JIFUNZE KUSEMA NA MUNGU KATIKA HALI ZOTE.

JIFUNZE KUSEMA NA MUNGU KATIKA HALI ZOTE.

Kumbuka Mungu yupo katika masumbufu, Na pia Mungu yupo katika utulivu. Katika majira yote na wakati wote jifunze kuzungumza na kuisikia sauti ya Mungu.

Unaweza ukajiuliza ni kwanini Mungu alimtokea Ayubu katika upepo wa kisulisuli na kuzungumza naye, (Ayubu 38:1), lakini Eliya alimtokea katika mazingira ya utulivu mkuu?.(1Wafalme 19:11-13)

Jibu ni kuwa sio kwamba alikuwa anataka kumtisha Ayubu hapana bali alikuwa anataka kumuonyesha kuwa katikati ya misukosuko, katikati ya tufani za Maisha, katikati ya dhiki, katikati ya shida, katikati ya magonjwa, na umaskini yeye yupo hapo kuzungumza naye na kumsaidia. Biblia inasema..

Nahumu 1:3b “..Bwana ana njia yake katika kisulisuli na tufani,…”

Vilevile alipojifunua kwa Eliya katika sauti ya upole na utulivu, alikuwa hamwonyeshi kuwa yeye anajua kuongea kwa utulivu sana, na upole hapana, lakini alikuwa anamwonyesha kuwa katikati utulivu na amani yeye pia yupo kuzungumza na watu wake.

Mwanzoni Ayubu alidhani Mungu amemwacha kwa dhiki alizokuwa anazipitia ,alidhani hastahili tena mbele za Mungu, hata Mungu alipokuwa anasema naye kwa kinywa cha Elihu mwana wa Barakeli, hakutambua, alidhani Mungu kakaa mbali naye, mpaka akadhubutu kusema laiti kama Mungu angekuja nihojiane naye (Ayubu 13:3) akidhania kuwa Mungu yupo mbali naye.

Kumbe hakujua Mungu alikuwa karibu naye kuliko alivyokuwa anadhani. Leo hii lipo kundi kubwa la wakristo, linadhani pale palipo na amani tu, pale palipo na mafanikio tu ndio Mungu yupo hapo katikati yao, pale wanapopitia raha, wanapokuwa katika afya na mafanikio katika biashara zao, pale wanapopata heshima  hapo ndipo wanaweza kukaa chini na kuzungumza na Mungu.

Lakini pale mambo yanapoharibika kwa ghafla, tufani na upepo kidogo wa kusulisuli unapovuma juu yao wanamtupa Mungu nyuma yao, wanasema Mungu hawezi kuwepo hapa ameniacha, wanapopitia dhiki kidogo utaona ni rahisi kupoa kama sio kuuacha wokovu kabisa, wanapougua, hawategi sikio tena kusikia chochote kuhusu Mungu. Wanachofanya ni kukimbilia kutafuta njia mbadala kwa ajili ya suluhu za shida zao.

Kumbuka biblia inasema.. Nahumu 1:3b “..Bwana ana njia yake katika kisulisuli na tufani,…”

Unaona, sio tu katika mahali pa utulivu, lakini pia katikati ya Tufani na kisulisuli. Wakati mwingine Mungu atakujilia kwa njia hii. Hivyo uonapo hayo ikiwa wewe ni mkristo, usiogope.

Kuna wakati mtume Paulo alipitia njaa mara nyingi lakini hakumwacha Bwana. Kuna wakati alipitia kutajirika sana lakini bado aliendelea na Bwana.. mpaka akadhubutu kusema ninayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.

Wafilipi 4:12 “Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yo yote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa.

13 Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu”.

Je na sisi  tunaweza kusimama kwa ujasiri na  kuzungumza na Mungu katika tufani ? Bwana atusaidie tuyatambue na hayo ili tusiiache Imani, kwasababu maadamu tupo duniani, Mambo ya ghafla yanaweza kututokea, lakini hatupaswi kumtupa Mungu nyuma.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

Mtu mwenye “kitango” ni mtu wa namna gani kibiblia?

Shubaka ni nini kibiblia? (Mithali 7:6)

USIISHI KWA NDOTO!

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 9 (Kitabu cha Ayubu).

Maswali na Majibu

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments