USINIPITE MWOKOZI Lyrics

USINIPITE MWOKOZI Lyrics

Usinipite mwokozi Lyrics| Swahili, – “Pass me not, O Gentle Savior”


Historia ya nyimbo Usinipite mwokozi.


Wimbo huu uliandikwa mwaka 1868, na mwanamke wa kimarekani aliyeitwa Fanny Crosby. Mwanamke huyu mkristo alizaliwa akiwa mzima lakini wiki 8 baada ya kuzaliwa kwake alipatwa na opofu, ambao ulidumu mpaka kufa kwake, lakini katika maisha yake yote aliyoishi hapa duniani  (yaani miaka 94), haikuwa bure kwa Mungu wake, alifanikiwa kuandika  nyimbo zaidi ya 8,000..Hivyo hiyo ikamfanya apate umaarufu na kumfanya ajulikane kwa jina la “mtunzi-kipofu-wa-nyimbo-za-tenzi”, na  “Malkia wa nyimbo za Injili”.

Lakini siku moja alipokuwa amealikwa kwenda kuzungumza na wafungwa wa mji,  na alipokuwa akitembea kule gerezani alimsikia mfungwa mmoja akisema “Bwana mwema usinipite, usinigeuzie mgongo wako,unikumbuke”,

Fanny anasema aliguswa sana na maneno yale, jambo ambalo halikuondoka kwenye kichwa chake mpaka alipofika nyumbani. Na huko ndipo alipoandika beti zote nne za wimbo ujulikanao kama USINIPITE MWOKOZI.

Alipomaliza kuuandika akampa muhusika wa kuweka midundo, na mwaka, 1870 wimbo huo, ulizinduliwa rasmi katika machapisho..

Na kwa kipindi kifupi` sana ukapata umaarufu mkubwa  duniani kote.

*****

Usinipite wokozi,
Unisikie;
Unapozuru wengine,
Unisikie.
 
Yesu, Yesu, Unisikie;
Unapozuru wengine,
Usinipite,
 
Kiti chako cha rehema,
Nakitazama;
Magoti napiga pale,
Nisamehewe.
 
Yesu, Yesu, Unisikie;
Unapozuru wengine,
Usinipite.
 
Sina ya kutegemea,
Ila wewe tu;
Uso wako, uwe kwangu,
Nakuabudu.
 
Yesu, Yesu, Unisikie;
Unapozuru wengine,
Ila wewe tu,
Usinipite.
 
U Mfariji Peke yako;
Sina mbinguni,
Wala Duniani pote,
Bwana mwingine.
 
Yesu, Yesu, Unisikie;
Unapozuru wengine,
Usinipite.

*****

Jambo hili tunaliona kwa wale kipofu wawili waliomsikia Yesu anapita..

Mathayo 9:27 “Yesu alipokuwa akipita kutoka huko, vipofu wawili wakamfuata wakipaza sauti, wakisema, UTUREHEMU, MWANA WA DAUDI.

28 Naye alipofika nyumbani, wale vipofu walimwendea; Yesu akawaambia, Mnaamini kwamba naweza kufanya hili? Wakamwambia, Naam, Bwana. 29 Ndipo alipowagusa macho, akasema, Kwa kadiri ya imani yenu mpate”.

Na itakuwa hivyo na kwako:

Ikiwa wewe umeokoka, na unaona unapita katika hali ngumu, ambayo unaona kwa namna ya kawaida huwezi kutoka, basi wakumbuke watu kama hawa, wakutie nguvu,..Zidi kumwita Yesu, atakuonekania kwa wakati wake. Kwasababu yeye anatupenda na kutujali, na yote yanawezekana kwake.

Lakini kama hujaokoka, basi ni vizuri leo ukamwita kwanza mwokozi akuokoe maisha yako, usiruhusu akupite, anapokwenda kuwapa wengine uzima wa milele, sema na mimi leo nauhitaji huo uzima, hivyo kama upo tayari kufanya hivyo, basi fungua hapa, kwa ajili ya Sala ya Toba..>>>  KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki..

Tazama historia ya nyimbo nyingine za Tenzi chini.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

MWAMBA WENYE IMARA

CHA KUTUMAINI SINA lyrics

BWANA MUNGU NASHANGAA KABISA lyrics

NI SALAMA ROHONI MWANGU Lyrics

TENZI ZA ROHONI

Mungu aliposema Yesu ni mwanawe pekee, alimaanisha hakuwa na wengine?

MUONEKANO MPYA WA YESU BAADA YA KUFUFUKA.

UNYAKUO.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments