NAMWANDAMA BWANA Lyrics~ Trust and Obey

NAMWANDAMA BWANA Lyrics~ Trust and Obey

NAMWANDAMA BWANA Lyrics~ Swahili?| Trust and Obey


Nyimbo hii iliandwa mwaka 1887, na Mchungaji  mmoja aliyeitwa  John H Sammis, (Mmarekani), ambaye alifanikiwa pia kuandika nyimbo nyingine Zaidi ya 100 zenye maudhi ya tenzi.

Historia ya wimbo huu ilianza siku moja, katika mkutano wa injili uliofanyika huko  Massachusetts   Marekani mwaka 1886, katika mkutano huo alisimama kijana mmoja ambaye alitoa ushuhuda wa wokovu wake, Kijana huyu alikuwa hajui mambo mengi kuhusu Mungu, ni mchanga katika wokovu, Lakini katika maneno yake machache alisema..

“Sina uhakika sana, lakini nitakwenda kuamini na kutii”

Maneno hayo yalimgusa sana mwendesha mziki aliyekuwa katika mkutano huo aliyeitwa Danieli Towner, mpaka akaamua kuyaandika maneno yale kwenye kikaratasi, na kisha baadaye akamtumia Rafiki yake ambaye alikuwa mchungaji aliyeitwa John H Sammis, huyo ndiye akauandika wimbo huo, “Namwandama Bwana”. Ambao ndani yake una vina vya maneno ya huyo kijana, nitaamini nitii.

Alipokuwa anauandika, alizingatia vipengele  tofauti tofauti ya Maisha yetu tunayopaswa kutii.

NAMWANDAMA BWANA lyrics.

*****

Namwandama Bwana kwa alilonena,
Njia yangu huning’azia;
Nikimridhisha atanidumisha
Taamini nitii pia.
 
Amini utii, njia pweke ni hii
Ya furaha kwa Yesu: amini ukatii
 
Giza sina kwangu wala hata wingu,
Yeye mara huviondoa,
Woga, wasiwasi, sononeko, basi.
Huamini nitii pia.
 
Amini utii, njia pweke ni hii
Ya furaha kwa Yesu: amini ukatii.
 
Masumbuko yote, sikitiko lote;
Kwa mapenzi hunilipia,
Baa, dhara, dhiki, vivyo hubariki,
Taamini nitii pia.
 
 
Amini utii, njia pweke ni hii
Ya furaha kwa Yesu: amini ukatii
 
Mimi sitajua raha sawasawa
Ila yote Yesu kumpa;
Napata fadhili na radhi kamili,
Taamini nitii pia.
 
Amini utii, njia pweke ni hii
Ya furaha kwa Yesu: amini ukatii
 
Nitamfurahisha na kumtumaini,
Majumbani na njia-njia;
Agizo natenda, nikitumwa hwenda,
Huamini nitii pia
 
Amini utii, njia pweke ni hii
Ya furaha kwa Yesu: amini ukatii

******

Ni nini tunaweza kujifunza katika historia ya wimbo huu Namwandama Bwana ?

Ushuhuda wako, hata kama utakuwa ni mdogo vipi,  unaweza ukawa chanzo cha baraka cha watu wengine wengi duniani na kuwaokoa. Kama kijana huyu angeudharau ushuhuda wake, leo hii tusingekuwa na tenzi yenye faraja ya kipekee kama hii maishani mwetu.

Hivyo nawe pia usigope kushuhudia mambo makuu ya Mungu maishani mwako.

Shalom.

Mada Nyinginezo:

TENZI ZA ROHONI

USINIPITE MWOKOZI Lyrics

BWANA MUNGU NASHANGAA KABISA lyrics

NI SALAMA ROHONI MWANGU Lyrics

KUMTEGEMEA MWOKOZI Lyrics/Swahili.

UNYAKUO.

UFUNUO: Mlango wa 1

NI KITU GANI PETRO NA YOHANA WALIKIGUNDUA KABURINI?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments