KANISA NI NINI?

KANISA NI NINI?

Kanisa ni nini?..kanisa la Mungu ni kitu gani?

hili ni swali linalowachanganya watu wengi ikidhaniwa kuwa Kanisa ni jengo. Lakini hiyo sio maana halisi ya kanisa. Neno kanisa limetokana na Neno la kiyunani EKKLESIA, ikimaanisha “walioitwa”, Enzi za Agano jipya kasanyiko lolote la wakristo(yaani hao walioitwa) lilijulikana kama kanisa..Na kusanyiko hilo liliweza  kuanzia watu wawili au watu, kufuatana na maneno ya Yesu Kristo mwenyewe aliyosema katika..

Mathayo 18:20 “Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.”

Hivyo ilifahamika kuwa mahali popote walipokusanyika watu waliomwamini Kristo  iwe ni nyumbani, au hekaluni, au kwenye sinagogi, au popote pale kwa jina lake kutokujali mazingira yazungukayo basi hilo tayari ni kanisa.

Wagalatia 1:13 “Maana mmesikia habari za mwenendo wangu zamani katika dini ya Kiyahudi, kwamba naliliudhi kanisa la Mungu kupita kiasi, nikaliharibu”

Umeona?..Sentensi hiyo haioneshi kanisa kama jengo bali “wakristo” Paulo ndio aliowaudhi na kuwaharibu..Kwahiyo kanisa ni nini? Ni mkusanyiko wa watu walioitwa (au kwa lugha rahisi wakristo)

Hivyo kwa ufupi, mkusanyiko wowote usio wa kikristo, yaani usio usiomtambua Kristo kama kichwa cha kusanyiko hilo haijalishi ni mkubwa kiasi gani, haijalishi upo kwenye jengo lenye misalaba mingi kiasi gani, haijalishi linafuata utaratibu mzuri kiasi gani, hilo sio kanisa kibiblia. Ni sawa na mwili ambao hauna kichwa, ni mfu, vivyo hivyo na mkusanyiko wowote  usio na Kristo hauwezi kuwa ni Kanisa.

Waefeso1:20 “aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho;

21 juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia;

22 akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo

23 ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.”

AMEN.

Mada Nyinginezo:

WALIPO WAWILI AU WATATU KWA JINA LANGU.

NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE.

AGENDA KUBWA YA SHETANI KWA KANISA HILI LA LAODIKIA.

SIRI YA KUASI KATIKA KANISA LA MUNGU.

MADHARA YA KUKOSA MAJI YA UZIMA BAADA YA KIFO.

UNYAKUO.

JE KUJIUA NI DHAMBI?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments