Je Mungu anaangalia mwili na kuuhitaji?.. jibu ni Ndio!.. maandiko yanathibitisha hilo wazi kabisa..
1Wakorintho 6:13 “Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu atavitowesha vyote viwili, tumbo na vyakula. LAKINI MWILI SI kwa zinaa, BALI NI KWA BWANA, NAYE BWANA NI KWA MWILI”.
Nataka uone hayo maneno ya mwisho yanayosema “…mwili si kwa zinaa, BALI NI KWA BWANA, NAYE BWANA NI KWA MWILI”… Kumbe “miili yetu” ipo mahususi kwaajili ya “Bwana” na Bwana yupo mahususi kwaajili ya “miili yetu”.. Si ajabu tunapomwomba mahitaji ya mwilini anatujibu haraka sana kama tu vile ya rohoni.
Si ajabu tunapoteseka katika mwili hapendi, kwasababu miili yetu ni ya thamani sana kwake, kwaufupi ili tuwe wanadamu ni lazima tuwe na miili..
Sasa je! huu usemi ya kwamba Mungu haangalii mwili unatoka wapi?.. bila shaka ni kwa ibilisi!.
Maandiko yanazidi kusema kuwa “sisi si mali yetu wenyewe”
1Wakorintho 6:19 “Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe”.
Tuzidi kusogea mbele katika andiko hilo… tujifunze ni kwa namna gani MWILI ni Kwa BWANA na BWANA ni kwa MWILI.
Muunganiko wa Miili yetu na Kristo ni mpana sana kiasi kwamba Biblia inatafsiri “viungo vyetu vya mwili ni viungo vya Kristo pia”.. maana yake huo mkono unaouona kama ni wako, kibiblia ni mkono wa Kristo, hayo macho si yako bali ni ya Kristo, kwahiyo kama umemwamini Yesu halafu ukaenda kufanya zinaa, maana yake umechukua kiungo cha Kristo na kukifanyisha zinaa..ndivyo Biblia inavyosema..
1Wakorintho 6:15 “Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha!”
Huo mguu unaoona ni wako kiuhalisia kama umeokoka si wako tena bali ni wa Kristo… ndio maana Bwana Yesu alisema mahali watakapowakaribisha basi wamemkaribisha yeye Kristo..na wakiwakataa wamemkataa yeye Kristo… kwanini?.. ni kwasababu miili yetu si mali yetu wenyewe baada ya kuokoka!, bali viungo vyetu vyote vinakuwa ni vya Kristo na vina mhubiri Kristo.
Luka 10:16 “Awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi, naye awakataaye ninyi anikataa mimi; naye anikataaye mimi amkataa yeye aliyenituma”.
Umeona??.. maana yake mtu aliyeokoka ni “Kristo anayetembea”.. ukiendelea kujifunza zaidi katika habari ile ya hukumu ya kondoo na mbuzi katika Mathayo 25:31-46… utaona wale watu waliuliza “ni lini Bwana tulipokuona una njaa, upo uchi tukakulisha na kukuvisha” ndipo Yesu atawaambia “kwa kadri mlivyowatendea wadogo wale basi walimtendea yeye”… wadogo wanaozungumziwa pale ni “watu wa Mungu wanaohubiri habari njema”.
Kwahiyo kumbe matumbo yenye njaa ya watu wa kweli wa Mungu ni matumbo ya Kristo, kumbe miguu yenye vumbi ya watu wa Mungu wa kweli ni miguu ya Kristo.. kwaujumla kumbe miili ya watu wa Mungu ni miili ya YESU mwenyewe!… si ajabu pale alisema “…nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha!”
Sasa kama ni hivyo kwanini unauvika mwili wako mavazi ya jinsia nyingine…je ni Kristo yupi unayemhubiri kwa uvaaji wako?..kwanini unafanya zinaa?, kwanini unachora mwili wako?, kwanini unauvutisha sigara na kuunywesha pombe?
Yachukulie haya kwa uzito mtu wa Mungu, wala usipuuzie!, na kusema Mungu haangalii mwili?.. jihadhari na mafundisho ya uongo! Yanayokuambia kuutunza mwili ni mafundisho ya sheria na vifungo!.. Tunapookoka hatujapewa uhuru wa kufanya dhambi!, La! Hatujafunguliwa kufanya dhambi!.
Siku ya mwisho hatutafufuliwa roho bali miili ndio itakayofufuliwa, na Kristo hakutoa roho yake kwa ukombozi wetu, bali mwili wake wenye damu, mifupa, mishipa, nyama, moyo, miguu, mikono, ngozi !.. vyote Kristo alivitoa kwaajili ya ukombozi wetu..
Waebrania 10:5 “Kwa hiyo ajapo ulimwenguni, asema, Dhabihu na toleo hukutaka, Lakini mwili uliniwekea tayari”.
Biblia inazidi kutufundisha kuitoa miili yetu kwa Bwana..
Warumi 12:1 “Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana”..
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Mafundisho mengine:
MAAJABU YA AGANO LA UPENDO WA KRISTO.
Tofauti kati ya makuhani na walawi ni ipi?
Je Bwana YESU alimjibu Pilato au hakumjibu? Je biblia inajichanganya?
KILA MMOJA WENU AJUE KUUWEZA MWILI WAKE.
MTUMAINIE YESU ASIYEISHA MATUKIO.
Print this post
Kutoka 33:17 “Bwana akamwambia Musa, Nitafanya na neno hili ulilolinena, kwa maana umepata neema mbele zangu, NAMI NAKUJUA JINA LAKO
Jina la Mtu limebeba siri kubwa sana, lakini kabla ya kutazama jina la MUNGU.
Kitu pekee kilichomtambulisha na kinachomtambulisha MUNGU kwetu sasahivi ni JINA LAKE!.. Kamwe hajawahi kutuonyesha Sura yake, wala kuitangaza mahali popote pale!, bali jina lake amelitangaza na kulitukuza sana..
Sasa si kwamba anapenda kujificha kwetu!.. La bali ametuchagulia kilicho bora kwake tukijue!.. Kwahiyo kilicho bora kwake kwetu ni jina lake zaidi ya sura yake.
Na kilicho bora kwa MUNGU kwetu kukijua ni MAJINA YETU zaidi ya SURA ZETU… Utauliza kivipi?..
Kitu pekee kilichoko sasa mbinguni kinachotutambulisha sisi sio SURA ZETU bali ni MAJINA YETU.. Mbinguni hakuna picha zetu!, bali majina!..
Ufunuo 13:8 “Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye JINA LAKE HALIKUANDIKWA katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia”.
Soma pia Ufunuo 17:8, Ufunuo 3:5, Wafilipi 4:3 utaona hakuna sura za watu kule mbinguni… hivyo uzuri wako wa sura, weupe wako, weusi wako, urefu wako, ufupi wako, unene wako, ubounsa wako na wangu unaishia hapa!!!..
Hiyo pia ndio sababu ya Bwana YESU kuwaambia wanafunzi wake wasifurahie pepo wanavyowatii bali wafurahie majina yao yameandikwa mbinguni…
Luka 10:20 “Lakini, msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni”.
Na unajua, Mungu anatujua kwa majina zaidi ya Sura na rangi?…ndivyo alivyomwambia hata nabii Musa.
Kutoka 33:17 “Bwana akamwambia Musa, Nitafanya na neno hili ulilolinena, kwa maana umepata neema mbele zangu, NAMI NAKUJUA JINA LAKO”.
Umeona hapo?.. Mungu anamwambia Musa anamjua jina lake, sio sura yake…. Kwahiyo ni muhimu sana kuangalia MAJINA YETU na kuyatengeneza…. Maandiko yanasema ni heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi..
Mithali 22:1 “Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi…”
Sasa tunachaguaje majina??.. je tubadilishe majina tuliyonayo?.. jibu ni La!.. tutaendelea kuwa na majina yetu haya haya ikiwa kama yana maana njema.. Lakini majina yetu haya haya yanaweza kubadilika na kuwa BORA..
Kwa jinsi jina lako linavyozidi kuwa Bora mbele za Mungu, ndivyo nafasi yako mbinguni inavyozidi kuwa kubwa, na kwa kadiri linavyozidi kufifia mbele za Mungu ndivyo mbinguni linavyofutika kumbukumbu lako..
Sasa tunafanyaje majina yetu kuwa Bora?.. Si kwa kwenda kuyatolea sadaka ya ukombozi, au kuyaombea kwenye mkesha.. La!.. unaweza kutoa sadaka za aina zote duniani na jina lako lisiwe mbinguni, lakini bado likaendelea kuwa kubwa mbele za watu, na unaweza kuwa na jina la heshima mbele za watu lakini mbele za Mungu ukawa huna jina.
Ifuatayo ni njia pekee ya kulitakasa jina lako, na heshima yako, na hadhi yako.. na njia hiyo si nyingine zaidi ya KUMCHA MUNGU, na KUJITENGA NA DHAMBI.. Utauliza kivipi, tusome maandiko yafuatayo?.
Kutoka 32:31 “Musa akarejea kwa Bwana akasema, Aa! Watu hawa wametenda dhambi kuu wamejifanyia miungu ya dhahabu. 32 Walakini sasa, ikiwa utawasamehe dhambi yao — na kama sivyo, unifute, nakusihi, katika kitabu chako ulichoandika. 33 Bwana akamwambia Musa, MTU YE YOTE ALIYENITENDA DHAMBI NDIYE NITAKAYEMFUTA KATIKA KITABU CHANGU”.
Kutoka 32:31 “Musa akarejea kwa Bwana akasema, Aa! Watu hawa wametenda dhambi kuu wamejifanyia miungu ya dhahabu.
32 Walakini sasa, ikiwa utawasamehe dhambi yao — na kama sivyo, unifute, nakusihi, katika kitabu chako ulichoandika.
33 Bwana akamwambia Musa, MTU YE YOTE ALIYENITENDA DHAMBI NDIYE NITAKAYEMFUTA KATIKA KITABU CHANGU”.
Umeona kitu kinachochafua jina la Mtu?… ni DHAMBI, Hiko ndicho kinachomwondoa mtu kwenye kumbukumbu za MUNGU, na si tu mbinguni na hata duniani pia..
Kumbukumbu 29:20 “Bwana hatamsamehe mtu huyo, lakini wakati huo hasira ya Bwana na wivu wake vitafuka moshi juu ya mtu yule, na laana yote iliyoandikwa katika kitabu hiki itamkalia juu yake, na BWANA ATALIFUTA JINA LAKE CHINI YA MBINGU”.
Huenda dhambi imechafua jina lako!.. suluhisho ni moja tu, kutubu na kuacha dhambi!.. jina lako hilo litasomeka kwenye kitabu cha mwanakondoo mbinguni.
MSINGI WA NYUMBA YA MUNGU, NI JINA LA MUNGU.
KWANINI TUNAOMBA KWA JINA LA YESU?
HAPO NDIPO WATU WALIPOANZA KULIITIA JINA LA BWANA.
FAIDA NYINGINE YA MAOMBI YA KUSHUKURU.
FUNDISHA KILE UNACHOKITENDA NA KUKIISHI
WhatsApp
Ulishawahi kuona mwanamke anajifungua mtoto bila kusikia utungu wowote? Hilo jambo bila shaka Litakuwa ni la ajabu… kwasababu haliendani kabisa na kanuni za asili …
hata maandiko yanasema hivyo..
Isaya 66:7-8
[7]Kabla hajaona utungu alizaa; Kabla maumivu yake hayajampata, Alizaa mtoto mwanamume. [8]Ni nani aliyesikia neno kama hili? Ni nani aliyeona mambo kama haya? Je! Nchi yaweza kuzaliwa siku moja? Taifa laweza kuzaliwa mara?..
[7]Kabla hajaona utungu alizaa; Kabla maumivu yake hayajampata, Alizaa mtoto mwanamume.
[8]Ni nani aliyesikia neno kama hili? Ni nani aliyeona mambo kama haya? Je! Nchi yaweza kuzaliwa siku moja? Taifa laweza kuzaliwa mara?..
Ni kanuni ya asili ili kiumbe kipya kizaliwe, mzaaji ni lazima apate utungu tu kama malipo ya kile akizaacho ..kila mwanadamu unayemwona chini ya jua, kuna mtu alipata maumivu kwa ajili yake..
Kanuni hii ipo rohoni pia…Kila mtakatifu unayemwona (aliyesimama), haikuwa bure bure…au kirahisi rahisi tu kama unavyodhani, kuna Waliopitia utungu juu yao…
Utauliza hili lipo wapi Kwenye maandiko?.
Paulo kwa Wagalatia,aliandika maneno haya;
Wagalatia 4:19
[19]Vitoto vyangu, ambao kwamba nawaonea utungu tena mpaka Kristo aumbike ndani yenu;
Paulo anawalilia wagalatia, kwa jinsi walivyoiacha neema ya Kristo, na kurudia mafundisho ya kiyahudi..anasema nawaonea utungu tena….tafsiri yake ni kuwa hapo nyuma alishawahi kuwaonea utungu…akawazaa…lakini sasa ni kama vile wanahitaji kuzaliwa tena….
Hivyo watu wote waliozaliwa mara ya pili wapo Waliowanea utungu.
1). Hulia na kuugua:
Maana yake hiki ni kipindi cha machozi na kuomba juu ya wale wote unaotamani wampokee Kristo..ndiyo tabia waliokuwa nayo mitume.
Matendo ya Mitume 20:31
[31]Kwa hiyo kesheni, mkikumbuka ya kwamba miaka mitatu, usiku na mchana, sikuacha kumwonya kila mtu kwa machozi.
Watu wengi wanatamani kuona geuko la dhati kwa jamii zao, rafiki zao, waume zao, watoto wao lakini hawana muda wa kuwaombea kwa kuzama sana kwa kipindi kirefu na wakati mwingine kufunga huku wakiwahubiria…wanaikwepa Kanuni hii ya kiumbe kipya kuzaliwa.
Hichi kipindi wanawake wengi huchungulia kifo, kwa sababu ya maumivu, au shinikizo au kutokwa na damu nyingi sana.
Ndivyo ilivyo pale unapojaribu, Kumvuta mwenye dhambi aifikie toba ya kweli, adui huanza kuinua vita, dhidi yako wewe na huyo unayemzaa.. lile joka litataka kufanya vita na wewe.
Ufunuo wa Yohana 12:1-4
[1]Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili. [2]Naye alikuwa ana mimba, akilia, hali ana utungu na kuumwa katika kuzaa. [3]Ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu, alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba. [4]Na mkia wake wakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na yule joka akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, amle mtoto wake.
[1]Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili.
[2]Naye alikuwa ana mimba, akilia, hali ana utungu na kuumwa katika kuzaa.
[3]Ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu, alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba.
[4]Na mkia wake wakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na yule joka akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, amle mtoto wake.
Ukijikuta katika wakati huu fahamu ni kung’ang’ana kumfuatilia kondoo huyo bila kujali hali au vipingamizi…unaweza kuona visababu sababu visivyoeleweka, mara hataki tena kukusikiliza, mara anaumwa, mara ndugu zake wanampinga, mara anakuwa mzito.hapa hupaswi kukata tamaa..endelea kumfuatilia kwasababu hizo ni hila za adui kumzuia asikate shauri kwa Bwana Yesu..
Fahamu tu kazi yako si bure upo wakati ataamini na kugeuka kabisa kabisa kwasababu Nguvu uliyonayo na kuu kuliko ya ibilisi..na furaha yako itakuwa ni pamoja na malaika mbinguni. (Luka 15:10).
Pia Biblia inasema…
Yohana 16:21
[21]Mwanamke azaapo, yuna huzuni kwa kuwa saa yake imefika; lakini akiisha kuzaa mwana, haikumbuki tena ile dhiki, kwa sababu ya furaha ya kuzaliwa mtu ulimwenguni.
Upo wakati utayafurahia matunda yako. Siku utakapoona kupitia hao makumi, mamia, maelfu ya watu wanaokoka..na siku ile Bwana anakupa thawabu kwa tunda hilo ulilomzalia.
Swali ni je utungu wako upo wapi?.. ni wapi unaweza kusema yule ni mwana wangu nimemzaa mimi katika Kristo?..
Kwenda tu kusema Yesu anakupenda okoka, halafu ukamwongoza Sala ya toba na kumwacha…hili halimaanishi huyo ni mtoto wako. Ndio maana wapo watu wengi wanaosema leo wamemkiri Yesu, lakini ukiwaangalia sio viumbe vipya..kwasababu hawakuzaliwa, bali waliaminishwa tu.
Tukubali kuzaa kwa kuwafundisha, kuwaombea sana, na kuwafuatilia mpaka watakapokata shauri la kweli kumpokea Yesu.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >>
https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
DALILI ZIPI ZITAMTAMBULISHA MTU KUWA AMEFANYIKA KIUMBE KIPYA?
MAFUNDISHO MAALUMU KWA WAONGOFU WAPYA.
MAUMIVU NYUMA-YA-HUDUMA.
SWALI: Sulemani ana maana gani kusema..Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe.?
Wimbo Ulio Bora 2:7
[7]Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe.
[7]Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini,
Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe.
JIBU: Mwandishi anaeleza hekima ya kweli juu ya mapenzi halisi yanavyoundwa.. na hivyo anawaasa wale wote wanayoyatafuta…wajue kanuni hizo ili wasiingie katika hasara kama sio majuto.
Andiko hilo linalenga nyanja zote mbili;
Anaposema nawasihi enyi binti za Yerusalemu..
Anawakilisha kanisa, au watu wote wanaotaka kuingia katika mahusiano ya kindoa..
Anasema;
Kwa paa na kwa Ayala wa porini… Anaapa Kwa wanyama hawa, lakini tunajua mara nyingi kwenye agano la kale watu walikuwa wanaapa kwa jina la Mungu…lakini hapa anatumia wanyama hawa ambapo ni Paa na Ayala.
Ni aina ya swala, ambao kwa eneo la Mashariki ya kati ilikuwa ni kawaida sana kuwaona kwenye mapori tulivu..
Wanyama hawa wana sifa ya:
Hivyo mwandishi anawasihi watu wanapotaka kuingia katika mapenzi wayaone Kama ni kuwawinda Ayala na Paa… Ambao hawahitaji pupa…
Ndio maana anasema;
“Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe.”
Akiwa na maana kuwa unapochochea mapenzi kwa haraka utayapoteza…mfano tu unapomvamia Ayala kwa pupa, hutampata atapotelea mbali…
Bali unapokuwa mtulivu na kumsogelea kidogo kidogo, ni rahisi kumnasa…
Hivyo Katika mahusiano ya mwilini anatuasa kuwa mahusiano ya kweli, yanajengwa katika muda…sio kwa kuyapaparikia…vijana wengi, wanang’ang’ania kuingia katika mahusiano kabla ya umri sahihi, au nyakati sahihi au wengine wakikutana hata wiki haijakwisha, ndani ya muda mfupi sana, utaona wameshaahidiana kuoana, na hatimaye kujikuta, wapo kwenye mahusiano hayo, kipindi kinapopita na kugundua uhalisia wao, na kasoro nyingi wanaanza kujuta kulitokea nini? Ni kwasababu walikurupukia mapenzi wala hawakuruhusu yaamke yenyewe katika wakati wake.
Lakini katika Roho, Bwana anaeleza mahusiano kati ya yeye na mtakatifu wake..Upendo kwa Kristo thabiti, hujengwa kwa jinsi tunavyokaa na kudumu ndani yake, na kujua sifa zake, tabia zake, na uweza wake, Na hiyo inakuja kwa kusoma Neno, maombi, na ibada…watu wanaotembea katika mambo hayo kwa kipindi kirefu ndio wanaozama katika mapenzi ya kweli na Kristo.
Lakini mtu anayempenda Yesu kwasababu kaponywa ugonjwa, au kwasababu kasaidiwa Biashara yake kustawi, au Bwana amemwonekania mahali fulani kipekee, mwingine anamtumikia Mungu kwasababu ya shinikizo fulani la watu…Hapo ni sawa na kumrukia Ayala kwa pupa…hatimaye utamkosa..
Watu hawa wanakuwa ni upendo wa kitambo tu, mambo yakishabadilika waanza kusema mioyoni mwao, kama Yesu mwenyewe ndio huyu ni heri nirudie tu maisha yangu ya nyuma…
Hiyo yote ni kwasababu alikurupuka…bila kujua sifa na tabia za ampendaye.
Usikubali upendo wako kwa Kristo ujengwe kwa matukio ya ghafla…ujenge upendo katika mahusiano ya muda.. ndipo yatakapokuwa thabiti.
JAWA NA UPENDO UNAOTAFUTA.
USIKAWIE- KAWIE KUUFUNGUA MOYO WAKO
Maombi Maalumu ya Kuombea Ndoa.
SWALI: Naomba kufahamu Tafsiri vifungu hivi Mhubiri 4:13-16, isemayo ‘Kwa maana kutoka gerezani alikuja kumiliki’ Nini maana ya habari ile?
Mhubiri 4:13 Heri kijana maskini mwenye hekima Kuliko mfalme mzee mpumbavu. ambaye hajui tena kupokea maonyo. 14 Kwa maana kutoka gerezani alikuja kumiliki; naam, hata katika ufalme wake alizaliwa hali ya umaskini. 15 Nikawaona wote walio hai waendao chini ya jua, ya kwamba walishikamana na huyo kijana, huyo wa pili aliyesimama badala ya yule. 16 Hawakuwa na kikomo hao watu wote, hao wote ambao alikuwa juu yao; lakini hata hivyo wale wafuatao baada yake hawatamfurahia. Hakika hayo pia ni ubatili, na kujilisha upepo.
JIBU:
Mstari wa 13. Unazungumzia jinsi hekima, ilivyo bora kuliko cheo, au umri wa mtu. Yawezekana mtu akawa na vyote, lakini akipungukiwa na hekima, ni hatari kubwa sana, Na dalili moja wapo ya kupungukiwa hekima kama anavyofafanua mhubiri ni kukataa kupokea maonyo.
Mfano wa viongozi wa namna hii kwenye biblia ni Rehoboamu(mtoto wa Sulemani), Nebukadreza (nyakati za mwanzoni), Belshaza, Ahabu, Herode. Unaweza kuona jinsi utawala wao ulivyokuwa mwiba mkubwa kwa taifa, na wengine hata kwa vizazi vya mbeleni, kwasababu hawakukubali maonyo ya ki-Mungu..
Ni lazima tukubali kufundishika, kwasababu huo ndio msingi wa hekima (Mithali 13:1, 13:18, 15:5)
Lakini mstari wa 14
Anaeleza, jambo lingine, linalohusiana na ubatili… anazungumzia habari ya kijana aliyetoka katika umaskini, mpaka kuwa mfalme, aliyetoka vifungoni mpaka kuwa mfalme..
Kufunua kuwa mafanikio ya mwanadamu hayatabiriki, sio tu walio na cheo, au waliozaliwa katika familia ya kifalme, ndio wanaofanikiwa, Bwana anaweza kumwinua maskini, mtu asife faa, na kumfanya mtawala na mkuu, mfano wa Yusufu, na Daudi.
Pia Mstari 15,
Unaeleza kuinuka kwa mtawala mwingine, baada ya huyo kijana. Halafu watu wakashikamana naye huyo..Kuonyesha kuwa sifa za kibinadamu, huwa hauzidumu, maana yake kuwa hata uweje shujaa, ufanye mambo mazuri kiasi gani, utafurahiwa kwa kitambo tu, baadaye utachokwa, siku atakaponyanyuka mwingine, atapendwa, na kufuatawa..na wewe utasahaulika..
Mstari 16
Unaendelea kusema, bado watu waliendelea kumfauta huyo mfalme mpya, yaani walimfurahia pia sawa tu na walivyofurahiwa wafalme wengine nyuma waliopita, lakini ghafla baada ya muda wakamchoka naye pia..Mzunguko ukawa ni huo huo..
Ndipo mhubiri anahitimisha kwa kusema ni ubatili mtupu..Maana yake heshima, sifa, na mapokeo ya kibinadamu hayana umilele nyuma nyake, ni sawa tu na kufuata, upepo, ambapo unaweza kukupa matumaini ya muda, kukupelekea mbali, lakini katikati ya safari, ukayeyukia mbali na usijue unapokupeleka.
Haya ndio mambo tunayoyaona hata sasa katika ulimwengu, ni rahisi sana kuona watu wakimfurahia kiongozi mpya, tena yule mpambanaji, lakini baada ya muda wanaanza kupoteza furaha naye, na hatimaye kumpinga, wakitaka mwingine, na yule mwingine ajapo, huwa vivyo hivyo, wanamfurahia kwa muda, baadaye wanamchoka, mzunguko huo umekuwepo ulimwenguni wakati wote..
Lengo lao ni wakitumainia, kumpata kiongozi bora, lakini hajawahi kutokea..
Hawajui kuwa yupo kiongozi bora, mwema, asiyechokwa, asiye na hila, asitafuta vya kwake, aliyejitoa nafsi yake yeye mwenyewe, anayedumu milele, ambaye huyo mwanadamu akimkubali basi matarajio yake yanafikiwa, kwasababu ankuwa naye wakati wote moyoni mwake.. Na huyo si mwingine zaidi ya YESU KRISTO.
Amwaminiye, anapokea uzima wa milele. Wengine wote unafuata upepo..
Je! Upo tayari kumpokea leo, Kama ni ndio, basi fungua hapa kwa mwongozo wa sala ya Toba >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Maana ya Mhubiri 9:18 Hekima ndiyo bora kupita silaha za vita;
Nini maana ya hekima ya maskini haisikilizwi? (Mhubiri 9:16)
Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa watoto wake wote.
Ayubu 41:7 Je! Waweza kuijaza ngozi yake na vyuma vyenye ncha, Au kichwa chake kwa vyusa?
Vyusa ni mikuki maalumu iliyoundwa kwa ajili ya kunasia samaki, ambayo wavuvi hutembea nayo, kuvizia samaki, hususani wale waliokaribia na kilele, kisha huwachoma kwa nguvu, na kuwavuta nje ya maji, na kwasababu ya ukali na mvuvi, na wepesi wa ngozi zao, mara nyingi mkuki ule hauwezi kunasuka mwilini mwao.
Sasa katika habari hiyo, ukianzia mistari ya juu hata katika sura nzima na zile zilizotangulia, ni Ni mahojiano kati ya Ayubu na Mungu, ambapo Mungu anamuuliza maswali Ayubu ayajibu, ni maswali ambayo mpaka sasa hayana majibu, mambo makuu ya Mungu na uweza wake usiofafanulika kwa ufahamu wa kibinadamu. Sasa moja ya mambo aliyokuwa anamuuliza Ayubu ni kuhusu, mnyama “Mamba”, kwa jinsi alivyomuumba kwa namna ya kipekee, tofauti na samaki wengine, Anamweleza jinsi alivyo jasiri, asiye na woga, anamuuliza Ayubu je unaweza kutupa ndoano yako ukamvua kama vile ufanyavyo kwa samaki wengine?(Ay 41:1).
Kwa jinsi magamba yake yalivyo magumu, anasema hata upanga ukipita juu yake haumwingii..
41:26 Mtu akimpiga kwa upanga, haumwingii; Wala fumo, wala mshale, wala mkuki wenye ncha.
Ndio hapo sasa mbeleni anasema tena, je! Je unaweza kukitoba kichwa chake kwa vyusa, kama vile ufanyavyo kwa sangara, na perege? Si itakuwa sawa na unautoboa ukuta na chelewa.
Mungu kwa urefu ameeleza sifa zake mnyama huyu katika sura yote ya 41 (japo kimsingi alikuwa anamwelezea Kristo Yesu, kwa mfano wa wanyama), akimfananisha na mnyama huyu jinsi alivyokuwa thabiti kiasi kwamba hakukuwa silaha yoyote ya adui iliyompata, na jinsi alivyotisha na kuwa na nguvu za kushinda hata mauti..
Kwa uerfu wa habari hiyo fungua hapa usome>>>> SIFA ZA MAMBA YULE MKUBWA WA AYUBU.
Je! Umempokea mfalme huyu moyoni, mwenye nguvu za kutisha, asiyetikiswa na kitu chochote?. Kumbuka wokovu ni kwa faida yako mwenyewe, hakuna njia unaweza ukamshinda adui, kama Kristo hajakuficha ndani yake. Utavuliwa tu na adui kama samaki dhaifu, lakini uwapo ndani ya Kristo hakuna awezaye kukuvua. Ikiwa upo tayari kuyasalimisha maisha yako kwa Bwana Yesu..wasiliana na sisi kwa namba uzionazo mwisho wa makala hii.
Pia kwa maana za maneno mengine ya kwenye biblia fungua hapa >>>> Maana ya Maneno Kwenye Biblia
Madongoa ni nini? (Ayubu 7:5)
Nini maana ya Selahamalekothi?
Ayubu alimaanisha nini kusema ‘nami nitarudi tena huko uchi vilevile;?
Wimbo Ulio Bora 2:10-13
[10]Mpendwa wangu alinena, akaniambia, Ondoka, mpenzi wangu, mzuri wangu, uje zako, [11]Maana tazama, kaskazi imepita, Masika imekwisha, imekwenda zake; [12]Maua yatokea katika nchi, Wakati wa kupelea umefika, Na sauti ya mwigo husikiwa kwetu. [13]Mtini wapevusha tini zake, Na mizabibu inachanua, Inatoa harufu yake nzuri; Ondoka, mpenzi wangu, mzuri wangu, uje zako.
[10]Mpendwa wangu alinena, akaniambia, Ondoka, mpenzi wangu, mzuri wangu, uje zako,
[11]Maana tazama, kaskazi imepita, Masika imekwisha, imekwenda zake;
[12]Maua yatokea katika nchi, Wakati wa kupelea umefika, Na sauti ya mwigo husikiwa kwetu.
[13]Mtini wapevusha tini zake, Na mizabibu inachanua, Inatoa harufu yake nzuri; Ondoka, mpenzi wangu, mzuri wangu, uje zako.
Mahusiano yoyote yale hukumbwa na vipindi tofauti tofauti.ni sawa na dunia na misimu yake, kuna vipindi Vya kiangazi, vipindi vya masika, vipindi vya joto, na vipindi vya baridi…
Vivyo hivyo pia mahusiano yoyote hukumbwa na nyakati kama Hizi..
Watu wa agano la kale walikuwa katika nyakati ngumu za upendo na Mungu, nyakati zao zilijawa na misuko-suko, ukame na kutaabika, nyakati za jasho na damu…Kwasababu shetani alikuwa na nafasi kubwa katika maisha ya wanadamu, lakini walikuwa hawajamjua bado Mungu vizuri.
Lakini mwokozi alipokuja, alituliza dhoruba zote, mawimbi yote, jua lote, mizigo yote, na taabu zote ..alilitimiza hilo kwa kujitoa kwake pale msalabani. Ndio maana akasema yeye ni Bwana wa sabato, ( pumziko). Kwasababu Alikuja kuleta pumziko haswaa la pendo lake, ili mtu asikae katika masumbufu ya aina yoyote rohoni.
Hivyo leo hii anasema nasi kama mtu amwambiaye mpenzi wake habari za faraja..
10]Mpendwa wangu alinena, akaniambia, Ondoka, mpenzi wangu, mzuri wangu, uje zako, [11]Maana tazama, kaskazi imepita, Masika imekwisha, imekwenda zake; [12]Maua yatokea katika nchi, Wakati wa kupelea umefika,
10]Mpendwa wangu alinena, akaniambia, Ondoka, mpenzi wangu, mzuri wangu, uje zako,
[11]Maana tazama, kaskazi imepita, Masika imekwisha, imekwenda zake; [12]Maua yatokea katika nchi, Wakati wa kupelea umefika,
Huu ni wakati wa kuitikia wito wake mkuu wa upendo usio na usumbufu.. mpokee sasa ukuburudishe maishani. Akupe uzima wa milele, akupe faraja na tumaini uone maana ya maisha. Nyakati hizi ni za hatari, ulimwengu hauwezi kukupeleka popote, kinyume chake utaishia jehanamu tu ukiufuata, lakini ukimgeukia mwokozi na kumfuata utapata uzima wa milele.
SHALOM.
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 11 (Mithali, Wimbo ulio bora, Mhubiri)
Wimbo Ulio Bora 8:6-7
[6]Nitie kama muhuri moyoni mwako, Kama muhuri juu ya mkono wako; Kwa maana upendo una nguvu kama mauti, Na wivu ni mkali kama ahera. Mwako wake ni mwako wa moto, Na miali yake ni miali ya Yahu. [7]Maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo, Wala mito haiwezi kuuzamisha; Kama mtu angetoa badala ya upendo Mali yote ya nyumbani mwake, Angedharauliwa kabisa.
[6]Nitie kama muhuri moyoni mwako, Kama muhuri juu ya mkono wako; Kwa maana upendo una nguvu kama mauti, Na wivu ni mkali kama ahera. Mwako wake ni mwako wa moto, Na miali yake ni miali ya Yahu.
[7]Maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo, Wala mito haiwezi kuuzamisha; Kama mtu angetoa badala ya upendo Mali yote ya nyumbani mwake, Angedharauliwa kabisa.
Habari hiyo inamzungumzia Bwana arusi ambaye anataka kuingia katika mahusiano ya ndani na bibi arusi wake, hivyo anaanza kwa kumwomba amkubali Kama “Muhuri” .
muhuri huwa unawakilisha umiliki halali wa kitu hicho..
Hivyo huyu Bwana arusi anamtaka bibi arusi akubali muhuri wake, katika moyo wake na katika mkono wake…pande mbili…moyoni ikiwakilisha ndani yake na mkononi nje, yaani upendo wa ndani na ule upendo wa nje…kumilikiwa kwa ndani lakini pia kumilikiwa kwa nje..
Na matokeo Ya kufanya hivyo ndio hapo anaendelea kueleza sifa za huo upendo akisema upendo una nguvu kama mauti…yaani Kama vile mauti isivyo pingika juu ya mtu, kwamba kufa atakufa tu, vivyo hivyo upendo wa kweli ukimnasa mtu haupingiki..atamlinda tu.
lakini pia anasema wivu wake ni mkali kama Ahera, ni mfano huo huo, maana yake hauvumilii maovu, pale unaponajisiwa…ni lazima utatoa tu matokeo..unakula Kama moto moyoni…ndio Uliomla Bwana Yesu alipoona nyumba ya Baba yake imegeuzwa kuwa pango la wanyang’anyi akatengeneza kikoto na kuanza kuharibu kwa makusudi kazi zote za kipepo zilizokuwa zinaendelea pale hekaluni…wivu wa upendo huharibu lakini vile vilivyo viovu.
Bado anasema ‘maji mengi na mito Haviwezi kuuzima, Kama mtu angetoa badala ya upendo Mali yote ya nyumbani mwake, Angedharauliwa kabisa’
yaani hata mtu akijaribu kuuzimisha kwa hongo za kifedha anafanya kazi bure…
Nguvu ya upendo wa Kristo kwetu pale tunapoupokea vizuri..tunakuwa salama milele ndani Yake..
Lakini Hatua ya kwanza Kristo anataka kututia muhuri wake moyoni na mkononi…na muhuri huo ni Roho Mtakatifu (Waefeso 4:30), anataka udhihirisho wa Roho uonekane mioyoni mwetu, lakini pia mwilini (kwa matendo yetu).
Utakatifu wa ndani na nje.
Kuna Watu wanampokea Yesu moyoni tu, lakini badiliko la nje hawana habari nalo, wanamkiri kwa vinywa vyao lakini kwa matendo yao wanamkana..
Tito 1:16
[16]Wanakiri ya kwamba wanamjua Mungu, bali kwa matendo yao wanamkana; ni wenye machukizo, waasi, wala kwa kila tendo jema hawafai.
Hapo bado upendo wa kweli haujafunuliwa…lakini pale tunapodhamiria kumpokea Kristo Kwelikweli, basi nguvu ya upendo wake inatunasa na matokeo yake yanakuwa hata tufani ya namna gani ije, yeye mwenyewe anatushika, hata dunia nzima itutenge bado hatuwezi tikiswa, hata tuahidiwe utajiri na mali zote duniani, bado upendo wetu hauwezi kupungua kwa Kristo, kwasababu ni yeye mwenyewe aliyetunasa kwa agano la muhuri rohoni na mwilini.
Yesu alisema…
Warumi 8:35-39
[35]Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?
Je upo tayari leo kuokoka? Kama ni ndio basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo mwisho wa makala hii kwa msaada huo bure.
Wimbo Ulio Bora 5:2-6
[2]Nalikuwa nimelala, lakini moyo wangu u macho, Sikiliza! Mpendwa wangu anabisha! Nifungulie, umbu langu, mpenzi wangu, Hua wangu, mkamilifu wangu, Kwa maana kichwa changu kimelowa umande, Nywele zangu zina manyunyu ya usiku. [3]Nimeivua kanzu yangu; niivaeje? Nimeitawadha miguu; niichafueje? [4]Mpendwa wangu aliutia mkono wake tunduni, Na moyo wangu ukachomeka kwa ajili yake. [5]Nikaondoka nimfungulie mpendwa wangu; Mikono yangu ilidondoza manemane, Na vidole vyangu matone ya manemane, Penye vipini vya komeo. [6]Nalimfungulia mpendwa wangu, Lakini mpendwa wangu amegeuka amepita; (Nimezimia nafsi yangu aliponena), Nikamtafuta, nisimpate, Nikamwita, asiniitikie.
[2]Nalikuwa nimelala, lakini moyo wangu u macho, Sikiliza! Mpendwa wangu anabisha!
Nifungulie, umbu langu, mpenzi wangu, Hua wangu, mkamilifu wangu,
Kwa maana kichwa changu kimelowa umande, Nywele zangu zina manyunyu ya usiku.
[3]Nimeivua kanzu yangu; niivaeje? Nimeitawadha miguu; niichafueje?
[4]Mpendwa wangu aliutia mkono wake tunduni, Na moyo wangu ukachomeka kwa ajili yake.
[5]Nikaondoka nimfungulie mpendwa wangu; Mikono yangu ilidondoza manemane, Na vidole vyangu matone ya manemane, Penye vipini vya komeo.
[6]Nalimfungulia mpendwa wangu, Lakini mpendwa wangu amegeuka amepita;
(Nimezimia nafsi yangu aliponena),
Nikamtafuta, nisimpate, Nikamwita, asiniitikie.
Habari hii inaeleza kisa cha mtu na mpenzi wake, ambayo inafunua mahusiano ya mtu na Kristo, na jinsi mwitikio Wake unavyopaswa uwe.
Hapa anaonyesha mwanamke mmoja akiwa ndani usiku amelala peke yake na mara akasikia mpenzi wake anabisha Mlango amfungulie,
Lakini alijawa na uzito, akaanza kukawia-kawia, pengine huwenda kwasababu ya starehe ya kitanda, au kuna mambo yake mengine ya siri alikuwa anayafanya
Lakini bado mpenzi wake aliendelea kugonga, bila mafanikio ya kufunguliwa…na safari hii akatoa mpaka maneno ya upendo yamkini yatamshawishi ili aje kufungua kwa haraka. Lakini bado hakufua dafu.
Mpaka dakika ya mwisho, alipogonga, na mbisho ule kuingia moyoni mwa yule mwanamke, ukamchoma ndipo akatoka haraka na kwenda kumfungulia..
Lakini kwa bahati mbaya hakumkuta, kumbe tayari alishaondoka…akaanza kutoka kumtafuta bila mafanikio..na matokeo yake huko nje kukutana na madhara mengine.
Hili ni jambo ambalo watu wengi humfanyia Kristo rohoni sasa…Anasema..anasema..
Ufunuo wa Yohana 3:20
[20]Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.
Lakini watu hukawia-kawia kwasababu ya udanganyifu wa mambo Ya duniani, mwingine atasema ngoja kwanza nimalize ujana, ndio nitaokoka, mwingine ngoja nipate kazi mwingine ngoja niolewe, mwingine ngoja ifike mwakani, mwingine ngoja nikimaliza masomo ndio nitampokea Yesu..n.k
Ndugu Saa ya wokovu ni sasa Kristo anakuita, wakati ndio huu, usipoufungua moyo wako sasa, utafika Wakati utamtafuta Kristo na hutampata…
Luka 13:24
[24]Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.
Luka 12:36-40
[36]nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao, atakaporudi kutoka arusini, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara. [37]Heri watumwa wale, ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesha. Amin, nawaambieni, atajifunga na kuwakaribisha chakulani, atakuja na kuwahudumia. [38]Na akija zamu ya pili, au akija zamu ya tatu, na kuwakuta hivi, heri watumwa hao. [39]Lakini fahamuni neno hili, Kwamba mwenye nyumba angalijua saa atakayokuja mwivi, angalikesha, wala asingaliacha nyumba yake kuvunjwa. [40]Nanyi jiwekeni tayari, kwa kuwa saa msiyodhani ndipo ajapo Mwana wa Adamu.
[36]nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao, atakaporudi kutoka arusini, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara.
[37]Heri watumwa wale, ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesha. Amin, nawaambieni, atajifunga na kuwakaribisha chakulani, atakuja na kuwahudumia.
[38]Na akija zamu ya pili, au akija zamu ya tatu, na kuwakuta hivi, heri watumwa hao.
[39]Lakini fahamuni neno hili, Kwamba mwenye nyumba angalijua saa atakayokuja mwivi, angalikesha, wala asingaliacha nyumba yake kuvunjwa.
[40]Nanyi jiwekeni tayari, kwa kuwa saa msiyodhani ndipo ajapo Mwana wa Adamu.
Okoka leo ndugu, neema ya wokovu ipo sasa lakini haitadumu milele..hiyo sauti inayoita moyoni mwako itii, haraka, starehe za duniani zinapita, maisha yanapita, ikiwa upo tayari kumkabidhi Bwana maisha yako, basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii bure kwa msaada huo..
Mshulami ni msichana gani?
Yahu ni nani? (Wimbo 8:6).
Kimiami ni nini? (Wimbo ulio bora 2:9).
Wimbo Ulio Bora 3:1-4
[1]Usiku kitandani nalimtafuta mpendwa wa nafsi yangu, Nalimtafuta, nisimpate. [2]Nikasema, Haya, niondoke nizunguke mjini, Katika njia zake na viwanjani, Nimtafute mpendwa wa nafsi yangu. Nikamtafuta, nisimpate. [3]Walinzi wazungukao mjini waliniona; Je! Mmemwona mpendwa wa nafsi yangu? [4]Kitambo kidogo tu nikiisha kuwaondokea, Nikamwona mpendwa wa nafsi yangu; Nikamshika, nisimwache tena, Hata nilipomleta nyumbani mwa mamangu, Chumbani mwake aliyenizaa.
[1]Usiku kitandani nalimtafuta mpendwa wa nafsi yangu, Nalimtafuta, nisimpate.
[2]Nikasema, Haya, niondoke nizunguke mjini, Katika njia zake na viwanjani,
Nimtafute mpendwa wa nafsi yangu. Nikamtafuta, nisimpate.
[3]Walinzi wazungukao mjini waliniona; Je! Mmemwona mpendwa wa nafsi yangu?
[4]Kitambo kidogo tu nikiisha kuwaondokea, Nikamwona mpendwa wa nafsi yangu; Nikamshika, nisimwache tena, Hata nilipomleta nyumbani mwa mamangu, Chumbani mwake aliyenizaa.
Kitabu cha wimbo ulio-bora, ni kitabu ambacho huchukiliwa kimwili na watu wengi kana kwamba kiliandikwa mahususi kwa wana-ndoa.. Jambo ambalo sio kweli, Ikumbukwe kuwa dhumuni kuu la biblia ni kutueleza WAZO la Mungu, juu yetu ambalo hilo alilikamilisha kifasaha kupitia Yesu Kristo. Hivyo popote pale unapopasoma kwa namna moja au nyingine inaeleza kusudi la Mungu kwetu, katika kuyatimiza mapenzi yake..
Na ni kawaida yake tangu zamani kutumia mifano halisi ya namna mbalimbali ili kudhihirisha kusudi lake kamilifu kwetu.
Kwamfano ameweka familia, tujue sifa za wazazi ili tunapomwita Mungu Baba, tujue tabia za ubaba hasaa zipoje…Ameweka mabwana na watumwa ili tunapomwita yeye Bwana tujue sisi tunapaswa tuweje kwake kama watumwa..
Vivyo hivyo ameweka ndoa, na akajifunua kwetu kama mume, na sisi kanisa ni mke wake…Hivyo anataka tujue kama vile upendo wa mke na mume ulivyo ndivyo alivyo yeye kwetu sisi.
Sasa Katika habari hii, tunaona sifa ya upendo ambao Mungu anataka sisi tuuonyeshe kwake, Upendo usio ule wa upande mmoja, bali na upande wa pili, yaani sio tu yeye kututafuta sisi wakati wote hapana bali Na sisi tumtafute yeye..
Anaeleza kwa mfano wa igizo picha ya mwanamke ambaye yupo sikuzote na mpenzi Wake kitandani, lakini ikatokea siku moja alipoamka usiku hakumwona kitandani Mwake…
Hivyo hakuweza kuendelea kulala angali mumewe hayupo, ikambidi atoke aanze Kumtafuta usiku ule ule, sio kwa siri Bali hadharani tena sehemu zenye hatari ambazo walinzi tu usiku hupita kufanya doria..Na alipokutana Nao akawauliza juu ya mpenzi wake kama wamemwona, lakini Baadaye kidogo alimwona..akamkumbatia na kurudi naye mpaka mahali pao maalumu.
Yapo majira wewe kama mwana wa Mungu utapitia pengine hali fulani ya kushuka viwango kiroho, (ukame wa kiroho)
Lakini ukiwa na upendo wa kweli kwa Mungu wako, ni wazi kuwa hutakaa tu na kusema Mungu nisaidie…Hapana Utachukua tu hatua kama za huyu mwanamke ya kuamka na kuanza kutafuta namna ya kumtafuta mpenzi wako (Kristo) yaani kurejesha viwango vyako vya mwanzoni, hata kwa kugharimika raha, au vitu n.k..
Ndio hapo mtu hutenga muda mwingi wa maombi, mikesha, mifungo n.k.
Na kama vile yule Mwanamke alipowafuata walinzi usiku, kuwauliza habari za mumewe…Ndivyo ilivyo kwa mtu mwenye kiu na pendo na Mungu hataridhika kutembea yeye kama yeye tu, ataulizia msaada mpaka kwa viongozi wake wa kiroho apate mwongozo..(ambayo hufunua wale walinzi). Na hatimaye kufikia kilele cha mahusiano na Mungu wake tena.
Ndugu, kumbuka kuwa furaha, na amani, uzuri wa Kristo sio tu wa kuletewa sikuzote, bali pia wa kutafuta…Ni kweli siku za kwanza za wokovu uliona Kristo akijifunua Kwako kwa namna za ajabu, hata kama hukufanya lolote lakini sasahivi ni kama huoni moto ule ule uliokuwa nao…jua tu si kwamba umetenda dhambi au umemkosea Mungu…hapana ni kwamba Mungu anataka amke sasa mtafuta mpenzi wako..kudhihirisha upendo wa kweli..
Ndicho Yesu alichowaambia wale waandishi na mafarisayo juu ya wanafunzi wake..
Marko 2:18 Nao wanafunzi wake Yohana na Mafarisayo walikuwa wakifunga; basi walikuja, wakamwambia, Kwani wanafunzi wa Yohana na wanafunzi wa Mafarisayo hufunga, bali wanafunzi wako hawafungi? 19 Yesu akawaambia, Walioalikwa arusini wawezaje kufunga maadamu bwana-arusi yupo pamoja nao? Muda wote walipo na bwana-arusi pamoja nao hawawezi kufunga. 20 Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana-arusi, ndipo watakapofunga siku ile
Ongeza mikesha, mifungo, kusoma Neno sana…Na hatimaye utavipata na furaha yako itazidi ile ya kwanza…
Kwasababu upendo wa kweli hutafuta…
Naomba kujua maana ya haya maneno katika biblia..“Siti Msharifu”, “Mitalawanda” na “kulalama”
Mimi ni mweusi-mweusi, lakini ninao uzuri.