SWALI; Naomba kuuliza katika ufunuo 21:27 kwamba hakitaingia kilicho kinyonge hili neno kinyonge linamaanisha nini? Je ni watu dhaifu mfano vilema?
Ufunuo wa Yohana 21:27 [27]Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.
JIBU: “Kinyonge” kinachozungumziwa hapo si mtu mlemavu, kama ingekuwa hivyo Bwana Yesu asingesema..kiungo chako kimoja kikikukosea king’oe ni heri uingie mbinguni mlemavu kuliko kuwa viungo vyako vyote na kuishia kuzimu.(Mathayo 5:29-30)
Lakini kinyonge kinachozungumziwa hapo ni kipi?
Kitu kinyonge sikuzote ni kitu kisichokuwa na nguvu ya kustahimili mtikisiko fulani aidha mapigano,ugonjwa,Dhoruba, mateso n.k.
Vivyo hivyo katika roho mtu asiyekuwa na nguvu ya kuushinda ulimwengu huyo ni sawa na mnyonge. Na ndio maana Bwana Yesu alisema maneno haya..
Mathayo 11:12[12]Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.
Utajiuliza ni kwanini Bwana arejee siku za Yohana mbatizaji, na sio siku za labda, Isaya, au Musa, au Samweli? Bali Yohana Mbatizaji?
Alisema hivyo, ili kutupa picha na sisi tunapaswa tuishi Maisha ya kuukana ulimwengu, mfano wa Yohana mbatizaji..Ambaye biblia inasema Maisha yake yote, aliishi majangwani mbali na ulimwengu, na matokeo yake akawa akiongezeka nguvu rohoni kila siku (Luka 1:80).
Hivyo na sisi tunapaswa tuushinde ulimwengu, ili tuweza kuuteka ufalme wa Mungu, ikiwa uzinzi utatushinda, ikiwa anasa na tamaa za ujanani zitatushinda, basi sisi ni wanyonge, na hivyo, kamwe hatutakaa tuuingie ule mji mpya wa Yerusalemu, utakaoshuka kutoka mbinguni. Kwasababu watakaoingia kule ni watakatifu tu walioushinda ulimwengu, na si vinginevyo.
Huu si wakati wa kuikumbatia dhambi..na kusema kwamba mimi siwezi kuushinda ulimwengu, ni wajibu wako kushindana mpaka ushinde…hupaswi kuwa mnyonge. Kumbuka wewe ukishindwa haimaanishi kuwa mwingine kashindwa.
Lakini tutawezaje kufikia hapo?
Tutafika kwa njia moja tu nayo ni kwa kumaanisha kabisa kuacha dhambi, na kujitwika misalaba yetu na kumfuata Yesu kwa gharama zozote zile.
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
MAANA WEWE, BWANA HUKUWAACHA WAKUTAFUTAO”.
KWANINI MIMI?
Je aliyezungumza na Musa kule jangwani ni Mungu mwenyewe au malaika wake?
Kama tunaokolewa kwa neema kwanini wokovu tuupate kwa nguvu?
Rudi nyumbani
Print this post
UBARIKIWE
Amen nawe pia..
Mbarikiwe sana Watumishi wa Mungu kwa mafundisho mazuri ya kiimani hakika tuko pamoja kulitukuza jina la Kristo
Amen utukufu kwa Bwana..
Barikiwa Sana Mtumishi MUNGU akuinue zaidii… Tumebarikiwa Sana kwa ujumbe mzuri
Amen..uzidi kubarikiwa..Tafadhali share na rafiki zako whatsapp na facebook