Jumatano ya majivu, ni mojawapo ya mapokeo ya kanisa katoliki..ambapo Ni kipindi cha mwanzo wa mfungo wa siku 40… Siku hii yanachukuliwa “matawi ya Mitende” na kuchomwa mpaka yawe jivu. Na kisha lile jivu linachukuliwa na kwenda kupakwa katika paji la uso la mwamini, ishara kama ya msalaba.
Na wakati mhudumu anampaka mwamini majivu yale anakuwa anayasema maneno haya “kumbuka u mavumbi wewe na mavumbini utarudi”.. Na baada ya hapo ndipo muumini ataanza mfungo wa siku 40
Je Tendo hilo la Jumatano ya Majivu ni la kimaandiko?
Jibu ni la! si la kimaandiko hata kidogo. Hakuna mahali popote katika biblia wakristo walikuwa wanadesturi za kufanya hayo mapokeo ya jumatano ya majivu. Ni mapokeo tu yaliyoanzishwa na wanadamu. Ingawa Tendo la Mfungo ni la kimaandiko, ambalo kila mwamini anapaswa alitekeleze pia, lakini jumatano ya majivu sio ya kimaandiko.
Kwahiyo hakuna ulazima wowote wa mkristo kushika hiyo siku ya “jumatano ya majivu” kana kwamba ni siku takatifu isiposhikwa au kuenziwa ni dhambi mbele za Mungu. Na kwamba yale majivu yana nguvu fulani ya kiMungu, kana kwamba ukipakwa au ukipaka kuna jambo fulani la kiroho linaongezeka kwa msharika. Hapana, vilevile Mtu anaweza kuanza kufunga siku alizozipanga yeye pasipo huo utaratibu.
Kwahiyo hayo sio mambo ya msingi hata kidogo na wala hayamwongezei chochote Muumini, zaidi ya kumfanya awe wa kidini kuliko kuwa wa kiroho kuamini kuwa kuna kitu cha kipekee kinaongezeka ndani yake anapopakwa yale majivu.
Mambo ya lazima na ya sharti kuyafanya tuliyoagizwa na Roho Mtakatifu sisi wakristo yapo manne nayo ni…. 1)KUUMEGA MKATE, 2)KUKUSANYIKA PAMOJA, 3)KUDUMU KATIKA FUNDISHO LA MITUME (yaani kudumu katika Neno la Mungu) na 4) KUSALI. (Matendo 2:42). Hayo ndio mambo manne na ya muhimu na ya lazima kufanya kwa kila Mwamini. Na sio kushika sikukuu ya majivu wala ijumaa kuu. Na hilo la Nne la kusali linajumuisha pia KUFUNGA..Kwasababu kufunga na kusali vinakwenda pamoja.
Bwana akubariki.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
KWARESMA IPO KIMAANDIKO?
TUWATAFAKARI NZIGE WA JANGWANI.
AMEFUFUKA KWELI KWELI.
Mbona Mungu anaruhusu watu wapate shida, ilhali ana uwezo wa kutuepusha?
KUOTA MAFURIKO,KUOTA MAJI MENGI,KUOTA MAWIMBI.
JE SALA YA ROZARI TAKATIFU NI YA KIMAANDIKO?
Rudi Nyumbani:
Print this post