Je! Mwandishi wa kitabu cha Warumi alikuwa ni Paulo au Tertio?

Je! Mwandishi wa kitabu cha Warumi alikuwa ni Paulo au Tertio?

SWALI: Je! Mwandishi wa kitabu cha Warumi alikuwa ni Paulo au Tertio? kulingana na mstari huu;

Warumi 16:22 “Mimi Tertio, niliyeandika waraka huu, nawasalimu katika Bwana”.


JIBU: Paulo katika maneno yake ya utangulizi alishatupa  mwangaza kuwa yeye ndiye aliyekiandikia kitabu hicho, kiwaelekee watakatifu wote waliokuwa Rumi. Tusome;

Warumi 1:1 “PAULO, MTUMWA WA KRISTO YESU, ALIYEITWA KUWA MTUME, NA KUTENGWA AIHUBIRI INJILI YA MUNGU;

2 ambayo Mungu amekwisha kuiahidi kwa kinywa cha manabii wake katika maandiko matakatifu;

3 yaani, habari za Mwanawe, aliyezaliwa katika ukoo wa Daudi kwa jinsi ya mwili,

4 na kudhihirishwa kwa uweza kuwa Mwana wa Mungu, kwa jinsi ya roho ya utakatifu, kwa ufufuo wa wafu, Yesu Kristo Bwana wetu;

5 ambaye katika yeye tulipokea neema na utume ili mataifa yote wapate kujitiisha kwa imani, kwa ajili ya jina lake;

6 ambao katika hao ninyi mmekuwa wateule wa Yesu Kristo;

7 KWA WOTE WALIOKO RUMI, WAPENDWAO NA MUNGU, WALIOITWA KUWA WATAKATIFU. Neema na iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo”.

Lakini baadaye karibia na mwishoni mwa waraka huu tunakuja kumwona mtu mwingine aliyeitwa Tertio akijitokeza na kusema ameuandika waraka ule. Sio kwamba mtume Paulo hakuhusika hapana, Jibu ni kwamba Tertio alikuwa ni mwandishi wa mtume Paulo, aliyekuwa anamwandikia nyaraka zake. Aidha kwa kuandika kile alichokuwa anaambiwa au kwa kunakili kile alichoandikiwa na Paulo, japo hakuna sehemu nyingine katika biblia Tertio anaonekana akitajwa.

Na kulikuwa na sababu ya mtume Paulo kutokutumia mkono wake mwenyewe kuandikia waraka huu, pengine Tertio alikuwa ni mwandishi  mwaminifu anayejulikana sana  na watakatifu waliokuwa Rumi kwa umahiri na ufanisi wa kazi zake zilizothibitishwa. Hivyo mtu akiona waraka ulionakiliwa na yeye, basi ilikuwa ni rahisi kuamini uhalisia wa yule mwandishi husika. Kwasababu wakati huo walikuwepo pia watu waliojifanya ni mitume, na kutoa kopi zao wakidai kuwa ni za mitume, ili tu kuwachanganganya watu.

Na ndio maana mtume Paulo ili kuthibitisha nyaraka zake, sehemu nyingine alikuwa anatia sahihi yake mwishoni, soma(2Wathesalonike 3:17), na pia na hapa aliona  ni vema amtumie huyu Tertio kuuandika kwa warumi, iwe kama sahihi yake.

Hivyo waraka huu uliandikwa na Paulo, lakini aliyeunakili ni Tertio.

Hii ni kutufundisha kuwa, si kila kazi ya Mungu, hata kama tutaiona  ni nyepesi kiasi gani, tuifanye sisi mwenyewe, wakati mwingine tutahitaji tushirikiane na viungo vingine vya Kristo, ili kuleta ufanisi Zaidi wa kazi hiyo kwa watu wake.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 6

Je Musa yupo anawashitaki watu..kulingana na Yohana 5:45?

Tofauti kati ya mtume na mwanafunzi ni ipi kibiblia?

MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA FILEMONI.

Kwa herufi gani kubwa nimewaandikia kwa mkono wangu mimi mwenyewe.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments