Baghala kwa jina lingine ni nyumbu, lakini sio Yule nyumbu wa porini, bali ni mnyama chotara anayezalishwa kwa kukutanishwa Farasi na Punda. Tazama picha juu.
Utalisoma Neno hilo (Baghala) katika kifungu hichi.
2Wafalme 5:16 “Lakini akasema, Kama Bwana aishivyo, ambaye nimesimama mbele yake, sipokei kitu. Akamshurutisha apokee; lakini akakataa.
17 Naamani akasema; Kama sivyo, lakini mtumwa wako na apewe mzigo wa udongo wa BAGHALA wawili; kwa maana mtumwa wako hatatoa tena sadaka ya kuteketezwa wala dhabihu kwa miungu mingine, ila kwa Bwana”.
Zamani wana wa Israeli walikuwa wanatumia aidha punda au farasi, lakini baadaye tunakuja kuona sehemu nyingi walianza kuwatumia nyumbu katika shughuli zao nyingi, badala ya punda au farasi, kwasababu waligundua ni wavumilivu, na wagumu, na aanabeba mizigo mikubwa zaidi kuliko punda, na wanaishi mara zaidi ya farasi, japo ni wafupi kidogo ya farasi.
Hivyo sehemu zote utakazokutana nazo kwenye biblia zinamzungumzia nyumbu, basi ujue ni mnyama huyu chotara. Vifuatavyo ni baadhi ya vifungu vinavyomwelezea;
Zaburi 32:9 “Msiwe kama farasi wala nyumbu, Walio hawana akili. Kwa matandiko ya lijamu na hatamu Sharti kuwazuia hao, au hawatakukaribia”.
Ezra 2:66 “Farasi zao walikuwa mia saba thelathini na sita; nyumbu zao, mia mbili arobaini na watano”;
2Samweli 18:9 “Na kwa bahati Absalomu akakutana na watumishi wa Daudi. Naye Absalomu alikuwa amepanda nyumbu wake, na yule nyumbu akapita chini ya matawi manene ya mwaloni mkubwa, hata kichwa chake kikakwama katika mwaloni huo, akanyakuliwa juu kati ya mbingu na nchi; na yule nyumbu aliyekuwa chini yake akaenda mbele”.
1Wafalme 10:25 “Wakaleta kila mtu zawadi yake, vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu, na mavazi, na silaha, na manukato, na farasi, na nyumbu, hesabu yake ya mwaka kwa mwaka”.
Soma pia Nehemia 7:68.
Hivyo kwa kuhitimisha, ni kwamba Baghala ndio huyu nyumbu, tunaliyemsoma. Tofauti na farasi na Punda.
Ubarikiwe.
Tazama maana ya maneno mengine ya biblia chini.
Pia ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
About the author