Bawabu ni nani/nini?

Bawabu ni nani/nini?

Bawabu (kwa kiingereza -Doorkeeper/Porter) ni nani katika biblia?


Bawabu maana yake ni msimamzi wa mlangoni, anayefunga na kufungua, na anayeruhusu na kutoruhusu mtu au vitu kuingia, Hawa wanakuwa hususani katika mageti ya kuingilia miji mikubwa na kwenye majumba ya kifalme na mahekalu,

2Samweli 18:26 Kisha huyo mlinzi akaona mtu mwingine anapiga mbio; mlinzi akamwita bawabu, akasema, Angalia, mtu mwingine anakuja mbio peke yake. Mfalme akasema, Huyu naye analeta habari.

Soma pia 2Wafalme 7:10,11

1Nyakati 9:23 “Basi watu hao na wana wao walikuwa na usimamizi wa malango ya nyumba ya Bwana, yaani, nyumba ya maskani, kwa zamu….

27 Nao wakalala kandokando nyumbani mwa Mungu, kwa kuwa ulinzi wake ulikuwa juu yao, nayo ilikuwa kazi yao kuyafungua malango asubuhi baada ya asubuhi.”.

Kazi hii ni kazi iliyokuwa inaonekana kama nyonge kuliko kazi zote kwenye utumishi wa Majumbani au kwenye ulinzi, hata sasa ndivyo zinavyoonekana..

Lakini Daudi alisema..

Zaburi 84:10 “Hakika siku moja katika nyua zako Ni bora kuliko siku elfu. Ningependa kuwa bawabu nyumbani mwa Mungu wangu, Kuliko kukaa katika hema za uovu”.

Daudi alitumia kazi yenye cheo cha chini kabisa, katika jumba kubwa akasema kama na kwa Mungu ipo hivyo, basi angependelea walau apate hata kazi hiyo ndogo tu, maadamu ni ya Mungu, kuliko kupata cheo kikubwa na kibali katika mambo ya kidunia.

Akasema tena siku moja nyuani kwa Bwana ni bora kuliko siku elfu penginepo..

Alijua faida ya kazi ya Mungu, hata kama ni ndogo kiasi gani, alijua akipoteza siku moja kuitenda kazi ya Mungu ni sawa zaidi ya siku elfu kujisumbua na shughuli nyingine za kidunia..Firikia siku elfu ni karibia na miaka 3, Hivyo miaka 3 yako wewe kwenye masumbufu yako ni siku moja kwa mtu anayedeki choo cha kanisa.

Hivyo na wewe jiulize kazi yako ni nini kwenye nyumba ya Mungu? Mchango wako wa kusambaza kazi ya Mungu ni ipi? Nguvu zako za kifedha unazimalizia wapi ndugug? Au kwako kazi ya Mungu haina faida yoyote..

Daudi anasema ni heri “Ni heri niwe bawabu nyumbani mwa Mungu..”

Shalom.

Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara katika email yako au Whatsapp yako basi tutumie ujumbe kwenye namba hii :+255 789001312

Mada Nyinginezo:

Bwana alimaanisha nini kusema JIKANE mwenyewe?(Mathayo 6:24)

JE NI LAZIMA MKRISTO AOE/AOLEWE?

Je Mungu anawapenda watu wote au ana chuki?

Mwaloni ni nini? Na je unafunua nini rohoni?

MTU ASIYE PAMOJA NAMI YU KINYUME CHANGU.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments