli imeshakuwa taifa huru, wayahudi wanaanza kuyagundua makosa yao kidogo kidogo..Je! Unadhani ni kitu gani kitatokea muda mfupi baadaye.. Bila shaka watamgeukia na kutubu..Na biblia inasema siku watakapomgeukia uovu wao utaondolewa wote ndani ya siku moja..

Kama unabii inavyosema..

Zekaria 12:10 “Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimchoma; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza.

11 Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu huko Yerusalemu, kama maombolezo ya Hadadrimoni katika bonde la Megido.

12 Nayo nchi itaomboleza, kila jamaa peke yake; jamaa ya nyumba ya Daudi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Nathani peke yao, na wake zao peke yao;

13 jamaa ya nyumba ya Lawi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Shimei peke yao, na wake zao peke yao.

14 Jamaa zote zilizosalia, kila jamaa peke yake, na wake zao peke yao”.

Sasa tukishaona mambo hayo yanatokea, basi ujue kuwa Neema ya wokovu imeshaondoka kwetu, na Unyakuo tayari umeshapita.

Ni nyakati za mwisho tunazoishi, Je, bado na wewe upo vuguvugu? Unataka na wewe uachwe ukiwa kwa mfano wa Wayahudi walivyoachwa zamani kwa kutokutubu kwao? Wakati ambao utamtafuta Bwana hutamwona, utautafuta wokovu hutaupata?. Usitamani kabisa wakati huo ukukute hali bado upo dhambini, tubu, itii injili inapohubiriwa kwako kila siku,..UNYAKUO upo mlangoni.

Maran atha!.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

MAOMBI YA VITA

WATAMTAZAMA YEYE AMBAYE WALIMCHOMA; NAO WATAMWOMBOLEZEA.

BUSTANI YA NEEMA.

UMUHIMU WA KUZALIWA MARA YA PILI.

JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments