VICHEKESHO NA UTANI MADHABAHUNI

VICHEKESHO NA UTANI MADHABAHUNI

Je madhabahu ni sehemu ya kufanyia mizaha, utani, vichekesho au vituko?..

Zaburi Sura ya kwanza kabisa na mstari wa kwanza unasema…

” Heri mtu yule asiyekwenda katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha”.

Mtu anayefanya mizaha madhababuni au utani ni wazi kuwa hamheshimu Mungu..na hofu ya Mungu imeshaondoka ndani yake..hamwogopi tena Mungu…Yeye pale madhabahuni haoni tofauti na kumbi za kidunia. Na mtu akishafikia hali kama hiyo ni ngumu kutubu. Kama ilivyokuwa kwa wana wa Eli, ofni na Fineasi…waliidharau Nyumba ya Mungu na kuigeuza kituo cha kufanyia ukahaba..kwani walikuwa wanalala na wanawake waliokuwa wanahudumu katika hema ya Mungu(1Samweli 2:22)…Na walipoonywa hata hawakutaka kusikia.

Mithali 15:12 “Mwenye mzaha hapendi kukaripiwa; Wala yeye hawaendei wenye hekima”.

Madhabahuni sio sehemu ya kufanyiana mizaha, sio sehemu ya kujipigia piga picha (selfie), sio sehemu ya kupigia stori, sio sehemu ya kulia chakula, sio sehemu ya kuchumbiana, wala si sehemu ya kusimama huku unatafuna vitu mdomoni…wala si sehemu ya kupanda pale na huku umevaa kihuni au kikahaba…

Kadhalika madhabahuni  si sehemu ya kuchezea DANSI, Kwamba  unapanda na kucheza kidunia…wala si sehemu ya kwenda kufanya vituko kama vile jukwaa la vichekesho…Ni sehemu ya Ibada kwa Mungu wetu..

Mungu wetu hashuki pale kuja kukutana na vichekesho vyetu au mizaha yetu, au utani wetu…. anashuka pale kuja kukutana na haja zetu na dua zetu na mahitaji yetu…Hivyo kuigeuza kuwa sehemu ya vichekesho na mizaha ni kumkufuru Mungu na hivyo kujitafutia laana badala ya baraka.

Hata madhabahu za mashetani huwa hazifanyiwi mizaha si zaidi madhabahu ya Mungu aliye hai?

Kumbuka pale ni sehemu iliyorasimishwa kwa Mungu muumba wa mbingu na nchi, aliye msafi na mtakatifu na wala asiyekuwa na mizaha..Hivyo kama yeye mwenyewe anapaheshimu  na kushuka hapo inatupasaje sisi?..Ukisoma katika kitabu cha Ufunuo 4 utaona Mungu anaonekana ameketi katika kiti chake cha enzi huku akiwa amezungukwa na wazee 24..Wale ni wazee na sio vijana, ikimaanisha kuwa wamekomaa kiakili na wenye busara na si mizaha…Hao ndio wanaomsogelea Mungu mbinguni..

Na sisi tunapomsogelea Mungu katika nyumba yake hatuna budi kuivaa hekima kama ya wazee ili tuweze kumkaribia Mungu kwa baraka na si laana..kwasababu yeye hapendi mizaha na wanaofanya utani.. kwasababu anatuheshimu sana hivyo na sisi tunapaswa tumheshimu zaidi sana.

Kama ni mchungaji, mwalimu au Askofu…

>ACHA! kufanya mizaha madhabahuni mwa Mungu aliye hai.

>ACHA KUTUMIA MASAA KUCHEKESHA WATU BADALA YA KUTIMIZA WAJIBU WAKO WA KUHUBIRI INJILI KAMILI YA YESU KRISTO

>ACHA Kutaniana na watu madhabahuni..Siku ile utatoa hesabu kila Neno lisilo na maana linalotoka katika kinywa chako.

> Kama wewe ni muumini, Madhabahuni na hata kanisani kwa ujumla sio mahali pa kukatiza katiza bila kuwa na shughuli yoyote ya maana, wala si mahali pa kupiga piga makelele…Ufikapo nyumbani mwa Mungu paheshimu, zima simu yako.. Na ukae utulie..Hata kama ni mtoto wa mchungaji au mke wa Mchungaji…Huna Ruhusa ya kupageuza pale Nyumbani..Hiyo ni kwa faida yako binafsi.

BWANA WETU ANAKUJA.


Mada Nyinginezo:

FIMBO YA HARUNI!

JE KUJIUA NI DHAMBI?

USIPOKUWA MWAMINIFU, NAFASI YAKO ITACHUKULIWA.

JISHUSHE ILI MUNGU AKUHUDUMIE.

KUTAHIRIWA KIBIBLIA

IFANYE KAZI YA MUNGU PASIPO HOFU!

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Benjamin
Benjamin
6 months ago

Amen