KUABUDU SANAMU/IBADA ZA SANAMU.

KUABUDU SANAMU/IBADA ZA SANAMU.

Kuabudu Sanamu ni nini? Na ibada za sanamu ni zipi?


Kuabudu sanamu: Katika  agano la kale ni kitendo chochote cha kwenda kuabudu au kusujudia, au kutumika kitu kingine chochote, tofauti na Mungu mkuu mmoja aliye hai (YEHOVA).

Moja ya amri 10 Mungu alizowapa wana wa Israeli, ilikuwa ni pamoja na kujiepusha na ibada za sanamu za aina yoyote..

Amri ya pili inasema hivi..

Kutoka 20:4 “Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. 

5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, 

6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu”.

Hivyo mtu akikigeuza kitu chochote, kuwa mbadala wa Mungu, huko  ni sawa na kuabudu sanamu, ukiweka mdoli nyumbani kwako na kwenda kumpigia magoti na kumwomba kana kwamba ni Mungu, ujue hapo unafanya ibada za sanamu..

Ukitengeneza kinyago chenye sura ya mtakatifu Fulani labda Mariamu, au Bwana Yesu akiwa pale msalabani, kisha ukakihusianisha na mambo ya ibada kwa mfano  kukisujudia, au kukiabudu, au kuombea dua zako kwa kupitia hicho, tayari hiyo ni ibada za sanamu,

Ukining’iniza picha ukutani ya mtu Fulani maarufu, au mnyama , au kitu Fulani kwa lengo la kukifanya kama kipatanishi chako na Mungu, au kitu chako kinachoweza kukupa bahati Fulani, hiyo tayari ni ibada za sanamu.

Hata ukipanda mti, au Ua fulani, ukiamini kuwa linaweza kukulinda, au kueleza hatma ya maisha yako, tayari hiyo nayo ni ibada za sanamu.

Kumbukumbu 16:21 “Usipande mti uwao wote kuwa Ashera kwako kando ya madhabahu utakayofanya ya Bwana, Mungu wako.”

Na ni machukizo makubwa sana mbele za Mungu, yanayomtia wivu kiasi cha Mungu kukupatilizia maovu hata ya baba zako, uone ni jinsi gani kitendo hicho kinavyomuudhi Mungu..

Ipo mifano mingi sana katika biblia, ya watu walioadhibiwa kwa makosa kama haya..Kumbuka hili ndilo lililowafanya wana wa Israeli wengi wasiione Kaanani, kadhalika hili ndilo lililochangia wana wa Israeli tena baadaye kuchukuliwa utumwani Babeli.

Hivyo kuhusianisha kitu chochote na Ibada ni hatari sana, Ibada zako zote zinapaswa zimwelekee Mungu peke yake.

JE! KUABUDU SANAMU/IBADA ZA SANAMU KATIKA AGANO JIPYA KUKOJE?.

Tukirudi katika agano jipya, kuabudu sanamu sio tu kwenda kusujudia vinyago tu peke yake n.k., hapana ni Zaidi ya hapo, biblia inasema..

Waefeso 5:5  “Maana neno hili mnalijua hakika, ya kwamba hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu”.

Unaona, mtu yeyote ambaye ni mchafu, mbele za Mungu ni mwabudu sanamu, Mtu yeyote aliye na tamaa mbele za Mungu huyu naye ni mwabudu sanamu.

Hawa wote biblia inasema hawana urithi katika ufalme wa Mungu.

Hivyo mimi na wewe tunapaswa tujiepushe na Ibada zote mbili, yaani sanamu za nje, Pamoja na zile Sanamu za ndani. Ili Mungu atupokee tukaurithi uzima wa milele aliyotuandalia tumpendao.

Bwana akubariki.

Ikiwa hujaokoka na unataka kufanya hivyo leo, basi uamuzi huo utakuwa ni wa busara kwako. Fungua hapa kwa ajili ya sala ya toba.>>  KUONGOZWA SALA YA TOBA

Ubarikiwe.

Mada Nyinginezo:

Je! Bikira Maria ni MALKIA WA MBINGUNI?

USIABUDU SANAMU.

CHAPA YA MNYAMA

CHUKIZO LA UHARIBIFU

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!

NEEMA YA MZALIWA WA PILI.

HERI YULE ATAKAYEKULA MKATE KATIKA UFALME WA MUNGU.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Nikolas
Nikolas
1 year ago

Rejea hesabu 21:8-9 Hii maan yake waisrael waliabudu sanamu za NDANI Kwa amari ya MUNGU gan maan Maan Musa asi ngeweza kumweka nyoka mtini