Category Archive Home

Kwanini Yeremia ailaani siku yake ya kuzaliwa? (Yeremia 20:14)

Swali: Kwanini Nabii Yeremia ailaani siku aliyozaliwa?, na je ni sahihi kulaani siku tulizozaliwa?

Jibu: Turejee maandiko hayo kuanzia ule mstari wa 14 hadi wa 17..

Yeremia 20:14 “Na ilaaniwe siku niliyozaliwa, isibarikiwe siku ile aliyonizaa mama yangu.

15 Na alaaniwe mtu yule aliyemletea baba yangu habari, akisema, Umezaliwa mtoto mwanamume; akimfurahisha.

16 Mtu huyo na awe kama miji ile, ambayo Bwana aliiangamiza, asijute; na asikie kilio asubuhi, na kelele za fujo adhuhuri;

17 kwa sababu hakuniua nilipotoka tumboni, na hivyo mama yangu angekuwa kaburi langu, na mimba yake sikuzote nzito”.

Utaona sababu kuu ya Nabii Yeremia kuzungumza maneno yale ni “mateso aliyokuwa anayapitia katika huduma yake”.. kwani alipitia mapigo na  vifungo vingi na aliwindwa kila mahali kwasababu ya maneno ya Mungu (Soma Yeremia 20:1-2, Yeremia 37:15-16, Yeremia 38:6, Yeremia 15:5)…kama mstari wa 18 unavyoelezea.

“..18 Nalitoka tumboni kwa sababu gani, kuona taabu na huzuni, hata siku zangu ziharibike katika aibu?”

Na si tu Nabii Yeremia aliyeilaani siku yake aliyozaliwa, bali tunaona pia Ayubu naye alisema hayo hayo..

Ayubu 3:1 “Baada ya hayo Ayubu akafunua kinywa chake, na kuilaani siku yake.

2 Ayubu akajibu, na kusema;

3 Na ipotelee mbali ile siku niliyozaliwa mimi, Na ule usiku uliosema, Mtoto mume ametungishwa mimba.

4 Siku hiyo na iwe giza; Mungu asiiangalie toka juu, Wala mwanga usiiangazie.

5 Ishikwe na giza, giza tupu, kuwa yake; Wingu na likae juu yake; Chote kiifanyacho siku kuwa giza na kiitishe.

6 Tena usiku huo, na ushikwe na giza kuu; Usihesabiwe katika siku za mwaka; Wala kutiwa katika hesabu ya miezi”.

Sasa swali ni je! Walifanya sahihi kuzilaani siku zao?, na sisi je tunapopitia dhiki zilizozidi ni sahihi kuzilaani siku tulizozaliwa na watu waliotuzaa, na matumbo yaliyotuzaa?.

Jibu ni La! Si sahihi kabisa kuzilaani siku tulizozaliwa, wala kulaani matumbo yaliyotuzaa, hata tupitie dhiki kiasi gani?..

Nabii Yeremia na Ayubu walisema maneno yale kwakuwa yalionekana kama ni mambo mapya kwao, kwamba inawezekanaje uwe Nabii uliyetumwa na Mungu, unayesema maneno ya kweli, au inakuwaje uwe mtu wa Mungu, mwelekevu na mkamilifu halafu unakubwa na mambo mazito kama yale?.

Kwahiyo yale yaliyowapata yalikuwa ni mambo mapya kwao, hawakuwa na mifano ya waliowatangulia waliopitia kama hayo katika kiwango hiko, hivyo walisema yale kwa udhaifu wa kibinadamu, lakini hawakuwa sahihi, ndio maana baadaye utaona Ayubu anakuja kutubu, kwa kusema “amesema maneno yazidiyo”

Ayubu 42:3 “Ni nani huyu afichaye mashauri bila maarifa? Kwa maana, nimesema maneno nisiyoyafahamu, Mambo ya ajabu ya kunishinda mimi, nisiyoyajua.

4 Sikiliza, nakusihi, nami nitanena; Nitakuuliza neno, nawe niambie.

5 Nilikuwa nimesikia habari zako, kwa kusikia kwa masikio; Bali sasa jicho langu linakuona.

6 Kwasababu hiyo NAJICHUKIA NAFSI YANGU, NA KUTUBU Katika mavumbi na majivu”.

Umeona? Hapa Ayubu anakuja kutubia maneno yake, baada ya kumjua Mungu zaidi, na ni hivyo ivyo Yeremia alikuja kuona makosa yake, soma Yeremia 15:18-19.

Na hatuoni tena Ayubu baada ya kuponywa msiba wake wala Yeremia baada ya kustahereshwa wakirudia kusema hayo maneno, hivyo wao walipitishwa katika mapito hayo ili iwe darasa kwetu sisi, kwamba ukiwa mtumishi wa Mungu, au mtu mkamilifu mbele za MUNGU, sio tiketi ya kutopitia majaribu!, LA! Majaribu yanawapata watu wote (wakamilifu na wasio wakamilifu), hivyo hatupaswi kulalamika wala kulaani yanapokuja bali kuomba na kumngoja BWANA.

Na hiyo ndio sababu ya Bwana wetu YESU kuwatahadharisha wanafunzi wake, na hivyo anatutahadharisha hata sasa kwamba tutakapopitia dhiki kwaajili ya Imani tunapaswa tuwe wapole kama hua na wenye busara kama nyoka.

Mathayo 10:16 “Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.

17 Jihadharini na wanadamu; kwa maana watawapeleka mabarazani, na katika masinagogi yao watawapiga;

18 nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa”.

Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba si sahihi kuzilaani siku za kuzaliwa au siku nyingine yoyote, wakati wote tunapaswa tuwe watu wenye busara, na watulivu..hakuna faida yoyote katika kunung’unika wala kulalamika.

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Laana ya torati maana yake ni nini?

JE NI LAANA KULELEWA NA BABA AU MAMA WA KAMBO?

Nini maana ya mstari huu: (Mtu ambarikiye mwenzake kwa sauti kuu asubuhi na mapema; Itahesabiwa kuwa ni laana kwake.Mithali 27:14 )?

NAKUJUA JINA LAKO!

Print this post

Mwandishi wa kitabu cha wimbo uliobora.

Aliyekiandika kitabu hiki ni Sulemani, mwana wa Daudi. Kufuatana na utambulisho wake mwanzoni kabisa mwa kitabu hichi.

Wimbo 1:1 Wimbo ulio bora, wa Sulemani

Mfalme Sulemani alijaliwa hekima na Mungu kuandika nyimbo nyingi sana Pamoja na Mifano mingi. Kama 1Wafalme 4:32 inavyosema aliandika Nyimbo elfu moja, na tano.

Sasa miongoni mwa hizo nyimbo, basi huu ulikuwa mmojawapo. Na ndio uliokuwa bora kuliko zote. Ndio maana umeitwa wimbo ulio bora.

Ni sawa na kusema Mfalme wa Wafalme, au Patakatifu pa Patakatifu. Ikiwa na maana kuna pazuri  kweli, lakini papo pazuri Zaidi ya kote, au kuna wafalme kweli lakini yupo aliyezidi wote. Ndivyo ilivyo katika vitabu vya Sulemani.

Hichi ndio kitabu ambacho, kimebeba hekima ya juu kuliko zote Sulemani alizojaliwa na Mungu kuziandika. Ni kitabu chenye maudhui ya kimahusiano kati ya mtu na mpenzi wake, ikifunua mahusiano yaliyopo kati yetu sisi na Kristo rohoni.

Kwa Maelezo mapana juu ya uchambuzi wa kitabu hichi bofya hapa >>> VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 11 (Mithali, Wimbo ulio bora, Mhubiri)

Lakini pia kwa mafunzo mbalimbali yaliyomo ndani ya kitabu hichi, bofya masomo yafuatayo.>>

Nini maana ya Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, (Wimbo 2:7)

USIKAWIE- KAWIE KUUFUNGUA MOYO WAKO

NYAKATI TOFAUTI- TOFAUTI ZA UPENDO.

MAAJABU YA AGANO LA UPENDO WA KRISTO.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Print this post

KISIMA BADO KINA MAJI, KIFUKUE TENA.

Isaka, alipofika mahali panaitwa Gerari alivikumbuka visima vilivyochimbwa na baba yake Ibrahimu zamani, lakini alipotazama na kuvikuta vimeharibiwa, alianza kazi ya kuvichimba tena, Alipokifukua cha kwanza na kutoa maji maandiko yanatuambia wachungaji wa mahali pale wakakigombania..

Akakiita Eseki, akasogea mbele kidogo akakichimba Kingine tena nacho kikagombaniwa akakiita Sitna, akasogea tena Mbele akachimba kingine cha tatu..

Hicho hawakukigombania akakiita..Rehobothi

Kisha akasema..Kwa kuwa sasa BWANA ametufanyia nafasi, nasi tutazidi katika nchi.

Mwanzo 26:18-22

[18]Isaka akarudi akavichimbua vile visima vya maji walivyovichimba siku za Ibrahimu babaye; maana wale Wafilisti walikuwa wamevifukia baada ya kufa kwake Ibrahimu; naye akaviita majina kufuata majina alivyoviita babaye.

[19]Watumwa wa Isaka wakachimba katika lile bonde, wakapata kisima cha maji yanayobubujika.

[20]Wachungaji wa Gerari wakagombana na wachungaji wa Isaka wakisema, Maji haya ni yetu. Ndipo akakiita jina la kile kisima Eseki, kwa sababu waligombana naye.

[21]Wakachimba kisima kingine, wakagombania na hicho tena. Akakiita jina lake Sitna.

[22]Akaondoka huko akachimba kisima kingine, wala hicho hawakukigombania. Akakiita jina lake Rehobothi, akasema, Kwa kuwa sasa BWANA ametufanyia nafasi, nasi tutazidi katika nchi.

Sauti ya Mungu nyuma ya habari hii ni nini?

Fahamu ukishaokoka, kuna kisima cha maji ya uzima kinapandwa ndani yako na Yesu Kristo mwenyewe. Kisima hiki licha ya kukupa uzima wa milele..lakini kina kazi ya kukupa raha, kukustawisha na kukufanikisha, maisha yako hapa duniani na mbinguni.

Yohana 7:38

[38]Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.

Anasema tena..

Yohana 4:14

[14]walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele.

Lakini ni kazi ya adui kukifukia kisima hicho, na hatimaye uwe mkavu kabisa usione raha ya wokovu au matunda yoyote ya imani yako ndani ya Kristo.

Hapo mwanzo ulikuwa ni moto rohoni, ulikuwa unaweza kuomba, kusoma Neno, Bwana alijifunua kwako kwa viwango vya juu..Ukitembea uliuhisi uwepo wa Roho Mtakatifu karibu na wewe…lakini sasa huhisi chochote, huwezi tena kuomba, kushuhudia n.k ukiona hivyo fahamu kuwa kisima kimefukiwa…lakini tumaini ni kuwa maji yapo chini waweza kuanza tena kuchimba na kurudia viwango vyako vya juu hata na zaidi..

Ulirudi nyuma, mpaka ukafikia hatua ya kuyatenda yale machafu ya dunia uliyoyaacha, Ukahisi kama Mungu hawezi kukusamehe tena…ukweli ni kwamba tumaini lipo, anza tu kukichimba kisima chako, maji utayaona.

Ulikuwa na maono mazuri, Na shauku ya kufikia hatma yako, ulikuwa unaona mwendelezo mzuri wa kile ulichokuwa unakifanya hata katika magumu hukutikisika lakini yale maono yamekufa, huelewi ni nini kimetokea, ujue kisima kimefukiwa…anza Upya tena.

Ila ni lazima ukubali kuchukua hatua bila kukata tamaa..Ilimgharimu Isaka visima vitatu lakini hakukata tamaa, hata alipofukua cha kwanza alisumbuliwa, akaendelea tena na tena…alipofikia cha tatu..ambacho ni Rehobothi..basi ikawa ni pumziko lake la daima.

Sisi kama watoto wa Mungu ni Lazima tujue adui ana wivu na hapendi kuona chemchemi za uzima na mafanikio zinabubujika ndani yetu…atafanya juu chini kuhakikisha vinafukiwa na hatimaye kutoona matokeo yoyote ya wokovu kwenye maisha yetu, na wakati huo sio mpango wa Mungu ..ataleta majaribu, misuko-suko, tufani n.k. Lakini ukistahimili Mpaka mwisho utashinda..na hatimaye utakaa mahali pa kudumu pa raha yako kama Isaka..

Ufanye nini?

Anza sasa kujizoesha kwa nguvu kusoma Neno, hata kama mwili hautaki, omba, hudhuria Mikesha acha uvivu, jitenge na dhambi zote. Na hatimaye utaona mwanzo mpya tena wenye nguvu rohoni mpaka mwilini.

Chimba kisima chako

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >>

https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Print this post

UJUE UZIMA WA MILELE.

Mtu akikuuliza “Kufanikiwa nini?”..bila shaka unaweza kumjibu ni kuwa na “kazi nzuri yenye kipato kizuri na kuwa na afya njema”. (Hii ni tafsiri nyepesi na rahisi tu).

Sasa tukirudi katika roho, Uzima wa milele ni nini?..biblia imetupa majibu mafupi na marahisi..

Yohana 17:3 “Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma”

Ukimjua MUNGU na YESU KRISTO unao uzima wa milele..

Sasa si kwamba MUNGU na YESU ni vitu viwili tofauti.. La! ni MUNGU mmoja katika madhihirisho mawili tofauti..

Mfano mtu anaweza kukuona wewe mubashara (live)…au akakuona kupitia picha yako. Sasa wewe kwenye picha na wewe wa mubashara sio watu wawili tofauti ni mtu mmoja katika madhihirisho mawili tofauti.

Wakati mwingine badala ya kuonekana wewe mubashara unaweza kutuma picha yako au kuibandika katika nyaraka zako muhimu kama vyeti, au vitambulisho au barua na ikawa ni wewe yule yule.

Na YESU ni picha kamili ya Mungu, aliyemwona YESU amemwona MUNGU BABA, kwahiyo hatuwezi tena kutafuta kujua Baba yupoje, tukimwona Yesu tumemwona Baba, ndivyo maandiko yasemavyo..

Yohana 14:8 “Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha.

9 Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?”

Yohana 14:7 “Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona”

Sasa turudi kwenye “UZIMA WA MILELE”...anasema…“Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma”.

Maana yake ukisema unamjua MUNGU halafu unamkataa YESU maana yake huna UZIMA WA MILELE, Kwasababu YESU ni ufunuo kamili wa Mungu katika mwili.

Utaona watu wanasema, mimi namwamini Mungu lakini simwamini YESU, sasa utaikanaje picha ya mtu na kumkiri mtu?..

Nimekuletea picha yangu, halafu unaikana, na bado unakiri kunijua?.. kama ukiikana picha yangu maana yake unanifanya mimi kuwa mwongo.

Vile vile ukimkana YESU na kukiri kumjua MUNGU unamfanya MUNGU kuwa mwongo. (Soma 1Yohana 5:10).

Kama humwamini YESU ni moja kwa moja umwamini MUNGU pia, hiyo haina kutafakari mara mbili..kama humjui Yesu ni moja kwa moja humjui Mungu Baba hiyo haina kutafakari mara mbili pia.

Yohana 8:19 “Basi wakamwambia, Yuko wapi Baba yako? Yesu akajibu, Mimi hamnijui, wala Baba yangu hammjui; kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba yangu”.

Kwahiyo wakati huu Uzima wa milele unapatikana kwa YESU tu pekee yake, zingatia hilo: YESU TU PEKE YAKE!!.…usijaribu kumtafuta Mungu nje ya YESU, ni kupoteza muda.

Usijaribu kumtumikia Mungu nje ya Yesu, ni kupoteza muda, usitafute uzima wa milele nje ya Yesu, ni kupoteza muda na uzima wako wa milele, akitokea mtu, awe nabii, mtume au mchungaji amshuhudii Yesu kama ndie njia pekee ya kufika mbinguni, mkimbie!

Akitokea kuhani na kukufundisha kuna mwingine au wengine wanaoweza kufanya kazi kama ya YESU, mkimbie!.. Kristo YESU hana pacha, wala msaidizi kwamba pia kupitia mtakatifu fulani aliye hai au aliyekufa tunaweza kumwona Mungu, kwamba tukimwamini huyo tunaweza kumwona MUNGU, kimbia!

YESU si mtu wa pembeni aliyeletwa kutuokoa, ni Mungu mwenyewe aliyevaa mwili… yaani Mungu aliyetengeneza mwili na kuweka tabia zake zote ndani ya huo mwili, akaja ili atuonyeshe njia na kutukomboa, hivyo hana msaidizi, kajitosheleza kwasababu yeye ni MUNGU. (1Timotheo 3:16).

Kwahiyo tusipomwamini Yesu kwa namna hiyo hatuna uzima wa milele, haijalishi tutajitahidi kufanya mema kiasi gani, kama tumeshamsikia na hatutaki kumwamini, hatuna uzima wa milele.

Swali ni je?.. Unao uzima wa milele?..je umemwamini YESU na kuyafanya anayoyasema?.

Luka 6:46 “Na kwa nini mnaniita, Bwana, Bwana, walakini hamyatendi nisemayo?

47 Kila mtu ajaye kwangu, na kuyasikia maneno yangu na kuyatenda, nitawaonyesha mfano wake.

48 Mfano wake ni mtu ajengaye nyumba, na kuchimba chini sana, na kuweka msingi juu ya mwamba; na kulipokuja gharika, mto uliishukia nyumba ile kwa nguvu, usiweze kuitikisa; kwa kuwa imejengwa vizuri.

49 Lakini yule aliyesikia ila hakutenda, mfano wake ni mtu aliyejenga nyumba juu ya ardhi pasipokuwa na msingi, mto ukaishukia kwa nguvu, ikaanguka mara; na maangamizi yake nyumba ile yakawa makubwa”.

Mwamini YESU na tenda ayasemayo.

Maran atha!

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

TENDA AGIZO LA YESU, HILO NDIO LITAKALOKULINDA.

UJIO WA BWANA YESU.

MAASI KUONGEZEKA NI ISHARA YA NINI?.

Na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa?. Ni mwamba gani huo?(Mathayo 16:18)

Print this post

Anaposema Nisiaibike milele” Ni aibu ipi? (Zab 31:1)

SWALI: Maandiko yanasema “Nimekukimbilia Wewe, Bwana, Nisiaibike milele”, Je! ni aibu gani anaomba aepushwe nayo?. Mbona tunapitia kuaibishwa, ijapokuwa tumemkimbilia Mungu?


JIBU: Vifungu kadha wa kadha kwenye zaburi vinaeleza, habari hiyo,

Zaburi 31:1 Nimekukimbilia Wewe, Bwana, Nisiaibike milele. Kwa haki yako uniponye

Zaburi 25:20 Unilinde nafsi yangu na kuniponya, Nisiaibike, maana nakukimbilia Wewe

Soma pia Zaburi 22:5, 71:1

Daudi ni mtu ambaye alizungukwa na maadui pande zote, na hivyo alijua nguvu zake zipo kwa Mungu tu, hivyo akishindwa nao basi itakuwa ni fedheha na aibu kwake, Vilevile ni mtu ambaye aliahidiwa mambo makubwa na Mungu, ikiwemo kudumishiwa kiti chake cha enzi milele, lakini kutokana na mapito na masumbufu mengi aliyokuwa anapitia na kukawia katika ufalme, ilionekana kama jambo hilo haliwezekani..Lakini hakuacha kumwomba Mungu, azitazame ahadi zake asiabike, kwa kumtumaini yeye.

Zaburi 89:49 Bwana, zi wapi fadhili zako za kwanza, Ulizomwapia Daudi kwa uaminifu wako?
50 Ee Bwana, ukumbuke, Wanavyosimangwa watumishi wako; Jinsi ninavyostahimili kifuani mwangu Masimango ya watu wengi.
51 Ambayo adui zako wamesimanga, Ee Bwana, Naam, wamezisimanga hatua za masihi wako.
52 Na ahimidiwe Bwana milele. Amina na Amina.

Hapo ndio utaona sasa kwanini sehemu nyingi, kwenye Zaburi Daudi anamwambia Bwana, akumbuke asiabike milele, kwa kuzitumainia fadhili zake..

AGANO JIPYA.

Lakini katika agano jipya pia,

Nasi pia tunamtumaini Mungu ili tusiabike milele. Na Aibu kuu ni ile ya kutengwa na uso wa Mungu milele, ambayo watakutana nayo wenye dhambi, ile aibu ya kufukuzwa mbele ya uso wa Mungu.

2 Petro 3:13 Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake.
14 Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia mambo hayo, fanyeni bidii ili mwonekane katika amani kuwa hamna mawaa WALA AIBU mbele yake.

Hiyo ndiyo Bwana atatuepusha nayo sisi tuliomtumainia.

Ni vema kufahamu kuwa tukiwa kama watoto wa Mungu, haimaanishi kuwa hatutaaibishwa au kudhalilishwa kwa ajili ya jina lake, vipindi hivyo tutapitia, lakini mwisho wetu utakuwa ni kutukuzwa katika utukufu mkuu milele..

Ni heri leo ukubali aibu ya kidunia, kuliko kukutana na ile ya Kristo wakati ule..

Mathayo 7:23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.

Mathayo 25:31-34, 41

31 Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake;
32 na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi;
33 atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto.
34 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu…
41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Print this post

Kwanini Bwana Yesu alitumia neno “wewe wasema”(Mathayo 27:11)

SWALI: Kwanini Bwana Yesu alitumia neno “wewe wasema” alipoulizwa maswali na sio kujibu moja kwa moja?(Mathayo 27:11)


JIBU: Ni kweli tunaona mahali kadha wa kadha Bwana Yesu alipoulizwa maswali Na baadhi ya wayahudi na wapagani, majibu yake hayakuwa yamenyooka moja kwa moja alitumia kauli ya “wewe wasema”…kwa mfano tazama vifungu vifuatavyo;

Mathayo 27:11

[11]Naye Yesu akasimama mbele ya liwali; liwali akamwuliza, akasema, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi? Yesu akamwambia, Wewe wasema.

Luka 22:68-71

[68]Tena, nikiwauliza, hamtajibu.

[69]Lakini tangu sasa Mwana wa Adamu atakuwa ameketi upande wa kuume wa Mungu Mwenyezi.

[70]Wakasema wote, Basi, wewe ndiwe Mwana wa Mungu? Akawaambia, Ninyi mwasema kwamba mimi ndiye.

[71]Wakasema, Basi, tuna haja gani tena ya ushuhuda? Maana, sisi wenyewe tumesikia maneno ya kinywa chake.

Soma pia…Luka 23:3

Maana rahisi ya neno hilo ni ipi?

Maana yake ni

 “ndio, wewe umesema hivyo, sio mimi”

Au “ndio, wewe umeona kuwa ni hivyo

Sasa kwanini Atumie kauli hiyo?

Kwasababu alijua waliokuwa wanamuuliza hawakuwa na nia ya kutaka kufahamu ukweli, bali kutafuta neno la kumshitaki, au kumdhihaki, ndio maana kujibu kwake hakukuwa kwa moja kwa moja, yaani upande mmoja anaonyesha kukubali, lakini upande mwingine anaacha hukumu watoe wao wenyewe…

Hiyo ilikuwa ni desturi yake sio tu kwenye maswali bali hata kwenye Mafundisho yake kadha wa kadha…Alizungumza na makutano kwa mifano..kisha wale waliokuwa tayari kupokea aliwafunulia yote baadaye.

Hii ni hekima ambayo tunaweza jifunza hata sisi..

Kwamfano wewe ni mchungaji, kisha ukajikuta watu wasiopenda wokovu, wamekushitaki na kukupeleka Mahakamani halafu hakimu anakuuliza je wewe ndio wale wachungaji ambao, mnaweka Makapu ya sadaka mbele, ili mle Sadaka za waumini.

Sasa unajua kabisa kauli kama hiyo ni ya mtego, kukudhihaki, au kutaka sababu ya kukushitaki, sasa Ili kuikata kauli yake..kukataa Kuwa wewe sio mchungaji watasema unadanganya, kukataa kuwa chombo cha sadaka hakiwekwi mbele watu kutoa, watakuona Pia mwongo, lakini kukusingizia unakula sadaka za waumini unajua ni uongo…

Hivyo kujibu vema hiyo kauli ni kukubali upande mmoja, na mwingmwingiwaachia wao aaamue..

“Wewe Wasema”

Yaani *ndio, wewe umesema hivyo*

“Ndio wewe Umeona kuwa ndivyo ilivyo”.

Hapo umekata maneno yote..atakachoamua, Ni kulingana na mawazo yake mwenyewe lakini sio yale yaliyothibitishwa kikamilifu na wewe..

Hivyo yatupasa tutumie busara. katika ujibuji wetu wa maswali hususani kwa wale wanaotushitaki na kutushambulia

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Print this post

WALAKINI MIMI SI PEKE YANGU.

Jina la Mwokozi YESU libarikiwe, karibu tujifunze Biblia.

Ni muhimu kupambana sana mpaka kufikia hatua ya Mungu kuwa kila kitu kwetu, maana yake hata watu wote wakikuacha, au kukutenga, au kukusahau, bado MUNGU ni faraja tosha kwako zaidi ya watu elfu, au ndugu elfu.

Tukifikia hii hatua tutakuwa watu wa furaha siku zote, na watu wa kuishi bila kutegemea sana hamasa kutoka kwa watu au vitu.

Tukiweza kufikia kiwango kwamba faraja kutoka kwa watu haziwi sababu kuu za msukumo wetu kuendelea mbele, tutakuwa watu wakuu sana mbele za Mungu.

Pia tukiweza kufikia kiwango kwamba maneno mabaya au dhihaka au kukatishwa tamaa na watu haziwi sababu ya kukata tamaa na kuumia, pia tutakuwa watu wakuu sana mbele za watu.

Wakristo wengi tunahamasika sana pale tunapohamasishwa na watu, tunapata nguvu zaidi pale tunapotiwa nguvu na watu, na pia tunavunjika moyo sana pale tunapovunjwa moyo na watu, lakini haikuwa hivyo kwa Bwana wetu YESU KRISTO, yeye faraja yake na huzuni yake ilikuwa kwa Baba..

Kiasi kwamba hata watu elfu wangemtukuza na kumtia moyo kama kutiwa huko moyo hakujatoka kwa Baba yake, hakukuweza kumhamasisha kitu.

Hali kadhalika hata watu wote wakitoa maneno ya kuvunja moyo au watu wote wakimwacha na akabaki peke yake, maadamu anaye Baba yake haikumvunja moyo wala kumkatisha tamaa, ndivyo maandiko yasemavyo..

Yohana 16:32 “Tazama, saa yaja, naam, imekwisha kuja, ambapo mtatawanyika kila mmoja kwao kwao, na kuniacha mimi peke yangu; walakini mimi si peke yangu, kwa kuwa Baba yupo pamoja nami”.

Hapo Bwana YESU aliona saa inakuja kwamba kila mtu atamkimbia na atabaki peke yake na kweli huo wakati ulitimia pale askari wa Herode walipokuja kumkamata Bwana Yesu pale bustanini, maandiko yanatuonyesha walikimbia wote, na hata wengine walikimbia uchi (Marko 14:51-52).

Lakini hatuoni Bwana Yesu akivunjika moyo kwa hilo tendo, kwasababu anajua na ana uhakika kwamba Baba yupo naye..

Anajua watu wote wakimwacha haimaanisha Baba yake kamwacha…

Lakini ulipofika wakati wa Baba kumwacha kwa kitambo kwasababu ya dhambi za ulimwengu, ndipo tunaona Kristo anajali na kuhuzunika..

Mathayo 27:46 “Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”

Na sisi hatuna budi kufika hii hatua, Mungu wetu, na Baba yetu abaki yeye kuwa faraja yetu ya mwisho, kiasi kwamba hata dunia nzima ikiondoka, Baba yetu atabaki kuwa hamasa yetu, faraja yetu, yaani awe mwanzo na mwisho kwetu.

Na hata dunia nzima ikitusifia na kutupa maneno ya hamasa, bado hamasa ya Baba yetu ndio itakayokamilisha furaha yetu.

Bwana Yesu atusaidie sana.

Zaburi 9:10 “Nao wakujuao jina lako wakutumaini Wewe, Maana Wewe, BWANA hukuwaacha wakutafutao”

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

UTENDAJI KAZI MWINGINE WA ROHO MTAKATIFU USIOUFAHAMU.

FUNGUO ZA UZIMA, MAUTI NA KUZIMU.

Je, kama hauna ubatizo sahihi hauwezi kuwa na Roho Mtakatifu?

WALIKUWA WAKINUNUA NA KUUZA, WAKIOA NA KUOLEWA KAMA ISHARA YA KANISA !

MFALME ANAKUJA.

Print this post

KATAZO LA MUNGU, NI MAFANIKIO.

Ukikatazwa na Mungu, haimaanishi kuwa umenyimwa unachoomba, kinyume chake amepewa kwa uzuri wa juu zaidi.

Kuna kipindi Daudi aliingiwa na Nia ya kutaka kumjengea Mungu nyumba ..Hivyo akaanda Mali zake nyingi ili aanze ujenzi…lakini alipolileta Hilo wazo kwa Mungu, ilikuwa ni tofauti na alivyotarajia..

Mungu hakumruhusu bali kinyume chake akamwambia wewe hutanijengea mimi nyumba…kwasababu umemwaga damu ya watu wengi, lakini mwanao ndiye atakayenijengea…

1 Mambo ya Nyakati 22:7-8

[7]Daudi akamwambia Sulemani mwanawe, Kwangu mimi nia yangu ilikuwa kujenga nyumba kwa ajili ya jina la BWANA, Mungu wangu.

[8]Lakini neno la BWANA likanijia, kusema, Wewe umemwaga damu nyingi, na vita vikubwa umevifanya; wewe hutajenga nyumba kwa ajili ya jina langu, kwa sababu umemwaga damu nyingi juu ya nchi machoni pangu;

Jiweke katika hiyo hali unatamani ufanye kitu fulani chema, lakini Mungu anakuambia (aidha kwa maneno au vitendo) hapana wewe hustahili kufanya au kuchukua nafasi hiyo, kwasababu hii na hii na hii, bali ataichukua kijakazi wako, mtumwa wako, rafiki yako, mpendwa mwenzako…Sasa Kibinadamu hilo linaweza likaleta ukakasi lisikuvutie Masikioni mwako…kwasababu unajua litampa cheo mwenzako.

Pengine ndivyo angeweza kufikiri Daudi… Lakini alijifunza kunyenyekea, na kumtii Mungu na kuachilia kijiti kwa mwingine…

matokeo yake ikawa ujenzi ule ukadumishwa na jina lililodumishwa halikuwa lingine bali la Daudi kwa vizazi vyote vijavyo..aliyejenga alikuwa ni Sulemani, lakini utukufu ulikuja kwa jina la Daudi mpaka leo linatajwa.

Hii ni kutufundisha kukubali kunyenyekea Katika mapenzi yote ya Mungu..Zipo nyakati hutafanya wewe, hata kama umeomba na kuitamani hiyo nafasi yakupasa ukubali wengine wafanye, upo wakati hutatukuzwa wewe kubali wengine watukuzwe kupitia wewe, hutaheshimiwa wewe lakini fanya bidii wengine waheshimiwe kupitia wewe…kwasababu hiyo ndio ngazi ya kuinuliwa na Mungu, na matokeo yake utayaona..

Makatazo ya Mungu ni fursa ya mafanikio, unaweza ukawa hujapewa uzao, lakini ukamlea mtoto wa mwingine, Mungu akaja kumfanya raisi wa nchi, ukaitwa mama wa Taifa. Hivyo maadamu unatembea katika njia za Bwana na umeomba, amini kuwa Mungu amekupa zaidi ya kile ukiwazacho.

Kamwe Using’ang’anie jambo, bali jifunze kuachilia neema ya Mungu yenyewe kuamua, kwasababu hutapoteza chochote..

Waefeso 3:20

[20]Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu;

Bwana awe nawe…

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Print this post

Kwanini Bwana aliwaambia wanafunzi wasihame- hame? 

SWALI: Kwanini Bwana Yesu alipowatuma wanafunzi wake kuhubiri aliwaambia wasihame- hame nyumba watakazo Karibishwa?

Luka 10:7

[7]Basi, kaeni katika nyumba iyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao; maana, mtenda kazi amestahili kupewa ujira wake. Msihame-hame kutoka nyumba hii kwenda nyumba hii.


JIBU: Luka 10, Mathayo 10, Na Marko 6, Kristo inawafundisha mitume wakee nidhamu ya kimisheni. Pale ambapo watu wa Mungu watatoka na kwenda kuhubiri injili kwenye miji, mataifa au nyumba za Watu.

Ukisoma pale utaona Kristo anawapa maagizo kadha wa kadha mfano amri ya kutoa huduma zao bure, anawaagiza wawe wapole kama Hua, na wenye busara kama nyoka, vilevile nyumba watakazokaribishwa kisha chakula kikawekwa mbele yao wale bila kuuliza- uliza…

Lakini agizo lingine lilikuwa ni kutohama-hama nyumba moja kwenda nyingine. Kwamfano wameingia mji fulani halafu ikatokea familia moja ikawaalika kukaa kwao kwa kipindi chote cha huduma, hawapaswi kuhama- hama bali wakae pale mpaka watakapotoka na kwenda mji mwingine ikiwa yule mfadhili hana neno nao. Hata kama wakialikwa nyumba nyingine hawapaswi kuhama- hama..

Swali linakuja kwanini iwe hivyo?

Bwana Yesu alijua kuwa katika ziara mialiko kwa watumishi wa Mungu, huwa ni mingi. Na hivyo ili kuzuia dhamiri mbaya na wengine kuvunjika mioyo, akatoa agizo hilo Kwasababu mfano imetokea mtumishi amealikwa kisha kesho yake akahamia nyumba nyumba nyingine, Yule wa kwanza atajisikiaje? Pengine picha itakayoonekana hapo ni kuwa wanatafuta maisha mazuri, au matajiri wenye hadhi ya kuwatunza..

Lakini wakitulia sehemu moja huleta adabu na kuonyesha tabia ya kuridhika.

Lakini pia Kristo alitaka akili zao zijikite zaidi kwenye huduma.. Kwani kitendo cha kila siku kuhama hapa kwenda kule, hupoteza umakini kihuduma, ni sawasawa na mtu ambaye kila siku anahama nyumba moja ya kupanga kwenda nyingine…unaelewa ni usumbufu gani anaokutana nao.. kuanza tena kuyazoelewa mazingira mapya ni gharama.

Hasa sasa kama watumishi wa Mungu…tunafundishwa utulivu tuwapo ziarani…Mara nyingi ule mlango wa fadhili ambao unafunguliwa wa kwanza, huwa ni wa Mungu…tulia katika huo huo…nyumba ile ya wageni unayoingia ya kwanza…ikiwa amani ya Kristo imekaa ndani yako…tulia hiyo hiyo mpaka utakapomaliza ziara zako…usiwe mtu wa kutafuta makao mazuri, Kwasababu kumbuka upo ziarani… mahali pa muda tu.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >>

https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Print this post

MAOMBI YA KAMBI

Huu ni mwongozo wa maombi yetu ya kambi July 30 – Aug 2.

Kanisa la Nuru ya Upendo

Daresalaam Tegeta.  Bofya hapa

👇 📥 

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Miongozo mingine.

MWONGOZO WA MAOMBI YA KUJIKUZA KIROHO.

MWONGOZO WA MAOMBI YA WAHUDUMU/ WASIMAMAO MADHABAHUNI.

MWONGOZO WA MAOMBI YA FAMILIA

Print this post