Je! ni sahihi kuning’iniza picha nyumbani mwako kama ya Yesu?

Je! ni sahihi kuning’iniza picha nyumbani mwako kama ya Yesu?

Swali linaendelea…maana imeandikwa kutoka 20:4 “Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. “

Sasa naomba kufahamu kufanya hivyo ni makosa?


JIBU: kwa kulijibu hili swali tumalizie kusoma mstari huo..

Kutoka 20:4-5″ Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,”…

Sasa tunaona katika huo mstari wa tano msisitizo umewekwa pale katika neno “USIVISUJUDIE WALA KUVITUMIKIA”, lakini sio kwamba ukiweka picha yoyote kama ya Yesu nyumbani mwako ni vibaya hapana! unaweza kuweka picha yoyote upendayo ilimradi iwe ni njema,

Maana tukisema tusiweke picha yoyote basi hata tunaponing’iniza picha zetu wenyewe ukutani majumbani mwetu tunafanya vibaya kwasababu maandiko yanasema usijifanyie mfano wa kitu chochote sio tu kilicho juu mbinguni bali hata kilichopo chini duniani.

Unaona hapo msisitizo ni kwamba unapoweka picha yoyote au sanamu yoyote hupaswi kuiabudu wala kuisujudia kwa kufanya hivyo ni machukizo makubwa mbele za Mungu. Lakini leo hii kuna baadhi ya watu,na dini na madhehebu yanaabudu sanamu za Yesu na bikira Mariamu au watakatifu waliokufa zamani za kale hao ni dhahiri kuwa wanamwabudu shetani aidha kwa kujua au kwa kutokujua.

Ikiwa wewe ni mkatoliki na unayo sanamu ya Yesu au sanamu ya bikira Maria nyumbani mwako, nashauri iondoe haraka sana, kwasababu dini hiyo inahusisha ibada zao na sanamu, vinginevyo utamtia Mungu wivu na kujikuta umeenda Jehanamu.

Lakini kama picha ipo kwa ajili ya urembo au kwa ajili ya kufikisha tu ujumbe fulani katika mazingira yanayokuzunguka au nyumbani kwako, wala husujudii wala kuabudu basi hakuna shida yoyote. Zingatia tu hilo neno ”USIVISUJUDIE WALA KUVITUMIKIA’ kwasababu yeye ni Mungu mwenye wivu.

Biblia inasema;

1 Wakorintho 10:14

[14]Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu.
[15]Nasema kama na watu wenye akili; lifikirini ninyi ninenalo.

Ubarikiwe sana.

 
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada nyinginezo

Bwana aliposema kuwa yeye ni “Mungu wa miungu” alikuwa na maana gani?..je! yeye ni Mungu wa sanamu?

Hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge.(Ufu 21:27)

LITANIA YA BIKIRA MARIA JE! NI SALA YA KIMAANDIKO?

KUFUKIZA UVUMBA NDIO KUFANYAJE?

 


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
1 year ago

AMEN