SWALI: Watu ambao hawajasikia kabisa injili, halafu wakafa katika kutokujua chochote kuhusu Yesu, je wao huhesabika kuwa hawana dhambi? Kufuatana na andiko hili?
Yohana 15:22 “Kama nisingalikuja na kusema nao, wasingalikuwa na dhambi; lakini sasa hawana udhuru kwa dhambi yao”.
JIBU: Yesu hakumaanisha kuwa mtu yoyote ambaye hakusikia habari zake, kuwa hatahukumiwa kabisa hapana, bali alimaanisha kuwa watu wa namna hiyo hawatahukumiwa kwa maneno yake, bali watahukumiwa kwa kitu kingine..
Na ndio maana biblia inasema..
Warumi 2:11 “kwa maana hakuna upendeleo kwa Mungu. 12 Kwa kuwa wote waliokosa pasipo sheria watapotea pasipo sheria, na wote waliokosa, wenye sheria, watahukumiwa kwa sheria”.
Warumi 2:11 “kwa maana hakuna upendeleo kwa Mungu.
12 Kwa kuwa wote waliokosa pasipo sheria watapotea pasipo sheria, na wote waliokosa, wenye sheria, watahukumiwa kwa sheria”.
Unaona hapo anasema,..”waliokosa” pasipo sheria “watapotea” pasipo sheria, hasemi wataokolewa pasipo sheria, hapana bali watapotea..kwasababu walikosa katika mambo mengine, na ndio katika hayo hayo Mungu atawahukumia, lakini hatatumia ile sheria ya torati kuwahukumu, kwasababu hiyo hawakuijua hapo kwanza.
Ni vizuri tukafahamu kuwa kuna mambo ya asili ambayo Mungu kayaweka mioyoni mwa wanadamu wote, kiasi kwamba hata kama hajawahi kusikia sheria imekataza kuua, wao wenyewe hawataua, kwasababu wanajua ni makosa..Ukienda kwenye jamii za watu ambao wanaishi maporini hawajui utandawazi ni nini, hawajafikiwa na chochote, bado utawakuta na ustaarabu wao wa maisha na utakuta wamejiwekea mipaka ambayo wanajua kabisa yoyote atakayeivuka ni makosa.
Wanajua kabisa mwanaume kulala na mwanaume mwenzake ni makosa, wanajua, kuiba mali ya mwingine sio sawa, wanajua, kuwapiga wazazi wao ni vibaya, n.k.…hayo mambo hawahitaji kufundishwa na Mungu au mtu yeyote, ni sheria ambayo tayari ipo ndani ya mioyo yao.
Ukisoma tena sehemu nyingine utaona Bwana YESU anasema..
Luka 12:47 “Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana. 48 Na yule asiyejua, naye amefanya yastahiliyo mapigo, atapigwa kidogo”.
Luka 12:47 “Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana.
48 Na yule asiyejua, naye amefanya yastahiliyo mapigo, atapigwa kidogo”.
Unaona tena, anasema yeye asiyejua, lakini amefanya yastahiliyo mapigo atapigwa kidogo.. Kwahiyo, hakuna mwanadamu yoyote ambaye hataingia hukumuni, wote wataingia.
Lakini mbaya Zaidi itakuwa kwetu sisi ambao tumeshasikia habari za Kristo, lakini hatuzitendei kazi, tumeshasikia habari za wokovu wa msalaba lakini tunazipuuzia, sasa sisi tutahukumiwa kwa injili yake. Na adhabu yetu itakuwa ni kubwa sana, kuliko za watu ambao hawajawahi kabisa kusikia habari za Yesu.
Hivyo tuikwepe hukumu ya Mungu. Inatisha.
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika? Ina maana gani?
Nini maana ya “Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati”
Maashera na Maashtorethi ni nini?
TAZAMA, NASIMAMA MLANGONI.
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 6
Je! Kusoma biblia kwenye simu ukiwa kanisani ni dhambi?
Rudi nyumbani
Print this post