JE KIFO NI NINI? NA JE KUNA AINA NGAPI ZA VIFO?

JE KIFO NI NINI? NA JE KUNA AINA NGAPI ZA VIFO?

Je Kifo ni nini? Na kuna aina ngapi za vifo?


Kifo ni pale uhai unapoondoka ndani ya  kiumbe hai chenyewe. Kwa ufupi kifo ni Mwisho wa Maisha ya mwilini.

Lakini katika Biblia vipo vifo vikuu vya aina tatu.

  1. Kifo cha mwili, lakini Roho inaishi
  2. Kifo cha rohoni
  3. Kifo cha Roho yenyewe (hichi kinajulikana kama mauti ya pili)

Kifo cha Mwilini:

Hichi ni pale mwili na roho vinapotengana. Kifo hichi kinamkuta kila mmoja wetu, pale anapomaliza safari yake ya Maisha ya duniani ikiwa unyakuo utakuwa haujakukuta basi utakufa na kuzikwa.

Mwanzo 3:19 “…. kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi”.

Kifo cha namna hii haikuhusishi roho ya mtu..Roho  inakuwa bado inaendelea kuishi sehemu nyingine..Bwana Yesu alisema..

Mathayo 10:28  “Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum.”

Kifo cha Rohoni:

Hichi ni kifo ambacho kinamkumba mtu kwa ndani, lakini kwa nje bado anakuwa anaendelea kuishi kana kwamba hakuna chochote kinachoendelea.. Na kifo cha namna hii, kila mmoja wetu anacho aidha kwa kujua au kwa kutokujua..Leo hii ikiwa Maisha yako yapo mbali na dhambi (yaani umeokoka), tayari wewe rohoni unaonekana kuna mauti imetokea ndani yako, yaani unaonekana tayari umeshakufa kwa Habari ya dhambi, biblia inasema hivyo..

Warumi 6:1  “Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? 2  Hasha! SISI TULIOIFIA DHAMBI tutaishije tena katika dhambi..

6:11  “Vivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu”.

Vilevile ikiwa injili inahubiriwa kwako halafu hubadiliki, fahamu kuwa katika ulimwengu wa roho umekufa kwa Habari ya haki hata kama  utakuwa unaishii..

1Timotheo 5:6  “Bali, yeye asiyejizuia nafsi yake amekufa ingawa yu hai”.

Kifo cha Roho:

Kifo hichi ndio kibaya Zaidi, Na ndio kifo cha mwisho kinachojulikana kama Mauti ya pili. Kifo hichi ni pale, unapotenganishwa moja kwa moja na uso wa Mungu milele, katika lile ziwa la moto.. Ambapo utatetezwa huko na roho yako itaangamia milele.

Ufunuo 20:13  “Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.

14  Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto.

15  Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto”.

Lakini Pamoja na hayo sisi tulio ndani ya Kristo tunalo tumaini la uzima wa milele  ikiwa tutakufa leo. Kwasababu Yesu Kristo ambaye alishinda mauti, atakuja kutufufua tena, katika hii hii miili yetu, kisha atatuvika miili mingine mipya ya utukufu ya kimbinguni isiyo kufa wala kuugua, wala isiyo na madhaifu, na hiyo ndiyo tutakayoishi nayo milele.

Lakini ikiwa wewe ni mwenye dhambi bado hujamkabidhi Kristo Maisha yako ayaokoe, ukifa leo hii, huna tumaini lingine lolote Zaidi ya kungojea ile mauti ya pili ambalo ni ziwa la moto..

Lakini kwanini hayo yote yatukute angali tunayo nafasi bado?..Ikiwa wewe ni mmojawapo ambaye yupo bado katika dhambi, Na leo hii unataka Bwana Yesu akuokoe, hutaki neema ya wokovu ikupitie, basi popote pale ulipo anaweza kukusamehe dhambi zako ikiwa tu utamaanisha kufanya hivyo.

Kama upo tayari kutubu sasa dhambi zako, basi fungua hapa kwa ajili ya maelekezo ya sala ya Toba. >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki sana.

Ikiwa umemfuata maelekezo hayo ya kuokoka, sasa, upo tayari kujifunza na masomo mengine ya rohoni.Tafadhali tazama chini vichwa vya masomo kisha bofya lolote upendalo uzidi kujifunza zaidi.

Mada Nyinginezo:

MAUTI YA PILI NI NINI?

NINI KINATOKEA BAADA YA KIFO?

MADHARA YA KUKOSA MAJI YA UZIMA BAADA YA KIFO.

JIFUNZE KUJITOA KWA MUNGU NA KUWA MKARIBISHAJI.

RABI, UNAKAA WAPI?

KAMA MMOJA TU NDIO HIVI! SI ZAIDI 153?

Kwanini Mungu awachome watu kwenye ziwa la moto na hali yeye ndiye aliyewaumba?

KIFO CHA REINHARD BONKEY KINAACHA UJUMBE GANI KWETU?

PENGINE MUNGU ALISHASEMA NAWE KWA NJIA HII.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Samwel
6 months ago

Nimesoma hii mada,napata swali baada ya mwili kufa,roho inaishi wapi?