Je ni kweli siku ya mwisho dunia itakunjwa kama karatasi na kutupwa motoni?

Je ni kweli siku ya mwisho dunia itakunjwa kama karatasi na kutupwa motoni?

Jibu: Hakuna mstari wowote katika biblia takatifu unaosema kwamba dunia siku moja itakunjwa kama karatasi na kutupwa motoni. Mstari ambao unawachanganya wengi ni ule wa Isaya 34:4 unaosema..

Isaya 34:4 “Na jeshi lote la mbinguni litafumuliwa, NA MBINGU ZITAKUNJWA KAMA KARATASI, na jeshi lao lote litanyauka kama vile jani la mzabibu linyaukavyo na kupukutika, na kama jani la mtini linyaukavyo na kupukutika.”

Ukiisoma hiyo Isaya 34, utaona ni unabii wa Siku ya mwisho. Na katika huo mstari wa 4,  unabii unasema kuwa siku hiyo  “mbingu zitakunjwa kama karatasi”. Hapo anasema “mbingu” na si “nchi” au “ardhi” au “dunia”  bali mbingu!!. Hizo ndizo zitakazokunjwa kama karatasi… Na mbingu inayozungumziwa hapo sio ile Malaika watakatifu waliyopo, La!.. bali ni hii tunayoiona yenye nyota, mwezi na jua, na sayari.

Na hazitakunjwa kama karatasi na kisha kutupwa motoni!.. La! Maandiko hayajasema hivyo, yameishia tu hapo kusema kuwa zitakunjwa kama karatasi. Na kukunjwa kunakozungumziwa hapo sio kukunjwa  kwa kusokotwa sokotwa kama uchafu, hapana! Bali kukunjwa kama vile mtu anayekunja ngozi.

Sasa ili tuelewe vizuri zitakunjwaje kunjwaje siku hiyo kama karatasi, twende pamoja kwenye kitabu cha Ufunuo.

Ufunuo 6: 12 “Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu,

13  NA NYOTA ZIKAANGUKA JUU YA NCHI KAMA VILE MTINI UPUKUTISHAVYO MAPOOZA YAKE, UTIKISWAPO NA UPEPO MWINGI.

14  MBINGU ZIKAONDOLEWA KAMA UKURASA ULIVYOKUNJWA, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake.

15  Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima,

16  wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo.

17  Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?”

Umeona hapo?.. Katika siku ile ya mwisho, muhuri wa 7 utakapofunguliwa, wakati Yesu atakaporudi na watakatifu wake aliowanyakua. Siku hiyo, nyota zitaanguka, (maana yake zitaondolewa). Ghafla tu, watu watashangaa jua limezama wakati wa adhuhuri, na mwezi umekuwa mwekundu kama damu.. na juu nyota zinaanza kujikusanya pamoja na kuanguka..kama vile ukurasa (Yaani karatasi) linavyofunguliwa..

Tunaweza kulisoma tena jambo hilo vizuri katika kitabu cha Mathayo..

Mathayo 24:27  “Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.

28  Kwa kuwa po pote ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai.

29  Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, NA NYOTA ZITAANGUKA MBINGUNI, NA NGUVU ZA MBINGUNI ZITATIKISIKA;

30  ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi”

Unaweza kusoma pia unabii huo katika Isaya 13:9-11.

Kwahiyo dunia haitakunjwa kunjwa na kutupwa motoni, bali ni mbingu, na mbingu hizo hazitakunjwa na kutupwa motoni, bali zitaanguka (maana yake zitaondolewa!!). Na tendo hilo litatokea baada ya unyakuo wa kanisa kupita na  dhiki kuu kupita, wakati ambapo Kristo atarudi kwa mara nyingine pamoja na watakatifu wake wale walionyakuliwa, sasa wale  ambao watakuwa wamesalia duniani, waliopokea chapa, na kunusurika katika mapigo ya vitasa saba, watalishuhudia hilo tendo la mbingu kuondolewa kama ukurasa, siku hiyo jua litazima ghafla na mwezi utakuwa kama damu, na wataona nyota zinashuka kama vile vimondo vinavyoonekana usiku… Na kutokana na hilo tendo, itasababisha dunia iwe katika giza nene sana, kwasababu hakuna jua, mwezi unaoangaza wala nyota..

 Na wakiwa katikati ya hilo giza nene watamshuhudia Kristo akitokea mawinguni kwa utukufu mwingi kama umeme, pamoja na wale watakatifu wake aliowanyakua, na chini ya ardhi visiwa vitahama, na kutatokea na tetemeko ambalo halijawahi kutokea mfano wake,  watu wote watakufa, isipokuwa kundi dogo, ambalo lilihifadhiwa kuingia katika ule utawala wa miaka elfu, Kristo atakapotawala na bibi arusi wake hapa duniani.

Bwana atusaidie tusiukose unyakuo, ili siku moja tutawale naye tukiwa kama makuhani na wafalme. Ni heri tukose kila kitu katika huu ulimwengu lakini tusiikose mbingu.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Nini maana ya ‘kuhuluku’ kama tunavyosoma katika biblia?

“Kinga kilichotolewa motoni “Kinafunua nini kibiblia?

UPUMBAVU WA MUNGU.

MATARAJIO YA KILA MWANADAMU DUNIANI NI YAPI?

KRISIMASI (CHRISTMAS) NI NINI? JE IPO KATIKA BIBLIA?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments