Title mtakatifu ni

Jina la Bwana na Mwokozi wetu YESU KRISTO libarikiwe, karibu tujifunze maandiko.. Ipo tofauti kati ya “kufahamu jambo” na “kulijua jambo”.. Unaweza kulifahamu jambo lakini usilijue kwa undani, vivyo hivyo kuna tofauti ya “kuyafahamu maandiko” na “kuyajua maandiko”.  Hivi ni vitu viwili vyenye tofauti kubwa sana, hebu tujifunze kidogo kwa namna gani. Tusome habari ifuatayo kisha tufafanue.. Mathayo 22:23 “Siku ile Masadukayo, watu wasemao ya kwamba hakuna kiyama, wakamwendea, wakamwuliza, 24 wakisema, Mwalimu, Musa alisema, Mtu akifa, akiwa hana watoto, ndugu yake na amwoe yule mkewe, ili ampatie nduguye mzao. 25 Basi, kwetu kulikuwa na ndugu saba; wa kwanza akaoa, akafariki, na kwa kuwa hana mzao, akamwachia nduguye mke wake. 26 Vivyo hivyo wa pili naye, na wa tatu, hata wote saba. 27 Mwisho wa wote yule mwanamke akafa naye. 28 Basi, katika kiyama, atakuwa mke wa yupi katika wale saba? Maana wote walikuwa naye. 29 Yesu akajibu, akawaambia, MWAPOTEA, KWA KUWA HAMYAJUI MAANDIKO WALA UWEZA WA MUNGU. 30 Kwa maana katika kiyama hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika mbinguni”. Nataka tuzingatia hilo neno “MWAPOTEA, KWA KUWA HAMYAJUI MAANDIKO WALA UWEZA WA MUNGU”. Kumbuka hawa watu waliokuja kumwuliza Bwana hilo swali ni MASADUKAYO, ni watu wa dini, wanayoyafahamu maandiko karibia yote ya kwenye torati, na hapa wanamjia YESU kwa swali linalotoka katika maandiko ya MUSA (torati), wakisema “Mtu akifa basi mke wake anaruhusa ya kuolewa na ndugu wa karibu”.. jambo ambalo ni kweli kabisa lipo kwenye Biblia. Lakini pamoja na kwamba walikuwa wanayafahamu hayo maandiko, bado Bwana YESU anawaambia “Hawayajui maandiko” na tena wanapotea sana. “29 Yesu akajibu, akawaambia, MWAPOTEA, KWA KUWA HAMYAJUI MAANDIKO WALA UWEZA WA MUNGU. 30 Kwa maana katika kiyama hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika mbinguni”. Tuirudie tena habari hii katika Marko.. Marko 12:24 Yesu akajibu, akawaambia, JE! HAMPOTEI KWA SABABU HII, KWA KUWA HAMYAJUI MAANDIKO wala uweza wa Mungu? 25 Kwa maana watakapofufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika walioko mbinguni. 26 Na kwa habari ya wafu ya kwamba wafufuliwa, hamjasoma katika kitabu cha Musa, Sura ya Kijiti, jinsi Mungu alivyomwambia, akisema, Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo? 27 Yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai. Hivyo mwapotea sana”. Kumbe wakati ambao wanajidhania kuwa wanayajua maandiko kwa wingi wa mistari wanayoifahamu vichwani mwao, Kristo alikuwa anawaona hawajui chochote, na hiyo ndio sababu kuu ya kupotea kwao, hawayajui maandiko bali wanayafahamu tu. Ndugu hatupaswi kuwa kama compyuta au simu ambao inaweza kuwa na vitu vingi pamoja na biblia nzima, lakini haiyajui maandiko, na wala yale maandiko hayaisaidii kwa chochote. Hatupaswi kuwa na idadi kubwa ya mistari vichani ambayo haina ufunuo wowote. Mistari yenye nguvu na ibilisi anayoigopa ni ile iliyopo moyoni iliyobeba ufunuo, maana yake yenye uhai katika maisha ya mtu, na inayomwongoza, na yenye nguvu, na inayothibitisha imani. Masadukayo walikuwa wanafahamu tu Musa kasema, na kujitamba katika hayo, pasipo kujua kuwa andiko bila ufunuo ni bure.. Sasa swali ni je!, tutayajuaje maandiko badala ya kuyafahamu tu? Kinachotangulia ni kuyafahamu, ni lazima tuyafahamu na kufahamu kunakuja kwa kuyasoma au kuyasikia yanaposomwa.. baada ya kuyafahamu hatua inayofuata ni kuyajua. Na njia pekee ya kuyajua maandiko ni kwa kupitia Roho Mtakatifu.. Huyu peke yake ndiye anayeweza kutuhamisha kutoka katika kuyafahamu maandiko mpaka kuyajua, kwani anapoingia ndani ya Mtu, anakuwa ni Mwalimu mwingine wa ziada, kukufundisha maana za ndani ya maandiko uyasomayo, anakuchambulia na kukufundisha mambo ambayo hata ukirudia kusoma tena hilo andiko ulilolisoma utaona kama vile ni jingine kabisa, na huo ndio uhudumu wa agano jipya unaotajwa katika 2Wakorintho 3:6, ambao unatutosheleza. 2Wakorintho 3:6 “Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha”. Je tayari umempokea Roho Mtakatifu?.. kama bado mwamini YESU na tubu dhambi kwa kumaanisha kuziacha, kisha tafuta ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Bwana YESU KRISTO, baada ya hapo Roho Mtakatifu ataingia ndani yako na kukaa na wewe siku zote, kwani ahadi ya Roho Mtakatifu ni kwa kila mtu. Matendo 2:38 “Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie”. Bwana akubariki. Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii. Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10 Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312 Bwana akubariki. Mafundisho mengine: JE UNAZAA MATUNDA NA KUWAPONYA MATAIFA? Ipi tofauti ya “Majibu” ya Maombi na “Majaribu”. Ipi Tofauti ya Agano jipya na Agano la Kale?. TOFAUTI KATI MAASKOFU, MASHEMASI, WAZEE WA KANISA NI IPI? Nini tofauti kati ya kileo na divai ?

Roho Mtakatifu ni nani?.

Watu wengi wanajiuliza Roho Mtakatifu ni nani? Jibu  rahisi ni kuwa Roho Mtakatifu ni Roho ya Mungu, Mungu anayo Roho kama vile mwanadamu alivyo na roho, hakuna mwanadamu yeyote asiye na roho.

Na Biblia inasema katika Mwanzo 1:26 kwamba Mwanadamu aliumbwa kwa mfano na sura ya Mungu. Ikiwa na maana kuwa kama mwanadamu ana nafsi halikadhalika Mungu naye anayo nafsi, na kama mwanadamu anayo roho vilevile na Mungu naye anayo Roho. Kwasababu tumeumbwa kwa sura yake na kwa mfano wake. Na kama vile mwanadamu anao mwili halikadhalika Mungu naye anao mwili.

Na Mwili wa Mungu si mwingine zaidi ya ule uliodhihirishwa pale Kalvari miaka 2000 iliyopita. Nao ni mwili wa Bwana Yesu Kristo, hivyo Yesu Kristo ndiye Mungu mwenyewe aliyedhihirishwa katika Mwili. Hivyo aliyemwona Yesu amemwona Mungu (Yohana 14:8-10)

1Timotheo 3:16 “Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu”.

Huyo ni Yesu anayezungumziwa hapo.

Na kadhalika roho iliyokuwepo ndani ya Mwili wa Bwana Yesu Kristo ndio Roho ya Mungu na ndiye ROHO MTAKATIFU MWENYEWE. Tunalithibitisha hilo katika kitabu cha.

Matendo 16:6 “Wakapita katika nchi ya Frigia na Galatia, wakikatazwa na Roho Mtakatifu, wasilihubiri lile neno katika Asia.

7 Walipofika kukabili Misia wakajaribu kuenda Bithinia, lakini Roho wa Yesu hakuwapa ruhusa,

8 wakapita Misia wakatelemkia Troa”.

Sasa utauliza kama Roho wa Yesu ndiye Roho Mtakatifu iweje mahali pengine Bwana Yesu anaonekana amejaa Roho Mtakatifu?. Na mahali pengine anaonekana Roho Mtakatifu akishuka juu yake?

Jibu ni kwamba, Roho wa Mungu hana mipaka kama roho zetu sisi wanadamu zilivyo na mipaka, sisi wanadamu Mungu alivyotuumba roho zetu mipaka yake ni katika miili yetu.

Haziwezi kutenda kazi nje ya fahamu zetu au miili yetu.Haiwezekani niongee na wewe hapa na wakati huo huo roho yangu ipo China. Hilo haliwezekani kwetu sisi wanadamu, isipokuwa kwa Mungu linawezekana. Roho wake anauwezo wa kuwa kila mahali, ndio maana wewe uliopo Tanzania utasali muda huu na mwingine aliyepo China atasali na mwingine aliyeko Amerika atakuwa anamwabudu Mungu muda huo huo na wote Roho Mtakatifu akawasikia na kuwahudumia kila mtu kivyake. Huyo huyo anao uwezo wa kuwepo mbinguni, na duniani ndani ya Mwili wa Bwana Yesu na wakati huo huo kuzimu, hakuna mahali asipofika.

Ndio maana utaona alikuwa ndani ya Kristo, na bado akashuka juu ya Kristo, na akaachiliwa juu yetu siku ile ya Pentekoste.

Hiyo ndiyo tofauti ya Roho wa Mungu na roho ya mwanadamu. Roho zetu zina mipaka lakini Roho wa Yesu hana mipaka.

Na ni kwanini Roho wa Yesu anajulikana kama Roho Mtakatifu?

Ni kwasababu yeye ni Roho Takatifu, hiyo ndio sifa kubwa na ya kipekee Roho wa Yesu aliyoibeba..Yeye ni mtakatifu na hachangamani na uchafu.

Na ndio maana uthibitisho wa Kwanza kabisa wa Mtu aliyempokea Roho Mtakatifu ni kuwa Mtakatifu. Umepokea uwezo wa kufanyika mwana wa Mungu, unakuwa kama YESU. Naamini mpaka hapo utakuwa umeshafahamu Roho Mtakatifu ni nani?

Je! Umepokea moyoni mwako? kama bado ni kwanini? Biblia imesema ahadi hiyo ni ya bure na tunapewa bila malipo, kwa yeyote atakayemwamini.

Matendo 2:39 “Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie”.

Gharama za kumpata huyo Roho si fedha bali ni Uamuzi tu! Ukimtafuta Mungu kwa bidii utampata Neno lake linasema hivyo..

Hivyo kanuni rahisi sana ya kumpata ni KUTUBU kwanza: Yaani unamaanisha kuacha dhambi kwa vitendo, kisha kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji tele (Yohana 3:23) na kwa jina la Yesu kwaajili ya ondoleo la dhambi kulingana na Matendo 2:38 ili kuukamilisha wokovu wako. Na Roho Mtakatifu ataingia ndani yako, atakayekupa uwezo wa kuwa kama yeye alivyo yaani Mtakatifu. Vilevile atakushushia na karama zake za Roho kwa jinsi apendavyo yeye juu yako. Hapo ndipo utakapopokea uwezo wa kuwa shahidi wake

Kumbuka biblia inasema wote wasio na Roho Mtakatifu hao sio wake (Soma Warumi 8:9), Hivyo ni wajibu wetu sote kumtafuta Roho Mtakatifu kwa bidii sana. Kwasababu hutaweza kumjua Mungu, wala kupokea uwezo wa kuishinda dhambi kama huna Roho Mtakatifu ndani yako.

Bwana akubariki.

Maran Atha !jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

KWANINI YESU KRISTO ALIKUJA DUNIANI?

JE UNATAMANI KUMJUA MUNGU, NA HUJUI PA KUANZIA?

KWANINI YESU KRISTO NI MWANA WA DAUDI?

ROHO HUTUOMBEA KWA KUUGUA KUSIKOWEZA KUTAMKWA!

KAMA MUNGU ANABORESHA KAZI ZAKE, KWANINI WEWE USIBORESHE ZA KWAKO?.

Rudi Nyumbani:

Mtakatifu ni Nani?

 JIBU: Tafsiri ya kibiblia ya MTU MTAKATIFU ni tofauti na tafsiri ya kiulimwengu.
 
Ulimwengu unatafsiri Mtu mtakatifu ni mtu yeyote anayetenda matendo mema! mtu asiyetenda dhambi!..mtu anayekubalika na asiye na mawaa,
 
Lakini Biblia haitafsiri hivyo, kwasababu hakuna mwanadamu yeyote anayeweza kusimama mbele za Mungu kwa Matendo yake, na kujigamba mbele zake, wanadamu wote tunatenda dhambi kwa namna moja au nyingine aidha kwa kujua au kwa kutokujua. Na hivyo wakati unapojiona upo sawa, kumbe haupo sawa..wakati unajiona ni msafi kumbe ni mchafu n.k
 
Sasa Biblia inamtaja mmoja tu ambaye hakuwa na dhambi hata moja na huyo si mwingine zaidi ya YESU KRISTO peke yake! huyo ndiye biblia imemtaja kuwa mtakatifu, kwasababu alizaliwa bila dhambi na aliondoka duniani bila dhambi hata moja. Huyo peke yake ndiye anayeweza kusimama mbele za Mungu kwa matendo yake. Na ndiye pekee Mungu anayemwangalia kuwa ni Mtakatifu. Wengine wote tumetenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.
 
Warumi 3: 23 “kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;
24 wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu”
 
Sasa Kwa kupitia huyo sisi wengine tutakaomwamini yeye ndio tutahesabiwa kuwa ni watakatifu,. Kama mtu yeyote hatakuwa ndani ya YESU hawezi kuonekana mtakatifu mbele za Mungu, hata kama anajiona ni mkamilifu kiasi gani, hata kama atatenda matendo ya haki kiasi gani…mbele za Mungu ni kama Uchafu tu!
 
Yesu ni kama vazi letu la nje sisi tulio wachafu! Ukimvaa Yesu mbele za Mungu hakuoni wewe, bali anamwona Yesu mwanawe ambaye ni Mtakatifu, hivyo na wewe unaonekana mtakatifu kwa ajili yake. Hiyo ndio maana ya NEEMA, Tunahesabiwa HAKI (yaani tunahesabiwa kuwa watakatifu) bure kwa njia tu ya kumwamini YESU KRISTO. Hapo ndipo mtu unaouna umuhimu wa YESU kuja duniani, Kwahiyo watakatifu ni wale walio ndani ya YESU tu!.
 
Hivyo wale wanaosema duniani hakuna watakatifu, ni kweli kwa mtazamo wa kibinadamu, lakini kwa mtazamo wa Mungu duniani wapo watakatifu maandiko yanatumabia hivyo katika:
 
Zaburi 16:3 “Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao”.
 
Na hawa ndio wale wale wote walio ndani ya YESU KRISTO.
Sasa utauliza! Ina maana tukiwa ndani ya Yesu hata kama tukitenda dhambi za makusudi, tutazidi kuonekana NI watakatifu mbele za Mungu? jibu ni la! hakuna mtu yeyote aliye ndani ya Kristo, akawaza tena kutenda dhambi za makusudi, hakuna mtu aliye ndani ya Kristo akafanya uasherati, au akalawiti au akaua..ukiona mtu anatenda dhambi za Makusudi huyo bado hajawa ndani ya YESU, bado ni wa Ulimwengu. (Soma 1Yohana 3:9 na Warumi 6:1-2 )..
 
Kwasababu mtu yeyote aliyempokea YESU huwa anapokea hapo hapo kipawa cha Roho Mtakatifu, ambaye huyo kazi yake ni kumwongoza, kumfundisha na kumpasha habari ya mambo yote..kwahiyo mtu wa namna hiyo moja kwa moja atajikuta anatamani kupiga hatua mbele kila siku kuelekea ukamilifu na sio nyuma…Hata ile tamaa ya kufanya dhambi huwa inakufa yenyewe ndani yake, na hivyo hawezi kutenda dhambi mwenyewe za makusudi.
 
Ubarikiwe.

Mada Nyinginezo:

JEHANAMU NI NINI?

MANENO YA MUNGU YANAPINDULIWAJE?

ROHO I RADHI, LAKINI MWILI NI DHAIFU.

USITAFUTE FAIDA YAKO MWENYEWE BALI YA WENGINE.

NJAA ILIYOPO SASA.

JIKANE NAFSI MTEULE WA MUNGU.

Rudi Nyumbani:

SWALI : Dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu ni ipi?

JIBU: Tukisoma;

Mathayo 12:25-32 ” Lakini Mafarisayo waliposikia, walisema, Huyu hatoi pepo, ila kwa Beelzebuli mkuu wa pepo.

25 Basi Yesu akijua mawazo yao, akawaambia, Kila ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, hufanyika ukiwa; tena mji au nyumba yo yote ikifitinika juu ya nafsi yake, haitasimama.

26 Na Shetani akimtoa Shetani, amefitinika juu ya nafsi yake; basi ufalme wake utasimamaje?

27 Na mimi nikitoa pepo kwa Beelzebuli, je! Wana wenu huwatoa kwa nani? Kwa sababu hiyo hao ndio watakaowahukumu.

28 Lakini mimi nikitoa pepo kwa Roho wa Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia.

29 Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Ndipo atakapoiteka nyumba yake.

30 Mtu asiye pamoja nami yu kinyume changu; na mtu asiyekusanya pamoja nami hutapanya.

31 Kwa sababu hiyo nawaambia, KILA DHAMBI, NA KILA NENO LA KUFURU, watasamehewa wanadamu, ILA KWA KUMKUFURU ROHO HAWATASAMEHEWA.

32 Naye mtu ye yote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao. “

Tunavyosoma mistari hiyo tunaona kabisa wale Mafarisayo walikuwa wanajua Bwana Yesu ni kweli alikuwa anatoa pepo, na kutenda mambo yote kwa uweza wa Roho wa Mungu, lakini wao kwa ajili ya wivu, na kwa tamaa zao wenyewe, ili tu wawavutie watu kwao, wakakusudia kwa makusudi kabisa, wawageuze watu mioyo ili watu wasimuamini Bwana Yesu,wawaamini wao, na ndipo wakaanza kutoa maneno ya makufuru wanawaambia watu kuwa BWANA anatoa pepo kwa uwezo wa belzebuli mkuu wa Pepo angali ndani ya mioyo yao walikuwa wanajua kabisa anachofanya ni kwa uweza wa Roho wa Mungu.

Ukweli wa jambo hilo unajidhihirisha kwa Nikodemo ambaye naye alikuwa ni mmoja wa wale mafarisayo alipomwendea Yesu usiku na kumwambia

Yohana 3:1-2″Basi palikuwa na mtu mmoja wa Mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi.

2 Huyo alimjia usiku, akamwambia, RABI, “TWAJUA” YA KUWA U MWALIMU, UMETOKA KWA MUNGU; KWA MAANA HAKUNA MTU AWEZAYE KUZIFANYA ISHARA HIZI UZIFANYAZO WEWE, ISIPOKUWA MUNGU YU PAMOJA NAYE. “

kwahiyo unaona walikuwa wanajua kabisa lakini kwa ajili ya wivu wakaanza kuzusha maneno ya uongo juu ya kazi ya Roho wa Mungu, sasa huko ndiko kumkufuru Roho Mtakatifu. hivyo basi Bwana Yesu alitoa angalizo tunapozitazama kazi za Mungu, pale mtu mwenye Roho wa Mungu anatenda kazi za Mungu kweli huku tunajua ni Mungu ndiye anayefanya kazi ndani yake, na kuanza kusema yule ni mchawi, au anatumia uchawi, au mshirikina, au tapeli, au mwizi, ili tu watu wasiziamini kazi za Mungu au vinginevyo, au unaanza kuzusha propaganda za uongo juu yake, pengine kwa kusudi la kumkomoa! hapo ndugu utakuwa unajimaliza mwenyewe. (Ni kweli si watumishi wote ni wa Mungu, hao ni sawa kuufunua uovu wao). Lakini Hapa tunamzungumzia yule unayemfahamu kabisa ni mtumishi wa BWANA,..wewe hujui umewakosesha wangapi, ambao kwa kupitia yeye, watu wengi wangeokolewa? kufanya hivyo ni hatari sana tuwe makini.

Hivyo hii dhambi inawahusu wale wanaozipinga kazi za Mungu kwa makusudi kabisa (Mfano wa mafarisayo). Hao kwao hakuna msamaha, hawawezi tena kutubu hata iweje wanachongojea ni ziwa la moto.

Lakini shetani naye anapenda kulitumia hili neno kuwafunga watu wajione kuwa wamemkufuru Roho Mtakatifu na kwamba dhambi zao hazisameheki hata wafanyeje,
Hii inakuja sana sana kwa watu waliowachanga ki-imani, kuna shuhuda nyingi za watu waliofungwa na shetani kwa namna hiyo wakidhani kuwa dhambi zao hazisameheki, kuna watu wamekata tamaa wanajiona kwa wingi wa dhambi zao, Mungu hawezi kuwasemehe tena, pengine wameua, wametoa mimba sana, n.k, Sasa jambo la namna hii likija katika mawazo yako likatae linatoka kwa yule mwovu kukufanya wewe ujione kuwa Mungu hawezi kukusamehe umemkufuru, hivyo usijisumbue kutubu kwasababu Mungu hatakusikiliza.

Kumbuka kama tulivyosema Dhambi hii inakaa kwa wale watu ambao ndani yao mioyo ya toba imekufa, au hofu ya Mungu haipo tena kwao, watu waliojikinai, wanaompinga Mungu katika fikra zao japo kuwa walimjua Mungu na uweza wake wote, wanazipotosha kazi za Mungu kwa makusudi kwa faida zao wenyewe, ili wawavute watu kwao, au wawe washirika wao na sio kwa Mungu. Hivyo basi kitendo tu cha wewe kuwa na hii hofu ya kumwogopa Mungu ujue Roho wa Mungu anatenda kazi ndani yako na hayo mawazo ya kwamba umemkufuru Roho Mtakatifu yapinge huyo ni adui ndio moja ya njia zake hizo ili usiufikie wokovu na anapenda kuwatesa watu wengi katika andiko hili.

Ubarikiwe sana.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada zinazoendana:

DHAMBI YA MAUTI

DHAMBI ILIYOMKOSESHA SHETANI.

DHAMBI ZINAZOTANGULIA NA ZINAZOFUATA.

DHAMBI ISIYO NA MSAMAHA.

Rudi Nyumbani:

Mtakatifu wa Israeli ni nani?

Swali: Mtakatifu wa Israeli anayetajwa katika Isaya 30:9-12 ni nani hasa? Na anakomeshwaje?

Jibu: Turejee..

Isaya 30:9 “Kwa maana watu hawa ni watu waasi, watoto wasemao uongo, watoto wasiotaka kuisikia sheria ya Bwana;

10 wawaambiao waonaji, Msione; na manabii, Msitoe unabii wa mambo ya haki, tuambieni maneno laini, hubirini maneno yadanganyayo;

11 tokeni katika njia, geukeni mtoke katika mapito; MKOMESHENI MTAKATIFU WA ISRAELI MBELE YETU”.

“Mtakatifu wa Israeli” anayezungumziwa katika maandiko hayo na mengine mengi, si mwingine zaidi ya MUNGU MWENYEZI, ALIYEUMBA MBINGU NA NCHI, Huyo ndiye aliye Mtakatifu ambaye alifanya Agano na Israeli, Tunalithibitisha hilo zaidi katika maandiko yafuatayo..

Sasa tukirejea hayo maandiko hapo anaposema “…MKOMESHENI MTAKATIFU WA ISRAELI MBELE YETU”.. kukomesha kunakozungumziwa hapo sio “kule kutoa adhabu” tunakokuelewa, bali ni kitendo cha “Kuzuia jambo lisiendelee kufanyika(kufikisha jambo kikomo)”.. Hivyo andiko hilo lilihusu watu waasi ambao hawapendi sheria za MUNGU, na hivyo wanataka kuambiwa tu maneno laini na manabii, maneno ya faraja si ya kukemewa makosa yao, na lengo la kutaka kusikia hivyo ni ili WAKOME (Yaani wasiendelee) kumwangalia MUNGU, na MUNGU pia aache kuwaangalia.

Kwahiyo Mtakatifu wa Israeli ni MUNGU MWENYEZI, na ndiye pekee anayestahili kuabudiwa na kutukuzwa, na mtu anayejitenga naye ni kwa hasara yake mwenyewe.

Isaya 48: 17 “Bwana, mkombozi wako, MTAKATIFU WA ISRAELI, asema hivi; Mimi ni Bwana, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata”.

Mistari mingine inayomtaja Mungu kama Mtakatifu wa Israeli ni pamoja na Isaya 12:6, Isaya 47:4, Isaya 17:7, Isaya 30:12,  Isaya 47:4, Isaya 48:2 na mingine mingi..

Je umemwamini YESU?.. Fahamu ya kuwa hakuna njia nyingine yoyote ya kumfikia MUNGU isipokuwa kwa kupitia yeye.

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

VILIO VINAVYOUFIKIA MOYO WANGU.

MWONGOZO WA MAOMBI YA WAHUDUMU/ WASIMAMAO MADHABAHUNI.

PALE MAOMBI YANAPOGEUKA KUWA MAPAMBANO.

HAKUNA MTU ANIONDOLEAYE, BALI MIMI NAUTOA MWENYEWE

HATARI YA KUTOKUITAFAKARI BIBLIA VIZURI?

Kwanini Roho Mtakatifu amzuie Paulo kuipeleka injili Asia? (Matendo 16:6-7).

Jibu: Turejee Matendo

Matendo 16:6 “Wakapita katika nchi ya Frigia na Galatia, WAKIKATAZWA NA ROHO MTAKATIFU, WASILIHUBIRI LILE NENO KATIKA ASIA.

7 Walipofika kukabili Misia wakajaribu kuenda Bithinia, lakini Roho wa Yesu hakuwapa ruhusa,

8 wakapita Misia wakatelemkia Troa”.

Biblia haijataja sababu za moja kwa moja kwanini Roho Mtakatifu awazuie wasiingie Asia kuhubiri injili lakini zifuatazo zinaweza kuwa sababu za Roho Mtakatifu kuwazuia Paulo na wenzake wasiingie hiyo miji kuhubiri injili.

   1. WAKATI WA INJILI KWA HIYO MIJI ULIKUWA HAUJAFIKA.

Kila mahali pana wakati wake wa kuhubiri injili kulingana na mapenzi ya Mungu, kwamfano kuna wakati ambao injili ilikuwa haijaruhusiwa kuhubiriwa kwa watu wa mataifa isipokuwa wayahudi tu peke yao, na kipindi hiko ni kile ambacho Bwana YESU alikuwa yupo bado duniani.

Mathayo 10:5 “Hao Thenashara Yesu aliwatuma, akawaagiza, akisema, Katika njia ya Mataifa msiende, wala katika mji wo wote wa Wasamaria msiingie.

6 Afadhali shikeni njia kuwaendea kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.

7 Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia”.

Maneno hayo ya Bwana Yesu yanaonyesha kuwa wakati wa injili kwa watu wa mataifa ulikuwa haujafika, lakini haikumaanisha kuwa Mataifa hawakuwa katika mpango wa Mungu wa kupokea Injili, walikuwepo lakini muda wao ulikuwa bado haujafika.

Na hapa katika Asia ni hivyo hivyo, huwenda muda wao wa kufikishiwa injili ulikuwa bado.

    2. WATUMISHI WENGINE WALIKUWEPO WAKIHUBIRI INJILI.

Kama muda wao wa kupokea Injili ulikuwa umefika na bado Roho Mtakatifu akawazuia akina Paulo kufika miji hiyo, sababu nyingine ni kwamba labda walikuwepo watumishi wengine wakihubiri katika hiyo miji, hivyo hakukuwa na haja ya akina Paulo kwenda huko tena wasije wakajenga juu ya msingi wa wengine kama Neno la Mungu linavyosema katika Warumi 15:20.

Warumi 15:20 “kadhalika nikijitahidi kuihubiri Injili, nisihubiri hapo ambapo jina la Kristo limekwisha kutajwa, nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine”

    3. WATUMISHI WENGINE WAMEKUSUDIWA KWENDA KUHUBIRI KATIKA HIYO MIJI.

Na kama hakukuwa na watumishi wengine waliokuwa wanahubiri katika miji hiyo, basi sababu nyingine ya Roho Mtakatifu kumzuia Paulo na wenzake kufika huko Asia huwenda ni kwasababu Roho Mtakatifu alikuwa amepanga/kusudia watumishi wengine ndio wakahubiri kwenye hiyo miji mbali na Paulo na wenzake.

Kikawaida Roho Mtakatifu ndiye anayepanga watu na mahali watakapokwenda..Paulo asingeweza kwenda miji yote peke yake, ni wazi kuwa ipo miji mingine ilikusudiwa kupelekewa injili na watumishi wengine/mitume.

    4. WALIIKATAA INJILI.

Hii yaweza kuwa sababu ya mwisho ya Roho Mtakatifu kuzuia injili isiingie Asia kupitia Paulo na wenzake… Inawezekana Roho Mtakatifu alishatanguliza watu huko waliohubiri Neno la Mungu lakini wakaikataa ile injili.. na matokeo yake ni kufungiwa dhambi sawasawa na  Yohana 20:22-23..

Yohana 20:22 “Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu.

23 Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wo wote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa”.

Kufungiwa dhambi kunakuja pale ambapo Neno la Mungu linahubiriwa kwa watu na wale watu wanalikataa kwa makusudi na hata kuwaua au kuwafukuza watumishi wa MUNGU, inapotokea wale watumishi wanakung’uta mavumbi kwenye miguu yao na kuondoka hapo wanakuwa wameufungia dhambi ule mji au mtaa, matokeo yake ni kwamba Roho Mtakatifu hawezi tena kupeleka wahubiri hapo mahali, wale watu watabaki vile vile kwasababu walishamkataa Roho Mtakatifu.

Mathayo 10:14 “Na mtu asipowakaribisha wala kuyasikiliza maneno yenu, mtokapo katika nyumba ile, au mji ule, KUNG’UTENI MAVUMBI YA MIGUUNI MWENU.

15 Amin, nawaambia, itakuwa rahisi nchi ya Sodoma na Gomora kustahimili adhabu ya siku ya hukumu, kuliko mji ule”.

Tunachoweza kujifunza ni kuwa Injili sio kitu kinachoweza kupatikana kila wakati, upo wakati ambapo Neema ikishaondoka mahali hairudi, au hata ikirudi yaweza kuchukua muda sana, hivyo hatuna budi kuiheshimu sana Neema ya Mungu.

Maran atha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Je Paulo, alihimiza kusikiliza nyimbo za kidunia kulingana na Matendo 17:28

Paulo aliwapaje watu karama ya rohoni?

Je ni sawa kuukubali udhaifu kama mtume Paulo alivyojisifia kwa huo? (2Wakorintho 12:9-10)

Kwanini Paulo, alihukumu wakati hukumu hairuhusiwi?

Paulo alikuwa anamaanisha nini kusema “Mnatenda vema kuvumiliana naye” (2Wakorintho 11:4).

Ni mji gani mtakatifu shetani aliomchukua Bwana YESU? (Mathayo 4:5)

Je huu mji mtakatifu shetani aliomchukua Bwana katika Mathayo 4:5 ni mji gani?.. maana tunajua shetani hawezi kumiliki vitu vitakatifu?

Jibu: Turejee..

Mathayo 4:5 “Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu.
6 akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.

7 Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako”.

Mji Mtakatifu unaozungumziwa hapo ambao shetani alimpeleka Bwana YESU ni YERUSALEMU (Ya duniani) iliyopo pale Israeli..

Kumbuka ipo YERUSALEMU YA MBINGUNI, ambayo itakuja kushuka baada ya hukumu ya mwisho, na Yerusalemu hiyo Mpya shetani hawezi kufika wala watu ambao hawajamwamini Bwana hawataingia (kulingana na maandiko).

Ufunuo 21:1 “Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.

2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.

3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao”.

Ruka mpaka mstari wa 23-27..

“23 Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-Kondoo.

24 Na mataifa watatembea katika nuru yake. Na wafalme wa nchi huleta utukufu wao ndani yake.

25 Na milango yake haitafungwa kamwe mchana; kwa maana humo hamna usiku.

26 Nao wataleta utukufu na heshima ya mataifa ndani yake.

27 Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo”.

Lakini Mji shetani aliompeleka Bwana ulikuwa ni Yerusalemu ya duniani, (ule mji ule wa Daudi), mahali pale ambapo Hekalu la Sulemani lilijengwa..Yerusalemu hii ya duniani shetani anaweza kufika wakati wowote na mtu mwingine yoyote anaweza kufika, (awe mtakatifu au asiwe mtakatifu), anaweza kufika, na hata leo watu wanafika pale..

Na shetani alimpomfikisha Bwana YESU katika Hekalu, alimpandisha mpaka kwenye kinara chake, na kumwambia ajirushe chini, kwa maana imeandikwa atawaagiza malaika nao watamwokoa na ajali ile (sawasawa na Zaburi 91:11-12).

Lakini Kwakuwa Bwana YESU alikuwa amejaa Roho Mtakatifu, alizijuza hila na mbinu zote za ibilisi, na aliweza kumjibu kwa Neno, kuwa imeandikwa tusimjaribu Bwana MUNGU wetu.

Ni jambo gani tunaweza kujifunza hapo?

shetani anapotaka kumjaribu mtu anayemcha MUNGU hampeleki kwa waganga wa kienyeji, wala hampeleki kwenye mazingira ya dhambi ili atende dhambi, bali anampeleka sehemu takatifu, kama kanisani, au katikati ya watu wanaomtafuta MUNGU,
Ndio maana utaona leo mtu amesimama lakini anaanguka/anaangushwa katika dhambi na mtu/watu wa kanisani.

Utaona Askofu, au mchungaji, au mwinjilisti, au Nabii, au Mtume au mwimbaji wa kwaya anaanguka katika uzinzi na watu wa kanisani, ni mara chache sana na watu wa nje, kwanini?.
Kwasababu shetani anajua sehemu pekee ya kumjaribu mtu aliyeokoka na kusimama ni kanisani, akimletea wanaojiuza huko barabarani ni ngumu kuanguka..

Ndicho alichotaka kujaribu kufanya kwa Bwana YESU kumpeleka Hekaluni, kwanini asingempekeka kwenye vinara vingine vya mahali pengine, badala yake akachagua Hekalu?.. ni kwasababu alijua hapo ni rahisi kumwangusha Bwana.

Hivyo na sisi tuliookoka ni muhimu kuwa makini katika nyumba ya MUNGU kwani huko huko shetani anaweza kupata nafasi.

Bwana atusaidie.
Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 2)

MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 3)

MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 1)

Je! Yesu aliwezaje kuchukuliwa na shetani juu ya kinara cha hekalu kujaribiwa?