IJUE NGUVU YA IMANI.

IJUE NGUVU YA IMANI.

ijue Nguvu ya Imani ipo wapi?


Imani ni ufunguo wa mambo yote.. Ukiwa na Imani timilifu Bwana Yesu alisema unaweza ukauambia hata Mlima Kilimanjaro uondoke pale, na ukajitupe Baharini, na ukakutii..

Watu wanadhani maneno hayo alimaanisha  milima ya rohoni, kwamba unaweza ukayaambia matatizo ondoka hapa uende kule, hapana, bali  maneno yale ni ya mwilini kabisa.. Jambo ambalo wengi hatukubali kukiri ni kuwa hatuna Imani timilifu ya kufanya hivyo (Nami pia sina).

Joshua aliweza kusimamisha Jua, ambalo ni kubwa Zaidi ya dunia, kwanini leo hii isiwezekane, kuamini kuwa mlima ambao ni sehemu ndogo sana ya dunia unaweza kuhamishwa.

Hivyo hakuna jambo lolote linaloshindikana ukiwa na Imani timilifu. Bwana Yesu alisema hivyo katika Marko 9:23.

Lakini kutoweza kuhamisha milima haimaanishi kuwa huna Imani kabisa, hapana, Imani zinatofautiana viwango..Ili kufahamu vizuri juu ya hilo fungua hapa >>> IMANI MAMA NI IPI?

Embu ngoja nikupe mfano wangu mdogo sana..naamini utakuongezea kitu..

Kuna wakati nilikuwa nimepanga jumba sehemu fulani, sasa ilikuwa kila mwisho wa mwezi, tunalipia bili ya maji sh. 7000, na  bili ya umeme sh.15,000. Na sehemu hiyo hao wanaokuja kuchukua bili hizo walikuwa ni wakali kweli, haziwezi pita siku mbili bila kuja kukugongea hodi..

ujue nguvu ya Imani..

Ilikuwa ni mwezi wa pili, wakati huo hali kwangu haikuwa nzuri sana, lakini nilimwambia Mungu nitakuamini wewe, na ni wewe ndiye utakayenipa hifadhi mimi na ndugu yangu..Hivyo ulipofika mwisho wa mwezi tulishangaa, wale hawakuja kutugongea wakati ilikuwa ni desturi yao, mpaka ukaanza mwezi mwingine wa tatu, lakini hatukuwaona..zikawa zinapita tu tarehe, bado tunashangaa hatuwaoni, wapangaji wengine walienda kulipia lakini sisi hatujafuatwa..Ikaendelea hivyo hivyo, hapo mfukoni hatuna kitu, mpaka ikafika tarehe 25,..kipindi hicho na gesi nayo ikaisha ndani, tukawa kama vile hatuna kitu na mwezi mwingine unakwenda kuishia bado tunayo madeni ya nyuma na hatuna pesa ya matumizi..

Lakini siku hiyo tulikuwa tumekaa, tukajikuta tunaangalia tu M-pesa, cha ajabu tukashangaa kule kulikuwa ni sh.50,000 na hiyo namba hatujawahi kuitumia kwa miamala yoyote ya kifedha, tukaenda kutoa ili tukanunue gesi sh. 20,000, lakini tulipomaliza tu kutoa , mara wale watu wa umeme, wanakuja kutugongea mlango, na kutuambia tuwalipe pesa ya umeme wa mwezi uliopita.. Ndipo tukatoa ile hela tukawapa saa ile ile, tukafiria kwamba kama  tusingewapa siku ile sijui hali ingekuwaje!.

Lakini tulimwamini Mungu, tukajua kweli nguvu ya Imani ni kubwa. Yapo na mambo mengine mengi Mungu aliyonitendea kwa kumwamini tu..

ijue Nguvu ya Imani.

Hiyo yote ni kutaka kukupa moyo na wewe, ukimwamini Mungu, basi anaweza kukufanyia mambo makubwa katika Maisha yako.

Mifano mingi sana ipo katika biblia, ambayo ukiisoma itaikuza Imani yako sana.. Na ndio maana tunaambiwa..

Warumi 10:17  “Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo”.

Hivyo unapoitafakari mifano mingi ya Imani katika Biblia ndivyo unavyoikuza Imani yako. Na ndio mpaka huko huko unajikuta unafanya mambo makubwa ya ki-imani yasiyoelezeka kibinadamu.

Lakini yote hayo ni mpaka uwe katika wokovu?

Je! Umeokoka?

Je! Unajua kuwa tunaishi katika siku za mwisho, na Yesu yupo karibuni kurudi? Na kwamba kanisa hili ndio kanisa la mwisho lijulikanalo kama Laodikia na kwamba hakutakuwa na kanisa lingine Zaidi ya hili? Unasubiri nini usimkaribishe Yesu maishani mwako akuokoe?

Fanya maamuzi upesi, kabla ya mlango wa neema haujafungwa.

Bwana akubariki.

ijue Nguvu ya imani ni kuu.

Mada Nyinginezo:

KIWANGO CHA TATU CHA IMANI.

ZIKIMBIE TAMAA ZA UJANANI! NA MTU YEYOTE ASIUDHARAU UJANA WAKO.

IMANI NI KAMA MOTO.

NGUVU YA SADAKA.

UNYAKUO.

CHUKIZO LA UHARIBIFU

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments