WATOTO WA YESE KATIKA BIBLIA.

WATOTO WA YESE KATIKA BIBLIA.

Watoto wa Yese katika biblia walikuwa ni wangapi?


Kitabu cha Samweli kinaonyesha Yese alikuwa na wana nane(8), Daudi akiwa ndio mwana wa mwisho kabisa, Lakini kitabu cha Mambo ya Nyakati  wa kwanza kinaonyesha Yese alikuwa na Wana saba (7). Sasa swali linakuja Je! takwimu zipi ni sahihi? Je! biblia inajichanganya yenyewe?

Jibu  ni hapana..

Tusome..

1Samweli 16:10 “Yese akawapitisha WANAWE SABA mbele ya Samweli. Samweli akamwambia Yese, Bwana hakuwachagua hawa.

11 Kisha Samweli akamwambia Yese, Watoto wako wote wapo hapa? Naye akasema, AMESALIA MDOGO WAO, na tazama, anawachunga kondoo. Basi Samweli akamwambia Yese, Tuma watu, wamlete; kwa sababu hatutaketi hata atakapokuja huku”.

Soma tena.

1Nyakati  2:13 “na Yese akamzaa Eliabu, mzaliwa wake wa kwanza, na wa pili Abinadabu, na wa tatu Shama;

14 na wa nne Nethaneli, na wa tano Radai;

15 na wa sita Ozemu, na wa saba Daudi;

16 na maumbu yao ni Seruya, na Abigaili. Na wana wa Seruya walikuwa, Abishai, na Yoabu, na Asaheli; hao watatu.”

Sasa ukiangalia hapo utaota kitabu cha Mambo ya Nyakati hakijatoa idadi Fulani kwamba wana wa Yese kuwa walikuwa ni saba tu, hapana badala yake kimeorodhesha majina, Sasa kama wewe ni msomaji mzuri wa biblia utagundua kuwa kitabu cha mambo ya Nyakati kiliandikwa miaka ya mbeleni sana ukilinganisha na kitabu cha Samweli. Na kitabu hicho cha Mambo ya Nyakati wa kwanza kilikuwa kimejikita zaidi katika kuelezea uzao wa makabila ya Israeli(Vizazi vya wana wa Israeli).

Hivyo ilikuwa ni kawaida mtu asiyekuwa na uzao hakuweza kuorodheshwa katika orodha hiyo. Kwahiyo ni sahihi kusema Yese alikuwa na wana 9,  lakini mmojawapo alifariki, pengine akiwa bado hajapata uzao, na hivyo mwandishi wa kitabu cha Mambo ya Nyakati akaona hakukuwa na haja ya kumworodhesha pale. Ni kama tu Samweli alivyoacha kuwaorodhesha dada zao wawili. Kama isingekuwa kitabu cha Mambo ya Nyakati kuwaorodhesha ni rahisi kudhani walizaliwa wana wa kiume tu kwao, lakini kulikuwa hakuna haja ya kuwaorodhesha pale, kutokana na muktadha ya maudhui ya pale, kwamba waliokuwa wanahitajika na wana wa kiume, tu.

Ndivyo ilivyokuwa hata kwa mwandishi wa kitabu cha Mambo ya Nyakati, walioorodheshwa na wale wenye uzao tu.

Kwahiyo kwa kuhitimisha ni kuwa Yese alizaa watoto nane (8) wakiume, na wawili (2) wa kike, Lakini mmoja baadaye alikuja kufa, wakabakia wana wa kiume 7 ndio wale walioorodheshwa katika 1Nyakati.

Shalom.

Tafadhali, angalia masomo mengine chini, ujifunze zaidi;

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo mballimbali kwa njia yaWhatsapp tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Adamu alikuwa na watoto wangapi?

Nuhu alikuwa na watoto wangapi?

JINSI ROHO MTAKATIFU ANAVYOWAFUNULIA WATU MAANDIKO.

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 8 (Kitabu cha Ezekieli)

JE KANISA LITAPITIA DHIKI KUU?

YAKINI NA BOAZI.

MANENO ALIYOWEZA KUTAMKA YESU TU PEKE YAKE.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments