Sehemu ya tatu:
Jina kuu la Bwana wetu YESU KRISTO litukuzwe. Karibu katika mwendelezo wa uchambuzi wa kitabu cha Ufunuo, Leo tukimalizia sehemu ya mwisho ya sura hii ya tatu. Ambapo tutaona kanisa lile la LAODIKIA. Tulishatazama makanisa mengine 6 yaliyotangulia pamoja na wajumbe wao, na jumbe walizopewa kutoka kwa Bwana.Kama haujayapitia unaweza ukayapitia kwanza ili tuende pamoja katika kanisa hili la mwisho, Tunasoma…
Ufunuo 3: 14 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu”.
Kama tulivyotangulia kujifunza tunaona ule utambulisho wa kwanza Bwana anaoutoa kwa kanisa, huwa una uhusiano mkubwa sana na ujumbe wenyewe wa kanisa husika. Hapa Bwana anasema ” yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu “. Na hasemi “yeye aliye na ule ufunguo wa Daudi, au yeye mwenye uso ung’aao kama jua. au yeye aliyekuwa amekufa kisha akawa hai” kama alivyokuwa anasema katika makanisa yaliyotangulia, hapana bali anasema “anenaye yeye aliye Amina, SHAHIDI MWAMINIFU na wa Kweli”. Ikiashiria kuwa katika kanisa hili anatazamia kuona UAMINIFU, kama aliokuwa nao yeye tangu mwanzo wa kuumba kwa Mungu.
Kwa ufupi kanisa hili la Laodikia lilianza kati ya kipindi cha mwaka 1906 WK na litaisha na siku ya ujio wa Bwana mara ya pili (yaani Unyakuo). Na mjumbe wa kanisa hili ni WILLIAM BRANHAM. Na tafsiri ya neno LAODIKIA ni “HAKI ZA WATU”. Katika Asia ndogo ambapo haya makanisa 7 yalikuwepo, Mji wa Laodikia ndio uliokuwa umeendelea kuliko miji mingine, kama efeso, smirna, pergamo n.k. Ni mji uliokuwa tajiri kuliko yote, ulikuwa upo juu kibiashara na kiuchumi na kiusomi, hivyo ikapelekea na watakatifu waliokuwa katika mji huo kuwa na hadhi ya kitofauti na watakatifu waliokuwa katika miji mingine. Na ndio maana hatushangai kwanini Bwana Yesu kutoa ujumbe ufuatao;
“15 Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. 16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu. 17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi”.
“15 Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.
16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.
17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi”.
Unaona hapo? kutokana na mafanikio makubwa yaliyokuwepo katika ya hao watu, Ikawafanya watakatifu waridhike na kupoa sana kiroho pasipo hata wao kujitambua. Watu wa mji ule (wasiomjua Mungu) wakaanza kuweka mambo kwenye mizani, kila kitu nusu kwa nusu, kama tafsiri ya jina lake lilivyo “HAKI ZA WATU” Mambo kama haki sawa, yakazaliwa wanaume kwa wanawake,
Sasa hii roho ya haki sawa nayo ikapenyeza mpaka kwenye kanisa la Mungu.. Kwamba kwa Mungu kuna haki sawa, nusu kwa nusu, Mungu kidogo na Ulimwengu kidogo, Unasali kidogo unafanya anasa kidogo, unakuwa mtakatifu leo kesho unaendelea na mambo mengine, unatenda mema leo, baadaye unakula rushwa, leo unakuwa wa rohoni kesho wa mwilini, hivyo hivyo leo moto kesho baridi (Yaani vuguvugu). Na kibaya kibaya zaidi kutokana na utajiri wake wa nje waliokuwa nao kanisa hili lilikuwa Laodikia, shetani akalipiga UPOFU mkubwa juu yake, likawa halijitambui tena kama linakwenda mbali na ukweli. Jaribu kutengeneza picha upo uchi, na hujitambui kama upo hivyo..Hiyo ni hatari kubwa sana.
Kwa kuwa Bwana anaona mbele alilifanya kanisa hilo kuwa unabii wa watu wa nyakati fulani itakayokuja miaka mingi huko mbele nao sio wengine zaidi ya sisi watu wa kizazi hichi tunachoishi leo ambacho kilianza tangu kipindi cha miaka ya 1906, Hivyo ndugu ni muhimu sana kufahamu kuwa tunaishi katika kanisa linalofanana na lile la Laodikia.
Kama vile mji ule ulivyokuwa tajiri kuliko miji mingine yote sita, kadhalika na dunia ya sasa tunayoishi ndio dunia iliyoendelea na iliyotajirika kuliko nyakati nyingine zote zilitangulia, kiuchumi, kiteknolojia na kielimu n.k.. Kiasi kwamba dunia leo hii ni kama kijiji, utandawazi umefikia viwango vya juu sana. Sayansi imefika hatua ya kwamba mwanadamu anaweza akaenda mwezini, mambo mengi sana yamevumbuliwa kuanzia karne ya 20, yaani kuanzia mwaka 1901 na kuendelea uvumbuzi wa mambo mengi ulitokea tukianza kueleza moja moja hatutamaliza. Mambo ambayo hayakuonekana katika karne zote zilizotangulia. Hii ni kuonyesha kwamba dunia ya sasa tunayoishi inafanana kabisa na mji ule wa LAODIKIA.
Kadhalika “haki za binadamu”, agenda za haki sawa kati ya wanawake na wanaume zilizuka katika karne hii hii ya 20, kwamba chochote mwanaume anachoweza kufanya hata mwanamke anaweza akafanya, hata mavazi mwanaume anayovaa hata mwanamke pia anaweza akayavaa, haki za watu kuoa mtu anayemtaka aidha mwanaume kwa mwanaume, au mwanamke kwa mwanamke haina shida n.k. mambo ambayo hayakuonekana katika karne zote za nyuma zilizotangulia.
Hivyo hiyo roho iliyokaa katika ulimwengu ikajiambukiza tena katika kanisa la KRISTO kama ilivyokuwa kwa wakati wa Laodikia. Kwa kuwa tunaishi katika kipindi cha mafanikio makubwa ya kielimu, kiuchumi na kiteknolojia, watakatifu wa wakati huu wakaanza kuendana pia na watu wa ulimwengu huu, na wao pia wakaanza kuiga mambo ya ulimwengu na kuyaleta katika kanisa la Mungu.
Kutokana na kwamba kuwa na utajiri wa vitu vingine vya nje, kama makanisa makubwa, vitendea kazi vya kisasa vya ibada kama vyombo vya muziki, vipaza sauti vikubwa vya kuwafikia watu wengi mambo ambayo hayakuwepo katika makanisa ya nyuma, vitu kama televisheni, radio na internet vimekuwa nyenzo rahisi za kuwafikia watu, kadhalika vyombo vya kisasa vya usafiri kama ndege, magari n.k. tofuati na hapo zamani watakatifu walikuwa wakitumia miguu, na punda kwenda kuhubiri injili, Ikawasababishia shabaha yao ihame kutoka katika mambo ya rohoni zaidi na kuhamia kwenye mambo ya mwilini. n.k. watakatifu wakaanza kujiona kwa vitu walivyonavyo Mungu anapendezwa nao,
Hivyo nguvu ile ile inayoiendesha dunia, ndio hiyo hiyo inayoiendesha kanisa, mambo yale yaliyotukuka katika dunia ndiyo yanayotukuka ndani ya kanisa la leo, Badala utakatifu utukuzwe ndani ya kanisa, inatukuzwa elimu, kwamba kipimo cha kuwa mchungaji au umekubaliwa na Mungu ni kiwango cha elimu na sio utakatifu, kadhalika utajiri wa Fedha imetukuzwa zaidi kuliko utajiri wa Rohoni, kiasi kwamba kipimo cha mtu kubarikiwa na Mungu sio kukua kiroho hapana bali kuwa na fedha nyingi..Injili inayoweza kumfaa mtu kwasasa ni injili ya mafanikio na sio injili ya toba.
Kadhalika vyeo vilivyotukuka duniani vinavyotumika kuongozea ustaarabu wa kidunia vimepewa heshima kubwa zaidi kanisani kuliko vyeo Mungu alivyovikusudia viwepo kwa uongozo wa kanisa. Kiasi kwamba ili uonekane umekubaliwa na Mungu ni lazima Uwe Raisi wa dhehebu fulani, M/kiti, Katibu/ Papa/ Mkurugenzi, Dokta, Profesa n.k. na sio Karama fulani ya rohoni kama unjilisti, uchungaji, ualimu, mitume na manabii, au karama nyingine za Roho kama miujiza,lugha, unabii uponyaji n.k. zimewekwa nyuma na hazina nafasi yoyote katika kanisa la sasa.
Dunia tunayoishi leo hii ni ya “HAKI ZA KIBINADAMU”, kadhalika na kanisa nalo limechukua hizo tabia, kwamba hata mavazi anayovaa mwanaume hata mwanamke wa kikristo anaweza kuyavaa, kwamba karama za uongozi ambazo Mungu aliziweka kwa wanaume tu, kulingana na (1Timotheo 2:12) kama vile uchungaji, ualimu na utume, hata mwanamke anaweza akazifanya; Imefikia hatua kwamba ndoa za jinsia moja zinazofungishwa na watu wa ulimwengu zinafungishwa pia Kanisani..Na bado watu hao wanajiita wakristo na kibaya zaidi shetani amewapiga upofu hawajijui kwamba wapo uchi, vipofu, maskini, na wanyonge….Ni uvuguvugu wa hali ya juu sana. Kristo ametupwa nje.
Kumbuka katika kila nyakati kulikuwa na mjumbe wa kanisa hilo ambalo Mungu alimnyanyua kutoa nuru ya wakati huo, Tuliona katika kanisa la Tano Bwana alimnyanyua Martin Luther na wengine kama wakina Calvin na Zingwli, kadhalika katika nyakati ya sita Bwana alimnyanyua John Wesley na wenzake. Vivyo hivyo na katika hili kanisa la mwisho Bwana alimnyanyua mjumbe wake WILLIAM BRANHAM na ujumbe wa kuwarudisha watu katika NENO na watoke katika hali ya uvuguvugu iliyopo sasa katikati ya madhehebu na kutoka katika mifumo ya yule mwanamke kahaba (Kanisa Katoliki) na pia Bwana alimpa ujumbe wa kutangaza kuja kwa pili kwa Kristo.
William Branham ni nani?.
William Branham alizaliwa huko Kentucky, Marekani mwaka 1909, alizaliwa katika familia ya kimaskini sana, baba yake alikuwa ni mtengenezaji wa pombe, hivyo aliishi katika mazingira ya kushawishika na ulevi, alipofikisha umri wa miaka 7 anasema siku moja wakati anatoka kuteka maji kisimani alisikia sauti juu ya mti ikimwambia, “Usikae unywe pombe, wala kuvuta sigara,kwani kuna kazi ya yeye kufanya utakapokuwa mtu mzima”, aliogopa sana lakini maneno hayo aliyaweka moyoni, kwani aliogopa kuwaeleza watu maono aliyokuwa anayaona kwasababu wengi miongoni mwa wachungaji walikuwa wakimwambia hayo ni maono kutoka kwa shetani, lakini ilifika kipindi akampa Kristo maisha yake, na kukata shauri kumtumikia Mungu, ndipo Bwana akaanza kumtumia kwa namna ya kipekee, Siku moja wakati anabatiza umati mkubwa wa watu katika mto mmoja huko Marekani unaitwa Ohio, alipokuwa anambatiza mtu kama wa 17, nyota kubwa ilishuka juu yake akiwa pale mtoni, watu wote wakaishuhudia na ndipo akasikia sauti ikimwambia “Kama vile Yohana mbatizaji alivyotumwa kutangaza kuja kwa kwanza kwa Kristo, vivyo hivyo ujumbe wako utatangaza kuja kwa pili kwa Kristo”. Habari ya tukio hilo ilisambaa sana na kuchapishwa katika magezeti na vyombo vya habari vya Marekani.
Na alipofikisha umri wa miaka 37, siku moja alipokuwa anasali usiku malaika wa Bwana alimjia na miongoni mwa maneno aliyoambiwa ni; “Kama akiwa mwaminifu atakapoomba hakuna kitachoweza kusimama mbele yake hata kansa, aliambiwa pia atawaombea wafalme na ujumbe wake utafika duniani kote,” . Hivyo kuanzia huo wakati Ishara na miujiza ya kupita kawaida viliambatana naye, mambo ambayo hapo nyuma yalikuwa hayaonekani, karama za upambanuzi wa roho ziliambata naye siku zote za huduma yake, siku moja wakati anahubiri Mungu kutaka kuithibitisha huduma yake NGUZO YA MOTO ambayo ilikuwa ikimfuata tangu kuzaliwa kwake, ilitokea hadharani na kukaa juu yake, mamia ya watu waliokuwa pale waliiona, na ikapigwa picha, hiyo ilikuwa ni mwaka 1950, Picha hiyo upesi ilipelekwa kwa George J. Lacy, Mchunguzi Mweledi wa Hati Zinazoshukiwa wa F.B.I. ya Marekani, ambaye aliihakiki picha hiyo kwa maoni yake ya kitaalamu. Hati rasmi iliyotolewa na Bw. Lacy kuhakiki kuwa ile ilikuwa ni picha ya kwanza ya kimiujiza iliyothibitishwa kisayansi. Hii ilikuwa ni mapema zaidi kabla ya kompyuta na kamera za tarakimu, wala haingeweza kuelezewa kwa njia zozote zinazojulikana na sayansi, mbali na kwamba kulikuwa na Nuru halisi juu ya kichwa cha William Branham. Leo hii picha hiyo hiyo inaweza kuonekana kwenye Maktaba ya Bunge la Marekani, katika makao makuu ya taifa, Washington DC. (Tazama picha chini).
Kwahiyo historia ya maisha na huduma ya William Branham ni ndefu kidogo hatuwezi kuielezea yote hapa ila kama utahitaji utaipata mwisho wa ukurasa huu.
Hivyo ishara zote na miujiza Mungu aliyomjalia William Branham viliambata na ujumbe, Na ujumbe wenyewe ulikuwa ni Kuwarudisha watu kwenye misingi ya Neno la Mungu, Kuwarejesha watu katika Imani ya kanisa la mwanzo, na kwamba watu wa Mungu watoke katika mifumo ya dini na madhehebu ambayo Mungu ameikataa, na kujiandaa kwa kuja kwa pili kwa Kristo, Kadhalika Bwana aliwanyanyua na wengine kama ORAL ROBERT, TL OSBORN, na BILL GRANHAM na wengine baadhi. Wote hawa ni ili kuangaza nuru ya Mungu katika kanisa la mwisho tunaloishi sasa. Hivyo uamsho wa Roho ulikuwa ni mkubwa sana katikati ya karne ya ishirini, tofuati na tunavyoona sasa hivi, kuzuka kwa wimbi kubwa la manabii wa uongo na waalimu wa uongo, na miujiza bandia kama tunavyoona sasa.
Sasa turudi katika kanisa hili la LAODIKIA Bwana anasema;
Unaona hapo, kanisa tunaloishi ni vuguvugu, kwa wingi wa vitu tulivyonavyo tumejikinai, Na Bwana anasema atatupika kama tusipotubu.. Bwana anasema..
“18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona. 19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu. 20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami”.
“18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.
19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.
20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami”.
Ujumbe huo unajieleza wenyewe kwamba ni wakati wa kurudi na kufahamu ujumbe wako wa saa wa nyakati unayoishi.. unaweza ukajiona ni moto kumbe ni baridi kwasababu umeshindwa kufahamu ni nyakati gani unaishi. na ujumbe wa wakati huu ni kurudi kwenye misingi ya NENO LA MUNGU ambayo tumeiacha ili tuwe moto na sio vuguvugu, tuache kuchanganya neno la Mungu mapokeo ya kidini, tuache kuchanganya Neno la Mungu na mambo ya ulimwengu huu kama kanisa la Laodikia lilivyokuwa (Kwani ni sawa na kufanya uasherati wa kiroho)..Leo hii unafanya ibada, kesho upo disco, jumapili unavaa vizuri, jumatatu unavaa vimini, leo unakuwa mwaminifu kesho unakula rushwa, leo unazungumza ukweli kesho unadanganya na kutukana, n.k.huko ndio kuwa vuguvugu, au KUTOKUWA MWAMINIFU na Kristo katika kanisa hili anataka kuona UAMINIFU kama yeye alivyojitambulisha hapo mwanzo kuwa YEYE NI MWAMINIFU TANGU MWANZO.
Na Bwana anamalizia kwa kusema..
“21 Yeye ashindaye, nitampa KUKETI PAMOJA NAMI KATIKA KITI CHANGU CHA ENZI, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi. 22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa”.
“21 Yeye ashindaye, nitampa KUKETI PAMOJA NAMI KATIKA KITI CHANGU CHA ENZI, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.
22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa”.
Unaona hapo? Kanisa hili ndilo lililopewa thawabu kubwa kuliko makanisa yote yaliyotangulia, kwamba kwa yeye atakayeshinda kwa kuwa mwaminifu kama yeye alivyokuwa atapewa nafasi ya kuketi pamoja naye katika kiti chake cha Enzi” Je! hupendi thawabu kama hiyo?..Wote tunaipenda hivyo tukizijua thawabu hizi njema Mungu alizotuandalia huko, tutaishi maisha ya kujilinda sana asije mwovu akalitwaa taji letu katika nyakati hizi za hatari.. Kumbuka pia hakutakuwa na kanisa linguine zaidi ya hili. Hatua iliyobaki ni unyakuo tu.
Ubarikiwe sana.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Huu ndio mwisho wa ujumbe Bwana alioutoa kwa yale makanisa saba. Kwa neema za Mungu tutazidi kuzitazama sura zinazoendelea. Kwa Mwendelezo >>>Ufunuo: Mlango wa 4
Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara, kwa njia ya whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255789001312. Na kama utapenda kwa njia ya E-mail basi tuandikie email yako katika boksi la maoni chini.
Mada Zinazoendana:
MAVAZI YAPASAYO.
Rudi Nyumbani
Print this post
Sehemu ya pili:
Bwana wetu YESU KRISTO atukuzwe. Karibu katika kujifunza kitabu cha Ufunuo, leo tukiendelea na ile sehemu ya pili ya sura hii ambapo tutajifunza juu ya kanisa la sita linalojulikana kama FILADELFIA. Tulishayatazama makanisa matano ya kwanza na tukaona kila moja ujumbe wake, thawabu zake pamoja na wajumbe au Malaika zake. Hivyo kama bado hujazipita ni vema ukazianza hizo kwanza kisha tuendelee kwa pamoja na kanisa hili la sita.
Tunasoma…
Ufunuo 3: 7 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye”.
Kama tulivyokuwa tunajifunza katika sura zilizopita kuwa ule utambulisho wa kwanza wa Bwana kabla hajatoa ujumbe unakuwa na mahusiano makubwa sana na ujumbe wenyewe wa kanisa husika..Kwamfano hapa anaanza kwa kusema ” Haya ndiyo anenayo yeye aliye MTAKATIFU, aliye wa kweli, aliye na UFUNGUO WA DAUDI, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye”.
Unaona hapo anasema yeye “aliye mtakatifu” hajasema “yeye aliye na hizo Roho saba” kama alivyofanya katika kanisa lililopita la Sardi, au “yeye aliye na huo upanga mkali utokao kinywani mwake kama alivyosema katika kanisa la tatu” hapana! Bali hapa anasema “yeye aliye mtakatifu na mwenye UFUNGUO wa Daudi”. Ikiashiria kuwa “Anategemea kuona UTAKATIFU kama yeye alivyo katika hilo kanisa”..Kadhalika na ufunguo pia alionao inaamaanisha “Anakwenda kufungua au kufunga kitu fulani katika hilo kanisa”. Hivyo tutakuja kuona hizo funguo za Daudi alizonazo ni zipi?..
Kwa ufupi kanisa hili la FILADELFIA lilianza mwaka 1750WK na kuisha mwaka 1906WK. Lilidumu kwa kipindi cha miaka 156, na Mjumbe/Malaika wa kanisa hili aliitwa JOHN WESLEY. Na tafsiri ya neno Filadelfia ni “UPENDO WA NDUGU”..Hivyo hili ni kanisa lililoonyesha utofauti mkubwa na makanisa mengine yote. Baada ya ule uamsho wa Luther wa kuwahubiria watu watoke katika ule mfumo wa yule mwanamke Yezebeli (Kanisa Katoliki). Bwana alimnyanyua tena Mjumbe wake mwingine mwaminifu, John Wesley na nuru ya ziada kwamba pamoja na “kuhesabiwa haki kwa imani kwa Mungu”, mtu anapaswa aongezee juu yake “UTAKATIFU“
1Petro 1: 15 “bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; 16 kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu. “
1Petro 1: 15 “bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;
16 kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu. “
Na tena inasema… Waebrania 12: 14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo UTAKATIFU, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao”
Mambo ambayo Kanisa la Sardi halikuonekana wala mjumbe wa kanisa lile Martin Luther hakulifundisha sana, yeye alitilia mkazo sana kuhusu “kuhesabiwa haki kwa imani”. Hivyo mjumbe wa hili kanisa la FILADELFIA John Wesley alianza kuhubiri UTAKATIFU kwa nguvu, na kwamba usafi katikati ya maisha ya waumini ni jambo la muhimu sana.
Wesley alizaliwa huko Epworth, nchini Uingereza mwaka 1703 na alipokuwa chuoni Oxford ndipo Bwana alipoanza kubadilisha maisha yake, yeye na kaka yake aliyeitwa Charles waliunda kikundi pamoja na wengine kinachosimamia itikadi ya “Kuishi maisha kama ya Kristo aliyoishi”, kuliko maisha ya kidini, walianza kwenda kuwatembelea wagonjwa mahospitalini, na wafungwa, na kuwahurumia maskini, n.k na kujifanya wao wenyewe kuwa vielelezo(njia ya kufuata) hivyo wakajiundia uongozi wa kiroho wakauita “(METHOD yaani NJIA”)..na kuanzia huo wakati wakaitwa WAMETHODISTI. Baada ya hapo Wesley na wenzake Bwana aliwagusa kwa namna ya kipekee, wakaona umuhimu wa kwenda kufanya kazi ya umishionari duniani kote. Hapo ndipo injili ikaanza kupelekwa duniani kote kwa nguvu, kasi na kwa bidii hata zile sehemu ambazo zilikuwa ngumu kufikiwa kama Afrika zikafikiwa na nuru ya neno la Mungu, ndio wakati wamishionari wengi wakaanza kufika sehemu za Afrika,Asia na Marekani ya kusini.
Wesley alikuwa ni mtu aliyeimarika kiroho sana, anasema hakumbuki kama alishawahi kupunngua nguvu rohoni hata kwa robo saa tangu siku aliyozaliwa. Alisema hakuwahi kulala zaidi ya masaa 6 siku zote za huduma yake, kila siku alikuwa akiamka saa 11 alfajiri, na kwenda kuhubiri zaidi ya mara nne kwa siku, ili kwamba kwa mwaka afikishe kwa wastani wa mafundisho 800. Alikuwa akisafiri maelfu ya maili kwa farasi kwenda kuhubiri. Kwa mwaka inakadiriwa alikuwa anasafiri zaidi ya maili 4,500 kwenda kuhubiri.
Tukiendelea na mistari inayofuata…
Ufunuo 3:8 “Nayajua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe umelitunza neno langu, wala hukulikana jina langu”.
Bwana anasema amewapa mlango uliofunguliwa mbele yao.? Sasa huu mlango ni upi?.
Kumbuka hapo awali BWANA alijitaja kama “yeye aliye na ufunguo wa Daudi“. Na ni kwanini aseme funguo za Daudi na asiseme funguo za Musa, au Ibrahimu?. Ni kwa nini Daudi?. Hii inatupa picha halisi kuwa upo ufunguo ambao alikuwa nao Daudi na Bwana naye akawa nao. Hivyo ni vizuri tukaufahamu huu ufunguo kwanza ni nini ili tupate msingi mzuri wa huko tunapoelekea?..
Kumbuka Baada wa Wana wa Israeli kutoka Misri na kuingia katika nchi yao ya ahadi, watu wote baada ya kuiona ile nchi ni nzuri walitawanyika na kila mtu kwenda kukaa sehemu yake, walijenga na kupanda na kufanikiwa wakamsahau Mungu, Wao walifanikiwa lakini Mungu katikati hao hakuwa na nafasi yoyote, wao walikaa kwenye makasri lakini Mungu alikaa kwenye mahema ya giza. Na iliendelea hivyo kwa kipindi kirefu cha zaidi ya mamia ya miaka, na hakukuwa na mtu yeyote kutia moyo wake ufahamu kuona kwamba kwanini sanduku la Mungu linakaa kwenye mahewa yenye giza leo huku kesho kule, Mungu mkamilifu anayetujali hapaswi kukosa sehemu ya kukaa, Ndipo Daudi siku moja akatia moyo wake ufahamu na kusema nimtengenezee Mungu wangu mahali pa kukaa, haiwezekani yeye akae kwenye jumba la kifahari wakati, Bwana Mungu wake hajamjengea nyumba, ndipo Daudi kwa bidii akaiteka ngome ya Sayuni (YERUSALEMU), Kisha akakusudia kuanzia huo wakati amjenge Mungu wake nyumba ( yaani HEKALU). Na ndipo Mungu akamwambia Daudi.
2 Samweli 7: 2 “Mfalme akamwambia Nathani, nabii, Angalia sasa, mimi ninakaa katika nyumba ya mierezi, bali sanduku la Mungu linakaa ndani ya mapazia. 3 Nathani akamwambia mfalme, Haya, fanya yote yaliyomo moyoni mwako; maana Bwana yu pamoja nawe. 4 Ikawa usiku uo huo, neno la Bwana likamfikia Nathani kusema, 5 Enenda, ukamwambie mtumishi wangu, Daudi, Bwana asema hivi, JE! WEWE UTANIJENGEA NYUMBA, NIKAE NDANI? 6 Kwa maana mimi sikukaa ndani ya nyumba, tangu siku ile niliyowatoa wana wa Israeli katika Misri, hata leo, lakini nimekaa katika hema na maskani. 7 Mahali mwote nilimo kwenda na wana wa Israeli wote, JE! NIMESEMA NENO LOLOTE NA MTU YO YOTE WA WAAMUZI WA ISRAELI, NILIYEMWAGIZA KUWALISHA WATU WANGU ISRAELI, NIKISEMA, MBONA HAMKUNIJENGEA NYUMBA YA MIEREZI? 8 Basi, sasa, mwambie mtumishi wangu, Daudi, maneno haya, Bwana wa majeshi asema hivi, Nalikutwaa katika zizi la kondoo, katika kuwaandama kondoo, ili uwe mkuu juu ya watu wangu, juu ya Israeli; 9 nami nimekuwa pamoja nawe kila ulikokwenda, na kuwakatilia mbali adui zako wote mbele yako; nami nitakufanyia jina kuu, kama jina la wakuu walioko duniani. 10 Tena nitawaagizia mahali watu wangu Israeli, nami nitawapanda, wapate kukaa mahali pao wenyewe, wasiondolewe tena; wala wana wa uovu hawatawatesa tena, kama hapo kwanza;”
2 Samweli 7: 2 “Mfalme akamwambia Nathani, nabii, Angalia sasa, mimi ninakaa katika nyumba ya mierezi, bali sanduku la Mungu linakaa ndani ya mapazia.
3 Nathani akamwambia mfalme, Haya, fanya yote yaliyomo moyoni mwako; maana Bwana yu pamoja nawe.
4 Ikawa usiku uo huo, neno la Bwana likamfikia Nathani kusema,
5 Enenda, ukamwambie mtumishi wangu, Daudi, Bwana asema hivi, JE! WEWE UTANIJENGEA NYUMBA, NIKAE NDANI?
6 Kwa maana mimi sikukaa ndani ya nyumba, tangu siku ile niliyowatoa wana wa Israeli katika Misri, hata leo, lakini nimekaa katika hema na maskani.
7 Mahali mwote nilimo kwenda na wana wa Israeli wote, JE! NIMESEMA NENO LOLOTE NA MTU YO YOTE WA WAAMUZI WA ISRAELI, NILIYEMWAGIZA KUWALISHA WATU WANGU ISRAELI, NIKISEMA, MBONA HAMKUNIJENGEA NYUMBA YA MIEREZI?
8 Basi, sasa, mwambie mtumishi wangu, Daudi, maneno haya, Bwana wa majeshi asema hivi, Nalikutwaa katika zizi la kondoo, katika kuwaandama kondoo, ili uwe mkuu juu ya watu wangu, juu ya Israeli;
9 nami nimekuwa pamoja nawe kila ulikokwenda, na kuwakatilia mbali adui zako wote mbele yako; nami nitakufanyia jina kuu, kama jina la wakuu walioko duniani.
10 Tena nitawaagizia mahali watu wangu Israeli, nami nitawapanda, wapate kukaa mahali pao wenyewe, wasiondolewe tena; wala wana wa uovu hawatawatesa tena, kama hapo kwanza;”
Unaona hapo sababu kubwa iliyomfanya hata Bwana Yesu kuitwa mwana wa Daudi, ni tabia aliyoionyesha Daudi ya kumuundia Mungu wake mji wa kukaa pamoja na Hekalu la kuweka Jina lake, katika ya makuhani, kati ya wafalme, kati ya waamuzi, kati ya manabii, ni Daudi pekee ndiye aliyeliona jambo hilo?. Na Mungu alikaa kimya makusudi aone ni nani atakayekuwa na akili ya kufanya hivyo. Na akaonekana Daudi peke yake. Na huo ndio UFUNGUO Daudi aliokuwa nao KUFUNGUA ukimya wa Mungu.
Kadhalika na Bwana wetu Yesu Kristo aliposema “yeye mwenye Ufunguo wa Daudi” alimaanisha na yeye pia anaunda Yerusalemu yake na Hekalu kwa Mungu wake. Isipokuwa yeye YERUSALEMU yake ni ya rohoni sio ya mwilini,na hekalu kwa Mungu wake ni la rohoni sio la mwilini. Daudi hasaa asingeweza kabisa kumwandalia Mungu mji utakayomfanya ashuke yeye mwenyewe na kukaa katikati ya watu lakini Bwana Yesu anaandaa mji utakaoleta makao ya Mungu katikati ya watu..na huu “MJI” anaoundaa ni watakatifu wake. Tukisoma…
1 Wakorintho 3: 16 ” Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? 17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, AMBALO NDILO NINYI “.
1 Wakorintho 3: 16 ” Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?
17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, AMBALO NDILO NINYI “.
Tutakuja kuona vizuri juu ya mji mtakatifu wa Mungu (Yerusalemu mpya) ni nini, tutakapofika katika Ufunuo sura ya 21.
Hivyo alipoliambia hili kanisa la Filadelfia “Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako”, Alimaanisha kuwa ni mlango wa kuujenga mji wake pamoja naye. Hivyo wale watu walipoanza kwenda huku na huko kufanya umishionari wa kuwaleta watu wengi (Ikiwemo) wapagani kwa Kristo, ndio ulikuwa mlango uliofunguliwa mbele yao. JOHN WESLEY na mamisionari wengine waliifanya kazi hiyo duniani kote, kipindi hicho pia ndio biblia kusambazwe duniani kote, hakuna nchi ambayo haikufikiwa na nuru ya Neno.
Tukiendelea ..
“9 Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uongo. Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda. 10 Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi”.
“9 Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uongo. Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda.
10 Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi”.
Sinagogi la shetani halikuanzia tu kwenye hili kanisa la sita, bali lilikuwepo pia katika makanisa ya nyuma, lilitajawa pia katika kanisa la pili (Ufunuo 2:9), Hili ni kanisa la uongo ambalo walikuwepo watu waliojifanya kama kanisa la kweli la Mungu na kuiga mambo yaliyokuwa yanafanywa na watakatifu lakini ndani yao walikuwa ni mbwa-mwitu wakali, wanaliharibu kundi, ni tabia ya shetani popote palipo na nuru ya kweli ya Mungu, atanyanyuka na kupanda magugu yake katikati yao. Lakini katika hili kanisa kwa kuwa walilishika Neno la subira ya Mungu kwa uaminifu wote, Mungu akayadhoofisha hayo makundi mengine ya uongo shetani aliyoyanyanyua katikati yao na kumtukuza sana bibi-arusi wake zaidi yao.
Bwana anaendelea na kusema…
“10 Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi. 11 Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako”.
“10 Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi.
11 Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako”.
Unaona hapo Kanisa hili liliahidiwa pia kulindwa kutoka katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwenguni wote (Na hii saa ya kuharibiwa itakuwa ni kipindi cha dhiki kuu), Ikiwa na maana kuwa dhiki hii kuu ingepaswa itokee tangu wakati wa hili kanisa la Filadelfia lakini kwasababu ya Subira na uaminifu wao, Bwana akawaepusha, hivyo itatokea katika kanisa linalofuata la mwisho la Laodikia. Na kama anavyosema saa hiyo itakuwa ni ya “kuwajaribu hao wakaao juu ya nchi”, ina maana kuwa ulimwengu mzima utapitia jaribu moja zito la “aidha kupokea chapa ya mnyama uishi au kuikataa ufe” litakuwa ni jaribu kubwa sana kwa wale watakaoachwa kwenye unyakuo. Ndugu Unaona wakati tunaoishi?, ni hatari kubwa sana ipo mbele yetu kama tusipokuwa waangalifu?.
Na anazidi kusema “11 Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako”.
Hapa anasema “naja upesi” ikiwa na maana kuwa “hakawii” biblia inasema waebrania 10: 37 “Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, YEYE AJAYE ATAKUJA, WALA HATAKAWIA”.
Na pia anasema “shika sana ulicho nacho” ikiwa na maana kuwa, kile ulichokipokea ukiihifadhi, kwa kuwa “mtakatifu” na kujiepusha na “mafundisho yadanganyayo” asije “MTU”, akatwa taji yako, kumbuka ni “mtu” na sio “malaika” ikifunua kuwa mataji tunapewa hapa hapa duniani, mbinguni tukifika ni kuvikwa tu. Na tukiwa hapa duniani kuna mtu anaweza akatwaa mataji yetu, SASA huyu “MTU” atafutaye kutwaa mataji yetu (au THAWABU) zetu ni nani??
2 Wathesalonike 2: 3 ” MTU awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule “MTU WA KUASI”, mwana wa uharibifu; 4 yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu. 5 Je! Hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwapo pamoja nanyi naliwaambieni hayo? “
2 Wathesalonike 2: 3 ” MTU awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule “MTU WA KUASI”, mwana wa uharibifu;
4 yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.
5 Je! Hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwapo pamoja nanyi naliwaambieni hayo? “
Unaona hapo huyu MTU anayezungumziwa hapo ni mpakwa mafuta wa shetani (yaani MPINGA-KRISTO ndani ya cheo cha UPAPA), na mifumo yake yote,na mitume wote wa uongo wajigeuzao kuwa mitume wa Kristo, ambao kwa kipindi hichi cha siku za mwisho wamezagaa kila mahali, wasiofundisha toba na msamaha wa dhambi wala wasiofundisha ujio wa Bwana bali mungu wao ni tumbo..Mtume aliwataja katika…
Wafilipi 3: 17 Ndugu zangu, mnifuate mimi, mkawatazame wao waendao kwa kuufuata mfano tuliowapa ninyi. 18 Maana wengi huenenda, ambao nimewaambieni mara nyingi habari zao, na sasa nawaambia hata kwa machozi, KUWA NI ADUI ZA MSALABA WA KRISTO; 19 mwisho wao ni uharibifu, MUNGU WAO NI TUMBO, utukufu wao u katika fedheha yao, WANIAO MAMBO YA DUNIANI. 20 Kwa maana sisi, WENYEJI WETU UKO MBINGUNI; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo; 21 atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake.
Wafilipi 3: 17 Ndugu zangu, mnifuate mimi, mkawatazame wao waendao kwa kuufuata mfano tuliowapa ninyi.
18 Maana wengi huenenda, ambao nimewaambieni mara nyingi habari zao, na sasa nawaambia hata kwa machozi, KUWA NI ADUI ZA MSALABA WA KRISTO;
19 mwisho wao ni uharibifu, MUNGU WAO NI TUMBO, utukufu wao u katika fedheha yao, WANIAO MAMBO YA DUNIANI.
20 Kwa maana sisi, WENYEJI WETU UKO MBINGUNI; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo;
21 atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake.
Na mwisho kabisa Bwana anamalizia kwa kusema…..
” 12 Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa NGUZO katika HEKALU LA MUNGU WANGU, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya. 13 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. “
” 12 Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa NGUZO katika HEKALU LA MUNGU WANGU, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya.
13 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. “
Bwana aliwaahidia watu wa kanisa hili la Filadelfia, wale ambao waliokuwa watakatifu, na kujiepusha na mafundisho ya uongo na kujitoa kwa bidii yote kupeleka injili huku na kule duniani kote, na kuusimamisha mji wa Bwana Yerusalemu yake ya rohoni, na hekalu ndani yake, kama Daudi alivyoadhimia kumjengea Bwana nyumba, hata BWANA kuuchagua Yerusalemu kuwa makao yake makuu, na mji wake mtakatifu, kadhalika hawa wa Filadelfia Bwana aliwaahidia kuwafanya kama nguzo, katika ule mji uliotukuka Yerusalemu mpya ambao tutakuja kuuona habari zake katika sura ile ya 21..
Tukiyajua hayo, ni wakati wa kuzifanya taa zetu ziwe zinawaka, kwa kumuamini, Bwana Yesu Kristo, na kutubu, na kubatizwa katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa na kwa JINA LA YESU na kupokea Roho Mtakatifu, na kuishi maisha yanayolingana na wokovu,(yaani maisha matakatifu), na zaidi ya yote kuipeleka habari njema kwa watu wote ulimwenguni kote, na kujihadhari “mtu” asije akayatwaa mataji yetu.
Ubarikiwe na Bwana Yesu, aliyetoa maisha yake kuwa dhabihu hai, kwa Mungu kwa ajili yetu.
Tafadhali “share” kwa wengine ujumbe huu na Mungu atakubariki. Kwa Mwendelezo >>> Ufunuo: Mlango wa 3 Part 3
WEWE NI HEKALU LA MUNGU.
MPINGA-KRISTO
Sehemu ya kwanza.
Bwana na mwokozi wetu YESU KRISTO atukuzwe daima. Karibu katika mwendelezo wa uchambuzi wa kitabu cha Ufunuo, Leo tukiliangalia lile kanisa la TANO kati ya yale makanisa SABA, na Ujumbe aliopewa Mtume Yohana ayapelekee. Kanisa hili linaitwa SARDI. Tunasoma.
Ufunuo 3:1 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho saba za Mungu, na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa”.
Kumbuka hapa Bwana anajitambulisha kama “yeye mwenye hizo Roho saba za Mungu, na zile nyota saba”. Katika kanisa hili hakujitambulisha kama “yeye mwenye macho kama mwali wa moto au yeye mwenye huo upanga mkali utokao kinywani mwake n.k.” bali alijitambulisha kama yeye mwenye hizo Roho saba, akifunua asili yake ya ndani, Sasa Hizi Roho saba, sio kwamba Mungu anazo Roho 7 na kila moja inajitegemea kivyake hapana, bali ni Roho ile ile moja isipokuwa inatenda kazi katika nyakati tofauti tofauti saba. Mfano tuna siku 7 katika juma, na kila siku tunaona jua likichomoza na kuzama, sasa hatuwezi tukasema kwa wiki tuna ma-jua 7, hapana tunafahamu kuwa jua ni lile lile moja isipokuwa limetenda kazi katika siku saba tofauti, na ndivyo ilivyo kwa Roho wa Mungu. Kwanza ni vizuri kufahamu Mungu ni Roho, na ni mmoja, na Roho yake ni moja, kadhalika na nafsi yake ni moja. Kwahiyo hapo ni ile ile Roho moja ikitenda kazi katika nyakati tofauti tofauti saba za Kanisa.
Kwahiyo kwanini Bwana alijitambulisha kama yeye mwenye Roho 7, ni kwasababu “Roho ndiyo inayotia uzima”. Na ndio iliyokuwa inatia UZIMA kwa makanisa yote 7 kuanzia la kwanza mpaka la mwisho. Ikiwa na maana kuwa kanisa hilo la SMIRNA lilihusiana na kupungukiwa na Roho wa Mungu. Hivyo kama tunavyofahamu mtu akikosa Roho wa Mungu ni sawa na kakosa uzima,na Kinachobakia ni kifo. Wakati fulani Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake katika
Yohana 6: 63 “ROHO NDIYO ITIAYO UZIMA, mwili haufai kitu; MANENO HAYO NILIYOWAAMBIA NI ROHO, TENA NI UZIMA”.
Unaona hapo anasema ni Roho tena ni uzima. Hivyo kanisa hili limehusiana na kuacha maneno ya Bwana ambayo ndio Roho yenyewe itiayo uzima kwao. Na ndio maana Bwana anasema anayajua matendo yao ya kwamba “wana jina lililohai lakini WAMEKUFA”.
Tulichunguze kidogo hili kanisa la SARDI; Tafsiri ya neno SARDI ni “WALE WALIOTOROKA”..Na kanisa hili lilianza mwaka 1520WK na kuisha mwaka 1750WK, Kanisa hili halikudumu kwa muda mrefu sana kama Kanisa lililopita la Thiatira ambalo lenyewe lilidumu kwa muda wa zaidi ya miaka 900. Kipindi hichi cha kanisa hili kinajulikana maarufu kama “wakati wa matengenezo ya kanisa”, Ni wakati ambao lile giza ambalo lilikuwa limetanda duniani kutoka katika nyakati za kanisa la nne lilianza kumezwa na Nuru ya kweli ya Mungu kidogo kidogo baada ya kanisa kuharibiwa kwa muda mrefu na mafundisho ya dini ya uongo (Katoliki).
Hivyo Mungu akaanza kunyanyua watumishi wake waaminifu ambao waliyashika yale maneno ya Bwana aliyosema katika lile kanisa la Nne lililotangulia kwamba “wanamridhia yule mwanamke YEZEBELI”. Hivyo hawa baada ya kuzijua fumbo za shetani na kwamba makao yake makuu yapo katika dini ya uongo inayofanana sana na ukristo (Katoliki), hawakumridhia kama watu wa kanisa la nne walivyofanya.. Hivyo wakaanza kunyanyuka na kwenda kinyume na kuyapinga mafundisho yake kwa kuhubiri UKWELI WA NENO kwa watu wote pasipo kumwogopa. Ndipo tunakuja kuona Mungu akamnyanyua mtu kama “MARTIN LUTHER”, Ambaye yeye ndiye aliyekuwa mjumbe/Malaika wa kanisa hilo (SARDI), na wengine pia kama wakina Calvin, Zwingli, na wengineo..Wote hawa kwa pamoja hawakumridhia yule mwanamke YEZEBELI. Na kama vile tafsiri ya jina la Kanisa hili lilivyo (Sardi=wale waliotoroka), hivyo hawa wakristo wa nyakati hii walifanikiwa kutoroka kwa sehemu kutoka kwa yule mwanamke Yezebeli.
Tunaona Martin Luther ambaye mwanzoni alikuwa ni kasisi wa kikatoliki, baada ya kuona njia ya kanisa Katoliki haiendani na kweli ya Mungu, aligeuka na kuyapinga mafundisho ya kanisa hilo, siku moja katika safari yake ya kuutafuta ukweli, alisikia sauti ikimwambia..“Mwenye haki ataishi kwa Imani” (Warumi 1:17). Hivyo baada ya kupokea ufunuo huo akaanza kuyakataa mafundisho yote ya “wanikolai” ya “Balaamu” na ya “Yezebeli” kwamba mtu hatapitia kwa kuhani fulani au Padre fulani au Papa ili amfikie Mungu, Bali kwa IMANI kwa Mungu kila mtu atamfikia yeye na kumpendeza..kwamba mtu anasamehewa dhambi zake kwa IMANI kwa Mungu, na sio kwa kupitia mwanadamu yoyote, kadhalika na uponyaji na mahitaji na mambo mengine yote…
Hivyo kuanzia huo wakati Martin Luther alizidi kupinga kwa Nguvu mifumo ya kanisa Katoliki siku moja aliandika HAYA 95 zinazopinga mfumo wa kipapa na kuzigongelea kwenye mlango wa ngome ya kanisa kubwa la kiKatoliki lililokuwepo huko wittenberg Ujerumani mwaka 1517. Na ndipo uprotestant ulipoanzia ikasababisha uamsho mkubwa wa roho, watu wengi wakaanza kutoka kwenye hiyo dini ya uongo kwa kupitia injili za hawa wana matengenezo.
Biblia zikaanza kutafsiriwa jambo ambalo hapo kwanza zilikuwa zinasomwa tu na makuhani wa kikatoliki, Hivyo ndivyo nuru ya kweli ilivyoanza kurejeshwa kidogo kidogo.
Lakini ilifikia wakati miaka kadhaa baada ya wale wajumbe kuondoka, watu wakaanza kujisahau, na kuanza kujiundia dini badala ya kuuendeleza uamsho wa Kweli ya Mungu, badala ya kuendelea kujitakasa kutoka katika yale mafundisho ya uongo zaidi na zaidi wakajiundia ngome, nao pia wakaanza kujiita Walutheran, wacalvism, wabrownist, wamennonite n.k. watu wakaanza kujivunia wanadamu na dini, badala ya kujivunia Kristo hivyo ikawafanya wasahau kabisa ule msingi wa uprotestant ambao haukuwa na lengo la kuanzisha dini nyingine bali ulikuwa na lengo la kuwatoa katika uongo wa yule mwanamke Yezebeli (Katoliki) na kuwarejesha watu kwenye NENO LA MUNGU.
Jambo ambalo Mtume Paulo alilikemea pia kwa nguvu katika…
1wakorintho 1: 11 “Kwa maana, ndugu zangu, nimearifiwa habari zenu na wale walio wa nyumbani mwa Kloe, ya kwamba iko fitina kwenu. 12 Basi, maana yangu ni hii, ya kwamba kila mtu wa kwenu kusema, Mimi ni wa Paulo, na, Mimi ni wa Apolo, na, Mimi ni wa Kefa, na, Mimi ni wa Kristo. 13 Je! Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulibiwa kwa ajili yenu? Au je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo? “
1wakorintho 1: 11 “Kwa maana, ndugu zangu, nimearifiwa habari zenu na wale walio wa nyumbani mwa Kloe, ya kwamba iko fitina kwenu.
12 Basi, maana yangu ni hii, ya kwamba kila mtu wa kwenu kusema, Mimi ni wa Paulo, na, Mimi ni wa Apolo, na, Mimi ni wa Kefa, na, Mimi ni wa Kristo.
13 Je! Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulibiwa kwa ajili yenu? Au je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo? “
Hivyo mbele za Mungu hawa watu wa Sardi ambao mwanzoni walianza vizuri kwa nje walionekana kama wapo hai, lakini kwa ndani walikuwa WAMEKUFA kwasababu Roho ya uhai, na UZIMA haikuwa tena ndani yao, ya kuwafanya waweze kuuendeleza ule UAMSHO walioanzana nao hapo mwanzo.
Tukiendelea kusoma tunaona…
“2 Uwe mwenye kukesha, ukayaimarishe mambo yaliyosalia, yanayotaka kufa. Maana sikuona matendo yako kuwa yametimilika mbele za Mungu wangu. 3 Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. Walakini usipokesha, nitakuja kama mwivi, wala hutaijua saa nitakayokuja kwako”.
“2 Uwe mwenye kukesha, ukayaimarishe mambo yaliyosalia, yanayotaka kufa. Maana sikuona matendo yako kuwa yametimilika mbele za Mungu wangu.
3 Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. Walakini usipokesha, nitakuja kama mwivi, wala hutaijua saa nitakayokuja kwako”.
Unaona hapo waliambiwa wakeshe, na wayaimarishe mambo yaliyoyasalia, (yaani kumalizia kuondoa mafundisho yote ya Yezebeli ndani ya Kanisa), na kwamba wasipofanya hivyo (yaani kukesha) atakuja kwao kama mwivi na wala hawatajua hiyo saa atakayokuja.
Swali ni saa gani hiyo anayoizungumzia atalijilia hilo kanisa? Angali wakati wa hilo kanisa ulishapita na unyakuo haujatokea?
Ni muhimu kufahamu kwamba kila kanisa Bwana alikuwa na wakati wake wa kulijilia kanisa hilo, na kujiliwa huko kulikuwa ni UAMSHO fulani wa kipekee ambao ni mahususi kwa kuwavusha watu katika hatua nyingine ya kiimani inayofuata na huo Uamsho huwa unakuja karibu na mwishoni kabisa mwa nyakati wa kanisa husika..Hivyo kwa kanisa la kwanza baada ya kuacha upendo wao wa Kwanza Bwana aliwajilia kwa kupitia uamsho wa Irenio mjumbe wa kanisa la pili hivyo kwa ile jamii iliyoweza kumtii Kristo kwa ujumbe wa wakati waliokuwa nao(Wa mtume Paulo) waliweza kuchukuliana na ujumbe wa nyakati iliyofuata..Hivyo kwao Bwana anakuwa amewajilia lakini sio kama mwivi kwasababu Roho wa Mungu hajazimishwa ndani yao, lakini wale waliokataa, kwao inakuwa kama mwivi ndio unakuta watu wanaishia kuupinga ule ujumbe wa kuwaua, Na kuishia kuchukuliwa na mafundisho ya shetani.
Kadhalika na kwa nyakati ya pili, kujiliwa kwao kulikuwa ni mwishoni kabisa mwa nyakati, jamii ya watu waliodumu na mafundisho ya Irenio (Mjumbe wa kanisa la pili) waliweza kuchukuliana na uamsho wa mjumbe anayefuata..Vivyo hivyo na kwa kwani la nne, la tano.
Sasa katika hili la tano saa ya kujiliwa kwao ilikuwa ni wakati wa uamsho wa kanisa lililofuata ambalo Bwana alimtumia Mjumbe wa Kanisa lile JOHN WESLEY kuja na ujumbe wa UTAKASO KWA DAMU YA YESU, na utakatifu Hivyo kwa wale wachache ambao waliruhusu Roho wa Mungu awatoe kutoka hatua moja hadi nyingine ya IMANI, na kukaa mbali na mifumo ya yule kahaba Yezebeli walipewa neema ya kuuamini na kuupokea ujumbe wa John Wesley na huko ndiko kulikokuwa kujiliwa kwao. Lakini wale wengine waliokuwa wanaonekana wapo hai lakini wamekufa kwa kujiundia “majina” na kutengeneza madhehebu, Bwana alipokuja na uamsho wa Roho wa Wesley hawakujua chochote Sasa hiyo ndiyo kujiliwa kama mwivi, walibaki na dini zao na madhehebu yao.wakawa hawataki kufahamu jambo lingine la ziada ya ulutheri, ucalvinism, umennonite n.k. wakati lile kundi dogo ambalo lilikuwa tayari kwenda na Roho wa Mungu lilipokea uvuvio mpya wa Roho. Kwamba kuhesabiwa haki kwa Imani peke yake hakutoshi bali pia na Utakatifu ambao hakuna mtu atakayemwona Mungu asipokua nao (Waebrania 12:14)
Kadhalika na kwa kanisa la sita Filadelfia vile vile Bwana alilijia na wale waliokuwa wanadumu katika mafundisho ya mjumbe wa kanisa la sita John Wesley ilipofika wakati kujiliwa waliweza kupewa neema ya kuonja Uamsho uliofuata lakini wale ambao waliridhika na kuchukulia ujumbe wa Wesley kama dini, walibakia katika madhehebu yao wakajifungia katika Umethodisti na wakati wa Pentekoste ya Bwana ulipokuja mwaka 1906 huko Asuza Marekani, hawakujua chochote, wengine waliishia kupinga na kusema hicho kitu ni cha shetani na wengine hawakuelewa ni kitu gani.. Kwamba kuhesabiwa haki kwa imani pamoja na utakaso havitoshi bali pia Ubatizo wa Roho Mtakatifu ndio ukamilifu wa mambo yote. (Waefeso 4:30) kwamba huo ndio muhuri wa Mungu.
Vivyo hivyo na kwa kanisa la mwisho tunaloishi linaloitwa Laodikia, wale wote watakaoupokea ujumbe wa mjumbe wa kanisa hili WILLIAM BRANHAM wakidumu katika kujitenga na mafundisho ya yule kahaba mkuu YEZEBELI na kuruhusu Roho ya Mungu ya uhai ifanye kazi ndani yao, Na kukua kutoka hatua moja kwenda nyingine kila siku, Sasa hawa Bwana atakapokuja watajua kwasababu Roho wa Mungu anatenda kazi ndani yao, na taa zao zinawaka, lakini wale wengine hawatajua chochote, wataishia aidha kupinga, au kutokuelewa juu ya huo uamsho wa mwisho unaokuja. na kwa vile hakuna nyakati nyingine zaidi ya saba..Umsho huo utakuwa ni kwa ajili ya unyakuo wa kanisa. Na zile ngurumo 7 kwenye ufunuo 10 (zilizobeba siri ambazo hazijaandikwa mahali popote ), hizo ndizo zitakazoleta uamsho wa mwisho zitakazomvusha bibi-arusi wa Kristo kutoka katika nyakati ya saba, na kuingia katika umilele. Na ndio maana Bwana alisema…
Marko 13: 33 “Angalieni, kesheni, [ombeni], kwa kuwa hamjui wakati ule utakapokuwapo. 34 Mfano wake ni kama mtu mwenye kusafiri, ameiacha nyumba yake, amewapa watumwa wake amri, na kila mtu kazi yake, naye amemwamuru bawabu akeshe. 35 Kesheni basi, kwa maana hamjui ajapo bwana wa nyumba, kwamba ni jioni, au kwamba ni usiku wa manane, au awikapo jimbi, au asubuhi; 36 asije akawasili ghafula akawakuta mmelala. 37 Na hilo niwaambialo ninyi, nawaambia wote, Kesheni”.
Marko 13: 33 “Angalieni, kesheni, [ombeni], kwa kuwa hamjui wakati ule utakapokuwapo.
34 Mfano wake ni kama mtu mwenye kusafiri, ameiacha nyumba yake, amewapa watumwa wake amri, na kila mtu kazi yake, naye amemwamuru bawabu akeshe.
35 Kesheni basi, kwa maana hamjui ajapo bwana wa nyumba, kwamba ni jioni, au kwamba ni usiku wa manane, au awikapo jimbi, au asubuhi;
36 asije akawasili ghafula akawakuta mmelala.
37 Na hilo niwaambialo ninyi, nawaambia wote, Kesheni”.
Na utaona maneno haya haya aliliambia hili kanisa la SARDI…
Ufunuo 3: 3 “Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. Walakini usipokesha, nitakuja kama mwivi, wala hutaijua saa nitakayokuja kwako”. …
Lakini pamoja na hayo walikuwepo wachache katika kanisa hilo, walioweza kuenenda kwa uongozo wa Roho na kujitenga na yule mnyama hao ndio Bwana aliowaambia wataenda naye katika uvuvio wa Roho utakaokuja wa John Wesley.
“4 Lakini unayo majina machache katika Sardi, watu wasioyatia mavazi yao uchafu. Nao watakwenda pamoja nami hali wamevaa mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili. 5 Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu, na mbele ya malaika zake. 6 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa”.
“4 Lakini unayo majina machache katika Sardi, watu wasioyatia mavazi yao uchafu. Nao watakwenda pamoja nami hali wamevaa mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili.
5 Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu, na mbele ya malaika zake.
6 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa”.
Anasema yeye ashindaye jina lake halitafutwa katika kitabu cha uzima, na zaidi ya yote yale mavazi meupe yanawakilisha usafi wa hali ya juu, ‘heri wenye moyo safi maana hao watamwona Mungu (Mathayo 5:8) inasema hivyo”..Hivyo kundi hili katika umilele unaokuja watakuwa na nafasi ya karibu sana na Mungu kuliko watu wengine.
Hivyo ndugu Ujumbe huo pia unatuhusu hata sisi watu wa kizazi hichi tunachoishi, wa kanisa hili la mwisho la laodikia. Je! unakesha? na taa yako inawaka? je! Roho wa Mungu bado yupo hai ndani yako?. au una jina lililo hai lakini ndani yako umekufa?..Kumbuka huu ni wakati wa jioni, ondoka katika madhehebu na vifungo vya dini kama umeupokea ujumbe wa wakati wako halafu unaugeuza kuwa kama dini au dhehebu huu ni wakati wa kugeuka. Hivi karibuni Bwana ataenda kuachilia uvuvio wa mwisho nao utakuwa ni wa kipindi kifupi sana, utakaompa bibi arusi imani ya kwenda kwenye unyakuo.
Luka 12: 35 “Viuno vyenu na viwe vimefungwa, na taa zenu ziwe zinawaka; 36 nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao, atakaporudi kutoka arusini, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara”.
Luka 12: 35 “Viuno vyenu na viwe vimefungwa, na taa zenu ziwe zinawaka;
36 nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao, atakaporudi kutoka arusini, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara”.
Tafadhali share ujumbe huu kwa wengine na Mungu atakubariki. Kwa Mwendelezo >>> Ufunuo: Mlango wa 3 Part 2
YEZEBELI NI NANI?
KAMA MWIZI USIKU WA MANANE
HATUA ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUTUONGOZA
NINI MAANA YA KUTOKA KATIKA MADHEHEBU?
Rudi Nyumbani.
Sehemu ya nne.
Shalom! mwana wa Mungu, karibu tujifunze Neno la Mungu, leo tukiwa katika mwendelezo wa kitabu cha Ufunuo. Hii ni sehemu ya nne, inayozungumzia juu ya lile kanisa la nne kati ya yale saba aliyoyachagua Bwana (Ufunuo 1:11), linaloitwa THIATIRA. Katika sura hii ya pili tulishayaona makanisa matatu ya mwanzo, tukaona ni jinsi gani yalivyokuwa yanaenenda na tabia zake kulingana na nyakati hayo makanisa yaliyopitia. Na leo tutamalizia sehemu ya mwisho ya sura hii ya pili, ambayo tutaliona kanisa hili la Thiatira na ujumbe wake waliopewa kutoka kwa BWANA.
Ufunuo 2:18 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Thiatira andika; Haya ndiyo anenayo Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho yake kama MWALI WA MOTO, na miguu yake mfano wa shaba iliyosuguliwa sana”.
Hapa tunaona Bwana ananza na utambulisho kama yeye azungumzaye ni “yule mwenye macho kama mwali wa moto, na miguu yenye mfano wa shaba iliyosuguliwa sana”..Kama tulivyojifunza kila utambulisho unaotangulia kabla ya ujumbe,huwa una mahusiano makubwa sana na ujumbe wenyewe wa kanisa husika. Mfano tuliona katika lile kanisa lililopita alijifunua kama “yeye aliye na huo upanga mkali ukatao kuwili utokao katika kinywa chake”, na tunajua upanga unaashiria vita, na tulipokuja kusoma tuliona alikuja kufanya vita na wale wote ambao hawakutubia matendo yao maovu ndani ya kanisa. Kadhalika na hapa Bwana anakuja kama mwenye macho kama mwali wa moto na miguu iliyosuguliwa, mfano wa shaba. Tunajua kuwa macho kazi yake ni kuona. Na kama yanatoka moto inamaana kuwa anachokiona kinastahili moto. Hivyo hapa katika hili kanisa vile vile anakuja kwa hukumu kwa kile anachokiona. Swali ni kitu gani alichokiona ambacho kinastahili hukumu?..Tutakuja kukiona mbeleni.
Tukiendelea kusoma..
“19 Nayajua matendo yako na upendo na imani na huduma na subira yako; tena kwamba matendo yako ya mwisho yamezidi yale ya kwanza”.
Kwa historia fupi kanisa la Thiatira lilianza mwaka 606WK hadi mwaka 1520WK, na mjumbe wake aliitwa KOLUMBA, Ni kanisa lililodumu kwa kipindi kirefu kuliko makanisa yote saba, takribani miaka 914. Kipindi hichi kinajulikana kama kipindi cha giza ni wakati ambao nuru ya NENO la Mungu lilikuwa imefifia sana kutokana na mafundisho ya kipagani kuongezeka na mambo mengine kama uchawi, na umaskini vilikuwa vimekithiri sana duniani. Lakini kulikuwa pia na kuna kundi dogo la wateule wa Mungu ambao walikusudia kutokujitia madoa na mambo maovu, walidumu katika Imani yao pasipo kujali mateso waliyoyapitia, walidumu katika upendo, na uvumilivu wa hali ya juu, na wenye bidii katika kujisafisha kila siku, wakihama kutoka utukufu hata utukufu na zaidi ya yote walikuwa na bidii sana ya kumtumikia Mungu(huduma), wakihubiri huku na kule mpaka kufikia Bwana kuwaambia matendo yao ya mwisho yamezidi yale ya kwanza, (je na sisi tunaweza tukafika hatua ya kuambiwa hivyo?)
Lakini pamoja na kwamba watu wa kanisa hilo ni watu waliokuwa na bidii nyingi na upendo na uvumilivu na subira lakini Bwana alikuwa na Neno moja juu yao ambalo ndilo lililomfanya aonekane mbele zao kama “mwenye macho kama mwali wa moto”…Unaona hapo na sisi tunaweza tukawa tunafanya mema na bidii lakini Bwana bado akawa na Neno juu yetu..tusome..
“20 Lakini nina neno juu yako, ya kwamba WAMRIDHIA YULE MWANAMKE YEZEBELI, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu. 21 Nami nimempa muda ili atubu, wala hataki kuutubia uzinzi wake. 22 Tazama, nitamtupa juu ya kitanda, na hao wazinio pamoja naye, wapate dhiki kubwa wasipotubia matendo yake; 23 nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye viuno na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake”.
“20 Lakini nina neno juu yako, ya kwamba WAMRIDHIA YULE MWANAMKE YEZEBELI, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu.
21 Nami nimempa muda ili atubu, wala hataki kuutubia uzinzi wake.
22 Tazama, nitamtupa juu ya kitanda, na hao wazinio pamoja naye, wapate dhiki kubwa wasipotubia matendo yake;
23 nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye viuno na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake”.
Tunaona pamoja na kwamba kanisa hili lilitenda mema mengi kiasi cha kusifiwa lakini kilionekana kikwazo ndani yao na hicho si kingine zaidi ya yule MWANAMKE YEZEBELI kama tunavyomsoma.
Yezebeli tunamwona katika agano la kale alikuwa ni mke wa mfalme Ahabu wa Israeli. Kumbuka mwanamke huyu hakuwa binti wa kiyahudi, bali Ahabu alimtoa katika mataifa ya kipagani,(huko Lebanoni) ingekuwa heri kama angebadilishwa imani yake na kuwa myahudi kama ilivyokuwa kwa Ruthu, lakini haikuwa hivyo kwake, yeye alitoka huko nchi za mataifa ya kipagani, akiwa na dini yake, ya kuabudu miungu mingi pamoja na Baali, na kibaya zaidi hakuja peke yake, bali alikuja na manabii wake wengi wa kumsaidia kufukiza uvumba kwa miungu yake akiwa Israeli hivyo akawa kikwazo kikubwa kwa Israeli kwasababu hakufanya hizo ibada za sanamu peke yake bali pia aliwafundisha na kuwalazimisha watu wote hata wale waliokataa kuiabudu miungu yake kufanya hivyo (1Wafalme 19).
Hivyo Bwana alilifananisha hili kanisa la Thiatira na Israeli kipindi cha Mfalme Ahabu. Kumbuka tafsiri ya neno THIATIRA ni “MWANAMKE ANAYETAWALA”..Hivyo kama Israeli kwa wakati ule kulikuwa na mwanamke anayetawala Yezebeli, Kadhalika na katika kanisa hilo yupo mwanamke anayetawala mwenye tabia zinazofananishwa na za Yezebeli. Na huyu si mwingine zaidi ya “KANISA KATOLIKI”., mwanamke huyu huyu tunamwona pia katika ile sura ya 17, ambayo tutakuja kuzisoma kwa undani habari zake hapo baadaye, ..
Ufunuo 17: 3 “Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona MWANAMKE, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.
4 Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake. 5 Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.
4 Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake.
5 Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.
6 Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu. “
Sasa kumbuka kwenye lile kanisa la kwanza, shetani alianza kujipenyeza kama “matendo ya wanikolai”, na katika kanisa la tatu na kuendelea akakomaa yale matendo yakabadilika na kuwa “mafundisho” ..Tunaona pia roho ile ile iliyokuwa kwa wanikolai ndio hiyo hiyo ilitenda kazi kwa Balaamu katika kanisa la tatu, na ndiyo hiyo hiyo inatenda kazi ndani ya Yezebeli katika Kanisa hili la Nne. Konstantini alisimama kama Balaamu, na Kanisa Katoliki linasimama kama mwanamke Yezebeli. Nao wote hawa ukiangalia kazi yao ilikuwa ni moja ni kuwakosesha watu wa Mungu wazini na kula vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu. Hivyo Kanisa katoliki liliwakosesha watakatifu wa wakati ule wamkosee Mungu kwa kufanya uasherati wa kiroho. Na uasherati wenyewe ni upi?. Ni dhahiri kuwa waliyapokea mafundisho mengine ambayo hawakukabidhiwa na Mungu tangu awali kupitia mitume wake watakatifu kwa kulichanganya Neno la Mungu na desturi za kipagani, kwamfano ibada za sanamu, kuomba kwa wafu, ibada za miungu mitatu, sala za mapokeo ya kipagani, ubatizo wa vichanga n.k.
Hivyo pamoja na kwamba walikuwa ni watakatifu, wanajitahidi kufanya mambo mema, na kutenda kazi ya Mungu kwa bidii lakini bado Mungu alikuwa anaona kasoro ndani yao, kwamba WAMEMRIDHIA yule mwanamke Yezebeli. Maana ya “kuridhia” ni kuvumilia / kukubaliana /kuchukuliana naye..Hivyo wale watakatifu wa kipindi hicho waliopewa macho ya kumtambua kwa kupitia Mjumbe wa Mungu aliyemteua kwa wakati huo (KOLUMBA) walimridhia yule mwanamke na kuchukuliana na mafundisho yake. Hivyo Bwana akawaonya watubu na kwamba wasipotubu atawaua kwa mauti na makanisa yote ndipo yatakapojua ya kuwa Bwana anachunguza viuno(fahamu za watu) na mioyo ya watu wote, kwamba yale macho yake yaonayo mpaka sirini na hakuna jambo lolote linalositirika kwake!
Kanisa Katoliki nalo Bwana alilipa muda wa kutubu, lakini halikutaka kutubu, kama tulivyoona hapo juu, hata hivyo
(Yeremia 51: 9 ilishatabiri habari zake na kusema ..“Tungependa kuuponya Babeli, Lakini haukuponyeka; Mwacheni, nasi twendeni zetu, Kila mtu hata nchi yake mwenyewe; Maana hukumu yake inafika hata mbinguni, Nayo imeinuliwa kufikilia mawinguni. “
Na ndio maana Bwana Yesu alisema ..” 21 Nami nimempa muda ili atubu, wala hataki kuutubia uzinzi wake. 22 Tazama, nitamtupa juu ya kitanda, na hao wazinio pamoja naye, wapate dhiki kubwa wasipotubia matendo yake;
Na ndio maana Bwana Yesu alisema ..” 21 Nami nimempa muda ili atubu, wala hataki kuutubia uzinzi wake.
23 nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye viuno na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake. “
Kumbuka Yezebeli alikuwa anao watoto, na mmoja wapo aliitwa “ATHALIA” (2Wafalme 9). Huyu naye alienda kuolewa na Mfalme wa Yuda na mambo yale aliyoyafanya mama yake aliyafanya na yeye vilevile na mabaya kuliko hayo. Aliutwaa ufalme kwa nguvu,na kutawala Israeli kwa muda wa miaka 7 jambo ambalo lilikuwa ni machukizo makubwa kwa Israeli taifa la Mungu kutawaliwa na mwanamke. Alidiriki pia kuuangamiza uzao wa Daudi kwa kuwaua wazao wote wa kifalme lakini mpango wake haukufanikiwa. Na zaidi ya yote aliwakosesha watu wa Yuda kama mama yake alivyowakosesha watu wa Israeli kwa kuabudu miungu migeni.
Hivyo kama Yezebeli alivyokuwa na binti anayefanana na yeye kitabia kadhalika Kanisa Katoliki (Yezebeli wa rohoni), amezaa mabinti wanaofanana na yeye kitabia na ndio maana anajulikana kama mama wa makahaba, na mabinti zake ni madhehebu yote yanayofanana na yeye. Na watu wanaoshikamana nayo Bwana atakuja kuwaua kwa mauti ( katika lile Ziwa la moto.)
Tukiendelea kusoma mistari inayofuata….
“24 Lakini nawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, wo wote wasio na mafundisho hayo, wasiozijua FUMBO ZA SHETANI, kama vile wasemavyo, Sitaweka juu yenu mzigo mwingine. 25 Ila mlicho nacho kishikeni sana, hata nitakapokuja”.
“24 Lakini nawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, wo wote wasio na mafundisho hayo, wasiozijua FUMBO ZA SHETANI, kama vile wasemavyo, Sitaweka juu yenu mzigo mwingine.
25 Ila mlicho nacho kishikeni sana, hata nitakapokuja”.
Unaona hapo? Bwana anasema kuna watu wasiojua “FUMBO ZA SHETANI” na walikuwa katikati ya kundi la Mungu..Hivyo shetani naye anazo fumbo zake, nazo zinahitaji hekima kuzitambua. Ikiwa na maana kuwa anajua namna ya kumdanganya mtu kulingana na jinsi anavyoenenda, ukiwa ni mwovu atakudanganya kwa njia ya uovu, na ukiwa mtakatifu atakuja kwa kivuli cha utakatifu. na ndio maana biblia inasema yule mwanamke jina lake limeandikwa kwa SIRI, kumbuka sio kwa wazi bali kwa siri, BABELI MKUU MAMA WA MAKAHABA, NA MACHUKIZO YA NCHI.. Hapo ndipo kiti cha enzi cha shetani kilipo..Yeye pamoja na watumishi wake wanajigeuza kuwa kama malaika na watumishi wa nuru. Hivyo ni kujichunguza na kujihakiki kila siku je! tupo kwenye NENO? hiyo ndiyo njia pekee ya kulifumbua fumbo la shetani na kumshinda. Lakini tukipuuzia mambo kama hayo yatatukuta kama hayo ya kanisa la Thiatira Bwana atatuua kwa mauti.
Unakumbuka watu wa kanisa hili waliambiwa matendo yao mema yamezidi hata yale ya kwanza, walijitahidi sana kuwa wakamilifu lakini walikosa kuzitambua mbinu za shetani, Kadhalika na sisi wa kanisa la mwisho tulilopo, Yule mwanamke YEZEBELI na MABINTI zake wapo, na wanazidi kuwakosesha watu na kuwapeleka mamilioni ya watu kuzimu (hususani wakristo), Kwahiyo kiini cha ujumbe ambao Bwana alikuwa anataka kuwaambia ni kwamba katika ukamilifu na utakatifu wao waongezee tu kumtoa yule mwanamke kahaha na uzinzi wake katikati yao kwa kutokuridhia mafundisho yake, na sisi vivyo hivyo katika bidii yetu yote tuliyonayo kwa Mungu katika upendo subira, uvumilivu, huduma tumalizie kwa kujitenga na yule kahaba Babeli mkuu (Katoliki) pamoja na mabinti zake wote (madhehebu).
Ufunuo 18:4 “Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, ENYI WATU WANGU, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.
5 Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake”.
Kwahiyo wote walioshinda katika kanisa hilo kwa kujitenga na yule mwanamke Yezebeli na kudumu katika Neno Bwana aliwaahidia thawabu..
” 26 Na yeye ashindaye, na kuyatunza matendo yangu hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa, 27 naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo, kama mimi nami nilivyopokea kwa Baba yangu. 28 Nami nitampa ile nyota ya asubuhi. 29 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. “
” 26 Na yeye ashindaye, na kuyatunza matendo yangu hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa,
27 naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo, kama mimi nami nilivyopokea kwa Baba yangu.
28 Nami nitampa ile nyota ya asubuhi.
29 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. “
Thawabu hizi ni katika ulimwengu unaokuja, Bwana atakapokuwa MFALME WA WAFALME, ni dhahiri kuwa atatwaa wafalme wachache chini yake ili yeye awe Mfalme wa Wafalme na ndio watakaokuwa watu wa kanisa hili, hawa ndio watakaopewa mamlaka juu ya mataifa, na hiyo fimbo ya chuma itakuwa ni kutoa amri na kutekelezwa. Na ile nyota ya asubuhi ina maana kuwa utukufu wao utakuwa ni wa kipekee tofauti na wengine, kumbuka nyota ya asubuhi ndio nyota pekee yenye kuangaza hata wakati wa mchana, wakati nyingine nguvu zao za kung’aa zinakuwa ni usiku tu. Hivyo kule katika mbingu mpya na nchi mpya watang’aa milele na milele pamoja na Bwana Yesu. Hivyo ndugu kwanini ukose mambo hayo yote mazuri?..Tafuta kwanza ukamilifu (UTAKATIFU) mpe Bwana maisha yako leo, kisha malizia kwa kujitenga na yule mwanamke kahaba, na mabinti zake kwa kudumu katika NENO LA MUNGU TU!.na sio katika mapokeo na dini.
Sehemu ya tatu.
BWANA wetu YESU KRISTO apewe sifa. Karibu katika kujifunza Neno la Mungu, leo tukiendelea na sehemu ya tatu, ya sura hii ya pili, ambapo tulishatangulia kuona lile Kanisa la Efeso na Smirna, pamoja na wajumbe na ujumbe wao kutoka kwa Bwana. Na hapa tutaona kwa ufupi kanisa lingine la tatu linaloitwa PERGAMO. Tunasoma
KANISA LA PERGAMO.
Ufunuo 2: 12 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Pergamo andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na huo upanga mkali, wenye makali kuwili”.
Kama tulivyotangulia kujifunza tunaona hapa Bwana anaanza kwa kujitambulisha kama “yeye aliye na huo upanga mkali,wenye makali kuwili”. Tulishaona katika makanisa yaliyopita,kwamba ule utambulisho wa kwanza Bwana anaoanzana nao, una uhusiano mkubwa na ujumbe wa kanisa husika..Sasa hapa anaposema “yeye mwenye upanga mkali”, haimaanishi jambo jema sana kwa kanisa hilo, kama alivyojitambulisha katika kanisa la Smirna aliposema “yeye aliyekuwa amekufa kisha akawa hai” kuonyesha kwamba kuna tumaini baada ya kifo,.Lakini hapa ni tofauti, anaanza kwa kutamka upanga na upanga siku zote unaashiria vita, na tena anasema unatoka katika kinywa chake ikiwa na maana kuwa ataenda kufanya vita kwa kinywa chake, (Ambalo ndio Neno lake). Na pia kumbuka hapa hazungumzi na watu wa mataifa (yaani wasio wakristo na wasiomjua Mungu) hapana bali anazungumza na wakristo, na hao ndio atakaofanya nao vita kwa huo upanga utokao katika kinywa chake.. Lakini ni kwanini afanye nao vita?, tutakuja kuona hapo mbeleni sababu zenyewe:
Tukiendelea kusoma..:
” 13 Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani. “
Neno “Pergamo” tafsiri yake ni “NDOA”. Na Historia inaonyesha kanisa hili lilianzia mwaka 312WK na liliisha mwaka 606WK. Lakini hapa tunaona Bwana anawaambia watakatifu wa wakati huo kwamba anafahamu kuwa mahali walipokaa ndipo penye kiti cha Enzi cha shetani, (mahali penyewe tutapaona mbeleni) na pia ameona kuwa wamelishika sana jina lake wala hawakuikana imani, licha ya kwamba shetani alikuwa anawaua wakristo wengi, tangu kanisa lililotangulia nyuma hadi huo wakati waliokuwepo wakristo wengi waliuawa, hata katika siku za Antipa, ambaye alikuwa pia ni shahidi mwamifu wa Bwana aliyeishindania Imani mpaka kufa bila kuikana.Hawa wote hawakutikisika kwa lolote pamoja na dhiki hizo zote.
Lakini Bwana anaendelea kusema;
” 14 Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki atie ukwazo mbele ya Waisraeli, kwamba wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini.
Baada ya shetani kuona kuwa watu bado wapo radhi kutoa hata maisha yao kwa ajili ya IMANI yao, akaona kwa njia ya vitisho na dhiki haina nguvu tena kuwatoa watu kwa Mungu, ndipo akabadilisha mbinu, na kuhamia kwenye njia ya udanganyifu, Na ndio maana hapo tunaona Bwana anasema ” unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu ” Swali ni je! haya mafundisho ya Balaamu ni yapi?.
Habari za Balaamu tunazipata katika agano la kale kitabu cha Hesabu 22. Tunasoma kuwa wakati wana wa Israeli wakiwa jangwani katika safari yao ya kuelekea nchi ya ahadi walikutana na wana wa Moabu njiani, na walipotaka kukatiza katika nchi yao mfalme wao aliyeitwa Balaki aliwazuia. Na zaidi ya yote akaenda kumwajiri Balaamu nabii wa uongo ili awalaani wana wa Israeli (Kuwaloga) wasifanikiwe katika safari yao. Hivyo Bwana alimzuia Balaamu mara tatu asiwalaani, na kinyume chake akawabariki. Lakini haikuishia hapo Balaamu yule nabii wa uongo kwa kupenda fedha ya udhalimu, kutoka kwa mfalme Balaki alitafuta njia mbadala ya kuwakosesha wana wa Israeli. Ndipo akamshauri Balaki afanye karamu na kuwaalika wanaume wa Israeli ili wafanye uzinzi na wanawake wa kimoabu na kutoa sadaka kwa miungu yao, ili iwe ukwazo kwao kwa Mungu wa Israeli na Mungu awaadhibu. Hivyo njama yake kweli ilifanikiwa, na hasira ya Mungu ikawaka juu ya Israeli, nao wakaadhibiwa kwa kosa lile. Hivyo tunaona hapo Balaamu ndiye aliyekuwa chanzo cha kuwakosesha Israeli.
Vivyo hivyo katika hili kanisa la Pergamo, Kumbuka kwa wakati ule Rumi ndiyo iliyokuwa inatawala dunia, na utawala ule ulikuwa ni utawala wa kipagani, Lakini ilifika wakati mtawala wa Rumi aliyeitwa KONSTANTINI alipokuwa anataka kwenda kupigana vitani dhidi ya maadui zake, aliota ndoto na akaona angani ya msalaba, Hivyo alipoenda vitani akaweka nembo ya msalaba katika mavazi yake ya kivita akiamini kuwa yale ni maono kutoka kwa Mungu, na aliposhinda ile vita akasema Mungu wa wakristo amemsaidia hivyo kuanzia huo wakati akataka kuifanya dini ya kikristo kuwa ya dini ya taifa, hivyo akaanza kufanya jitihada za kuunganisha pamoja warumi na wakristo hivyo akachukua desturi za dini za kipagani za Rumi(za kuabudu miungu mingi) na ukristo akavileta pamoja ili awapate wote. Kwa lugha nyepesi alichofanya Konstantini ni KUOANISHA ukristo na upagani..Na ndio maana tafsiri ya neno Pergamo ni NDOA.
Kwahiyo alichofanya mwaka 325WK ni kuitisha baraza kubwa la maaskofu, na viongozi wote wa Kikristo mahali panapoitwa NIKEA. Ambapo zaidi ya viongozi wa kidini 1,500 walihudhuria kuzungumzia suala hilo. Na ndipo wote wakafikia muafaka wa kuundwa Dini moja ya ulimwengu mzima (Kanisa Katoliki). Kumbuka tafsiri ya Neno Katoliki ni “ulimwengu wote” hivyo kanisa Katoliki maana yake ni “Kanisa la ulimwengu wote”.. Sasa kuanzia hapo ule ukristo ambao ulikuwa haujachanganyikana na mafundisho yoyote ya uongo, ukafa na kuzaliwa ukristo mpya bandia ambao umechukuliwa na desturi za kipagani za Rumi mfano wa kuabudu miungu mingi, na ndio hapo vitu kama ubatizo wa vichanga ukazaliwa, ubatizo wa kunyinyuziwa ukaundwa, ibada za sanamu,kusali rozari na za kuomba kwa watakatifu waliokufa zamani mambo ambayo huwezi kuyaona katika maandiko matakatifu au kufanywa na mitume wa zamani,pamoja na ibada za miungu mitatu, Ambazo utazikuta kwenye desturi za kirumi.
Sasa kumbuka huyu Konstantini ndio mfano wa Balaamu Bwana Yesu aliyemzungumzia kuwa anawakosesha watu wake (Kumbuka roho ile ile ya shetani iliyokuwa ndani ya Balaamu ndiyo hiyohiyo iliyokuwa ndani ya Konstantini). Kama vile Balaamu alivyotia ukwazo kwa wana wa Israeli wale vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu na kuzini vivyo hivyo Konstantini alianza kuwakosesha watu wa Mungu (wakristo) kwa kuwatoa katika mstari wa ukristo wa kweli wa mitume, na kuwaingiza katika dini ya kipagani aliyoianzisha yeye (Ukatoliki). Na kuwafanya wafanye uzinzi wa kiroho na kuamsha ghadhabu ya Mungu katikati yao.
Bwana Yesu aliendelea na kusema…
“15 Vivyo hivyo wewe nawe unao watu wayashikao mafundisho ya Wanikolai vile vile”
Kumbuka pia hawa wanikolai tuliwaona tokea Kanisa la kwanza la Efeso, isipokuwa kule walikuwa wanaonyesha matendo tu lakini hapa katika kanisa hili wamehama kutoka katika matendo na kuwa katika “Mafundisho” ikifunua kuwa ni kitu kilichotia mizizi sana, kimeundiwa kanuni na sheria za kufuatwa. Kumbuka tena tafsiri ya neno NIKOLAI ni “kuteka madhabahu”. Hivyo wanikolai ni watekaji madhabahu, watu wanaochukua nafasi ya madhabahuni ambayo ingepaswa iwe ya Roho Mtakatifu mwenyewe na kuifanya yao. Mfano vyeo vya upapa, ukadinali, upandre viongozi wakuu, n.k.kujengwa kwa madaraja yanayomtofautisha mkristo mmoja na mwingine mbele za Mungu. Kwamba ilikuwa huwezi kumfikia Mungu au kumwomba Mungu bila kupitia kwanza katika ngazi za juu yako.Ilikuwa ili kusamehewa dhambi ilimpasa mtu apitie kwa pandre wake amwombee, yeye mwenyewe hawezi kufanya hivyo. Hivyo uhusiano binafsi wa mtu na Mungu uliuliwa, ukaundwa uhusiano wa mtu na mtu kwa niaba ya Mungu..(Huo ndio unikolai), uongozi wa Karama za rohoni ukafa, ukanyanyuka uongozi wa kibinadamu kanisani… Na mafundisho haya yalipokomaa na kuhasiliwa na hiyo dini ya ulimwengu mzima (Kikatoliki) ndipo ukatokea UPAPA (ambao Unasimama kama mwakilishi wa Mwana wa Mungu duniani)..Hii ndiyo ngazi ya juu kabisa ya hii roho ya unikolai.
Lakini Bwana anamaliza na kusema…
” 16 Basi tubu; na usipotubu, naja kwako upesi, nami nitafanya vita juu yao kwa huo upanga wa kinywa changu. 17 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea. “
” 16 Basi tubu; na usipotubu, naja kwako upesi, nami nitafanya vita juu yao kwa huo upanga wa kinywa changu.
17 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea. “
Unaona kama vile wana wa Israeli walivyouliwa kwa upanga siku ile watu elfu 24, kwa kosa tu la Balaamu.. Vivyo hivyo Bwana aliwaonya na hao wakristo wa hilo kanisa la Pergamo kwamba watubu na wajiupushe na mafundisho ya Konstantini yaliyofananishwa na Balaamu (yaani dini iliyoundwa ya kikatoliki), inayowapelekea kufanya uasherati wa kiroho, na ibada za sanamu. Lakini walikuwepo watu ambao hawakutubu kipindi hicho wakachukuliana na hiyo dini ya uongo ya Konstantini, Bwana aliwaua hao wote kwa upanga utokao katika kinywa chake, Hao wote walikufa kiroho, na kabla ya kuangamizwa nafsi zao Bwana aliwanyanyulia mjumbe kwanza na kuwahubiria mambo hayo na kuwarudisha katika njia ya kweli ya mitume kwa udhihirisho wa kipekee kutoka kwa Bwana, na mjumbe huyo ni MARTINI ndiye aliyekuwa (Malaika/Mjumbe) wa hilo kanisa.
Kwahiyo wale wote walioupokea ujumbe wake,na kujitenga na uasi huo Mungu aliwalinda mpaka mwisho kama tunavyosoma..’
“17 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea”.
Hivyo wote walioshinda, Bwana alizidi kuwaongozea ufunuo wa ziada wa kuzijua siri zake, na kumtambua shetani na hila zake (Ndiyo ile mana iliyofichwa). Kumbuka ni mana iliyofichwa ikimaanisha kuwa sio watu wote wataiona isipokuwa bibi-arusi tu aliyejitenga na mifumo yote ya yule kahaba mkuu (Katoliki). Huyo tu ndiye atakayepokea hicho chakula cha kipekee kitokacho mbinguni. Kadhalika alisema pia yeye ashindaye atapewa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea..Sasa thawabu hii watapewa katika ule ulimwengu unaokuja..
Ni mfano wa zawadi na ndio maana anasema juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea. Kuashiria kwamba siku atakapolipokea ndipo atakapojua thamani ya alichopewa na watu wengine wataiona baadaye.. Sasa kumbuka anaposema kupewa jina, haimanishi kubadilishiwa jina, au kupewa jina lenye mvuto mzuri hapana, tunaweza tukajifunza kwa maisha tu ya kawaida unaweza ukapita mahali fulani ukasikia mtu fulani ana jina mahali pale.. Haimaanishi kuwa jina lake ni zuri au ni la kipekee sana hapana moja kwa moja utajua huyo mtu anayo nguvu fulani labda ya kifedha au kimamlaka, au ki-sifa ndiyo iliyompa jina hilo..Na ndivyo itakavyokuwa huko katika utawala wa milele unaokuja.. Kuna watu watakuwa na majina mazito na makubwa kutokana na uaminifu wao waliokuwa nao hapa duniani, na kuna watu pia watakuwa na majina madogo. Biblia inatuambia hata Bwana mwenyewe atakuja na Jina jipya, siku hiyo ndiyo kila mtu atamfahamu kwa mapana yeye ni nani na biblia ilikuwa inamaanisha nini ilipokuwa inasema kuwa yeye ni BWANA WA MABWANA na MFALME WA WAFALME. HALELUYA!!.
Kwahiyo ndugu yangu hata sasa haya mafundisho ya Balaamu yapo ndani ya Kanisa na yapo katika kiwango cha juu sana kuliko hata kile cha kipindi kile, roho ya mafundisho ya kipagani imejichanganya katikati ya watu wa Mungu. Hivyo toka huko. Bwana leo hii anaachilia mana yake iliyositirika kwa wachache waliotayari kutii, lakini wakati utafikia tusipotubu na kuyaacha mafundisho ya uongo na kuyakimbia.. Bwana atakuja kufanya vita nasi kwa Neno lake kwa kupitia vivywa vya watumishi wake. Na ukishafikia hiyo hatua, kutakuwa hakuna nafasi ya pili, hapo ni kuingojea ile siku ya Bwana inayowaka kama moto na kutupwa katika lile ziwa la moto. Hivyo huu ni wakati wa kutengeneza mambo yako sawa ili hayo yote yasikupate kabla ya mlango wa neema kufungwa.
Ubarikiwe.
1.Ufunuo: Mlango wa 2 Part 4
Nyumbani
Sehemu ya pili.
Libarikiwe jina la mwokozi wetu YESU KRISTO milele na milele AMINA!. Karibu katika kujifunza kitabu cha Ufunuo. Leo tukiendelea katika ile sehemu ya pili ya mlango huu. Kama tulivyotangulia kuona katika sehemu ya kwanza juu ya kanisa la Kwanza (EFESO) na ujumbe wake kutoka kwa Bwana..Kwamba watu wa kanisa lile waliuacha ule upendo waliokuwa nao hapo mwanzo, na jinsi Bwana alivyowaonya watubu na kwamba wasipotubu Bwana atakuja kukiondoa kile kinara chao cha taa. Lakini tukiendelea na Kanisa la Pili linaloitwa SMIRNA tunasoma;
KANISA LA SMIRNA.
Ufunuo 2:8 ” Na kwa malaika wa kanisa lililoko Smirna andika; Haya ndiyo aneneyo yeye aliye wa kwanza na wa mwisho, aliyekuwa amekufa, kisha akawa hai”.
Hapa tunaona Bwana anaanza kwa utambulisho kwamba “yeye ni wa kwanza na wa mwisho, aliyekuwa amekufa, kisha akawa hai”. Kumbuka Kama tulivyotangulia kujifunza utambulisho wa awali wa Bwana unakuwa na uhusiano mkubwa sana na kanisa husika kabla hata ya ujumbe wenyewe kutolewa. Mfano hapa Bwana anaposema aliyekuwa amekufa kisha akawa hai, kama alivyotangulia kujitambulisha hivyo hivyo katika ile sura ya kwanza (Ufunuo 1:18), Hii ikifunua kuwa kuna mapito ya mateso na dhiki nyingi mpaka kupelekea KIFO lakini pia kuna matumaini ya kufufuka baada ya kifo kama Bwana alivyopitia. Na ndio maana hapa hakujitambulisha kama yeye mwenye ule upanga mkali utokao kinywani mwake(maana upanga unawakilisha vita na hapa hajaja kufanya vita), au mwenye uso kama unaong’aa kama jua n.k bali ni “yeye aliyekuwa amekufa kisha akawa hai”
Tukiendelea kusoma;
Ufunuo 2: 9 “Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri) najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani. 10 Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima”.
Ufunuo 2: 9 “Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri) najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani.
10 Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima”.
Kumbuka neno “SMIRNA” tafsiri yake ni “(MANE MANE ILIYOSAGWA au CHUNGU)”. Hivyo kama jina lilivyo ndivyo kanisa lilivyokuwa, Hili kanisa lilipitia uchungu mwingi na mateso kutokana na IMANI yao. Kanisa hili lilianza mwaka 170WK na kuisha mwaka 312WK. Katikati ya hichi kipindi maelfu ya wakristo waliuliwa kwa kuingizwa magerezani, wengine walitupwa kwenye matundu ya simba, wengine waliburutwa,wanawake walikatwa matiti na kuachwa damu zichuruzike mpaka kufa, wengine walichomwa moto, wengine walisulibiwa n.k. Hivyo historia inarekodi walipitia dhiki nyingi sana kama vile tu Bwana alivyopitia akiwa hapa duniani. Na Bwana aliwaambia pia kuwa anajua UMASKINI wao, na dhiki yao lakini ni matajiri.
Ni kweli watakatifu wa wakati huo wa kanisa la Smirna walikuwa ni maskini, lakini mbele za Mungu walikuwa ni matajiri..Kama vile Bwana alivyokuwa duniani maskini lakini mbele za BABA alikuwa ni tajiri kuliko watu wote duniani. 2Wakorintho 8: 9 “Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake”. Vivyo hivyo na hawa watu wa hili kanisa hawakupenda maisha yao hata kufa kwa ajili ya BWANA. Walichekwa na kudharauliwa na kuonekana kama watu wasiostahili kuishi katikati ya jamii za watu wengine (Waebrania 11:38).
Tunaona pia Bwana aliwaambia ” huyo Ibilisi atawatupa baadhi yao gerezani ili wajaribiwe nao watakuwa na dhiki siku kumi “. Tunaona jambo hilo lilikuja kutimia katika utawala wa Rumi chini ya kiongozi mkatili aitwaye Diocletian ndani ya miaka 10 aliwaua maelfu ya wakristo katika magereza kuanzia mwaka 300WK hadi 310WK. (Hizo ndio zile siku 10 zilizozungumziwa na Bwana). Pamoja na hayo BWANA aliwaambia ” wawe waaminifu hata kufa, naye atawapa taji ya uzima. “..Haya ni maneno ya faraja kutoka kwa BWANA mwenyewe kwa watu wa kipindi kile ambapo Bwana alitumia kinywa cha IRENIO kama mjumbe wa kanisa hilo kuwafariji watakatifu na kuwarudisha kwenye Neno akiyapinga yale mafundisho ya Wanikolai ambayo tuliyoyaona katika lile kanisa la kwanza, na hapa Bwana anawaita sinagogi la shetani, wanajifanya kuwa watu wa Imani kumbe sio.
Kadhalika walikuwepo pia watu wengine waliokuwa waaminifu kama wakina Polycarp ambao Mungu aliwatumia pia kunyanyua imani za watu na kuwafariji kwa kufa vifo vya kishujaa kama Bwana.Waliishindania imani kwa nguvu zote katika kanisa hilo la Smirna.
Bwana alimalizia na kusema “11 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili. “. Hivyo Japo Bwana aliruhusu WAFE (wapate mauti ya kwanza ya mwili). Lakini aliwaahidia wale watakaoshinda kuwa hawatapatikana na mauti ya pili (Kifo cha Roho). Kumbuka mauti ya kwanza ni hii roho ya mtu kutenganishwa na mwili hivyo mwili unakuwa umekufa lakini roho ya yule mtu bado inaendelea kuishi. Sasa mauti ya pili ni roho inakufa kabisa kama vile mwili unavyokufa. Na hii inauliwa katika lile ziwa la moto tu. Na kama vile mauti ya kwanza inavyokuwa na uchungu, si zaidi sana mauti ya roho? itakuwa na uchungu mara nyingi zaidi.
Watu wa kanisa hilo walizingatia lile Neno Bwana alilosema katika Mathayo 10: 28 ” Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum”.
Unaona hapo, watu hawa japokuwa walikuwa ni maskini sana, watu wenye dhiki nyingi sana, mpaka kufikia wakati Bwana anawaambia “kifo kinakuja mbele” lakini hawakuikana IMANI, Walizidi kuishikilia imani mpaka kufa. Je! na sisi tunaweza tukawa kama hawa?. Jiulize leo hii unapopitia tabu kidogo, aidha magonjwa, au dhiki fulani unajitenga na Imani..Ujawezaje kupokea taji ya uzima . Na kuepuka madhara ya mauti ya pili? siku ile Bwana atakapokuja? .
Huu ni wakati wa kujihakiki na kujiweka sawa, ili wakati wa kujaribiwa utakapofika tuweze kuwa imara, kama Bwana wetu YESU KRISTO aliyapitia hayo, na watakatifu wake wa kanisa la mwanzo, kadhalika sisi nasi siku yatakapotujia hayo yatupasa tuyashinde kama Bwana.
Tafadhali share ujumbe huu kwa wengine na Mungu atakubariki. Kwa Mwendelezo >>> Ufunuo: Mlango wa 2 Part 3
JE! UKRISTO UNAMPA MTU DHAMANA YA KUWA TAJIRI?
NJIA YA ‘UTAJIRI MKUU’ KWA KIJANA NI IPI?
“HERI WALIO MASKINI WA ROHO” JE HATUNA RUHUSA YA KUWA MATAJIRI WA ROHO?
(Sehemu ya kwanza)
Jina kuu la BWANA wetu YESU KRISTO litukuzwe milele yote. Karibu katika mwendelezo wa uchambuzi wa kitabu cha Ufunuo, Leo tutaitazama ile sura ya pili. Kama tulivyotangulia kusoma katika ile sura ya kwanza, Tuliona Yohana akionyeshwa Sura na umbo la YESU KRISTO , na wasifa wake ambao alionyeshwa kwa lugha ya picha,(Kumbuka Bwana Yesu kiuhalisia hana muonekano kama ule), jinsi alivyokuwa anaonekana na nywele nyeupe kama sufu, macho ya moto, miguu ya shaba, upanga unaotoka kinywani mwake, mwenye sauti kama maji mengi, aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu n.k. hizo zote zilisimama kama viashiria (Nembo) vya tabia yake, ambayo kila moja ina nafasi yake katika hichi kitabu cha Ufunuo na ndio maana zilitangulizwa kuelezwa mwanzoni kabisa mwa kitabu hichi.
Hivyo katika sura ile ya kwanza mwishoni tuliona jinsi Yohana anaambiwa ayaandike yale aliyoyaona na ayapeleke kwa yale makanisa saba.
Ufunuo 1: 19 Basi, uyaandike mambo hayo uliyoyaona, nayo yaliyopo, na yale yatakayokuwa baada ya hayo.
20 Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhahabu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba; na vile vinara saba ni makanisa saba.”
Ni muhimu kufahamu Barua hizi Yohana alizopewa hazikuyahusu tu yale makanisa 7 yaliyokuwa Asia ndogo kwa wakati ule, bali pia na kwa makanisa yatakayokuja huko mbeleni na ndio maana hapa anaambiwa ayaandike mambo hayo YALIYOPO na YATAKAYOKUJA baada ya hayo. Ikiwa na maana kuwa yale yaliyoko ndio yale makanisa 7 yaliyokuwa Asia katika wakati wa Yohana, na yale yatakayokuja ni Makanisa 7 tuliopo sisi baada ya Yohana kuondoka. Kwahiyo Tunaposoma leo hii kitabu cha ufunuo tunajua kuwa yale makanisa 7 yaliyokuwa katika kipindi cha Yohana yameshapita. Na tangu kipindi cha Bwana YESU kuondoka hadi sasa ni takribani miaka 2,000 na kanisa la Kristo limekuwa likipita katika vipindi tofauti tofauti saba ndani ya huo muda wa miaka 2000, vijulikanavyo kama NYAKATI SABA ZA KANISA.
Sasa tukirudi katika sura ya pili. Tunaona Bwana Yesu akianza kutoa ujumbe kwa kanisa moja baada ya lingine, Kuanzia kanisa la Efeso mpaka Laodikia ambalo ndio la mwisho. Tunasoma;
KANISA LA EFESO:
Ufunuo 2:1 “Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika; Haya ndiyo anenayo yeye azishikaye hizo nyota saba katika mkono wake wa kuume, yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu”.
Awali ya yote tunaona Bwana Yesu anajitambulisha hapa kama “yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu na aliyeshika zile nyota saba”. Kumbuka hapa hajajitambulisha yeye kama yeye mwenye macho ya moto au uso ung’aao kama jua. Lakini alisema yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu ikiwa na maana kuwa uelekeo wake wote utakuwa katika kuchunguza kinara cha hilo kanisa na yale makanisa mengine. Kumbuka kinara ni taa iliyokuwa inawekwa katika nyumba ya Mungu (Hekaluni) Kwa ajili ya kutia Nuru kule ndani (Patakatifu) ili shughuli za kikuhani ziende sawasawa (Kutoka 27:20), na kilikuwa hakizimwi muda wote, sharti ni lazima kimulike daima usiku na mchana pasipo kuzimwa. Vivyo hivyo hapa Bwana alipoanza kwa kujitambulisha hivyo alikuwa anatazamia nuru isiyozimika ndani ya hilo kanisa husika (nyumba yake) ambalo analitolea habari zake hapo chini.
Na NURU hii ni ipi Bwana aliyokuwa aliitazamia kuiona inaangaza?. Biblia inatuambia
1Yohana 2: 8 Tena nawaandikia amri mpya, neno lililo kweli ndani yake na ndani yenu; kwa kuwa giza linapita na ile nuru ya kweli imekwisha kung’aa.
9 Yeye asemaye kwamba yumo NURUNI, naye amchukia ndugu yake, yumo gizani hata sasa.
10 Yeye ampendaye ndugu yake, akaa katika nuru, wala ndani yake hamna kikwazo.
11 Bali yeye amchukiaye ndugu yake, yu katika giza, tena anakwenda katika giza, wala hajui aendako, kwa sababu giza imempofusha macho.
Na pia tukisoma 1Wakorintho 13 inasema Upendo huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahimili yote, Upendo haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli n;k. Hivyo kwa ujumla NURU ni UPENDO. Ambao huo unaanza kwanza kwa KUMPENDA BWANA MUNGU WAKO kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote,na kwa nguvu zako zote, (Kwa kuzishika na kuzifuata amri zake) na pia kumpenda jirani yako kama nafsi yako. Kwa kuzingatia hayo mawili KINARA CHAKO kitakuwa kinatoa Nuru ya kutosha.
Sasa tukirudi katika Kanisa lile la EFESO, tunaona Bwana aliendelea kulitolea habari zake na kusema:
Ufunuo 2:2-5 “Nayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio, ukawaona kuwa waongo; 3 tena ulikuwa na subira na kuvumilia kwa ajili ya jina langu, wala hukuchoka. 4 Lakini nina neno juu yako, ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza. 5 Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu. 6 Lakini unalo neno hili, kwamba wayachukia matendo ya Wanikolai, ambayo na mimi nayachukia.”
3 tena ulikuwa na subira na kuvumilia kwa ajili ya jina langu, wala hukuchoka.
4 Lakini nina neno juu yako, ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza.
5 Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu.
6 Lakini unalo neno hili, kwamba wayachukia matendo ya Wanikolai, ambayo na mimi nayachukia.”
Kwanza kabisa maana ya neno EFESO ni “Kuacha mema yaondoke”. Hivyo hili kanisa kama jina lake lilivyo mwanzoni lilianza kuenenda katika Nuru ya Neno ambao ni UPENDO wa kiungu, lilikuwa japokuwa linapitia majaribu mengi liliendelea kumpenda Mungu, lilivumilia mabaya,Hii tunaona katika utawala wa Rumi chini ya kiongozi mkatili Nero, aliyewaua wakristo wengi wakati ule kwa kuwasingizia kuwa wameuchoma mji na hali sio wao. Kanisa hili pia mwanzoni lilijiweka katika utakatifu wa hali ya juu, liliwapima manabii wa uongo na kugundua kuwa sio, kwa muda mrefu sana. Walikuwa na uwezo pia wa kuyagundua matendo ya WANIKOLAI na kuyapinga katikati ya Kanisa. Kumbuka neno “Nikolai” tafsiri yake ni “Kuteka madhabahu” Hivyo kulikuwa na tabia zilizokuwa zimeanza kujitokeza katikati ya baadhi ya makanisa, watu(wasio wa Mungu) walianza kijipachikia vyeo vilivyoua uongozi wa Roho Mtakatifu. kwamfano watu badala ya kwenda kumuomba Mungu msamaha, walianza kuwafuata wanadamu wenzao wawaombee au wawaondolee dhambi zao kwa niaba ya Mungu, Badala karama za roho ziongoze kanisa, vyeo vya kibinadamu vikaanza kuongoza kanisa n.k. Huku ndiko kuteka madhabahu na hayo ndiyo yaliyokuwa matendo ya Wanikolai, ambayo kanisa la Kristo la kweli lilichukizwa nayo na Bwana vilevile.
Lakini Kanisa hili la Efeso lilifikia kipindi ule upendo waliokuwa nao hapo kwanza ukaanza kupoa (wakaanza kuacha mema yaondoke katikati yao kama vile Jina la kanisa lao lilivyo), uvumilifu kwa ajili Imani, utakatifu na subira vikaanza kupoa, zamani walikuwa wanawajaribu manabii wa uongo na kuwaondoa katikati yao lakini sasa hawafanyi hivyo tena.. Na ndio maana Bwana hapa anatokea na kuanza kukichunguza kinara chao na kuwaambia NURU yao imeanza kufifia na kukaribia kuzima Ukiendelea kusoma utaona Bwana anawaambia watubu
” 5 Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye MATENDO YA KWANZA. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu.”
Kama tulivyoona Pale mwanzoni katika ile sura ya kwanza juu ya ule mwonekano wake, jinsi alivyoonekana akipita katikati ya vile vinara vya taa, ikiwa na maana kuwa anapeleleza na kufanya masahihisho, kinara kilichofifia na kukaribia kuzima anakiondoa na kile kinachozidi kuwaka anakiongezea nuru, kwasababu biblia inasema “mwenye nacho ataongezewa asiye nacho hata kile kidogo alicho nacho atanyang’anywa” Hivyo kama wasingeimarisha matendo yao, hata ile nuru waliyokuwa nayo kidogo ingeondolewa kwao. Na ile taabu yao ya mwanzo waliyoisumbukia ingekuwa ni sawa na bure.
Sasa kanisa hili la Efeso lenye tabia hizi lilianza kati ya kipindi cha 53WK hadi mwaka 170WK. Na Malaika wa kanisa hilo alikuwa ni Mtume Paulo. Kumbuka Neno “malaika” tafsiri yake ni “mjumbe” hivyo wapo wajumbe wa kimbinguni(ndio malaika wa rohoni) na wapo wajumbe wa duniani. Hawa wanaotajwa katikati ya haya makanisa saba ni wajumbe wa kiduniani (yaani wanadamu). Kwahiyo malaika wa Kanisa hili la Efeso alikuwa ni Mtume Paulo. Kwasababu yeye ndiye mtume aliyepewa neema ya kupeleka Injili kwa mataifa. Na mafunuo mengi aliyopewa yalikuwa ni msingi katika makanisa ya wakati ule, na hata sasa.
Kadhalika na sisi tuliopo katika Kanisa la mwisho (Laodikia) ambalo tutakuja kusoma habari zake hapo baadaye na sisi pia tunaonywa tusipotubu kinara chetu kitaondolewa.. Kumbuka BWANA pale anaonekana akipita katikati ya vile vinara saba na sio “Kinara kimoja“. Hivyo anavichunguza vyote kuanzia cha kwanza mpaka cha mwisho. Na kama asipoiona ile nuru aliyoikusudia iwepo katika kinara chetu vile vile kitaondolewa.. Na tunafahamu madhara ya Nuru kuondolewa, anamaanisha giza linaachiliwa liingie ndani yako.
Ndugu Mwanzoni ulipoanza kuamini ulikuwa mtakatifu lakini sasa hivi utakatifu wako umepoa, ulikuwa unasali, ulikuwa unavaa vizuri, ulikuwa na huruma kwa ndugu, ulikuwa na upendo, ulikuwa na uvumilivu juu ya imani yako hata kama watu wanaokuzunguka wanakudhihaki, ulikuwa huwezi kuabudu sanamu au kuchukuliana na mafundisho ya uongo lakini sasahivi unayapokea mafundisho ya uongo na kuyafurahia, Injili zisizokufanya utazama ufalme wa mbingu ndio unazozipenda, huwezi tena kusali, kujisitiri huwezi tena, hukutazamii tena kuja kwa Bwana umechoka na kuishiwa nguvu. Hizo ni dalili za Kinara chako kuzima..Jitahidi kabla hakijaondolewa. Maana siku kitakapoondolewa ndugu hali yako ya mwisho itakuwa mbaya kuliko ile ya kwanza. Ule upendo uliokuwa nao kwanza wa Mungu unaondoka kabisa ndani yako, unafanana tena na watu wasiomjua Mungu, au unakua kama vile mtu ambaye hajawahi kumjua Mungu kabisa.
Hivyo tujitahidi na sisi TAA zetu ziwe zinawaka katika hizi siku za kumalizia kwasababu Bwana hivi karibuni anarudi.. yeye mwenyewe alisema; katika Luka 12: 35 Viuno vyenu na viwe vimefungwa, na TAA ZENU ZIWE ZINAWAKA; 36 nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao, atakaporudi kutoka arusini, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara.”
Endelea hapo chini sehemu ya pili ya sura hii ya pili ya kitabu cha Ufunuo,.ambapo tutakuja kuona ujumbe wa kanisa la pili (SMIRNA).
Tafadhali “Share” kwa wengine ujumbe huu na Mungu atakubariki.
1.Ufunuo: Mlango wa 2: Sehemu ya 2
Jina la BWANA wetu YESU KRISTO lihimidiwe daima. Karibu katika uchambuzi wa kitabu cha Ufunuo leo tukianza na ile sura ya kwanza.; Tunasoma…
“1 Ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi; naye akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumwa wake Yohana; 2 aliyelishuhudia Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu Kristo, yaani, mambo yote aliyoyaona.”
“1 Ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi; naye akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumwa wake Yohana;
2 aliyelishuhudia Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu Kristo, yaani, mambo yote aliyoyaona.”
Awali ya yote tunaona hapa Yohana akiandika na kusema “Ufunuo wa Yesu Kristo” akimaanisha kuwa alichokipokea sio ufunuo wake bali ni wa Yesu mwenyewe. Kumbuka Yohana ndiye Mtume pekee aliyekuwa karibu sana na Bwana, na aliyependwa na Bwana kuliko mitume wote, Kiasi kwamba hata siri za karibu sana za Bwana alikuwa anazipokea kwanza yeye ndiye ndipo wengine wafuate, ni mtume pekee aliyekuwa akiegema kifuani mwa Bwana muda wote (Yohana 13:23, na Yohana 21:20), Na ndio maana tunaona wakati ule wa jioni wa kuumega mkate, Bwana aliposema mmoja wenu atanisaliti, Petro alimpungia mkono Yohana amuulize Bwana ni nani atakayemsaliti, na Bwana akamfunulia Yohana ni yule atakaye mmegea tonge na kumpa, kwasababu Petro alijua Yohana ndiye kipenzi wa Bwana.
Kwasababu ya uhusiano wake wa kipekee na Bwana, ilimpelekea, mpaka kufikia hatua ya kupewa neema hii ya MAFUNUO na Bwana mwenyewe, mambo ambayo yatakuja kutokea katika siku zake na siku za mwisho. Yohana ni mfano wa Danieli ambaye naye alikuwa ni mtu aliyependwa sana na Mungu, Ikapelekea yeye naye kupewa mafunuo yanayofanana na ya Yohana. Kwahiyo kama ukichunguza utagundua watu wanaofunuliwa Mafunuo makuu kama haya sio tu kila mkristo, au mwamini yoyote bali ni mtu yule anayependezwa na Mungu, Vivyo hivyo na sisi tukimpendeza Bwana atatupa siri zake za ndani zaidi.
Mstari wa 3 unasema; “Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu”. Hapa Biblia inasema heri ikiwa na maana kuwa amebarikiwa mtu yule ASOMAYE, ASIKIAYE, na AYASHIKAYE ..Na kusikiwa kunakozungumziwa hapo ni kusikia kwa masikio ya ndani (yaani kupata Ufunuo ) na sio masikio ya nje, na kuyashika ikimaanisha kuyaishi uliyoyasikia. Hivyo Mtu yeyote afanye hivyo biblia inasema amebarikiwa. Kumbuka Si watu wote wanapata neema hii ya kukielewa kitabu hichi, kwasababu ni kitabu kilichofungwa hivyo kinahitaji kufunguliwa na Roho mwenyewe. Kwahiyo kama wewe umepata neema, jitahidi kuyaishi yaliyoandikwa humo ili na wewe uitwe HERI.
Tukiendelea mistari inayofuata;
“4 Yohana, kwa yale makanisa saba yaliyoko Asia; Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwake yeye aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja; na zitokazo kwa roho saba walioko mbele ya kiti chake cha enzi; 5 tena zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi aliye mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake, 6 na kutufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa Mungu, naye ni Baba yake; utukufu na ukuu una Yeye hata milele na milele. Amina”.
“4 Yohana, kwa yale makanisa saba yaliyoko Asia; Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwake yeye aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja; na zitokazo kwa roho saba walioko mbele ya kiti chake cha enzi;
5 tena zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi aliye mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake,
6 na kutufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa Mungu, naye ni Baba yake; utukufu na ukuu una Yeye hata milele na milele. Amina”.
Tunasoma hapa Yohana anaanza na salamu kwa yale makanisa 7 aliyopewa kuyaandikia maneno hayo. Anasema neema iwe kwenu na amani zitokazo kwa yeye “aliyekuwako, aliyeko na atakayekuja”, Hii inafunua umilele wa Mungu Elohimu, Yeye pekee ndiye asiyekuwa na mwanzo wala mwisho. Tena zitokazo kwa Roho saba walioko mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Sasa kumbuka Mungu hana Roho 7, Tunajua wote Mungu mwenyewe ni Roho(1),na nafsi moja, hapo anaposema hapa roho 7 haina maana kuwa anazo roho 7, bali anaonyesha jinsi Roho ya Mungu ilivyokuwa inatenda kazi katika yale makanisa 7 ambayo tutasoma habari zake hapo baadaye. Na pia anasema Neema na Amani zitakazo kwa Yesu Kristo aliyeshahidi mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa. Kama tunavyojua Mungu alitoka katika UMILELE akaingia katika MUDA ili kumkomboa mwanadamu. Hivyo akauandaa mwili ili akae ndani yake. Na huo mwili ukawa YESU.
Kwahiyo Mungu alikuwa ndani ya Yesu akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake (2Wakorintho 5:18-19). Kwahiyo hapa haizungumzii UTATU, hapana Mungu ni mmoja anayo nafsi moja, na Roho moja. Kwa mfano mimi ninaweza kuzungumza na wewe kwa kutumia account ya facebook, yenye jina, picha na utambulisho wangu. Ninazungumza, ninaongea na wewe ninajibu maswali, lakini haimaanishi sisi tupo wawili. kwamba wa kwanza ni mimi na wapili yule wa mtandaoni hapana mimi ni yule yule mmoja isipokuwa nimeingia ndani ya facebook ili nikutane na jamii ya watu fulani. vivyo hivyo na Mungu ambaye hana mwanzo wala mwisho aliingia ndani ya mwili wa kibinadamu (1Timotheo 3:16) ili tu kutupata sisi wanadamu..Na kama vile ile account yangu siku moja ilikuwa na mwanzo wake vivyo hivyo Bwana Yesu alikuwa na mwanzo, na ndio maana utakuja kuona kuna mahali anasema yeye ni ALFA NA OMEGA. Lakini haimaanishi kuwa Mungu (ELOHIM) ana mwanzo na mwisho…hapana Yeye hana mwanzo wala mwisho, kwasababu yeye ndio mwanzo na ndio mwisho.
“7 Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina. 8 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi”.
“7 Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina.
8 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi”.
Sasa Biblia inasema upo wakati Bwana aliouweka wa yeye kurudi tena ambao kila jicho litamwona na hao waliomchoma mkuki pale Kalvari (yaani wayahudi na watu wa mataifa) watamwombolezea, kumbuka hapa sio ule wakati wa kulichukua kanisa lake, hapana bali utakuwa ni ujio wa Bwana Yesu kuja duniani na watakatifu wake waliokuwa wameshanyakuliwa muda wa miaka 7 iliyopita tangu tukio hilo litokee. Hapo ndipo kila jicho la watu waliosalia ambao majina yao hayakuandikwa katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu watamwona na kumuombolezea..
Mathayo 24: 29 “
Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika; 30 ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi. (soma pia Yuda 1:14 na Ufunuo 19:11-21,)
Tukiendelea mistari inayofuata….
” 9 Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika MATESO na UFALME na SUBIRA ya Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu. 10 Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu, 11 ikisema, Haya uyaonayo uyaandike katika chuo, ukayapeleke kwa hayo makanisa saba: Efeso, na Smirna, na Pergamo, na Thiatira, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.”
” 9 Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika MATESO na UFALME na SUBIRA ya Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu.
10 Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu,
11 ikisema, Haya uyaonayo uyaandike katika chuo, ukayapeleke kwa hayo makanisa saba: Efeso, na Smirna, na Pergamo, na Thiatira, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.”
Yohana anasema “mimi ndugu yenu mwenye kushiriki pamoja nanyi”…Ikiwa na maana kuwa kile alichokuwa anakipitia, ndugu wengine walikuwa wanakipitia pia.mateso, dhiki,vifungo, na subira ya Yesu Kristo. Hii inaonyesha kabisa mojawapo ya utambulisho wa mkristo kwamba yupo katika safari ya Imani ni kupitia hayo kwa ajili ya Bwana.(Kumbuka ni kwa ajili ya Bwana, na si kwasababu nyingine zozote)
Lakini tunapokuwa wakristo lakini hatuna subira, kwa ajili ya Bwana, inaonyesha kabisa hatupo miongoni mwa hao ndugu waaminio.. Yohana anasema alikuwa katika kisiwa kiitwacho PATMO.Hichi ni kisiwa kilichokuwa maeneo ambayo sio mbali sana na yale makanisa 7 yaliyokuwepo Asia ndogo (ambayo kwasasa ni maeneo ya UTURUKI) umbali wa takribani km 60-120.
Ni kisiwa ambacho wafungwa walikuwa wanaenda kuachwa huko wafe, ni kisiwa kilichokuwa na mawe mawe tu, mijusi nyoka na kenge, na nge. Hakuna mimea kumezungukwa na maji kote, hivyo ni mahali pasipokuwa na jinsi yoyote ya kuishi au kutoroka mtu utaishia kufa kwa njaa au kuuawa na wanyama wakali. Hivyo Yohana naye alitupwa kule kama mmojawapo wa wafungwa. Na ndipo huko huko Bwana akamfunulia mambo ya siri kama tunavyoyasoma. Nasi pia tunajifunza wakati mwingine tukitupwa katika majaribu mazito (maadamu ni wakristo) tujue ni Bwana anaruhusu mwenyewe ili kutupa mafunuo zaidi.
Hivyo maono hayo Yohana aliyoonyeshwa hayakuwa ndani ya siku moja yote..Bali ulikuwa ni mfululizo wa maono kwa kipindi cha muda fulani.Ndipo akapewa maagizo kwamba ayaandike mambo yote anayoyaona na ayapeleke kwa yale makanisa saba yaliyopo Asia, yaani Efeso, na Smirna, na Pergamo, na Thiatira, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.
MTU MFANO WA MWANADAMU.
“12 Nikageuka niione ile sauti iliyosema nami. Na nilipogeuka, niliona vinara vya taa saba vya dhahabu; 13 na katikati ya vile vinara nikaona mtu mfano wa Mwanadamu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu matitini. 14 Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe, kama theluji; na macho yake kama mwali wa moto; 15 na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti yake kama sauti ya maji mengi”.
Tunaona Yohana alipogeuka aisikie ile sauti akaona mtu “MFANO” wa mwanadamu. aliyevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu matitini. Kumbuka Yohana kuonyeshwa vile haikuwa na maana kuwa Bwana Yesu anataka kuonyesha mwili wake jinsi ulivyo na utukufu au unavyotisha mbele za wanadamu, hapana, bali kila kitu alichokuwa anakiona katika mwili wake kilikuwa kina maana fulani.. Kumbuka lile lilikuwa ni ONO sio kitu halisi.
Tukisoma tunaona Mtu yule alikuwa na nywele kama sufu nyeupe. Ikiashiria kuwa ni HAKIMU. (Kumbuka mahakimu huwa ni desturi yao kuvaa wigi nyeupe kichwani) Hivyo yule ni Muhukumu wa mambo yote, na weupe wake inaashiria usafi na haki ya hukumu yake. Atakapokuja kuketi katika kiti chake cha enzi cheupe, atawahukumu kwa haki watu wote. Tutakuja kuona vizuri katika sura 20.
Na pia mtu huyu alionekana ana macho kama mwali wa moto, na miguu iliyosuguliwa kama shaba. Ikifunua hukumu yake juu ya waovu katika kanisa na wasiomcha yeye ulimwenguni kote,.Kumbuka na macho kazi yake ni kuona, na miguu ni kukanyaga. Hivyo anapoonekana na macho ya moto inamaanisha kuwa anaona mambo yote yanayopaswa kuhukumiwa kwa moto. Tutakuja kuona pia katika kanisa la tatu la Thiatira (jinsi Bwana alivyojionyesha kwao kama miale ya moto na miguu ya shaba, kutokana na maovu yaliyojificha ndani ya kanisa hilo,).
Na kama miguu yake ilivyokuwa ya SHABA atakanyaga mambo yote maovu ndani ya kanisa lake kwanza kisha baadaye atamalizia na kwa ulimwengu mzima tutakapofika katika sura ya 14 tutaona pia jinsi atakavyokuja kukanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu mwenyezi (Ufunuo 19:15).
Tukizidi kuendelea kusoma mistari inayofuata..;
“16 Naye alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume; na upanga mkali, wenye makali kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua liking’aa kwa nguvu zake. 17 Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho, 18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu. 19 Basi, uyaandike mambo hayo uliyoyaona, nayo yaliyopo, na yale yatakayokuwa baada ya hayo. 20 Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhahabu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba; na vile vinara saba ni makanisa saba”.
“16 Naye alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume; na upanga mkali, wenye makali kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua liking’aa kwa nguvu zake.
17 Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,
18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu. 19 Basi, uyaandike mambo hayo uliyoyaona, nayo yaliyopo, na yale yatakayokuwa baada ya hayo.
20 Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhahabu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba; na vile vinara saba ni makanisa saba”.
Tunaona pia mtu huyu anaonekana akiwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume. Hizi nyota saba tafsiri yake kama inavyoelezwa ni malaika saba, mkono tunajua kazi yake ni kubeba, na ukiwa wa kuume, inamaana unabeba kitu stahiki, hivyo wale malaika (wajumbe 7) watakuwa wamebeba ujumbe stahiki kwa kanisa husika. na pia alionekana akitembea katikati ya vile vinara 7 vya taa ambavyo ndiyo yale makanisa 7. Jiulize ni kwanini hakuonekana akiwa katikati ya madhabahu, au katika birika ya shaba Katika Hekalu la Mungu?, bali anaonekana katikati ya vile vinara 7 vya Taa akitembea katikati yake?. Inamaana kuwa makao yake ni katikati ya yale makanisa saba. Huko ndipo jicho lake lilipo na Roho yake ilipo.
Mtu huyu pia alionekana na Upanga mkali ukatao kuwili unaotoka kinywani mwake. Kwa kawaida mtu hawezi kutoa upanga mdomoni, Tunafahamu Neno la Mungu ndio upanga wa Roho (soma waefeso 6:17) na pia waebrania 4: 12 inasema …“Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo”.
Hivyo upanga huo ambao ni NENO lake ameuandaa tayari kwa ajili ya vita kwa watu wote wanaokwenda kinyume na mapenzi ya Mungu. Na kama anavyosema ni upanga ukatao kuwili anamaanisha kuwa ni upanga unaokata pande zote yaani watu walioko ndani ya kanisa na watu walioko nje ya Kanisa.
Jambo hili tutakuja kuliona jinsi Bwana alivyojifunua kwao(Kanisa la pili Pergamo) kwamba yeye ndiye mwenye ule upanga mkali ukatao kuwili…aliasema “anayajua matendo yao na kwamba watubu na wasipotubu atakuja kufanya vita nao kwa huo upanga wa kinywa chake.(Ufunuo 2:16).
Kadhalika na kwa watu wa mataifa wasiomjua Mungu wao nao Bwana atakuja kufanya nao vita kwa huo upanga, jambo hili tutakuja kuliona katika ile sura ya 19:15 katika siku ile atakapokuja mara ya pili na watakatifu wake.
Utaona pia baada ya Yohana kuuona muonekana wa nje wa yule mtu alianguka chini kwa hofu na kutetemeka, Tunasoma ” 17 Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho, 18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu. “
Ndipo baada ya hayo yule mtu akajitambulisha kwa tabia zake za ndani ambazo Yohana hakuziona kwa macho..nazo ni
1)yeye ni wa kwanza na wa mwisho,
2) aliye hai,aliyekuwa amekufa na sasa yu hai milele na milele na ambaye
3) anazo funguo za Kuzimu.
Sasa kwa tabia hizo TATU Yohana ndipo alipojua kuwa yule MTU ni YESU KRISTO mwenyewe. Hivyo ule muonekano wa Nje ni msingi utakaotusaidi kuelezea ujumbe na kuelewa utendaji kazi wa Yesu katika habari husika zinazofuata. Ni muhimu kuzingatia hivyo vipengele, mfano tunaweza kuona katika kila kanisa anaanza kwa kujitambulisha kwa kipengele kimoja wapo cha mwili wake au tabia zake.
Hivyo kwa ufupi Alichoonyeshwa Yohana ni mfano wa ile sanamu aliyoonyeshwa Nebukadreza juu ya zile Falme 4 zitakazokuja kutawala mpaka mwisho wa dunia. Na kwamba kila sehemu ya ile sanamu (Kichwa cha dhahabu, kifua cha fedha, kiuno cha shaba na miguu ya chuma) ilikuwa na maana, na ndio iliyounda msingi wa kuelewa undani wa kitabu cha Danieli katika sura za mbeleni.Kadhalika na hichi kitabu cha Ufunuo, sura hii ya kwanza (Ambayo Inayoonyesha muonekano na tabia za Yesu Kristo ) ni msingi wa sisi kuelewa ujumbe katika sura zinazofuata za kitabu cha Ufunuo.
Hivyo usikose mwendelezo wa sura zinazofuata..
Ubarikiwe sana
Washirikishe na wengine habari hizi.
Kwa Mwendelezo >>Ufunuo: Mlango wa 2 Part 1.
KWANINI YESU KRISTO ALIKUJA DUNIANI?
SIFA TATU ZA MUNGU
JE! HIZI ROHO SABA ZA MUNGU NI ZIPI?
Jina la Bwana wetu YESU KRISTO libarikiwe sana. Karibu tuongeze maarifa katika kulichambua Neno la Mungu leo tutajifunza juu ya chukizo la uharibifu, natumai ujumbe huu utakutoa sehemu moja ya kiroho hadi nyingine, sasa ili tuweze kwenda kwa uzuri ni vema uwe na biblia pembeni ili kukusaidia kufuatilia baadhi ya mistari tutakayokuwa tunaipitia katika somo hili.
Kwa kuanza ni vizuri tukifahamu nini maana ya “chukizo la uharibifu”: Kwa lugha nyepesi tunaposema chukizo la uharibifu ni sawasawa na kusema “chukizo linaloleta uharibifu” au “Chukizo linalopelekea uharibifu”..Kwahiyo hapo kuna mambo mawili, la kwanza ni CHUKIZO, na la pili ni UHARIBIFU. Sasa chukizo ni nini? Na uharibifu ni nini?.
CHUKIZO: Kwa tafsiri ya kibiblia hilo neno chukizo maana yake ni kuudhi/kuleta hasira, hususani pale panapohusishwa na uzinzi, Hivyo mambo yote yaliyokuwa yanafanywa na watu wa Mungu ambayo yalikuwa kinyume na sheria zake mfano kuabudu miungu mingine, kujichongea sanamu, kufanya uchawi, n.k. hayo yote mbele za Mungu yalijulikana kama MACHUKIZO (mambo ya kuudhi au kukasirisha).
Kwa mfano tunaweza kuona Bwana aliwaambia wana wa Israeli katika Kumbukumbu 18: 9-13 akisema:
“9 Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako usijifunze kutenda kwa mfano wa MACHUKIZO ya mataifa yale. 10 Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, 11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu. 12 KWA MAANA MTU ATENDAYE HAYO NI CHUKIZO KWA BWANA; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako. 13 Uwe mkamilifu kwa Bwana, Mungu wako”.
“9 Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako usijifunze kutenda kwa mfano wa MACHUKIZO ya mataifa yale.
10 Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,
11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.
12 KWA MAANA MTU ATENDAYE HAYO NI CHUKIZO KWA BWANA; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako.
13 Uwe mkamilifu kwa Bwana, Mungu wako”.
Unaona hapo mambo waliowafanya wafukuzwe (“mataifa yaliyokuwa Kaanani”) na kuondoshwa kabisa ni MACHUKIZO yao mbele za Mungu, hivyo Mungu akatangulia kuwaonya mapema watu wake kwamba watakapofika katika hiyo nchi ya Ahadi wasijaribu kutenda mfano wa mambo hayo. Kwani Watu wa mataifa walikuwa wana loga, wanaabudu miungu mingi, wanaabudu masanamu, wanapitisha watoto wao kwenye moto, wauaji, n.k. Kwasababu hiyo basi wana wa Israeli walionywa sana wakae mbali na hivyo vitu, kwani vitawasababisha wao nao yawapate yale yale yaliyowapata mataifa mengine.
UHARIBIFU: Kama tulivyoona hapo juu, sababu kubwa iliyowapelekea mataifa yale makubwa yafukuzwe na KUHARIBIWA kabisa haikuwa kwasababu ya kwamba Mungu anawachukia tu!au anawapenda Israeli kuliko wao hapana bali ni kwasababu ya machukizo yao na ndiyo ikawapelekea kuharibiwa na kutolewa katika ile nchi ya Kaanani na kupewa wana wa Israeli. Na kama tunavyojua siku zote kitu kikiwa kinachukiza mara kwa mara kinachofuata ni kuangamizwa au KUHARIBIWA kabisa.
Bwana aliwaaonya tena wana wa Israeli na kusema:
Mambo ya walawi 18: 24 “Msijitie unajisi katika mambo hayo hata mojawapo; kwa maana hizo taifa nitakazozitoa mbele zenu zimekuwa najisi kwa mambo hayo yote;
25 na hiyo nchi imekuwa najisi; kwa ajili ya hayo naipatiliza uovu wake juu yake, na hiyo nchi yatapika wenyeji wake na kuwatoa. 26 Kwa hiyo mtazishika amri zangu na hukumu zangu, wala msifanye MACHUKIZO hayo mojawapo; yeye aliye mzalia, wala mgeni aketiye kati yenu; 27 (kwa kuwa hao watu wa nchi wameyafanya MACHUKIZO HAYA YOTE, hao waliotangulia mbele zenu, na hiyo nchi imekuwa najisi;) 28 ili kwamba hiyo nchi isiwatapike na ninyi pia, hapo mtakapoitia unajisi, kama ilivyoitapika hiyo taifa iliyotangulia mbele yenu. 29 KWANI MTU AWAYE YOTE ATAKAYEFANYA MACHUKIZO HAYO MOJAWAPO, NAFSI HIZO ZITAKAZOFANYA ZITAKATILIWA MBALI NA WATU WAO. 30 Kwa ajili ya hayo yashikeni mausia yangu, ili kwamba msifanye kabisa desturi hizi ZICHUKIZAZO mojawapo, zilizotangulia kufanywa mbele zenu, wala msijitie unajisi katika mambo hayo; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.”
25 na hiyo nchi imekuwa najisi; kwa ajili ya hayo naipatiliza uovu wake juu yake, na hiyo nchi yatapika wenyeji wake na kuwatoa.
26 Kwa hiyo mtazishika amri zangu na hukumu zangu, wala msifanye MACHUKIZO hayo mojawapo; yeye aliye mzalia, wala mgeni aketiye kati yenu;
27 (kwa kuwa hao watu wa nchi wameyafanya MACHUKIZO HAYA YOTE, hao waliotangulia mbele zenu, na hiyo nchi imekuwa najisi;)
28 ili kwamba hiyo nchi isiwatapike na ninyi pia, hapo mtakapoitia unajisi, kama ilivyoitapika hiyo taifa iliyotangulia mbele yenu.
29 KWANI MTU AWAYE YOTE ATAKAYEFANYA MACHUKIZO HAYO MOJAWAPO, NAFSI HIZO ZITAKAZOFANYA ZITAKATILIWA MBALI NA WATU WAO.
30 Kwa ajili ya hayo yashikeni mausia yangu, ili kwamba msifanye kabisa desturi hizi ZICHUKIZAZO mojawapo, zilizotangulia kufanywa mbele zenu, wala msijitie unajisi katika mambo hayo; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.”
Unaona hapo, machukizo yote yaliyokuwa yanazungumiziwa mwisho wake yote yalipelekea UHARIBIFU kwa namna moja au nyingine kwa hilo taifa au mtu mmoja mmoja aliyeyafanya.. Sasa kumbuka vitu hivi kama uchawi, ulawiti, uuaji, uongo n.k. haya yote yalikuwa ni machukizo yanayoleta uharibifu lakini LIPO CHUKIZO MOJA, lililozungumziwa na BWANA YESU, na katika kitabu cha DANIELI, ambalo litakuja kusimama sehemu patakatifu na kuleta uharibifu mkubwa kwa watu wengi wa Mungu litakalosababisha kuwepo na dhiki kubwa ambayo haijawaki kutokea tangu ulimwengu kuwako, na ndilo litakalopelekea hata uharibifu wa dunia.
Kumbuka wakati wana wa Israeli walipokuwa wanaingia katika nchi ya Kaanani, Mungu hakuteua mahali popote katikati ya miji yao pa kuliweka jina lake, na kuwa sehemu takatifu, hivyo wakati huo wote waisraeli walipokuwa wanafanya machukizo Bwana aliwaharibu mara nyingine kwa kuwatia katika mikono ya maadui zao kama wafilisti na walipotubu Bwana aliwanyanyulia waamuzi ambao waliwaokoa na mikono ya maadui zao lakini hawakuwa wanaondolewa taifa lao. Lakini ulipofika wakati Bwana alipojiteulia mahali PATAKATIFU pake pa kuwekea Jina lake yaani YERUSALEMU, zamani za mfalme Daudi, mambo yalianza kubadilika, siku ile HEKALU LA MUNGU lilipokamilika kujengwa kwa mikono ya Sulemani mwana wa Daudi, Baraka na bila kusahau LAANA pia ziliongezwa makali, Na ndio maana Bwana alimwambia Sulemani baada ya kuijenga ile nyumba maneno haya..
1Wafalme 9: 6 “Bali mkighairi, mkaacha kunifuata, ninyi na watoto wenu, msizishike sheria zangu na amri zangu, nilizoziweka mbele yenu, TENA MKIENDA NA KUITUMIKA MIUNGU MINGINE NA KUIABUDU, 7 BASI NITAWAKATILIA ISRAELI MBALI NA NCHI HII NILIYOWAPA na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaitupilia mbali na macho yangu, na Israeli watakuwa MITHALI NA NENO LA TUSI KATIKA MATAIFA YOTE. 8 Na ijapokuwa nyumba hii imetukuka namna hii, lakini kila apitaye atasituka na kuizomea; nao watasema, Kwa nini Bwana ameitenda nchi hii na nyumba hii mambo haya? 9 Na watu watajibu, Kwa sababu walimwacha Bwana, Mungu wao, aliyewatoa baba zao katika nchi ya Misri, wakashikamana na miungu mingine na kuiabudu na kuitumikia, basi ndiyo sababu Bwana ameleta mabaya haya yote juu yao”.
1Wafalme 9: 6 “Bali mkighairi, mkaacha kunifuata, ninyi na watoto wenu, msizishike sheria zangu na amri zangu, nilizoziweka mbele yenu, TENA MKIENDA NA KUITUMIKA MIUNGU MINGINE NA KUIABUDU,
7 BASI NITAWAKATILIA ISRAELI MBALI NA NCHI HII NILIYOWAPA na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaitupilia mbali na macho yangu, na Israeli watakuwa MITHALI NA NENO LA TUSI KATIKA MATAIFA YOTE.
8 Na ijapokuwa nyumba hii imetukuka namna hii, lakini kila apitaye atasituka na kuizomea; nao watasema, Kwa nini Bwana ameitenda nchi hii na nyumba hii mambo haya?
9 Na watu watajibu, Kwa sababu walimwacha Bwana, Mungu wao, aliyewatoa baba zao katika nchi ya Misri, wakashikamana na miungu mingine na kuiabudu na kuitumikia, basi ndiyo sababu Bwana ameleta mabaya haya yote juu yao”.
Unaona hapo?. Baada ya Mungu kuichagua YERUSALEMU, kama mahali pake patakatifu na HEKALU kama mahali atakapoweka Jina lake alitarajia muda wote Israeli wakae katika hali ya usafi wa hali ya juu kuliko hapo kwanza, kwamba wakifanya machukizo mbele za Patakatifu pa Mungu, wakatakatiliwa mbali, na kutawanywa katika mataifa yote, na watakuwa mithali kwa kila wawatazamao.
Lakini tukirudi katika kitabu cha Wafalme tunaona hawakuisikia hiyo sauti ya Mungu, badala ya kudumu katika usafi kwa Mungu wakaanza kidogo kidogo kuingiza ibada nyingine katika Israeli na katika nyumba ya Mungu iliyoko Yerusalemu, licha ya kwamba Mungu aliwatumia manabii wengi kuwaonya lakini hawakutaka kubadilika (Kuyaacha machukizo yao mbele za Mungu) ikapelekea Mungu kutamka UHARIBIFU WAO. Kama alivyoahidi katika NENO lake, pale Nebukadneza Mfalme wa Babeli Bwana alipomruhusu kwenda kuuteketeza mji wa Yerusalemu, na kuliharibu kabisa lile hekalu la Sulemani, wakauawa majemedari wengi wa Israeli kwa upanga, wengine njaa, na wengine magonjwa, Dhiki ilikuwa kubwa sana, wakachukuliwa utumwani na Israeli ikabaki kama ukiwa, Kutokana na MACHUKIZO waliyoyasimamisha wao wenyewe hivyo yakawapelekea UHARIBIFU MKUBWA namna hiyo.. Naamini kidogo kidogo utakua umeanza kuelewa nini maana ya chukizo la uharibifu.
2Mambo ya nyakati 36:14 “Na zaidi ya hayo wakuu wote wa makuhani, na watu, wakakosa mno sawasawa na MACHUKIZO YOTE YA MATAIFA; WAKAINAJISI NYUMBA YA BWANA ALIYOITAKASA KATIKA YERUSALEMU. 15 Naye Bwana, Mungu wa baba zao, akatuma kwao kwa mikono ya wajumbe wake, akiondoka mapema, na kutuma; kwa sababu aliwahurumia watu wake, na makao yake; 16 lakini waliwadhihaki wajumbe wa Mungu, na kuyadharau maneno yake, na kuwacheka manabii wake, HATA ILIPOZIDI GHADHABU YA BWANA JUU YA WATU WAKE, HATA KUSIWE NA KUPONYA. 17 Kwa hiyo akaleta juu yao mfalme wa Wakaldayo{Wa-babeli}, aliyewaua vijana wao kwa upanga nyumbani mwa patakatifu pao, asiwahurumie kijana wala mwanamwali, mzee wala mkongwe; akawatia wote mkononi mwake. 18 Na vyombo vyote vya nyumba ya Mungu, vikubwa kwa vidogo, na hazina za nyumba ya Bwana, na hazina za mfalme, na za wakuu wake; vyote pia akavileta Babeli. 19 WAKAITEKETEZA NYUMBA YA MUNGU, wakaubomoa ukuta wa Yerusalemu, wakayateketeza kwa moto majumba yake yote, WAKAVIHARIBU vyombo vyake vyote vya thamani. 20 Na wale waliookoka na upanga akawachukua mpaka Babeli; wakamtumikia yeye na wanawe hata kulipoingia milki ya Uajemi;
2Mambo ya nyakati 36:14 “Na zaidi ya hayo wakuu wote wa makuhani, na watu, wakakosa mno sawasawa na MACHUKIZO YOTE YA MATAIFA; WAKAINAJISI NYUMBA YA BWANA ALIYOITAKASA KATIKA YERUSALEMU.
15 Naye Bwana, Mungu wa baba zao, akatuma kwao kwa mikono ya wajumbe wake, akiondoka mapema, na kutuma; kwa sababu aliwahurumia watu wake, na makao yake;
16 lakini waliwadhihaki wajumbe wa Mungu, na kuyadharau maneno yake, na kuwacheka manabii wake, HATA ILIPOZIDI GHADHABU YA BWANA JUU YA WATU WAKE, HATA KUSIWE NA KUPONYA.
17 Kwa hiyo akaleta juu yao mfalme wa Wakaldayo{Wa-babeli}, aliyewaua vijana wao kwa upanga nyumbani mwa patakatifu pao, asiwahurumie kijana wala mwanamwali, mzee wala mkongwe; akawatia wote mkononi mwake.
18 Na vyombo vyote vya nyumba ya Mungu, vikubwa kwa vidogo, na hazina za nyumba ya Bwana, na hazina za mfalme, na za wakuu wake; vyote pia akavileta Babeli.
19 WAKAITEKETEZA NYUMBA YA MUNGU, wakaubomoa ukuta wa Yerusalemu, wakayateketeza kwa moto majumba yake yote, WAKAVIHARIBU vyombo vyake vyote vya thamani.
20 Na wale waliookoka na upanga akawachukua mpaka Babeli; wakamtumikia yeye na wanawe hata kulipoingia milki ya Uajemi;
Tukio hili lililiathiri Taifa la Israeli kwa vizazi vingi, Kama ukifuatilia historia utaona kuwa Israeli halikuwahi kuwa tena taifa huru kwa muda wa miaka 2500, tangu ule wakati walipopelekwa Babeli mpaka juzi juzi tu mwaka 1948, ndio wamekuwa taifa huru tena, siku zote hizo walikuwa wanaishi kama wageni mahali popote walipopelekwa au kukaa. Na hata walipotoka Babeli walikuwa chini ya mataifa yaliyokuwa yanamiliki dunia kwa wakati huo. Unaweza ukaona ni MACHUKIZO MAKUBWA kiasi gani yaliyowasababishia kupitia uharibifu na adhabu kali kaisi hicho… Mungu ni Mungu mwenye WIVU hapendi mahali pake patakatifu panajisiwe kwa namna yoyote ile..
Na tunaona baada ya kutoka Babeli, Bwana aliwarehemu akawajalia kujenga tena hekalu la pili baada ya lile la kwanza lililotengenezwa na Sulemani kubomolewa na mfalme Nebukadneza wa Babeli. Kadhalika Mungu aliwaonya pia yale masalia ya wayahudi waliorudi wasifanye machukizo kama waliyoyafanya mababa zao. Mwanzo walitii lakini kilipopita kipindi Fulani walikengeuka, wakaanza kufanya mfano wa machukizo ya mataifa. (Kumbuka wakati huu Israeli ilikuwa haijiongozi yenyewe kama hapo kwanza) ilikuwa chini ya utawala wa wafalme wengine. Hivyo njia pekee shetani aliyoitumia kusimamisha machukizo katika nyumba ya Mungu kiurahisi sio kuwatumia wayahudi peke yake, bali alianza kuwatumia pia wafalme wa mataifa kwasababu wao ndio waliokuwa na nguvu juu ya taifa la Israeli,
Tukisoma katika kitabu cha Danieli tunaona Danieli akionyeshwa katika maono juu ya mfalme atakayenyanyuka katika utawala wa Umedi & Uajemi ambao ndio kwa wakati huo ulikuwa unatawala dunia, alionyeshwa kiongozi mkatili akilisimamisha chukizo la uharibifu tena katikati ya wayahudi na patakatifu na huyu hakuwa mwingine zaidi ya ANTIOKIA IV EPIFANE (Kumbuka mpaka Antiokia kuja kulitia unajisi hekalu ilikuwa ni matokeo ya kukengeuka kwa wana wa Israeli,mfano wasingeasi Bwana angewaepusha na hayo mambo) Tukisoma
Danieli 11: 31 Na wenye silaha watasimama upande wake, nao watapatia unajisi mahali patakatifu, ndiyo ngome, nao wataondoa sadaka ya kuteketezwa ya kila siku, NAO WATALISIMAMISHA CHUKIZO LA UHARIBIFU..
Kulingana na historia inavyoeleza, kiongozi huyu alinyanyuka na kuingia katika hekalu la Mungu na kufanya maasi yote ambayo hayapaswi kuwepo katika nyumba ya Mungu, aliweza kusitisha sadaka zote za kuteketezwa ambazo zilikuwa zinafanywa na makuhani katika nyumba ya Mungu, na kuiweka sanamu ya ZEU mungu ambayo ilikuwa inamwakilisha yeye, kadhalika akawa anatoa dhabihu ya viumbe najisi kwa wayahudi kama nguruwe katika madhabahu iliyokuwa ndani ya Hekalu la Mungu na kuwalazimisha wanywe damu zao hivyo viumbe, mambo ambayo yalikatazwa katika Torati ya Musa, hakuishia hapo tu, aliwaua wayahudi wengi sana na kuwakosesha kuabudu katika dini yao, hivyo ikawa ni machukizo makubwa sana mbele za Mungu…Lakini Mungu alikuja kumuua Antiokia, kwa mambo hayo lakini hekalu halikubomolowa,(Ni sadaka tu ya kuteketezwa ndio iliyokomeshwa) kwahiyo kile kitendo cha yeye kwenda pale pamoja na majeshi yake na kutia unajisi patakatifu pa Mungu, ni CHUKIZO LA UHARIBIFU,.kama Danieli alivyolinena.
Sasa huyu Antiokia alikuwa anatimiza sehemu ya kwanza ya chukizo la uharibifu juu ya Hekalu la pili..Sehemu ya pili ambayo ilipelekea tena Uharibifu mkubwa mpaka Hekalu la Mungu kubomolewa na wana wa Israeli kutawanya katika mataifa yote ilitokea mwaka wa 70WK. Wakati jeshi la Rumi chini ya jenerali TITO alipouzunguka mji wa Yerusalemu na kuuchoma moto, na kulibomoa hekalu na kuliteketeza kabisa, na kuwatawanya wana wa Israeli kutoka katika nchi yao, hii ikawa ni mara ya pili ya hekalu la Mungu kuteketezwa baada ya lile la kwanza lililobomolewa na mfalme Nebkadreza wa Babeli.
Na kama vile lile la kwanza lilivyoteketezwa kwasababu ya maovu na maasi ya wana wa-israeli kadhalika na hili la pili lilibomolewa kwasababu hiyo hiyo,? Tunasoma wana wa Israeli walianza kwa kumkataa Yohana mbatizaji kisha wakaja kumkataa BWANA YESU mwenyewe, na kibaya zaidi wakamsulibisha, Bwana aliwaambia katika Yohana 8: 24 “Kwa hiyo naliwaambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu”..Na ni kweli hawakumsadiki Bwana, na ndio maana siku ile alipoukaribia mji wa Yerusaleu aliulilia na kusema.
Luka 19: 41 “Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia, 42 akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako. 43 Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote; 44 watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya kujiliwa kwako”.
Luka 19: 41 “Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia,
42 akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako.
43 Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote;
44 watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya kujiliwa kwako”.
Unaona hapo? Sababu ya kwanza iliyowapelekea wana wa Israeli mpaka kuharibiwa mji wao tena pamoja na Hekalu na jeshi la Rumi ni zile zile kwani waliwakataa manabii wa Mungu kwa kuwaua (soma Luka 13:34) na kuwasulibisha na zaidi ya yote walimkataa aliyemkuu wa uzima wakamkataa mfalme wao (ambaye ni Yesu) wakamkubali mfalme mwingine wa kidunia (KAISARI) na kumkiri hadharani kuwa huyo ndiye mfalme wao.
Yohana 19: 15 “Basi wale wakapiga kelele, Mwondoshe! Mwondoshe! Msulibishe! Pilato akawaambia, Je! Nimsulibishe mfalme wenu! Wakuu wa makuhani wakamjibu, Sisi hatuna mfalme ila Kaisari”.
Hivyo wakaendelea na maovu yao, pamoja na wafalme wao wa kipagani, Ndipo wakati wa mapatilizo ulipofika mji kuteketezwa na watu kuuawa na dhiki kubwa ikatokea. Lakini kabla ya huo wakati kufika Bwana alishawaonya wale waliokuwa tayari kumsikiliza kwamba watakapoona ishara Fulani (Yaani majeshi ya Rumi) kuuzunguka Yerusalemu waondoke katikati ya mipaka ya Yerusalemu. Hivyo wale waliomwamini Bwana Yesu na maneno yake (yaani Wakristo) waliepuka hiyo dhiki kwa kuondoka Yerusalemu lakini wale waliosalia waliangamia wote, Yerusalemu iligeuka kuwa ziwa la damu. Jeshi la Rumi liliwaua watu wote na kubomoa Hekalu la Mungu.
Na ndio maana Bwana alisema hivi.
Luka 21: 20 “Lakini, hapo mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, ndipo jueni ya kwamba UHARIBIFU wake umekaribia. 21 Ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani, na walio katikati yake wakimbilie nje, na walio katika mashamba wasiuingie. 22 Kwa kuwa siku hizo ndizo za mapatilizo, ili yatimizwe yote yaliyoandikwa. 23 Ole wao wenye mimba na wanaonyonyesha katika siku hizo! Kwa kuwa kutakuwa na shida nyingi katika nchi, na hasira juu ya taifa hili. 24 Wataanguka kwa ukali wa upanga, nao watatekwa nyara na kuchukuliwa katika mataifa yote; na Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hata majira ya Mataifa yatakapotimia”.
Luka 21: 20 “Lakini, hapo mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, ndipo jueni ya kwamba UHARIBIFU wake umekaribia.
21 Ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani, na walio katikati yake wakimbilie nje, na walio katika mashamba wasiuingie.
22 Kwa kuwa siku hizo ndizo za mapatilizo, ili yatimizwe yote yaliyoandikwa.
23 Ole wao wenye mimba na wanaonyonyesha katika siku hizo! Kwa kuwa kutakuwa na shida nyingi katika nchi, na hasira juu ya taifa hili.
24 Wataanguka kwa ukali wa upanga, nao watatekwa nyara na kuchukuliwa katika mataifa yote; na Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hata majira ya Mataifa yatakapotimia”.
Kwahiyo yale maasi waliokuwa wanayafanya katika (nyumba ya Mungu) pamoja na kuwaua manabii wa Mungu kadhalika na kumkataa Masihi wao, ndio lililokuwa CHUKIZO lililopelekea UHARIBIFU wao.
Baada ya hapo wayahudi wote walitapanywa katika mataifa mengi duniani, pasipo kuwa na makao maalumu kama hapo mwanzo, lakini tunaona Bwana aliwakumbuka tena, akawahurumia mwaka 1948, pale Mungu alipowarudishia taifa lao tena. Na sasa wameshaanza kujitambua wao ni wakina nani mbele za Mungu ile neema imeshaanza kuwarudia kidogo kidogo Hivi karibuni wataenda kujenga HEKALU LA TATU, na hili litakuwa ni la mwisho. Maandalizi yote ya kulijenga yapo tayari, kinachongojewa ni kujengwa tu, na zile dhabihu walizokuwa wanatoa kama zamani, zitaanza kutolewa tena. Na mahali patakatifu pa Mungu patawekwa wakfu tena, Na Mungu ataikumbuka Israeli tena kama zamani.
Lakini kumbuka shetani yupo katika kazi siku zote,..Alilokuwa analifanya nyuma ndilo atakalokuja kulifanya katika siku za mwisho, tena na zaidi ya pale. Kumbuka “machukizo ya uharibifu” yote ya nyuma yaliyotangulia yalikuwa ni kivuli tu cha CHUKIZO LA UHARIBIFU hasaa litakalokuja katika siku hizi za mwisho.
Bwana Yesu alisema katika Mathayo 24: 15 “Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (ASOMAYE NA AFAHAMU),
16 ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani; 17 naye aliye juu ya dari asishuke kuvichukua vitu vilivyomo nyumbani mwake; 18 wala aliye shambani asirudi nyuma kuichukua nguo yake. 19 Ole wao wenye mimba na wanyonyeshao siku hizo! 20 Ombeni, ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato. 21 KWA KUWA WAKATI HUO KUTAKUWAPO DHIKI KUBWA, AMBAYO HAIJATOKEA NAMNA YAKE TANGU MWANZO WA ULIMWENGU HATA SASA, WALA HAITAKAKUWAPO KAMWE.
16 ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani;
17 naye aliye juu ya dari asishuke kuvichukua vitu vilivyomo nyumbani mwake;
18 wala aliye shambani asirudi nyuma kuichukua nguo yake.
19 Ole wao wenye mimba na wanyonyeshao siku hizo!
20 Ombeni, ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato.
21 KWA KUWA WAKATI HUO KUTAKUWAPO DHIKI KUBWA, AMBAYO HAIJATOKEA NAMNA YAKE TANGU MWANZO WA ULIMWENGU HATA SASA, WALA HAITAKAKUWAPO KAMWE.
22 Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo”.
Kumbuka kutakuwepo CHUKIZO LA UHARIBIFU la tatu na la mwisho litakalokuja kusimamishwa huko Yerusalemu katika Hekalu la TATU. Wakati ule wana wa Israeli kwasababu ya makosa yao Ikasababisha Nebukadneza kuja kuliteketeza hekalu la kwanza, na kwasababu ya makosa yao tena ya kumkataa Masihi ndipo Jeshi la Rumi likaja kuuteketeza mji na Hekalu la pili. Kadhalika na kwa makosa yao tena ndiyo yatakayokuja kupelekea Mpinga-kristo kunyanyuka na kupatia unajisi patakatifu na kuleta uharibifu, pamoja na dhiki kuu katika hekalu la tatu.
Sasa kosa lenyewe litakuwa ni lipi?
Danieli alionyeshwa kosa hilo, tunasoma katika
Danieli 9:26 “27 NAYE {mpinga-kristo} ATAFANYA AGANO THABITI NA WATU WENGI KWA MUDA WA JUMA MOJA; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama CHUKIZO LA UHARIBIFU; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu”.
Kwahiyo unaona hapo kuna AGANO ambalo mpinga-kristo ataingia na watu wengi, na hawa watu si wengine zaidi ya wayahudi ambao wataingia agano hilo na huyu mpinga-kristo ambalo litakuwa kwa kipindi cha miaka 7, agano hili litahusisha kupewa nafasi mpinga-kristo katika Hekalu la Mungu, jambo ambalo Mungu alishalikataza kwamba kisionekane kitu chochote katika hekalu la Mungu isipokuwa wayahudi tu tena makuhani wa uzao wa Walawi, lakini hawa wayahudi baadhi watampa heshima mpinga kristo wakijua tu ni mtu anayeheshimika duniani, hivyo anastahili kuwa na sehemu katika hekalu la Mungu, kama tu wale wa wayahudi wa kipindi cha Bwana Yesu walivyompa Heshima Kaisari, lakini hawatajua kama Yule ndio mpinga-kristo mwenyewe (ambaye atakuwa ni PAPA wa wakati huo) , na hiyo itapelekea kuwa CHUKIZO KUU kuliko yote, na ndipo Mungu ataruhusu hili agano livunjwe, lakini Yule mpinga-kristo ataghadhibika na kuleta dhiki kuu, ambayo haijawahi kuwako tangu ulimwengu kuumbwa.
Na ndio maana biblia inamtaja..katika
2Thesalonike 2: 3 “Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi{MPINGA-KRISTO}, mwana wa uharibifu;
4 yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe KUKETI KATIKA HEKALU LA MUNGU, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu. 5 Je! Hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwapo pamoja nanyi naliwaambieni hayo? 6 Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake. 7 Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa.{kumbuka bibi-arusi wa Kristo ndiye azuiaye mpaka atakapoondolewa kwa kwenda kwenye unyakuo} 8 Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake; 9 yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo;
4 yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe KUKETI KATIKA HEKALU LA MUNGU, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.
5 Je! Hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwapo pamoja nanyi naliwaambieni hayo?
6 Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake.
7 Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa.{kumbuka bibi-arusi wa Kristo ndiye azuiaye mpaka atakapoondolewa kwa kwenda kwenye unyakuo}
8 Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake;
9 yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo;
10 na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa”.
Hivyo huyu mpinga-kristo ataleta dhiki duniani kwa kuihimiza chapa ya mnyama kutenda kazi,ataua wayahudi wengi sana, japokuwa sio wote kwasababu wapo ambao wataiepuka ile dhiki kwa kupitia ile injili ya manabii wawili (Ufunuo 11),na kwenda kujificha hawa watakuwa ni wale wayahudi 144,000 wanaozungumziwa katika (Ufunuo 7), lakini waliosalia wote wataungana na wale wanawali wapumbavu (yaani watu wa mataifa ambao hawakwenda kwenye unyakuo) kwa pamoja watapitia dhiki kuu ambayo itakudumu kwa muda wa miaka mitatu na nusu. Kama inavyosema katika Danieli:
Danieli 12:11 “Na tangu wakati ule ambapo sadaka ya kuteketezwa ya daima itaondolewa, na hilo chukizo la uharibifu litakaposimamishwa, itapata siku elfu na mia mbili na tisini”.
Kwahiyo hilo chukizo ni pale wayahudi watakapokuja kuingia agano na mpinga-Kristo, ambaye atataka kuja kuabudiwa kama Mungu..Hayo ni Machukizo makubwa ambayo yatasababisha Uharibifu kwa Wayahudi na kwa Dunia nzima, na kwa mpinga-kristo mwenyewe kwa kupatia unajisi patakatifu pa Mungu.( kumbuka pia Msikiti wa OMAR(Al-aqsa) uliopo pale Yerusalemu sio chukizo la uharibifu kama inavyodhaniwa na wengi .)
Kwahiyo ndugu hili chukizo la uharibifu sio tu kwa Yerusalemu peke yake hapana hata kwa KANISA, maana Kanisa ni HEKALU la Mungu biblia inasema hivyo. Na hili chukizo pia limesimama patakatifu pa Mungu, mahali ambapo pangepaswa YESU KRISTO peke yake aabudiwe, pamekuwa sehemu ya kuabudiwa sanamu pamoja na wanadamu. Bwana anasema Ufunuo 18: 4 “……..Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake. Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake”.
Tukijua kuwa tunaishi katika siku za hatari ni wakati wa kujiweka sawa, je! Bwana akija leo utaenda nae kwenye unyakuo?. Umeamini na kubatizwa?, je! wewe Ni miongoni mwa watakatifu?. Kama sivyo fanya hima katika muda huu wa nyiongeza tuliopewa. Weka mambo yako sawa siku ile isije ikakujia kama mwivi.
Tafadhali “share” kwa wengine ujumbe huu na Mungu atakubariki.
Mada Nyinginezo:
MAFUMBO YA MUNGU.
TOFAUTI KATI YA SHERIA YA ROHO WA UZIMA NA SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI!
NAOMBA KUJUA UTOFAUTI KATI YA DHAMBI, UOVU NA KOSA KIBIBLIA.
1Wakoritho 13: 11 “Nilipokuwa mtoto mchanga, nalisema kama mtoto mchanga, nalifahamu kama mtoto mchanga, nalifikiri kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto”.
Yeremia 31: 31 “Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda.
32 Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema Bwana. 33 Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; NITATIA SHERIA YANGU NDANI YAO, NA KATIKA MIOYO YAO NITAIANDIKA; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
34 Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena”.
Wagalitia 5: 18 “Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria”. Na pia inasema…
Warumi 8: 2 “Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti”.
Warumi 8: 4 “ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho”.
Warumi 8: 9 “Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake”.
Hivyo ndugu, na wewe upo katika uchanga au utu uzima?. Umejazwa Roho Mtakatifu au bado unaongozwa na dini?. Tafuta Roho Mtakatifu kumbuka Roho Mtakatifu ndio muhuri wa Mungu (Waefeso 4:30) pasipo huyo hakuna UNYAKUO.
JIRANI YAKO NI NANI?
UMUHIMU WA KUISHI MAISHA YAMPENDEZAYO MUNGU SASA.
JIHADHARI NA ROHO ZIDANGANYAZO
JE! SISI NI WAFALME NA MAKUHANI KWA NAMNA GANI?
PETRO ALIAMBIWA NA BWANA YESU UKIONGOKA WAIMARISHE NA NDUGU ZAKO. JE! KUONGOKA MAANA YAKE NINI?