ijue Nguvu ya Imani ipo wapi?
Imani ni ufunguo wa mambo yote.. Ukiwa na Imani timilifu Bwana Yesu alisema unaweza ukauambia hata Mlima Kilimanjaro uondoke pale, na ukajitupe Baharini, na ukakutii..
Watu wanadhani maneno hayo alimaanisha milima ya rohoni, kwamba unaweza ukayaambia matatizo ondoka hapa uende kule, hapana, bali maneno yale ni ya mwilini kabisa.. Jambo ambalo wengi hatukubali kukiri ni kuwa hatuna Imani timilifu ya kufanya hivyo (Nami pia sina).
Joshua aliweza kusimamisha Jua, ambalo ni kubwa Zaidi ya dunia, kwanini leo hii isiwezekane, kuamini kuwa mlima ambao ni sehemu ndogo sana ya dunia unaweza kuhamishwa.
Hivyo hakuna jambo lolote linaloshindikana ukiwa na Imani timilifu. Bwana Yesu alisema hivyo katika Marko 9:23.
Lakini kutoweza kuhamisha milima haimaanishi kuwa huna Imani kabisa, hapana, Imani zinatofautiana viwango..Ili kufahamu vizuri juu ya hilo fungua hapa >>> IMANI MAMA NI IPI?
Je! Umeokoka?
Je! Unajua kuwa tunaishi katika siku za mwisho, na Yesu yupo karibuni kurudi? Na kwamba kanisa hili ndio kanisa la mwisho lijulikanalo kama Laodikia na kwamba hakutakuwa na kanisa lingine Zaidi ya hili? Unasubiri nini usimkaribishe Yesu maishani mwako akuokoe?
Fanya maamuzi upesi, kabla ya mlango wa neema haujafungwa.
Bwana akubariki.
ijue Nguvu ya imani ni kuu.
Mada Nyinginezo:
KIWANGO CHA TATU CHA IMANI.
ZIKIMBIE TAMAA ZA UJANANI! NA MTU YEYOTE ASIUDHARAU UJANA WAKO.
IMANI NI KAMA MOTO.
NGUVU YA SADAKA.
UNYAKUO.
CHUKIZO LA UHARIBIFU
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE.
Rudi Nyumbani:
Print this post
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ