JIBU: Tukumbuke kuwa “sala ya Toba” sio wokovu, Sala ya toba ni njia mojawapo, inayotumiwa kuukaribisha wokovu ndani ya mtu, lakini sala kama sala yenyewe sio wokovu, Ikiwa na maana zipo njia nyingine, Na ndio maana huwezi kuona mahali popote mitume waliwaambia watu wafuatisha sala fulani, kwamba kwa hiyo ndio wataokoka..Huwezi kuona.
Wokovu unatoka moyoni. Pale mtu anapojitambua kuwa ni mwenye dhambi, na hivyo anahitaji kukombolewa kutoka katika mauti na Yesu Kristo, kitendo kinachompelekea kuyasalimisha maisha yake yote kwa Bwana Yesu ayaongoze, na kuachana na mambo ya ulimwengu, Huo ndio wokovu.
Sasa jambo kama hili likishatokea ndani ya mtu, udhihirisho wa nje ndio unafuata, ambao mojawapo ndio kukiri kwa kinywa chako, na cha pili ni Matendo yako.
Kutimiza lile andiko la Warumi 10:9
“Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka”.
Sasa mabubu, hawajajaliwa kuongea, hawawezi kumkiri Kristo kwa vinywa vyao..Lakini wanaweza kuonyesha kuwa wamemwanini Kristo kwa matendo yao. Wakifanya hivyo tayari huo ni wokovu tosha, kutoka kwa Bwana.. Hivyo mtu kama huyu ikiwa tayari ameshamwani Bwana muhimize tu, aanze kuenenda sawasawa na kuamini kwake.
Tutakumbuka kisa kile cha Yule mwanamke ambaye Bwana Yesu alisema alikuwa na dhambi nyingi, jinsi alivyomwendea na kulia sana miguuni pake, kudhihirisha majuto ya makosa yake, kisha kumpangusa kwa nywele zake, Utaona pale Bwana Yesu hakuzungumza naye maneno yoyote, kwamba njoo nikuongoze sala ya toba, au sema maneno haya au yale, hapana isipokuwa alipoona tu moyo wake wa toba ulivyomaanisha kwelikweli alimwambia.. “Mwanamke umesamehewa dhambi zako”
Luka 7:36-48
“36 Mtu mmoja katika Mafarisayo alimwalika ale chakula kwake; akaingia katika nyumba yake yule Farisayo, akaketi chakulani.
37 Na tazama, mwanamke mmoja wa mji ule, aliyekuwa mwenye dhambi, alipopata habari ya kuwa ameketi chakulani katika nyumba ya yule Farisayo, alileta chupa ya marimari yenye marhamu.
38 Akasimama nyuma karibu na miguu yake, akilia, akaanza kumdondoshea miguu machozi yake, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake, akiibusu-busu miguu yake na kuipaka yale marhamu.
39 Basi, yule Farisayo aliyemwalika alipoona vile, alisema moyoni mwake, Mtu huyu kama angekuwa nabii, angemtambua mwanamke huyu amgusaye, ni nani, naye ni wa namna gani, ya kwamba ni mwenye dhambi…..
44 Akamgeukia yule mwanamke, akamwambia Simoni, Wamwona mwanamke huyu? Niliingia nyumbani kwako, hukunipa maji kwa miguu yangu; bali huyu amenidondoshea machozi miguu yangu, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake
45 Wewe hukunibusu; lakini huyu tangu nilipoingia hakuacha kunibusu sana miguu yangu.
46 Hukunipaka kichwa changu mafuta; bali huyu amenipaka miguu yangu marhamu.
47 Kwa ajili ya hayo nakuambia, Amesamehewa dhambi zake ambazo ni nyingi, kwa kuwa amependa sana; lakini asamehewaye kidogo, huyo hupenda kidogo.
48 Kisha alimwambia mwanamke, Umesamehewa dhambi zako.
Hii kuonyesha kwamba, pale unaoonyesha geuko la kweli moyoni mwako, kabla hata hujazungumza chochote tayari umeshasamehewa.
Ndivyo ilivyo kwa mabubu, haijalishi hawataweza kukiri sala yoyote kwa vinywa vyao, lakini ikiwa moyoni mwao wameonyesha mabadiliko, hicho ndicho Mungu anachokitaka. Imekuwa desturi leo hii kuona kundi kubwa la watu wanasema wameongozwa sala ya toba na kumkiri Yesu , lakini ukitazama matendo yao hayaendani na walichokikiri. Huo ni unafki ambao unamchukiza Bwana sana.
Mathayo 15:7 “Enyi wanafiki, ni vema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu, akisema,
8 Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami”.
Bwana anataka tumfuata na tumwabudu katika Roho na kweli. Na sio katika maneno matupu. Ikiwa mtu asiweza kuongea, amesimama katika wokovu, huyo mtu ni wa thamani sana mbele za Mungu
Swali ni je wewe, uliyemkiri Bwana, unayemsifu, unayemuhubiri, unayemtangaza. Je! Ni kweli kitokacho mdomoni mwako, kimeambatana na badiliko la ndani?
Majibu tunayo.
Bwana atusaidie.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Utasi ni ugonjwa gani? (Marko 7:32).
Kiungo chako kimoja kikikukosesha kikate. Ina maana gani?
Dusumali ni nini katika biblia?
Matoazi na Matari ni nini? (Kutoka 15:20)
Je Malaika Mikaeli ndiye Yesu mwenyewe?
Tofauti kati ya mbinguni, peponi, Kuzimu, Jehanamu, na Paradiso ni ipi?
Jibu: Kuna tofauti ya “Utasi” na “Utasa”.. Utasa ni hali ya mtu kutokuwa na uwezo wa kuzaa, lakini Utasi ni tatizo la udhaifu wa ulimi (yaani ulimi kuwa mzito), Mtu mwenye ugonjwa huu anakuwa hawezi kuongea vizuri, anakuwa hawezi kutamka maneno vizuri..Na wengi wenye tatizo hili wanakuwa wanazaliwa nalo.
Katika biblia tunaona ugonjwa huu ukitajwa mara moja tu!, kwa mtu mmoja ambaye Bwana Yesu..
Marko 7:32 “Wakamletea kiziwi, NAYE NI MWENYE UTASI, wakamsihi amwekee mikono.
33 Akamtenga na mkutano faraghani, akatia vidole vyake masikioni mwake, akatema mate, akamgusa ulimi,
34 akatazama juu mbinguni, akaugua, akamwambia, Efatha, maana yake, Funguka.
35 Mara masikio yake yakafunguka, kifungo cha ulimi wake kikalegea, AKASEMA VIZURI”.
Maandiko yanasema Bwana Yesu ni Yule Yule, alimponya mtu huyo, hata leo bado anaponya!, na haponyi Utasi tu peke yake, bali anaponya kila shida.. Na uponyaji mkuu kuliko yote ambao Bwana anautoa ni uponyaji wa Roho zetu. Huo ndio muujiza mkubwa ambao Bwana anaweza kutufanyia endapo tukimwamini.
Anatuponya roho zetu na mauti ya kiroho, na anatuokoa na ghadhabu ya Mungu, iliyo karibuni kumwangwa kwa ulimwenguni kwa watenda dhambi.
Je umepokea uponyaji huo leo?.. kama bado Tubu, mwamini Yesu na ukabatizwe katika ubatizo sahihi na kisha utapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Na ulimi laini huvunja mfupa.(Mithali 25:15)
USIMLAANI KIZIWI, WALA USITIE KWAZO MBELE YA KIPOFU.
TATIZO LA NDANI LINALOWASUMBUA VIJANA, WALIOOKOKA.
USIKATE TAMAA UNAPOPITIA MAGONJWA.
Nini maana ya “Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati”
Jina la Bwana wetu, Yesu Kristo libarikiwe.. karibu tujifunze biblia, Neno la Mungu wetu.
Bwana Yesu alisema maneno haya katika Luka maneno haya..
Luka 16:8 “…..kwa kuwa wana wa ulimwengu huu katika kizazi chao wenyewe HUWA NA BUSARA KULIKO WANA WA NURU”.
Maana yake.. “Watu wa ulimwengu huu, wasiomjua Mungu, au walio mkataa Mungu, katika mambo yao wanayoyafanya yasiyo ya kiMungu, basi huyafanya kwa busara ya hali ya juu, Zaidi hata ya watu wanaokiri kumjua Mungu”.
Na hiyo ni kweli kabisa.. Huoni leo watu wa kidunia walivyo makini na kazi zao na shughuli zao?.. Utaona wanawahi kuamka mapema na kwenda kwenye shughuli zao hata kama ni haramu..(kamwe hawachelewi kazini).. Lakini leo hii, wana wa Mungu utaona kanisani wanachelewa na kuwa watu wa kutoa udhuru sana.
Lakini leo nataka tulitafakari jambo lingine, ambalo linafanywa na watu wa ulimwengu huu, ambalo si la kiMungu lakini lina busara ndani yake!..(Na kupitia hilo, basi sisi tupate hekima).. kwasababu biblia imeruhusu tuwatazame watu na viumbe vya ulimwengu, jinsi vinavyoenenda katika mambo yao, na kisha tupate hekima na mafunzo kutoka kwao..
Kwamfano utaona hekima inatufundisha tuwatazame chungu, kisha tujifunze kuacha uvivu kutoka kwao…
Mithali 6:6 “Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapate hekima”.
Chungu ni “SIAFU”.. Jinsi gani Siafu, wanavyofanya kazi usiku na mchana na kwa ushirikiano, (kamwe huwezi kukuta siafu kapumzika, muda wote yupo bize na mambo yake).. Vile vile na sisi wakristo hatupaswi kuwa na kipindi chochote cha kupumzika pindi, tuwapo katika mambano ya kiimani, hatuna budi kuendelea kuomba, kukesha, kuhubiri na kuwa watakatifu, hakuna kuchukua likizo, wala kupumzika katika mambo hayo, mpaka mwisho wa safari yetu ya hapa duniani. Mapumziko yetu yapo mbinguni, kule ndio kuna pumziko la kweli.
Lakini leo, tulitafakari jambo lingine ambalo linaendelea katika Taifa moja la Afrika mashariki, na Taifa hilo ni Tanzania, na tukio lenyewe ni “MBIO ZA MWENGE WA UHURU”.
Je! Umewahi kusikia au kufuatilia, juu ya Mwenge wa Uhuru wa Tanzania?. Kama bado basi jifunze leo hapa..
Mwenge ni Taa, inayotumia utambi wenye mafuta, kama vile kibatari.. tofauti ya kibatari na mwenge ni kwamba mwenge ni mkubwa kuliko kibatari, hivyo unamulika sehemu kubwa zaidi..Na mwenge kazi yake ni moja tu!, nayo ni kutoa Nuru!
Taifa la Tanganyika baada ya kupata Uhuru, Lilitengeneza Mwenge mdogo na kuuwasha na kwenda kuuweka juu ya mlima Kilimanjaro..(Ambapo ndio sehemu iliyoinuka kuliko zote katika Taifa hilo, na hata katika Afrika yote kwa ujumla).
Sawasawa na maneno ya Bwana Yesu aliyosema katika Luka..
Luka 11:33 “Hakuna mtu awashaye taa na kuiweka mahali palipositirika, au chini ya pishi; bali huiweka juu ya kiango, ili waingiao wapate kuuona mwanga”.
Na ndivyo, Taifa hilo lilivyoupandisha huo Mwenge, mahali pa juu kuliko pote.. Sasa sijui ni roho gani iliyowasukuma kufanya tendo hilo..
Lakini Tafsiri ya Mwenge huo na sababu ya kuuwasha na kuuweka juu ya mlima Kilimanjaro, kulingana na waasisi wa Tanganyika, ilikuwa ni hii…
“Mwenge wa uhuru ni Kiiashiria kinachoangaza nchi, lengo lake ni kuangaza Matumaini palipo na kukata tamaa, kuangaza Upendo palipo na Uadui, na kuhubiri heshima palipo na Chuki, na kutangaza amani katika nchi ya Tanganyika na hata nje ya mipaka ya nchi”.
Na zaidi sana, kifaa hicho hakikuishia kukaa tu juu ya mlima Kilimanjaro, bali kilishushwa na kufanywa kuzunguka nchi nzima, mkoa kwa mkoa, wiliaya kwa wilaya, kata kwa kata, na kitongoji kwa kitongoji.
Jambo ambalo lina hekima ndani yake!.. “kibatari kilichopo juu ya Meza hakiwezi kumulika, sarafu iliyopotea chini ya uvungu wa kitanda..” ili kuipata sarafu iliyopo chini ya kitanda, au nyuma ya kabati, mtu hana budi kukitoa kibatari mezani, na kukishusha chini, aweze kumulika, na kama sarafu haipo chini ya uvungu, basi kibatari kile kitazungushwa katika nyumba nzima..mpaka ipatikane..
Na Mwenge wa Uhuru wa Tanganyika ni hivyo hivyo.. unazungushwa katika Taifa zima, kuhubiri mambo hayo matatu.. (Upendo, Tumaini, amani na Heshima).
Swali la kujiuliza, Je!, Mwenge wa Uhuru umesaidia kuleta Amani, upendo na Heshima katika Taifa hilo?.. Jibu ni ndio!.. Kwasababu WALIKUWA NA HEKIMA KATIKA MAMBO YAO, Mungu akawajalia adhimio lao!. Huoni leo Taifa la Tanganyika lina Amani?..huoni jinsi makabila mengi yanavyakaa Pamoja kwa kuheshimiana??..ingawa kuna makabila Zaidi ya 100, lakini yote hayo yanakaa kwa Umoja.
Kwa kuona umuhimu wa Amani, Upendo na Heshima, na kwa kutumia kiashiria hicho cha Mwenge, Mungu amelikirimia Taifa hilo, Mambo hayo; Amani, Upendo na Heshima. Na tangu Mwenge huo uwashwe juu ya mlima Kilimanjaro, mpaka leo haujazimwa, na ni moja ya alama ya nembo ya Taifa.
Lakini je!.. Na Sisi wakristo Mwenge wetu wa Uhuru uko wapi? (tumeuweka wapi)?..Upo unawaka au umeshazima kitambo?
Bwana alipokufa pale Kalvari, tulipata uhuru, kutoka dhambini..Na Bwana Yesu alisema matendo yetu ndiyo Mienge ya Uhuru wetu tulioupokea, kwamba hatuna budi kuyafanya yaangaze mbele za Watu..
Mathayo 5:14 “Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima.
15 Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani.
16 Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni”.
Je Mwenge wako unaangaza?..Na kama ndio je unaangaza ukiwa wapi??.. Juu kabisa au chini peke yake!..Mwenge wa watu wa mataifa uliwekwa juu kabisa katika mlima mrefu kuliko yote, na vile vile ulikuwa ukizunguka zunguka kutafuta mahali uovu ulipojificha!…
Je wewe Mwenge wako upo wapi?..
Matendo yako ni taa kwa ulimwengu??..au ni vuguvugu, leo upo disko, kesho upo kanisani, leo unakunywa pombe kesho unaimba tenzi??.. leo unaimba kwaya kesho unazini.
Unadhani ni kwa faida ya nani?. Rejea leo kwa Bwana, na amua kumfuata kwa moyo mmoja, usiwe mtu mwenye moyo uliyegawanyika, kwasababu Bwana alisema atawatapika watu wa namna hiyo.
Ufunuo 3:15 “Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.
16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.
17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.
18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.
19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.
20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami”.
Bwana akubariki.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru
UPENDO NI NINI NA JE! KUNA AINA NGAPI ZA UPENDO?
Hawa ndege katika Walawi 11:13-19 ndio ndege gani kwasasa?
NITAUPATAJE UPENDO WA KI-MUNGU NDANI YANGU?
Kutia mkono chini ya paja kama ishara ya kiapo, kulimaanisha nini?