Sitara ni nini katika biblia?

Sitara ni nini katika biblia?

Sitara limetokana na neno “sitiri”, na kusitiri maana yake ni “kuficha kitu au jambo” hivyo kitu chochote kinachositiri kinaitwa “Sitara”. Nguo ni mfano wa Sitara, kwani inasitiri maungo yetu.. Kadhalika pazia linalowekwa mlangoni ni mfano wa Sitara, kwani linasitiri mambo yaliyopo ndani, au yanayoendelea ndani n.k

Kwamfano katika biblia tunaona, sehemu ile ambapo Sanduku la Agano lilikuwa linawekwa, paliwekwa pazia ambalo lilikuwa linatenganisha patakatifu, na patakatifu pa patakatifu, ili kulisitiri sanduku la agano lililokuwa ndani, sasa pazia lile lilikuwa linajulikana kama PAZIA LA SITARA.

Hesabu 4:5 “hapo watakapong’oa safari, Haruni ataingia ndani, na wanawe, nao watalishusha PAZIA LA SITARA, na kulifunika sanduku la ushahidi kwa hilo pazia;”

Pia unaweza kusoma juu ya pazia hilo katika Kutoka 35:12, Kutoka 39:34, Kutoka 40:21 na Kutoka 36:37.

Na katika wakati wetu huu, sitara yetu ni YESU KRISTO. Yeye pekee ndiye aliyechukua dhambi zetu, na kusitiri uovu wetu kupitia msalaba, maana yake pale tunapomwamini na kutubu, dhambi zetu zote zinasitirika mbele za Baba, na tunaonekana kama hatujawahi kutenda dhambi kabisa, yeye ndio kama vazi letu , kufahamu zaidi, ni kwa namna gani Yesu ni vazi letu (Sitara yetu) fungua hapa >> Mtakatifu ni nani?.

Pamoja na hayo, Yesu ni sitara yetu dhidi ya madhara yote yanayoletwa na yule adui yetu shetani, kama  vile shida, magonjwa na adha.

Zaburi 32:7 “Ndiwe sitara yangu, utanihifadhi na mateso, Utanizungusha nyimbo za wokovu”.

Zaburi 119:114 “Ndiwe sitara yangu na ngao yangu, Neno lako nimelingojea”.

Hivyo ni Baraka kubwa kumfanya Bwana, sitara yetu…Lakini ni laana kubwa kumfanya shetani au wanadamu kuwa sitara yetu.

Yeremia 17:5 “Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana

6 Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu.

 7 Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake.

  8 Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa hari ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda”

Ukimkataa Bwana moyoni mwako, na kuikubali sayansi, hutaona mema yatakapotokea, utakuwa umelaaniwa biblia inasema hivyo.

Bwana atusaidie tuzidi kumfanya yeye SITARA YETU YA DAIMA. Ngome yetu, kimbilio letu, msaada wetu na jabali letu.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

NAMNA YA KUITAMBUA SAUTI YA MUNGU INAPOZUNGUMZA NA WEWE

WAPE WATU WANGU RUHUSA ILI WAPATE KUNITUMIKIA.

KUNA MAJIRA MUNGU ATAIVURUGA MIPANGO YETU.

NI KWA NAMNA GANI ROHO HUTUTAMANI KIASI CHA KUONA WIVU?

MANA ILIYOSHUSHWA KUTOKA MBINGUNI.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Mangala Tambatamba Augustin
Mangala Tambatamba Augustin
1 year ago

Mungu akubariki sana mtumishi wa Mungu