Mtambo kwenye biblia ni neno linalomaanisha aidha kifaa kinachonasa kitu, au kinachorahisisha kazi Fulani.
Kwamfano tukisoma
Ayubu 18:9
[9]Tanzi litamshika kisigino chake, Na mtambo utamgwia.
Hapo ni Bildadi rafiki yake Ayubu anaeleza hatma ya mtu mwovu, anasema ni sawa na mtu atembeaye katika njia ya mitego, na ghafla hunaswa asiweze kunasuka ndio mtu mwovu katika njia zake mbaya hukumbwa na hayo.
Anasema mtambo utamgwia, maana yake kitu kinasacho Kitamkamata.
Neno hilo pia utalisoma…kwenye mistari ya juu yake..Bildadi anasema..
Ayubu 18:2
[2]Je! Hata lini utayategea maneno mitambo? Fikiri, kisha baadaye tutanena.
Akitumia lugha ya picha…
akimaanisha hata lini utayanasa maneno yako? (yaani utaacha kuongea?).
Lakini sehemu nyingine Inayolitaja Neno hili Ni..
2 Mambo ya Nyakati 26:14-15
[14]Uzia akawafanyizia jeshi lote ngao na mikuki, na chapeo, na deraya za madini, na nyuta, na mawe ya kupiga kwa teo. [15]Akafanya katika Yerusalemu mitambo ya vita, iliyobuniwa na watu wastadi, iwekwe juu ya minara na juu ya buruji, ili kutupa mishale na mawe makubwa. Jina lake likaenea mbali sana; kwa kuwa alisaidiwa mno ajabu, hata akapata nguvu.
[14]Uzia akawafanyizia jeshi lote ngao na mikuki, na chapeo, na deraya za madini, na nyuta, na mawe ya kupiga kwa teo.
[15]Akafanya katika Yerusalemu mitambo ya vita, iliyobuniwa na watu wastadi, iwekwe juu ya minara na juu ya buruji, ili kutupa mishale na mawe makubwa. Jina lake likaenea mbali sana; kwa kuwa alisaidiwa mno ajabu, hata akapata nguvu.
Inazungumzia nguvu za kijeshi alizokuwa nazo mfalme Uzia, hata kufikia kubuni mitambo mikubwa ya kivita.. ya kufyatulia silaha kwa maadui zake.
Bwana akubariki
Je umeokoka?
Kumbuka saa Tulizopo ni za majeruhi, siku yoyote wakati wowote Kristo anarudi jiulize umejiandaaje ndugu?. Unyakuo wa kanisa ukipita leo utakuwa wapi mpendwa…
Jitathmini maisha yako? Itakufaidia nini uupate ulimwengu wote na mambo yake halafu upate Hasara ya nafsi yako. Tubu mgeukie Kristo uoshwe dhambi zako, upokee uzima wa milele.
Ikiwa upo tayari kumpokea Yesu leo.. basi fungua hapa kwa mwongozo Wa Sala ya Toba.. >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Mafundisho mengine:
Print this post
Haya ni mafundisho maalumu kwa viongozi aidha wachungaji, au wasimamizi ndani ya kanisa..Maadamu una kundi la watu aidha 2-3 au zaidi la kuwasimamia, basi mafunzo haya yatakusaidia sana.
Kutoka 32:9-10
[9]Tena BWANA akamwambia Musa, Mimi nimewaona watu hawa, na tazama, ni watu wenye shingo ngumu [10]basi sasa niache, ili hasira zangu ziwake juu yao, niwaangamize, nami nitakufanya wewe uwe taifa kuu.
[9]Tena BWANA akamwambia Musa, Mimi nimewaona watu hawa, na tazama, ni watu wenye shingo ngumu
[10]basi sasa niache, ili hasira zangu ziwake juu yao, niwaangamize, nami nitakufanya wewe uwe taifa kuu.
Mungu alipomuita Musa kwenda kuwaokoa watu wake, alijua asili ya hao watu watakuwa ni wa namna gani. Pengine Musa alidhani anawaokoa watu ambao ni wema sana, watulivu, na wapole.
Lakini mambo hayakuwa kama hivyo, licha ya kuona miujiza mikubwa namna ile, bahari kupasuka, mana kushuka Mbinguni, miamba kutoa maji, nguzo ya moto kuwaongoza usiku kila siku…
Bado walitengeneza sanamu za ndama na kusema hii ndio miungu yetu iliyotutoa Misri tuiabudu..walinung’unika, walimsengenya kiongozi wao, waliasi na kujiundia Makundi..Ni watu ambao walikuwa ni wagumu kuongoza, wazito kutii na wapesi kulalamika.
Ni vema kujua kuwa kila kiongozi wa kweli kuna siku atapitia kama Musa alivyopitia..
Ikifikia hatua hii wengi wanasema kama utumishi ndio huu ni heri niache, kama naonyesha fadhila zote hizi kinyume chake narudishiwa masengenyo na uasi, ni heri niache…
Ukifikiria hivyo bado hujawa kiongozi, Mungu alijua asili yao kwamba ni watu wenye shingo ngumu..alijua Yuda ni msaliti lakini bado alimpatia mwanae, amchunge.
Hao hao bado aliwaokoa na akataka wachungwe..
Shingo ngumu ni mtu wa namna gani?. Ni mtu anayefananishwa na ng’ombe ambaye hataki kufungwa Nira na Bwana wake…shingo inakuwa ngumu kuvishwa nira..
Hii ni aina ya watu ambao Hawana utii, hawachungiki, hata waone miujiza mikubwa namna Gani, hata wasaidiweje, si rahisi kuacha tabia zao za usengenyaji, wizi, uasi. Kiburi N.k.
Lakini bado Mungu anawaacha chini ya mchungaji waangaliwe..
Musa alikutana na waabudu sanamu, wanung’unikaji, Na wasahaulifu wa fadhili za Mungu…
Lakini alifanyaje?
Hata pale ambapo Mungu alitaka kuwaangamiza Musa aliwaombea. Alisimama kufanya upatanisho kwa ajili yao.
Ni ujumbe gani tunapewa?
Kiongozi wa kweli badala ya kughahiri kumchunga kondoo wake humwombea kwa bidii ili Bwana amponye asipotee kabisa kwenye dhambi.
Kiongozi wa kweli, huwa tayari hata kupoteza maisha yake kwa kondoo wake.. Musa alisema..
Kutoka 32: 32 Walakini sasa, ikiwa utawasamehe dhambi yao – na kama sivyo, unifute, nakusihi, katika kitabu chako ulichoandika.
Uongozi sahihi sio Kuongoza Watu wakamilifu, lakini kuongozo Watu dhaifu Kwa Mungu mkamilifu.
Uongozi Sahihi huweka katika uwiano sahihi “neema na kweli”
Ni vema kufahamu pia si kila wakati Musa alikuwa anasimama kuwatetea Waovu, hapana wakati mwingine aliruhusu upanga wa Mungu upite, Ili dhambi iogopwe…utakumbuka wakati ule walipotengeneza Sanamu ya ndama, na hasira Ya ki-Mungu ilimvaa Musa, ndipo Akazivunja zile mbao mbili, kisha akawaita watu walio upande wa Bwana wamfuate, Na wale waliosalia waliadhibiwa vikali kwa mauti.
Dhambi iwapo kanisani, haipaswi kuvumiliwa..Kutoa adhabu na wakati mwingine kuwaondoa wale wabaya ndani ya kundi ili lisiendelee kuharibiwa..
Lakini katika yote wewe kama kiongozi, huna budi kujifunza Uvumilivu, kuwaombea kondoo wako, na kuwa mpole, lakini pia kushughulika na dhambi Vikali katika nyumba ya Bwana.
Lakini kumbuka ijapokuwa Ni kazi, yenye mapito mengi ya masumbufu na maumivu Lakini thawabu yake na faida yake haifananishwi na gharama ulizoingia.. Hivyo penda kuchunga watu wa Mungu…Ndio heshima ya juu ya upendo kwa Mungu wako.
Mithali 14:4
[4]Zizi ni safi ambapo hapana ng’ombe; Bali nguvu za ng’ombe zaleta faida nyingi.
TEMBEA NDANI YA SUKOTHI YAKO.-Maafundisho maalumu kwa watumishi
TOFAUTISHA KATI YA MAFUNDISHO YA YESU, NA YA WAANDISHI.
MHESHIMU MCHUNGAJI WAKO.
Huu ni mfululizo wa mafunzo maalumu ya wazazi kwa watoto..
Ukiwa kama mzazi, Njia bora ya malezi, sio kumjali mtoto wako, kwa kila kitu sasa.. Hata kama ni haki yake kukipata, Usiwe mwepesi kumfanyia kila jambo leo hata kama una uwezo wa kumfanyia, Usimjali sasa, mjali kwa baadaye. Tumia nguvu hizo kumwekezea kwa baadaye lakini sasa shughulika naye kitabia, kinidhamu, ki-utu..Acha hiyo tabia ya kujali-jali utamuharibu mtoto.
Wengi wetu tunashindwa kujua, kuwa ni kanuni ya ki- Mungu mtoto aishi kama mtumwa, hata kama yeye ndio mrithi wa yote.
Wagalatia 4:1 Lakini nasema ya kuwa mrithi, wakati wote awapo mtoto, hana tofauti na mtumwa, angawa ni bwana wa yote; 2 bali yu chini ya mawakili na watunzaji, hata wakati uliokwisha kuamriwa na baba
Mzazi mwenye Akili na maono bora kwa wanawe, haangalii mali zake anazitumiaje kwa mwanawe sasa, bali huangalia tabia gani anamjengea leo, ili kesho aweze simamia vema maisha yake, au mali zake.
Embu fikiria vema, yule Baba Tajiri aliyekuwa na wana wawili, ambao kwa siku nyingi waliishi na baba yao bila kuona faida ya utajiri wa baba yao. Mpaka siku moja mmojawao (yule mdogo) uzalendo ukamshinda, akamwambia baba yake nipe sehemu ya mali yangu inayoniangukia, hatimaye akapewa akaondoka, lakini maisha yalipo-mgeukia hali ikawa mbaya, mwishowe akazingatia kurudi kwa baba yake. Na baba yake akampokea akamfanyia karamu kubwa. Lakini yule mwana mwingine aliporudi mashambani, na kuona sherehe kubwa kwa ndugu yake, akachukizwa, ndipo akamwambia baba yake “Tazama, mimi nimekutumikia miaka mingapi hii, wala sijakosa amri yako wakati wo wote, Lakini hujanipa mimi mwana-mbuzi, nifanye furaha na rafiki zangu;”
Tusome;
Luka 15:11-31
11 Akasema, Mtu mmoja alikuwa na wana wawili; 12 yule mdogo akamwambia babaye, Baba, nipe sehemu ya mali inayoniangukia. Akawagawia vitu vyake. 13 Hata baada ya siku si nyingi, yule mdogo akakusanya vyote, akasafiri kwenda nchi ya mbali; akatapanya mali zake huko kwa maisha ya uasherati. 14 Alipokuwa amekwisha tumia vyote, njaa kuu iliingia nchi ile, yeye naye akaanza kuhitaji. 15 Akaenda akashikamana na mwenyeji mmoja wa nchi ile; naye alimpeleka shambani kwake kulisha nguruwe. 16 Akawa akitamani kujishibisha kwa maganda waliyokula nguruwe, wala hapana mtu aliyempa kitu. 17 Alipozingatia moyoni mwake, alisema, Ni watumishi wangapi wa baba yangu wanaokula chakula na kusaza, na mimi hapa ninakufa kwa njaa. 18 Nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu na kumwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; 19 sistahili kuitwa mwana wako tena; nifanye kama mmoja wa watumishi wako. 20 Akaondoka, akaenda kwa babaye. Alipokuwa angali mbali, baba yake alimwona, akamwonea huruma, akaenda mbio akamwangukia shingoni, akambusu sana. 21 Yule mwana akamwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; sistahili kuitwa mwana wako tena. 22 Lakini baba aliwaambia watumwa wake, Lileteni upesi vazi lililo bora, mkamvike; mtieni na pete kidoleni, na viatu miguuni; 23 mleteni ndama yule aliyenona mkamchinje; nasi tule na kufurahi; 24 kwa kuwa huyu mwanangu alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana. Wakaanza kushangilia. 25 Basi, yule mwanawe mkubwa alikuwako shamba na alipokuwa akija na kuikaribia nyumba, alisikia sauti ya nyimbo na machezo. 26 Akaita mtumishi mmoja, akamwuliza, Mambo haya, maana yake nini? 27 Akamwambia, Ndugu yako amekuja, na baba yako amemchinja ndama aliyenona, kwa sababu amempata tena, yu mzima. 28 Akakasirika, akakataa kuingia ndani. Basi babaye alitoka nje, akamsihi. 29 AKAMJIBU BABA YAKE, AKASEMA, TAZAMA, MIMI NIMEKUTUMIKIA MIAKA MINGAPI HII, WALA SIJAKOSA AMRI YAKO WAKATI WO WOTE, LAKINI HUJANIPA MIMI MWANA-MBUZI, NIFANYE FURAHA NA RAFIKI ZANGU; 30 lakini, alipokuja huyu mwana wako aliyekula vitu vyako pamoja na makahaba, umemchinjia yeye ndama aliyenona. 31 Akamwambia, Mwanangu, wewe u pamoja nami sikuzote, na vyote nilivyo navyo ni vyako.
Nataka uone sifa ya huyo baba, kwa wanawe, ijapokuwa alikuwa na mali, lakini hakutaka Watoto wake, waishi kwa mali zake, bali waishi kama watumwa wengine. Sio kwamba alikuwa anawatesa, Hapana, alikuwa anawatengeneza ili baadaye wakishajua maisha hasaa ni nini kivitendo, ndipo awaache huru, wapewe vyote na baba yao, wafurahie maisha wayapendayo.
Leo hii imekuwa kinyume chake, utaona mtu ndiye anayetumia nguvu zake, na mali zake, kumdekeza mtoto, kama yai, kumletea wafanyakazi ndani, wawapikie, wawafulie, wawapigie deki, na pasi, wenyewe wakae wakitazama muvi Netflix, na kucheza magemu, kwenye Ipad, na computa,
Akidhani anamlea mtoto, kumbe anamlea mwana-mpotevu. Mtoto akikosea tu, hawezi kuadhibiwa, mzazi anasema sitaki mtoto wangu ateseke kama mimi nilivyoteseka, kwani ni nani kakwambia mtoto akiadhibiwa ni lengo la kuteswa? Watoto hawafundishwi kufunga, hata kwa sehemu (nusu siku), au kupelekwa mikesha mara moja moja wajifunze kanuni za kiroho, wazazi wanasema hawa bado wadogo. Hivi ni kizazi gani tunakilea??
Si lazima kila siku ale mboga saba, si lazima umpe chakula anachokitaka yeye, siku nyingine fululiza ugali maharage, wiki mbili nyumbani, mwache alie, mpaka azoee..Mambo kama hayo unaweza kuona unamtesa mtoto, lakini ndio njia sahihi ya malezi..unamtengeneza mtu imara sio lege-lege.
Likizo inapofika, kuliko kumpeleka beach kwenye mabembea, na masherehe, mpeleke kijijini kwenu, aone mazingira ya asili, ale vyakula vya kule, atumie vyoo vya kule ambavyo sio vya kuflash, aende akakatie ng’ombe majani, aende na wachungaji machungani akae huko mpaka likizo iishe, ndipo arudi..
Lakini wewe mwenyewe huku nyuma unajua ni nini unafanya, ukimwandalia akiba, nzuri, ili baadaye atakapoelimika kiroho na kimwili, ukimpa vya kwako, au ukimdekeza atakavyo, ataweza kujisimamia mwenyewe, na kuwa mtu mkakamavu thabiti, na Jasiri, mwenye utu na kiongozi awezaye kuishi katika jamii, na kuwajali na walio wanyonge na wenye shida.
Hayo ndio malezi bora ya mtoto. Mfanye leo mtumwa ili kesho awe mfalme, lakini ukichagua kumfanya leo mfalme, jiandae kesho kuwa mtumwa mfano wa mwana- mpotevu.
Mithali 22:6 Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee
NI NINI KINATOKA KINYWANI MWA MTOTO WAKO?
MRUDI MWANAO NAYE ATAKUSTAREHESHA
NAFASI YAKO WEWE MAMA KWA MTOTO NA WAJUKUU WAKO NI IPI?.
WhatsApp
SWALI: Tumekuwa tukisikia kuwa mtu akifa, huko aendako anakutana na mateso makali ya jehanamu. Sasa napenda kufahamu je ni roho ndio itakayoteketezwa au na miili pia?
JIBU: Maandiko yanatueleza siku ya mwisho ya hukumu, wafu wote watafufuliwa. (Iwe ni wema au waovu), wote watairudia miili yao ya asili yaliyokuwa nayo duniani.
Yohana 5:28
28 Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake.29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu
Ufunuo 20: 12-13
12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake
Waliokufa katika Kristo (Watakatifu) watavikwa miili mipya ya utukufu, isiyoharibika (1Wakorintho 15:42-54) lakini waovu watakuwa na miili yao ya asili. Ambayo katika hiyo watahukumiwa na kutupwa katika lile ziwa la moto, lililo maalumu kwa mateso ya mtu milele.
Hivyo ni vizuri ifahamike, kuwa kitakachoteketezwa sio roho tu, bali na mwili pia, Bwana Yesu aliliweka hilo wazi katika maneno haya;
Mathayo10:28 Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum.
Umeona hapo?.. Awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum. Kuonyesha kuwa mwili nao utashiriki mateso ya milele.
Tukishayajua hayo, tunapaswa tufanyaje?
Je! Umemwamini Bwana Yesu ndugu? Wokovu ni sasa, mgeukie akuponye, uwe salama, hata ukifa uwe na uhakika wa kuurithi uzima wa milele, Itakufaidia nini kuupata ulimwengu mzima, kisha upate hasara ya nafsi yako? Fanya uamuzi wa busara.
Okoka, leo uponywe. Ikiwa upo tayari kufanya hivyo, basi fungua hapa kwa mwongozo wa sala ya Toba >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
HERI WAFU WAFAO KATIKA BWANA
MWOMBENI BWANA WA MAVUNO APELEKE WATENDA KAZI.
MAUTI NA KUZIMU ZIKAWATOA WAFU WALIOKUWAMO NDANI YAKE.
Mtume Paulo, alipokamatwa kule Yerusalemu na kupelekwa mbele ya wafalme kuhukumiwa, tunaona ujasiri wake ulikuwa wa ajabu, badala atumie nafasi ile kujitetea, kimahakama, kinyume chake alitumia nafasi ile kuhubiri injili, kiasi cha kumfanya mfalme Agripa kushawishwa kwa muda mfupi kuiamini injili.. Ujasiri wa namna hiyo hakika, ni wa kuigwa sana.
Matendo 26:28
25 Lakini Paulo akasema, Sina wazimu, Ee Festo mtukufu, bali nanena maneno ya kweli na ya akili kamili. 26 Kwa maana mfalme anajua habari za mambo haya, nami naweza kusema naye kwa ujasiri, kwa sababu najua sana ya kuwa hapana neno moja katika hayo asilolijua; kwa maana jambo hilo halikutendeka pembeni. 27 Mfalme Agripa, je! Wawaamini manabii? Najua ya kuwa wawaamini. 28 AGRIPA AKAMWAMBIA PAULO, KWA MANENO MACHACHE WADHANI KUNIFANYA MIMI KUWA MKRISTO. 29 Paulo akamjibu, Namwomba Mungu kwamba, ikiwa kwa machache au ikiwa kwa mengi, si wewe tu ila na hao wote wanaonisikia leo wawe kama mimi, isipokuwa vifungo hivi.
Lakini Tunaona jambo moja, huyu mfalme Agripa alichomwa sana na maneno ya mtume Paulo, alishawishwa ipasavyo na injili ile, lakini hakuwa tayari kugeuka moja kwa moja kwa Kristo, aliishia tu kushawishwa.. Ukweli ni kwamba mtu katika hatua hiyo bado hujaokolewa..
Ni sawa na leo hii, watu wengi wanapoisikia injili, ni kweli wanashawishwa, wanaiheshimu, wanaifurahia, wanachomwa mioyo yao, wengine wanaomboleza na kuhuzunika juu ya dhambi zao, lakini je! Wameikubali na kutii?
Utaona wataishia tu kusema, nimebarikiwa!, wataishia kusema Neno zuri linaonya!, wataishia kusema, Mungu nisaidie, nimeguswa leo, ndugu hiyo haimaanishi kuwa umeokoka, huna tofauti na Agripa.
Watu walioshawishwa kwelikweli, waliochomwa mioyo, ni lazima utaona kuna kitu cha ziada watafanya watauliza “Tufanyeje ndugu zetu?”
Matendo 2: 37 Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, TUTENDEJE, NDUGU ZETU? 38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie. 40 Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi. 41 Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu. 42 Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.
Matendo 2: 37 Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, TUTENDEJE, NDUGU ZETU?
38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie. 40 Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi. 41 Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu. 42 Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.
Umeona?, hawakuishia tu kusema “asante Petro kwa Neno” hawakuishia kusema “ubarikiwe mtumishi” ..“Umetujenga mchungaji”. Walisema, tutendeje ndugu zetu?..Tuchukue hatua gani?
Utaona Wakabatizwa, wote siku ileile, wakajazwa Roho, Wakadumu katika fundisho la mitume, kila siku. Ndio hao walioisambaza injili ulimwenguni kote.
Leo ndio tunahitaji kuona Kundi la watu wa namna hii, ambao wanachukua hatua ya kumpokea Yesu kikamilifu na kumfuata kwa mioyo yao yote, kimatendo. Na sio kama akina Agripa, ambaye hakuwa na matunda ya kuitii injili.
Saa ya wokovu ni sasa, usiseme kesho nitaokoka, hakuna wokovu wa kesho, acha kujidanganya, bali ni leo. Aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi usifurahie mafundisho, usifurahie miguso ya ki-mahubiri swali ni je umeokoka? Kristo leo akirudi utaenda naye?
Na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao.
WOKOVU NI SASA
Sauli (Mtume Paulo) alipokuwa anaelekea Dameski kwa lengo la kuwafunga na kuwatesa watakatifu, kama tunavyoifahamu habari alitokewa na Yesu njiani, mwanga Mkali ulimpiga machoni, akashindwa kuona, Wakamchukua mpaka ndani ya mji akiwa kipofu.
Lakini tunaona alipokuwa kule, hakuwa katika hali ya kawaida, bali katika maombolezo makubwa rohoni, hakula chakula chochote, wala maji..(maana Yake alikuwa katika mfungo), lakini si hilo tu zaidi sana alikuwa akiomba dua.
Baada ya hapo tunaona jambo lingine likitokea mtu mmoja aliyeitwa Anania anatokewa na Yesu, kisha anaagizwa amfuate Paulo. Lakini eneo analoagizwa ni katika njia iliyoitwa NYOFU…
Maana Yake “njia iliyonyoka”.
Matendo 9:8-12
[8]Sauli akainuka katika nchi, na macho yake yalipofumbuka, hakuona kitu; wakamshika mkono wakamleta mpaka Dameski. [9]Akawa siku tatu haoni; hali, wala hanywi. [10]Basi palikuwapo Dameski mwanafunzi jina lake Anania. Bwana akamwambia katika maono, Anania. Akasema, Mimi hapa, Bwana. [11]Bwana akamwambia, Simama, enenda zako katika njia iitwayo Nyofu, ukaulize katika nyumba ya Yuda mtu aitwaye Sauli, wa Tarso; maana, angalia, anaomba; [12]naye amemwona mtu, jina lake Anania, akiingia, na kumwekea mikono juu yake, apate kuona tena.
[8]Sauli akainuka katika nchi, na macho yake yalipofumbuka, hakuona kitu; wakamshika mkono wakamleta mpaka Dameski.
[9]Akawa siku tatu haoni; hali, wala hanywi.
[10]Basi palikuwapo Dameski mwanafunzi jina lake Anania. Bwana akamwambia katika maono, Anania. Akasema, Mimi hapa, Bwana.
[11]Bwana akamwambia, Simama, enenda zako katika njia iitwayo Nyofu, ukaulize katika nyumba ya Yuda mtu aitwaye Sauli, wa Tarso; maana, angalia, anaomba;
[12]naye amemwona mtu, jina lake Anania, akiingia, na kumwekea mikono juu yake, apate kuona tena.
Unaweza kujiuliza kwanini apelekwe njia ile ..tena iitwe kwa jina la NYOFU na si lingine labda “njia kuu”, au “nzuri” au “panda” bali nyofu?
Ni kwasababu rohoni, Kristo huwaweka watu wake Katika hiyo njia. Njia iliyonyoka.
Hapo mwanzo Paulo alikuwa katika njia iliyoharibika, mbovu, ya kuupinga ukristo, ya uuaji, ya utukanaji, ya dhambi, ya mauti.
Lakini alipokutana na YESU, akatolewa huko akawekwa katika njia iliyonyooka ya utumishi wake.
Ni ajabu kuona watu wengi leo wanampinga Kristo, hawataki kuokoka, wakidhani udini ndio utawanyooshea mapito yao, fedha ndio zitawasawazishia mabonde Yao, elimu ndio zitaangusha milima yao.
Kumbe hawajui kuwa njia iliyonyooka ni maisha ndani ya Kristo tu!. Kwingine kote ni mabonde, milima Na mwishowe shimoni na mauti. Hakuna pumziko Nje ya Kristo.
Yohana mbatizaji aliliona hilo akapaza sauti yake kwa nguvu Akisema..
Yohana 1:23
[23]Akasema, Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, Inyosheni njia ya Bwana! Kama vile alivyonena nabii Isaya.
Kumwamini Yesu ndio kuinyoshe njia ya Bwana..
Je upo katika njia ya nyofu.
Okoka leo, uponywe kila kitu ndugu, kumbuka Umepotea nje ya Kristo,hakuna mjadala na huo ndio ukweli, hakuna tegemeo kama Yesu hajakuokoa. Fanya haraka utubu, leo uiamini kazi ya Kristo ya ukombozi iliyokamilishwa kwa ajili yako pale msalabani. Muda ni mchache mlango wa neema hautadumu Milele.
Ikiwa upo tayari leo kumkabidhi Yesu maisha yako. Basi bofya bofya hapa kwa mwongozo wa sala ya toba. >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Jehanamu ni nini?
MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 1)
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
Je unafahamu asili ya kanisa la Kristo? Ni vema wewe kama mwamini ufahamu mapito ya Imani yako.
Mpaka leo hii injili iliyotokea Yerusalemu (Israeli) kunifikia mimi na wewe, fahamu kuwa kuna mapito ambayo waliyapitia , ambayo na sisi tunapaswa tuyafahamu ili tuweze kuifikisha injili hiyo kila mahali, duniani kote na kwa vizazi vyote bila kuwa na deni.
Mwanzoni kabisa kanisa lilikuwa mahali pamoja pale Yerusalemu, Lakini dhiki ilipotokea na kuwa kubwa, mpaka watakatifu kuuliwa hadharani mfano Stefano, iliwagharimu wengi wa wakristo wakimbie Israeli na kwenda mbali kwenye mataifa mageni.
Lakini kuondoka kwao haikuwa mwisho wa safari, kwenda kuanza maisha mapya ya utulivu..hapana kinyume chake kule walipofika ugenini waliendelea kulihubiri lile Neno, kama tu vile walivyokuwa nyumbani.
Matendo ya Mitume 8:1,4
[1]Siku ile kukatukia adha kuu ya kanisa lililokuwa katika Yerusalemu; wote wakatawanyika katika nchi ya Uyahudi na Samaria, isipokuwa hao mitume… [4]Lakini wale waliotawanyika wakaenda huko na huko wakilihubiri neno.
[1]Siku ile kukatukia adha kuu ya kanisa lililokuwa katika Yerusalemu; wote wakatawanyika katika nchi ya Uyahudi na Samaria, isipokuwa hao mitume…
[4]Lakini wale waliotawanyika wakaenda huko na huko wakilihubiri neno.
Umeona asili ya kanisa la Kristo.. Ni sawa na leo, kuhama-hama kwa watu, pengine kwasababu za kikazi, kivita, kimasomo, kijamii n.k. unajikuta unaenda kijiji jirani, mkoa mwingine, au taifa lingine geni. Jiulize Je! Unalihubiri Neno kama kule nyumbani ulipokuwepo au ndio unabadilika tabia.
Kanisa la kwanza halikupoteza ubora mahali popote ugenini..Kwamfano utaona mtume Petro Aliendelea kuandika nyaraka zake kwa watakatifu waliotawanyika..mataifa mbalimbali, akijua kuwa injili ya Kristo inaendelea,
1 Petro 1:1
[1]Petro, mtume wa Yesu Kristo, kwa wateule wa Utawanyiko, wakaao hali ya ugeni katika Ponto, na Galatia, na Kapadokia, na Asia, na Bithinia;
Mazingira hayapaswi kuwa kizuizi cha ushuhudiaji wako, kwasababu kanisa halizuiwi na mazingira..Shuhudia Kristo popote ulipo kwasababu popote walipo watu, Mungu yupo hapo. Usipumbazwe na fikra za kusema mimi nilipo nashindwa kushuhudia afadhali kule nilipotoka, hii kazi mpya niliyoipata siwezi kuwashuhudia watu, ndugu hilo si wazo la Mungu. Fikiri Mungu akupe hekima, na hakika utaona upenyo.
Shalom.
Uinjilisti kama agizo kuu la Bwana.
INJILI YA KRISTO HAITANGAZWI KWA HATI MILIKI.
TUTAFUTE KWA BIDII KUKAA NDANI YA YESU.
Sauli, Sauli, mbona waniudhi?
Kuna mambo unaweza ukayafanya ukadhani ni sawa machoni pako. Lakini kumbe hujui kama unaleta huzuni kubwa kwa Kristo.
Mtume Paulo ambaye hapo mwanzo aliitwa Sauli, alikuwa akishindana na mawazo, na jamii ya watu waliomwabudu Mungu akidhani anashindana na ubaya kumbe anashindana na Kristo mwenyewe.
mpaka alipokutana na Kristo mwenyewe njiani alipokuwa anakwenda Dameski..akaambiwa maneno haya..Sauli, Sauli, mbona waniudhi?
Matendo 9:4-5
[4]Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona waniudhi? [5]Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe.
[4]Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona waniudhi?
[5]Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe.
Hilo Neno waniudhi, kwenye tafsiri ya asili linamaanisha hasaa “wanitesa”? Biblia ya kiingereza inaeleza vizuri zaidi inatumia neno “persecutest”…yaani kutesa..
Paulo alikuwa mfano wa wapagani waliomtesa Kristo, pale alipokuwa anawaburuta watakatifu, anawafunga, anawapinga, na kuwatukana…hakujua kuwa anamtesa Kristo mwenyewe..Leo hii makundi ya watu wanaowapinga watakatifu, wanaoyapinga makanisa ya kweli, wanaowatukana watumishi wa Mungu, wanaowapiga na kuwaua wafahamu kuwa wanamtesa Kristo.
Ikiwa wewe ni mmojawapo kuwa makini, uache mara moja, ni heri utubu leo umpe Yesu maisha yako. Akuokoe.
Lakini kundi la pili ni wale waamini- waliorudi nyuma. Mtu ambaye ameshaokoka, Halafu anaiacha Njia kwa makusudi anayafanya yale machafu aliyoyaacha nyuma huyo anamtesa Kristo, tena yale mateso ya msalabani kabisa.
Waebrania 6:4-8
[4]Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, [5]na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo, [6]wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri. [7]Maana nchi inayoinywa mvua inayoinyeshea mara kwa mara, na kuzaa mboga zenye manufaa kwa hao ambao kwa ajili yao yalimwa, hushiriki baraka zitokazo kwa Mungu; [8]bali ikitoa miiba na magugu hukataliwa na kuwa karibu na laana; ambayo mwisho wake ni kuteketezwa.
[4]Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu,
[5]na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo,
[6]wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.
[7]Maana nchi inayoinywa mvua inayoinyeshea mara kwa mara, na kuzaa mboga zenye manufaa kwa hao ambao kwa ajili yao yalimwa, hushiriki baraka zitokazo kwa Mungu;
[8]bali ikitoa miiba na magugu hukataliwa na kuwa karibu na laana; ambayo mwisho wake ni kuteketezwa.
Acha tabia ya kuzoelea dhambi, ukishaokoka ukitenda dhambi, haihesabiki kama kosa kama la wapagani bali uasi.
Kama Ulimpokea Kristo ili umtese, kuokoka kwako kuna maana gani? Ulishawahi ona mtoto anampiga Baba yake? Hiyo si laana?
Ndivyo ilivyo kwako unapozini na huku umeokoka, unapokunywa pombe na kufanya anasa.. Tubu haraka sana umrudie Kristo
Penda utakatifu, Ishi maisha matakatifu..
IFAHAMU HUZUNI NA FURAHA YA MALAIKA.
Kwanini Yeremia ailaani siku yake ya kuzaliwa? (Yeremia 20:14)
Nini maana ya Mithali 16:30 Afumbaye macho, kusudi lake ni kuwaza yaliyopotoka;
Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.
Kwa lugha rahisi kuna tofauti ya kuhubiri na kushuhudia.Yesu alituita tuwe mashahidi duniani.. Na hiyo ni kazi ya kila mmoja, Wito wa kumtangaza Yesu, sio wa kimahubiri, bali ni wa kiushuhudiaji.
Mhubiri ni mtu anayesimama na biblia, anayefundisha maandiko, anayefafanua, hadithi mbalimbali na mafunzo katika biblia kisha kutarajia watu kugeuka kwa mafundisho hayo. Huyu anaweza akawa mchungaji, mwinjilisti, mtume, Askofu, shemasi n..k
Lakini shahidi ni mtu aliyeona ukweli wa jambo Fulani, kisha akasimama kama mteteaji au mthibitishaji wa ukweli huo.Ndio kazi tuliyopewa sisi sote kufanya kuhusu Kristo, kuwa mashahidi wake ulimwenguni kote. Wa yale yote aliyotutendea sisi katika maisha yetu. Yaani yale aliyoyasema tukayathibitisha sisi wenyewe kuwa ni kweli katika maisha yetu.
Kwamfano pale aliposema njoni kwangu ninyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha (Mathayo 11:28). Ulipokwenda kwake ukaona mzigo huo umetuliwa, Hivyo tukio hilo huna budi kusimama na kulithibitisha kwa wengine, na wao pia waamini, ili watendewe jambo hilo hilo.
Pale Yesu aliposema tukiamini tukabatizwa, tutapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.(Matendo 2:38) Na wewe sasa umepokea Roho Mtakatifu, umejua ni ukweli, sasa hapo ndipo unapokwenda kuwashuhudia wengine ukweli huo.
Pale ulipoponywa, ulipofunguliwa, ulipoonyeshwa ishara, ulipopewa nguvu ya kushinda dhambi fulani.. Hapo ndipo unapopashuhudia..Na kwa kupitia ushuhuda huo, mwingine atajengwa Imani na kumwamini Yesu kama wewe ulivyoamini hatimaye kuokoka.
Sasa kazi hii haihitaji theolojia ya biblia, haihitaji ukomavu wa kiroho, haihitaji mifungo na maombi, inahitaji tu kufungua kinywa chako na kuanza kueleza uzuri ulioupata ndani ya Kristo, na kwa njia hiyo ndio Mungu atamshawishi mtu na kuokoka.
Ukiwa kama mkristo umeokoka labda tuseme leo, Kumbuka tayari una deni la kuanza kushuhudia uzuri wa Kristo kwa maneno hayo hayo machache uliyonayo kinywani mwako.. Ndicho alichokifanya Paulo baada tu ya kubatizwa..
Matendo 9:17 Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani; akamwekea mikono akisema, Ndugu Sauli, Bwana amenituma, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu.Mara vikaanguka machoni pake vitu kama magamba, akapata kuona, akasimama, akabatizwa;19 akala chakula, na kupata nguvu. Akawa huko siku kadha wa kadha pamoja na wanafunzi walioko Dameski.20 Mara akamhubiri Yesu katika masinagogi, kwamba yeye ni Mwana wa Mungu.21 Na wote waliosikia wakashangaa, wakasema, Siye huyu aliyewaharibu walioliitia Jina hili huko Yerusalemu? Na hapa alikuwa amekuja kwa kusudi hilo, awafunge na kuwapeleka kwa wakuu wa makuhani?22 Sauli akazidi kuwa hodari, akawatia fadhaa Wayahudi waliokaa Dameski, akithibitisha ya kuwa huyu ndiye Kristo.23 Hata siku nyingi zilipopita, Wayahudi wakafanya shauri ili wamwue.
Tatizo linatokea pale ambapo tunaona kazi ya injili ni ya watu maalumu na ni nzito . Hapana, kumbuka anayeshawishi watu mioyo ni Mungu, sio kwa wingi wa vifungu vya maandiko au kwa uzoefu wa kuhubiri, bali kwa Roho Mtakatifu tu. Maneno mawili, tu yenye kumshuhudia Yesu, yana nguvu ya kugeuza mtu zaidi hata ya maneno elfu ya vifungu vya biblia.
Unapokwenda kushuhudia usifikiri fikiri ni nini utasema, wewe anzia pale ambapo ulitendewa na Yesu ikawa sababu ya wewe kuokoka.. muhadhithie huyo mtu Habari hiyo kwa taratibu. Utashangaa tu, huko huko Katikati Mungu anakupa hekima na kinywa cha kumhubiria mpaka utashangaa hekima hiyo umeitolea wapi. Pengine mtu atakuuliza swali umsaidie, lile jibu linalokuja kwenye kinywa chako liseme, wala usijidharau au usiogope, anayemshawi mtu ni Mungu, yeye kuelewa au kutokuelewa hiyo sio kazi yako ni ya Mungu, uwe tu na ujasiri, kwasababu hakuna Habari yoyote yenye maudhui ya Kristo ndani yake haina matokeo.
Anza sasa kumshuhudia Yesu, Na kwa Pamoja tuujenge ufalme wa Kristo. Anza na marafiki zako, familia, wafanyakazi wenzako, majirani zako kabla ya Kwenda hata mwisho wa nchi.
Mungu akubariki
JINSI YA KUSIMAMA NA KUFUNDISHA/ KUHUBIRI
YESU KATIKA KUCHOKA KWAKE.
Enendeni ulimwenguni mwote
SWALI: nini maana ya Yohana 17:20
[20]Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao.
Ni akina nani hao ambao wataamini Kwasababu ya Neno lao, Bwana Yesu aliotaka kuwaombea?
JIBU: Sura hiyo ya 17 ni sura iliyoelezea kwa kina dua ambayo Bwana Yesu aliifanya kwa mitume wake kwa Baba.
Ambapo aliwaombea mambo kadha wa kadha ikiwemo walindwe katika umoja wa Roho, walindwe na yule mwovu, watakaswe na ile kweli.. Lakini pia Bwana Yesu hakuishia kuwaombea wao tu, bali na wengine ambao mitume wake watawahubiria injili na kuamini baadaye. Na hao pia maombi yake yalikuwa ni yaleyale kwao.
Maana yake ni kuwa watu wote walioamini kwa injili ya mitume walishiriki dua hiyo ya Kristo, Na hao si wengine zaidi ya wale watakatifu wa kanisa la kwanza, hadi sisi tuliopo sasa, hadi na wale watakaokuja baadaye.. sisi wote ni washirika wa dua ile (Yohana 17), kwasababu tumeamini katika injili moja ya mitume..
Ndio sababu kwanini maandiko yanasema Kristo anatuombea…maana yake ni kuwa sasa anatuombea kwa yule Roho Mtakatifu auguaye ndani yetu, lakini pia analituombea alipokuwa duniani ambapo sala hiyo tunaona matokeo yake hata sasa.
Waebrania 7:25
[25]Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.
Hii ni kututhibitishia Kuwa pale tunapomwamini Kristo upo ulinzi usioelezeka unawekwa juu yetu, kiasi kwamba malango ya adui hayawezi Kushinda..kinachohitajika ni kutii tu.
Warumi 8:34
[34]Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea.
Je na wewe ni mshirika wa sala hiyo ya Bwana? Kwa kumpokea Bwana Yesu? Kama ni la! Basi nafasi ni sasa mwamini Yesu upokee uzima wa milele.
Lakini pia Bwana anatufundisha namna sahihi ya kuomba..hatupaswi tu kuyaombea yale matunda tunaoyaona..bali hata na yale yatakayokuja baadaye..wale watakaokoka baadaye kwasababu ya Neno letu.
WOSIA WA BWANA YESU KWA WANAFUNZI WAKE.
MTAIFAHAMU KWELI NAYO HIYO KWELI ITAWAWEKA HURU.
“Akaiona imefagiwa na kupambwa” Maana yake nini (Luka 11:26).