Ni watu gani hao ambao mahali pao hapakuonekana?

Ni watu gani hao ambao mahali pao hapakuonekana?

Ni watu gani hao ambao mahali pao hapakuonekana? (Ufunuo 20:11)


JIBU: Tusome..

Ufunuo 20:11 “Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana”.

Hao wanaozungumziwa hapo kwamba “mahali pao hapakuonekana” sio binadamu!..bali ni “MBINGU NA NCHI”. Tafsiri za lugha nyingine zinaelezea vizuri.

Na kwanini zikimbie uso wake?..ni kwasababu ya utukufu wake…kwasababu hakuna kitu chochote kinachoweza kusimama mbele ya uso wa Mungu kwa kuwa yeye mkuu sana  na mtakatifu!. Maserafi tu waliopo mbinguni ambao ni watakatifu, bado wanafunika nyuso zao na miguu yao mbele yake..si Zaidi viumbe vilivyopo katika mbingu na nchi tulizopo sisi?.

Ayubu 41:10 “….BALI NI NANI AWEZAYE KUSIMAMA MBELE YANGU MIMI?

Hivyo hakuna kiumbe chochote ambacho kinaweza kumkaribia Mungu kwa ukamilifu wake. Lakini ashukuriwe Mungu kwa sababu yupo mmoja ALIYESTAHILI KUMKARIBIA YEYE, na huyo si mwingine Zaidi ya mwanawe wa pekee aliyemtoa ambaye yeye alishinda na kustahili kumkaribia Mungu, na kuketi Pamoja naye katika kiti chake..Huyo pekee ndiye aliyestahili kumkaribia Mungu…na kwa kupitia yeye sisi tuliompokea tumepata nafasi ya kumkaribia Mungu..

Ufunuo 3:21 “Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi”.

 

Ufunuo 5:11 “Nikaona nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai, na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu,

12 wakisema kwa sauti kuu, ASTAHILI MWANA-KONDOO ALIYECHINJWA, kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka.

13 Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi ya juu ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na milele”.

Hivyo tukimwamini na kuingia ndani yake tunapata ujasiri wa kumkaribia Mungu sana, jambo ambalo katika hali ya kawaida lisingekaa liwezekane kabisa, lakini limewezekana kwa kupitia Yesu, lakini tukimkataa huyu Yesu, basi hatuna ujasiri wowote na hatuwezi kumkaribia Mungu kamwe…Tutaukimbia uso wake na kutengwa naye milele katika ziwa la moto.

Waebrania 10:19  “Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu,

20  njia ile aliyotuanzia iliyo mpya, iliyo hai, ipitayo katika pazia, yaani, mwili wake;

21  na kuwa na kuhani mkuu juu ya nyumba ya Mungu;

22  na tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa miili kwa maji safi”.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

UFUNUO: Mlango wa 20

DANIELI: Mlango wa 1

HAPO NDIPO WATU WALIPOANZA KULIITIA JINA LA BWANA.

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

MKUMBUKE MKE WA LUTU.

Kitabu cha YASHARI kinachozungumziwa katika 2Samweli 1:17-18, ni kitabu gani?

URIMU NA THUMIMU NI NINI KATIKA BIBLIA?

ALIYOKUTANA NAYO YESU, YERIKO.

ZIKIMBIE TAMAA ZA UJANANI! NA MTU YEYOTE ASIUDHARAU UJANA WAKO.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments