MAANA WEWE, BWANA HUKUWAACHA WAKUTAFUTAO”.

MAANA WEWE, BWANA HUKUWAACHA WAKUTAFUTAO”.

Zaburi 9:10 “Nao wakujuao jina lako wakutumaini Wewe, Maana Wewe, Bwana hukuwaacha wakutafutao”.

Shalom, tuzidi kujikumbusha kuwa..

Mungu anapenda sana watu wanaomtafuta, anapenda watu wanaoonyesha Nia ya dhati katika kumjua yeye, Mtu anayemtafuta Mungu kamwe Mungu hawezi kumuacha. Atakuwa naye bega kwa bega tu, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu, kwasababu ni ahadi yake kuwa hawaachi wamtafutao.

Mungu si kama sisi wanadamu, sisi ni rahisi kumuacha mtu mwenzetu ghafla tu, hususani pale tunapoona hana msaada wowote kwetu, au katuudhi kwa mara moja, lakini kwa Mungu hilo halipo, haangalii ulimuudhi mara ngapi huko nyuma, wala haangalii madhaifu yako, haangalii uchanga wako, au ujuaji wako, hivyo vyote sio vinavyomshawishi, hivyo hilo hata usilifikirie unapokusudia kumgeukia yeye, ikiwa leo hii utageuka na kusema naanza tena upya na Baba..Saa hiyo hiyo na yeye anaonyesha nia ya kuanza kupiga hatua na wewe,kama kwamba hakuna chochote kibaya ulichowahi kumtendea huko nyuma.

Shetani atakuambia Mungu hawezi kukusikia mtu kama wewe, atajifunuaje kwako, kumbuka dhambi ile uliyofanya zamani, au dhambi hii unayotenda sasahivi unadhani atakusamehe? Ukiona hivyo yapinge hayo mawazo anafanya hivyo ili kukuvunja tu moyo usiendelee au usiwaze kumtafuta Mungu..Lakini ahadi ya Mungu ni ile ile kuwa kamwe hawaachi hao wamtafutao.

Yohana 6:37 “Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe”.

Unaona? Mungu hawezi kuwaacha wale wote wanaomwendea yeye, hilo wazo halijawahi kuingia ndani yake, yaani kile kitendo tu cha kuamua na kusema namfuata Yesu, ujue ni tayari umeshapokelewa bila masharti yoyote, ni mlango ambao upo wazi wakati wote,kwa mtu yeyote haijalishi dini yake wala dhehebu lake, yaani ni jambo ambalo halina maswali maswali, au mashaka mashaka, ukimtafuta utajifunua kwako tu.

Sauti ya shetani inawadanganya wengi na kuwaambia, Mungu hawezi kujishughulisha na watu kama wao, bado huwajakidhi vigezo vya kusikiwa na Mungu, hawana upako wowote, wao ni takataka tu machoni pake, Ndugu hiyo sauti ikikuambia hivyo ijibu uiambie, ingekuwa mimi sina thamani yoyote machoni pake basi asingeniumba, lakini kama ameona vema kuniumba mimi mpaka nikawa hivi nilivyo mwanadamu kamili mwenye mfano wake na sura yake, na hakuniumba mende, au panya, au kononono basi mimi ni wa thamani nyingi machoni pake..

Hivyo ukishajipa moyo kwa namna hiyo halafu ukaanza kuutafuta uso wa Mungu wako, yeye mwenye atajifunua kwako, ni lazima afanye hivyo kwasababu anasema kamwe hawaachi wamtafutao, Mungu anafungwa na Neno lake, akisema hivi, amesema ni lazima atimize, sio kama sisi tulivyo.

Hivyo hatua ya kwanza kabisa inayothibitisha kuwa unamtafuta Mungu, ni kwa kutubu kwanza dhambi zako, kwa kumaanisha kabisa kuziacha, na pili kuwa tayari kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi wa kimaandiko wa kuzamishwa kwenye maji mengi na kwa jina la Bwana Yesu Kristo (Matendo 2:38) kama hukuwahi kubatizwa hapo kabla, na tatu ni kuanza kuzingatia kujifunza Neno la Mungu, na kuishi maisha yampendezayo Mungu na kufanya ushirika na kusali..

Ukizingatia hayo, nakutakia kila la heri katika kukutana na Mungu siku baada ya siku katika maisha yako yote hapa duniani, Kwasababu Bwana ni Mungu ambaye kamwe hawaachi wamtafutao.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

 Nini maana ya “Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati”

Nyamafu ni nini?

JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?

NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE.

Ni vitu vipi hivyo viwili visivyoweza kubadilika? (Ebr 6:18)

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
2 years ago

Amen