Behewa ni nini?

 Behewa ni nini?

Behewa kwa jina lingine ni UA, ni eneo la wazi lililokuwa limezungushiwa fensi mbele ya Hema ya kukutania , kwa ajili ya makuhani kutoa sadaka za kuteketezwa, na kufanya shughuli za kikuhani tazama picha juu..

Lakini  baadaye Hekalu lilipokuja kutengenezwa na Sulemani pale Yerusalemu, eneo la behewa/Ua lilizungushiwa ukuta, na pakawa na behewa kuu mbili, 1) ya ndani 2) na ya nje, ili ya ndani ikabakia kuwa ya makuhani tu, kufanya mambo ya upatanisho na sadaka za kuteketezwa, Na ile ya nje ikabakia kuwa ya Wayahudi  wote kukutanika kuabudu..Tazama picha chini..

hekalu la sulemani

Lakini pia behewa, kwenye biblia haikumaanisha tu ni lazima iwe mbele ya hema ya kukutania au mbele ya Hekalu la Mungu, biblia inayonyesha pia, zilikuwa pia kwenye majumba ya kifalme na ya kikuhani.

1Wafalme 7:1 “Naye Sulemani alikuwa katika kuijenga nyumba yake mwenyewe miaka kumi na mitatu, akaimaliza nyumba yake yote….11 Na juu kulikuwa na mawe ya thamani, mawe ya kuchongwa, sawasawa na cheo, na mierezi.

12 Na behewa kubwa pande zote ilikuwa na safu tatu za mawe ya kuchongwa, na safu moja ya mihimili ya mierezi; mfano wa behewa ya ndani ya nyumba ya Bwana, na ukumbi wa nyumba”.

 

Mathayo 16:3 “Wakati ule wakuu wa makuhani, na wazee wa watu, wakakusanyika katika behewa ya Kuhani Mkuu, jina lake Kayafa”;

Lakini pia katika kitabu cha ufunuo tunasoma, kuwa wakati wa mwisho, behewa/ua iliyo nje ya hekalu ambalo litakuja kujengwa na Wayahudi pale Yerusalemu siku za mwisho, litamilikiwa na watu wa mataifa kwa muda wa miezi 42..

 

Ufunuo 11:1 “Nikapewa mwanzi kama fimbo; na mmoja akaniambia, Inuka, ukalipime hekalu la Mungu, na madhabahu, na hao wasujuduo humo.

2 Na behewa iliyo nje ya hekalu uiache nje wala usiipime, kwa maana Mataifa wamepewa hiyo, nao wataukanyaga mji mtakatifu miezi arobaini na miwili”.

Ili kufahamu habari kamili, sababu na maana yake rohoni ya mambo hayo fungua vichwa vingine vya masomo tulivyovirodhesha chini.

 

Mada Nyinginezo:

UFUNUO: Mlango wa 12

CHUKIZO LA UHARIBIFU

YAKINI NA BOAZI.

 

CHAPA YA MNYAMA

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Leave a Reply