Napenda kujua watu wenye kuvunja maagano wanaozungumziwa katika Warumi 1:31, ndio watu wa namna gani?
Jibu: Tusome kuanzia mstari wa 28, ili tuweze kuelewa vizuri..
Warumi 1:28 “Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.29 Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya,30 wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao,31 wasio na ufahamu, WENYE KUVUNJA MAAGANO, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema;32 ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao”.
Warumi 1:28 “Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.
29 Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya,
30 wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao,
31 wasio na ufahamu, WENYE KUVUNJA MAAGANO, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema;
32 ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao”.
Umeona? watu wenye kuvunja maagano sio watu WANAOOMBA NA KUVUNJAA MAAGANO YA UKOO!! LA!. Bali wanaovunja maagano wanaozungumziwa hapo, ni watu wote ambao hawadumu katika AHADI ZAO, au MANENO YAO WENYEWE. Na hawa wamegawanyika katika makundi matatu.
1.WANAOVUNJA MAAGANO YA IMANI.
Mtu anapoamua kumfuata Yesu, na kuokoka anakuwa ameingia KATIKA AGANO LA DAMU YA YESU. Kuanzia huo wakati damu ya Yesu inaanza kunena juu yake, mtu huyo anakuwa rafiki wa Mungu, na mrithi wa ahadi za Mungu, kwasababu tayari kashaingia katika Agano la Mungu, kupitia damu ya Yesu.
Lakini huyu mtu anapoamua kuacha Wokovu, na kuurudia ulimwengu, tafsiri yake ni kwamba KALIVUNJA LILE AGANO TAKATIFU LA DAMU YA YESU, Ambalo kupitia hilo alitakaswa dhambi zake na kuwekwa huru mbali na utumwa wa dhambi.. Mtu wa namna hii maandiko yanasema hali yake itakuwa mbaya sana baada ya kufanya hivyo.
Waebrania 10:28 “Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu.29 Mwaonaje? HAIKUMPASA ADHABU ILIYO KUBWA ZAIDI MTU YULE ALIYEMKANYAGA MWANA WA MUNGU, NA KUIHESABU DAMU YA AGANO ALIYOTAKASWA KWAYO KUWA KITU OVYO, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?”
Waebrania 10:28 “Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu.
29 Mwaonaje? HAIKUMPASA ADHABU ILIYO KUBWA ZAIDI MTU YULE ALIYEMKANYAGA MWANA WA MUNGU, NA KUIHESABU DAMU YA AGANO ALIYOTAKASWA KWAYO KUWA KITU OVYO, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?”
Umeona?.. Ipo hatari kubwa sana ya KURUDI NYUMA baada ya kumpokea Yesu, kwasababu kwa kurudi nyuma kwako, ni sawa na UMELIVUNJA AGANO TAKATIFU.
2. AGANO LA NDOA.
Mtu aliyeoa au aliyeolewa katika Ndoa Takatifu, ambaye alisimama mbele ya kanisa la Kristo, na kuahidi mbele za Bwana kuwa ataishi na mwenzake katika hali yoyote ile atakayokutana nayo katika maisha, yaani katika hali ya shida na raha, na huzuni, na misiba na hata katika magonjwa na madhaifu..
Halafu ikatokea siku za mbeleni akamwacha Mwenzake, na kwenda kuoa au kuolewa na mwingine, Mtu wa namna hii ni MTU ANAYEVUNJA MAAGANO, ambaye adhabu yake ni kubwa sana.
Ndugu kama umeoa au umeolewa, fahamu kuwa hupaswi kumwacha mke wako au mume wako, unapaswa umvumilie katika kasoro zake, ukimwacha mke wako/mume wako kwasababu tu amekuwa mdhaifu katika mwili, au kwasababu anamepata ugonjwa fulani, au kwasababu amekuwa na hasira, au ameongezeka mwili au amezeeka..na ukaenda kuoa/kuolewa na mwingine, basi fahamu kuwa UMEVUNJA AGANO, na hatari ya kuvunja AGANO ni adhabu ya ziwa la Moto.
3.AGANO LAKO MWENYEWE.
Agano lako mwenyewe hilo linaweza kuwa NADHIRI uliyomwekea Mungu.. Kama umeweka Nadhiri Mbele za Mungu, basi hakikisha unaiondoa hiyo Nadhiri kwa kuitimiza..
Mhubiri 5:4 “Wewe ukimwekea Mungu nadhiri, usikawie kuiondoa; kwa kuwa yeye hawi radhi na wapumbavu; basi, uiondoe hiyo uliyoiweka nadhiri.5 Ni afadhali usiweke nadhiri, Kuliko kuiweka usiiondoe”
Mhubiri 5:4 “Wewe ukimwekea Mungu nadhiri, usikawie kuiondoa; kwa kuwa yeye hawi radhi na wapumbavu; basi, uiondoe hiyo uliyoiweka nadhiri.
5 Ni afadhali usiweke nadhiri, Kuliko kuiweka usiiondoe”
Vile vile kama umepanga kufanya jambo fulani Jema basi litimize hilo, KWASABABU HILO NI AGANO LAKO LA HIARI uliloingia WEWE NA ROHO YAKO.
Kuna mhubiri fulani alitokewa na Bwana Yesu katika maono, na Bwana akamwambia “Kama hutakuwa mwaminifu katika maneno yako mwenyewe, basi huwezi kuwa mwaminifu katika maneno yangu”.
Akimaanisha kuwa kama umesema utafunga hii wiki, au utasali masaa mawili leo, au utafanya hiki au kile kwaajili ya ufalme wa mbingu, halafu kitu hicho ulichokipanga katika roho yako, hutakitekeleza basi wewe Sio mwaminifu katika maneno yako mwenyewe, sio mwaminifu katika maagano yako mwenyewe, hivyo wewe ni mtu kigeugeu, unayevunja maagano yako…na Mungu hawezi kukuamini pia..
Yakobo 1:7 “Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.8 Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote”.
Yakobo 1:7 “Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.
8 Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote”.
Kumbukumbu 23:23 “Yaliyotoka midomoni mwako yashike kuyafanya; kwa mfano wa ulivyomwekea nadhiri Bwana, Mungu wako, ni sadaka ya hiari uliyoahidi kwa kinywa chako”.
Bwana atusaidie tusiwe watu wa kuvunja maagano, bali kutimiza maagano.Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Kwanini Paulo aungane na wale watu wanne wenye nadhiri?
Mtu mwenye “kitango” ni mtu wa namna gani kibiblia?
Ni kwa namna gani malaika wa mbinguni wanaweza kutuhubiria sisi injili?
Biblia inasema tusiwe kwazo kwa yeyote, je! inawezekanikaje kwa dunia hii ya sasa?(2Wakorintho 6:3).
SI MAPEPO YOTE NI YA KULIPUKA.
Rudi nyumbani
Print this post
Barikiwa sana na BWANA mwalimu,umeniongezea maarifa katika somo hili.