Hisopu/ Hisopo ni nini katika biblia?(Zaburi 51:7)

Hisopu/ Hisopo ni nini katika biblia?(Zaburi 51:7)

Hisopo au Hisopu ni jamii ya mmea, ambao ulitumiwa zamani na wana wa Israeli kwa matumizi mbalimbali. Tazama picha ya mmea wenyewe juu.

Lakini mmea huu sana sana ulitumiwa kwa kwaajili ya shughuli za utakaso wa kimaagano, Kwamfano Hisopo  ilitumika kuwatakasa watu waliokuwa na ukoma na nyumba zote zilizoathiriwa na ugonjwa huu,

Walawi 14:4 “ndipo huyo kuhani ataagiza kwamba watwae kwa ajili yake atakayetakaswa ndege wawili walio hai, ambao ni safi, na mti wa mwerezi, na sufu nyekundu, na hisopo;

5 kisha kuhani ataagiza ndege mmoja achinjwe katika chombo cha udongo kilicho juu ya maji ya mtoni;

6 kisha huyo ndege aliye hai atamshika, na huo mti wa mwerezi, na hiyo sufu nyekundu, na hisopo, naye atavichovya hivyo, pamoja na yule ndege aliye hai, katika damu ya huyo ndege aliyechinjwa juu ya maji ya mtoni;

7 kisha atamnyunyizia huyo atakayetakaswa na ukoma mara saba, naye atasema kwamba yu safi, kisha atamwacha yule ndege aliye hai aende zake nyikani”.

Soma pia Walawi 14:51

  • Hisopo ilitumika pia  kutakasa wana wa waisraeli na vitu vyote vilivyokuwa katika hema ya kukutania..

Waebrania 9:19 “Maana kila amri ilipokwisha kunenwa na Musa kwa hao watu wote, kama ilivyoamuru sheria, aliitwaa damu ya ndama na ya mbuzi, pamoja na maji na sufu nyekundu na hisopo, akakinyunyizia kitabu chenyewe, na watu wote”,

  • Tunaona tena hisopo ilitumika pia kama brashi,

utoka 12:22 “Nanyi twaeni tawi la hisopu, mkalichovye katika ile damu

Brashi la kupakia damu, wakati ule Mungu anawapiga wamisri kwa pigo la mwisho, la kuwaua wazaliwa wa kwanza wa kimisri aliwaambia wana wa Israeli, watwae damu ya kondoo, kisha watumie tawi la hisopo kama brash la kuipaka damu hiyo, kiashirio cha kutakaswa kwao.

Kutoka 12:22 “Nanyi twaeni tawi la hisopu, mkalichovye katika ile damu iliyo bakulini na kukipiga kizingiti cha juu, na miimo miwili ya mlango, kwa hiyo damu iliyo katika bakuli; tena mtu ye yote miongoni mwenu asitoke mlangoni mwa nyumba yake hata asubuhi”.

  • Na katika Zaburi tunaona tena Daudi akimwomba Bwana amsafishe kwa hisopo ili awe safi moyoni mwake,

Zaburi 51:7 “Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji”

  • Na mwisho kabisa tunaona tena, Bwana Yesu akiwa pale msalabani.

Wale askari walitumia ufito wa mmea huu, kushikilizia ile sifongo(sponji), ili kumnywesha Bwana Yesu siki,.

Yohana 19:29 “Kulikuwako huko chombo kimejaa siki; basi wakatia sifongo iliyojaa siki juu ya ufito wa hisopo, wakampelekea kinywani”.

Kama tunavyojua mmea huu ni mmea wa utakaso, ulitumika kusafishia, hatushangai, kuona kwanini Kristo alipelekewa siki kwa mmea huu. Ni kuonyesha kuwa tayari alikuwa ni dhabihu safi iliyotakaswa, iliyowekwa tayari kwa ajili ya kutundolea sisi dhambi zetu.

Hivyo, mimi na wewe, tutatakaswa kwa hisopo ya rohoni si kwa kitu kingine zaidi ya  damu ya Yesu Kristo tu. Kama hatutaoshwa kwa damu hii, kamwe tusitazamie ukoma wetu wa rohoni utaondoka, kamwe tusitazamia unajisi wetu utaondoka, kamwe tusitazamie tutamshinda shetani, na kamwe tusitazamie tutampendeza Mungu.

Swali ni Je! Umesafishwa kwa damu ya Yesu? Kama bado unasubiri nini mpendwa. Mkaribishe moyoni mwako akuokoe hizi ni siku za mwisho. Kuwa serious na maisha yako ya rohoni. Tubu dhambi zako, ufanywe mwana wa Mungu.

Maran Atha.

Tazama maana ya maneno mengine ya biblia chini,

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 693036618 / +255789001312

Mada Nyinginezo:

SIFONGO NA SIKI NI NINI?

Bisi ni nini? (Walawi 23:14, Ruthu 2:14)

Nini maana ya kumlingana Mungu?

Sharoni ni nini au ni wapi kibiblia?(1Nyakati 5:16)

Jabari ni nini, kama linavyotumika kwenye biblia?

Baradhuli/Mabaradhuli ni nini au ni nani kwenye biblia?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

4 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Zaburi lucas nahigombeye
Zaburi lucas nahigombeye
1 year ago

Dinar ni nin?

Lucas mhula
Lucas mhula
2 years ago

Amen