Haya ndio mambo ambayo baada ya kuokoka, wokovu hufanya juu ya maisha ya mtu
Yohana 3:3
[3]Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.
Maana yake ni kwamba pindi tu unapookoka, ni lazima ufahamu si kwamba unarekebisha yale maisha yako ya kale, na kuwa mtu mwema hapana bali unakuwa mtu mwingine kabisa. Kama mtoto mchanga aliyekuja duniani, katika mazingira mapya kabisa.
Kwasababu ukristo sio nembo, au kikundi, au mtindo fulani au aina fulani ya dini hapana bali ni ulimwengu mwingine kabisa ambao mtu anaanza kuuishi.
2 Wakorintho 5:17
[17]Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.
Wakolosai 1:13
[13]Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake;
Maana yake ni kuwa tunakuwa tayari kutoka chini ya utawala wote wa shetani, yaani kufuatisha mambo Ya kidunia, na anasa, wizi, tunaacha, Kama tulikuwa na vikoba vya kiganga, hirizi, mazindiko yote hayo tunayaondoa, na kuanza kumtumikia Kristo, mfalme mpya.
Wafilipi 2:12-13
[12]Basi, wapendwa wangu, kama vile mlivyotii sikuzote, si wakati mimi nilipokuwapo tu, bali sasa zaidi sana mimi nisipokuwapo, utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka. [13]Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.
[12]Basi, wapendwa wangu, kama vile mlivyotii sikuzote, si wakati mimi nilipokuwapo tu, bali sasa zaidi sana mimi nisipokuwapo, utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka.
[13]Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.
Maana yake ni lazima Tujue wokovu ni mwendelezo ijapokuwa tunaokolewa pindi tu tunapookoka, lakini hatuupokei tu, na kusema tayari imekwisha hapana bali unapaswa udumu Moyoni mwetu, na kuhakikisha kila siku tunaweka umakini kwa kuuzalia matunda, kwa kufanya bidii kuishi maisha yampendezayo Mungu.
Hivyo kwa ufupi wokovu sio tu, kipawa cha Mungu Kwetu, lakini pia kukubali maisha mapya, mfalme mpya, na njia mpya.
Maana yake ni nini?
Tangu siku hii ya leo wewe uliyookoka hakikisha unayaweka kando mambo yote ya kale ambayo ulikuwa unayafanya yasiyompendeza Mungu, kwasababu hiyo ndio TOBA pekee, kama ulikuwa mzinzi acha mara moja, ulikuwa mlevi, ulikuwa mwizi, ulikuwa mlanguzi acha, kama alivyofanya Zakayo alipokutana na Kristo. Kisha endelea kuishi maisha ya utakaso kila siku, ili Wokovu wako uzidi kuwa thabiti.
Bofya hapa kurudi kwenye mwongozo mkuu wa mafundisho ya mwongofu mpya. >>
Nini kinafuata? bofya hapa. >>>
Utambulisho wa kiumbe kipya
Vigezo vya neema ya Mungu
Kuzaliwa mara ya pili
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mungu ana makusudi makubwa na wewe, kwanza kukuokoa, na pili kukudhihirishia wema wake wote maishani mwako. Maamuzi haya ya kumpokea Bwana Yesu ni ya busara sana ambayo utayafurahia milele yote.
Ili kuupokea wokovu basi hapo ulipo unaweza kuchukua hatua ya imani, kwa kupiga magoti, kisha utafuatisha sala hii kwa imani. Na hakika wakati huu huu utaupokea wokovu bure.
Sema maneno haya kwa sauti:
“Bwana Yesu ninaamini kuwa wewe ni mwana wa Mungu, ninaamini kuwa ulikufa kwa ajili ya dhambi zangu, ukafufuka tena, na sasa unaishi milele. Ninakiri kuwa mimi ni mwenye dhambi, nimestahili hukumu na kifo. Lakini leo ninaungama makosa yangu na dhambi zangu zote, na kuyasalimisha maisha yangu kwako. Ninaomba msamaha wako Bwana Yesu, liandike sasa jina langu katika kitabu cha uzima. Nakukaribisha moyoni mwangu, uwe na Bwana na mwokozi wangu tangu sasa. Nimeamua kukutii na kukufuata wewe sikuzote za maisha yangu. Asante Bwana Yesu kwa kunisamehe na kuniokoa. Amen”
Kwa sala hiyo fupi, tayari Bwana Yesu ameshakusamehe dhambi zako, kumbuka kusamehewa sio kumlilia Mungu sana kwa wingi wa dhambi zako ulizomtenda..Kana kwamba unamshawishi Mungu akusamehe. Hapana.
Mungu tayari alishawasamehe wanadamu kwa kifo cha Yesu Kristo pale msalabani. Hivyo ni jukumu tu la wanadamu kuukubali msamaha wa dhambi mioyoni mwao kwa kuamini Kile ambacho Mungu alikifanya Kupitia Yesu Kristo.
Ndicho ambacho Mungu alikisema hapa
Warumi 10:9-10
[9]Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. [10]Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.
Kuamini kunakozungumziwa hapo ndio huko kukubali kwenyewe kazi ya Yesu aliyoifanya ya kuondoa dhambi za watu, kwa kufa kwake pale msalabani.
Ni sawa na mtu anakuja kukwambia nakupa hii almasi, ukiipokea basi umaskini wako wote umeondoka.
Sasa wewe kwa upande wako sio tena kukililia, hapana bali unawajibu tu wa kuamini kile kitu anachokupa, kwamba kinauwezo wa kuondoa umaskini..Ambapo sasa hudhihirishwa kwa kukipokea.
Ukishapokea sasa ndio matunda yake unayaona, kinyume chake ni kwamba bila kuamini kamwe huwezi kupokea, na umaskini utaendelea kubaki kwako daima.
Ndicho Yesu alichokileta Kwetu. Ambacho ni msamaha wa dhambi. Akasema ukiamini Kuwa nimekufa kwa ajili ya dhambi zako, ili zifutwe kabisa kabisa basi utaokoka. Hivyo pale unapoamini kwa kukubali kumfanya Yesu kuwa ndio Bwana na mwokozi wako tangu huo wakati na kuendelea, na kwamba alikufa kwa ajili yako..Basi dhambi zako zinakuwa zimeondolewa kuanzia huo wakati, haijalishi zilikuwa ni nyingi Kiasi gani.
Hilo tu, ndio maana sala hiyo fupi, ikiwa umeisema kwa dhati yatosha, kukufanya wewe kuwa mwana wa Mungu. Kwasababu tayari Umemkubali Yesu kama Bwana na mwokozi wako. Hilo ni hakikisho lake.
Kataa fikra za shetani
Neema ni nini?
Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo?
Mafundisho mengine:
Jina la Mkuu wa Uzima na Mfalme wa haki na pekee, YESU KRISTO libarikiwe, karibu tujifunze Biblia, Neno la Mungu wetu, lililo taa na Mwanga wa Njia yetu (Zab.119:105).
Kama Mkristo ni lazima uzijue alama hizi kuu nne (04), zitakazothibitisha kuwa unaye KRISTO maishani mwako, na alama hizo ni HEKIMA, HAKI, UTAKATIFU na UKOMBOZI.
1Wakorintho 1:30 “Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi”
Maana yake kupitia Yesu Kristo tunapata Hekima, Haki, Utakatifu na Ukombozi.
1. HEKIMA YA MUNGU.
Kama Yesu ni hekima ya Mungu kwetu, je hii hekima ni nini na tunaipataje..
Ayubu 28:28 “Kisha akamwambia mwanadamu, Tazama, kumcha Bwana ndiyo hekima, Na kujitenga na uovu ndio ufahamu”.
Kumbe kumcha Bwana ndio hekima, maana yake kumpata Yesu ni kupata kumcha Bwana, na ndio hekima ya Mungu, na pasipo Yesu hakuna kumcha Mungu.
2. HAKI.
Na kama Yesu ni haki ya Mungu, je hii haki inapatikanaje..
Warumi 3:21 “Lakini sasa, haki ya Mungu imedhihirika pasipo sheria; inashuhudiwa na torati na manabii; 22 ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti; 23 kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; 24 wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu”
Warumi 3:21 “Lakini sasa, haki ya Mungu imedhihirika pasipo sheria; inashuhudiwa na torati na manabii;
22 ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti;
23 kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;
24 wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu”
Tunapomwamini Yesu tunakuwa tumeipata haki ya Mungu, haki ya kupokea kila tuombacho, haki ya kuishi milele, haki ya kumkaribia Mungu, haki ya kuwa na afya, haki ya kuwa na amani, haki ya kuwa na furaha n.k
3. UTAKATIFU.
Na kama pia Bwana Yesu ni Utakatifu wa Mungu.. Je huu utakatifu tunaupataje?
Hiki ni kipengele muhimu sana, ambacho kinakwepwa na wengi, kumbuka huwezi kumtenganisha Yesu na UTAKATIFU, Ikiwa umemwamini Yesu ni lazima uishi maisha ya Utakatifu, hiyo ni kanuni. Na utakatifu sio ule wa rohoni tu, bali pia wa mwilini..
2Wakorintho 7:1 “Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku TUKITIMIZA UTAKATIFU katika kumcha Mungu”.
Utakatifu unakuja kwa kujitenga na vichocheo vyote vya dhambi, ambavyo vyanzo vyake ni tamaa ya macho na mwili, mfano wa hizo ni maudhui yote machafu yanayopatikana kwenye luninga, Mitandao na Magazeti, vile vile mazungumzo mabaya na makundi mabaya..
4. UKOMBOZI.
Yesu Kristo amefanyika pia ukombozi kwetu, kupitia kifo chake.. Na hii ndio alama ya mwisho inayomtambulisha Yesu, ambayo kimsingi hii ndio inayojulikana sana na wengi!
Wakolosai 1:13 “Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake. 14 ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi”
Wakolosai 1:13 “Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake.
14 ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi”
Ndugu ukimjua Yesu kama mkombozi tu! (yaani anayesamehe dhambi), pasipo kumjua kwamba yeye pia ni “Mtakatifu” na anataka tuwe watakatifu kuna shida katika kuaminini kwako, vile vile ukimjua tu kama ni mtakatifu pasipo kumjua kama ni Hekima ya Mungu na Haki ya Mungu, bado pia kuna kitu kitakuwa hakijakamilika.. Lakini tukimjua katika sifa hizo Nne na kuziishi basi tutakuwa tumemjua hasa, na kufikia ule utimilifu.
Waefeso 4:13 “hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo”
Bwana atusaidie tuweze kufikia cheo cha kimo cha utimilifu wake.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Maana ya Mithali 29:9 Mwenye hekima akijadiliana na mpumbavu; Akikasirika au akicheka, pia hapana raha.
Maana ya Mithali 10:1 Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye;
HEKIMA NANE(8) ZA KIUINJILISTI, KATIKA KUWAVUA WATU KWA KRISTO.
Nini maana ya hekima ya maskini haisikilizwi? (Mhubiri 9:16)
Maana ya Mhubiri 9:18 Hekima ndiyo bora kupita silaha za vita;
Huyu Imanueli tunayemsoma katika Isaya ni nani?
Swali: Tukisoma kitabu cha Isaya 7:14 tunamsoma Imanueli ambaye kimsingi ni Bwana YESU lakini tukiruka sura moja mbele (ile ya 8:8), tunamsoma Imanueli mwingine, juu huyu naye ni YESU au?
Jibu: Awali turejee mistari hiyo..
Isaya 7:14 “Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli”.
Ni wazi kuwa huyu si mwingine zaidi ya Bwana wetu YESU KRISTO.
Lakini hebu tuendelee na Isaya 8:8..
Isaya 8:8 “naye atapita, atapita kwa kasi na kuingia Yuda; atafurika na kupita katikati, atafika hata shingoni; na kule kuyanyosha mabawa yake kutaujaza upana wa nchi yako, Ee IMANUELI”.
Na hapa tunamwona Imanueli, sasa swali huyu naye ni Bwana YESU?.
Jibu ni la huyu si Bwana YESU.. awali ya yote ni vizuri kujua maana ya Imanueli..
Maana ya Imanueli ni “Mungu pamoja nasi”… hiyo ndio maana ya Imanueli, na ndio maana si ajabu neno hilo kuonekana katika biblia zaidi ya mara moja.
Sasa huyu Imanueli katika Isaya 8:8 ni Taifa la YUDA. Na hapa ametajwa kama Imanueli, kumaanisha uwepo wa Mungu kati ya Taifa hilo.
Ikiisoma habari hiyo kwa undani utaona kuwa ni kipindi ambacho mataifa mawili (Israeli na Shamu), yaliungana kutaka kupigana na Taifa la Ashuru, na kwasababu hiyo mataifa hayo mawili yalitaka kulishurutisha pia Taifa la Yuda liungane nao ili kwa pamoja wakampige Ashuru.
Lakini mfalme wa Yuda aliyeitwa Ahazi alikataa ushirika huo, na mataifa hayo mawili yakapanga njama kuvamia Yuda ili yamwue Ahazi na kumweka mfalme mwingine atakayekubaliana na wazo lao hilo la muungano…
Na matokeo yake mfalme Ahazi akataka msaada kwa waashuri (Taifa la Ashuru), dhidi ya hayo mataifa mawili yaliyoungana..
ndipo Isaya nabii kwa ujumbe wa Bwana akawaambia Ahazi na Yuda yote kuwa wasimtegemee huyo mfalme wa Ashuru katika kutafuta msaada, wala wasiogope hayo mataifa mawili yaliyoungana (yaani Israeli na Shamu) kwani wao (Yuda) ni IMANUELI yaani MUNGU yu pamoja nao.
Kwahiyo yeyote mwenye MUNGU ni Imanueli (iwe mtu au Taifa)..ni Imanueli, wote walio okoka ni Imanueli kwasababu MUNGU yu pamoja nao.
Je upo ndani ya YESU?.
Kumbuka Mungu hawezi kuwa pamoja nawe kama wewe hujafungua mlango wa kuwa pamoja naye
Yohana 15:4 “Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu”
Fungua mlango leo wa kumkaribisha YESU maishani mwako, nawe utamwona MUNGU katika viwango vingine vya kiroho.
Ufunuo 3:20 “Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami”.
Maran atha!
Ikiwa utahitaji Account yako nzima ifutwe moja kwa moja kwasababu zozote zile, pamoja na maudhui yake yote, basi wasiliana basi tutumie maombi hayo kupitia email yetu hii watakatifuwasikuzamwisho@gmail.com au namba zetu tajwa hapo chini na tutafanya hivyo mara moja.
+255789001312 au +255693036618
Ifuatayao ni Sera ya Faragha ya Tovuti/App ya Nuru ya Upendo (wingulamashahidi.org)
Tarehe ya Mwisho wa Marekebisho: [21/05/2025]
Tunapenda kukushukuru kwa kuchagua kutumia kituo cha Wingulamashahidi, jukwaa la injili ya YESU KRISTO, mafundisho ya Biblia, maombi, na jumbe za wokovu kupitia tovuti yetu na app yetu rasmi. Tunathamini faragha yako na tunajitahidi kuhakikisha taarifa zako zinalindwa kikamilifu.
Lengo la kukusanya taarifa zako ni kukuletea huduma ya kiroho iliyo bora zaidi. Na taarifa tuzikusanyazo ni:
Taarifa Binafsi (kama utazijaza): ambazo ni Jina lako, barua pepe, namba yako ya simu.
Taarifa za Kiufundi: Aina ya kifaa unachotumia, anwani ya IP, aina ya kivinjari, lugha, na mfumo wa uendeshaji.
Taarifa za Matumizi: Maudhui unayoyasoma, au kupakua, au kushiriki. Hii inatusaidia kujua aina gani ya masomo yanayopendelewa zaidi na watu.
Taarifa hizi zinahitajika kwa:
Kukurushia masomo mapya kwenye barua pepe yako.
Kuboresha muundo na mwonekano wa tovuti pamoja na app
Kujibu maswali yako, maombi ya maombi, au mawasiliano mengine ya kiroho..
Hatua za kiusalama tunazizingatia (kama SSL, uthibitisho wa watumiaji, na encryption) kuhakikisha taarifa zako hazidukuliwi na yoyote, wala kupotea, wala kutumiwa bila idhini ya mhusika. Pia tunazingatia kanuni za kimaadili kulingana na ukristo.
Hatutashiriki wala kuziuza, kusambaza, au kugawa taarifa zako binafsi kwa mtu mwingine yoyote bila idhini yako isipokuwa:
Kwa mujibu wa sheria au maelekezo ya mamlaka husika.
Kwa watoa huduma wanaotusaidia kutoa huduma hizi (mfano: huduma ya kutuma barua pepe), kwa masharti ya usiri.
Ikiwa kama utachagua kushiriki jumbe kwenye mitandao ya kijamii.
Hatukusanyi taarifa za watoto walio chini ya miaka 12 bila idhini ya wazazi au walezi. Ikiwa mzazi ataona kuwa kuwa mtoto wake ametoa taarifa binafsi bila idhini yao, basi tunaomba awasiliane nasi ili tuchukue hatua za kuondoa taarifa hizo mara moja.
Unayo haki ya:
Kufahamu ni taarifa gani tulizonazo kuhusu wewe.
Kuomba taarifa zako zifutwe au kurekebishwa inapohitajika.
Kujiondoa kwenye orodha ya wanaopokea pokea mafundisho kwa njia ya barua pepe au yoyote ile.
Kuhoji matumizi ya taarifa zako kwa ajili ya tafiti, chunguzi au matangazo (kama yatakuwepo).
Tovuti yetu hutumia cookies ili kuboresha matumizi yako. Unaweza kuchagua kuzima kama haitakuwa ni mapendekezo yako, lakini hii yaweza kuathiri usomaji wako wa tovuti.
Patakapotokea mabadiliko ya Sera hizi, tutakujuza mabadiliko hayo kupitia tovuti z. Mabadiliko huanza kutumika mara moja baada ya kuchapishwa.
Kwa maswali kuhusiana na sera hizi za faragha, tafadhali wasiliana nasi kupitia:
Barua pepe: wingulamashahidi@gmail.comTovuti: https://wingulamashahidi.org
Mungu akubariki sana kwa kuwa sehemu ya huduma hii. Tunakuombea baraka za Bwana YESU ziende nawe
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Shalom
SWALI: Nini maana ya Mithali 3:27 ?
[27]Usiwanyime watu mema yaliyo haki yao, Ikiwa katika uwezo wa mkono wako kuyatenda.
JIBU: Kuna mambo mawili yaliyogusiwa katika hicho kifungu..
Hili ni agizo la Bwana kuwasaidia wengine. Lakini pia Bwana anataka tujue ni akina nani wenye haki hiyo ya kusaidiwa.
Kibiblia Makundi ambayo ni haki yao kusaidiwa.(wawapo na shida), ni matatu (3)
i) Familia (yaani ndugu wa mwilini)
1 Timotheo 5:8
[8]Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.
Wazazi wako, wadogo zako, watoto wako. Ni haki yao kuwasaidia, kwasababu ni damu moja na wewe. Usipotimiza wajibu huo unahesabika sawa na mtu aliyeikana imani. Hakikisha jicho lako haliwapiti ndugu zako, ni sehemu ya wajibu.
ii) Ndugu wa rohoni:
Wagalatia 6:10
[10]Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.
Kanisa la kwanza lilitambua jukumu hili la kusaidiana, vivyo hivyo na sisi ikiwa mpendwa mwenzako yupo katika hali na uhitaji mkubwa hupaswi kufumba macho, bali msaidie, watumishi wa Mungu wanaojibidiisha kuhubiri kweli ya Mungu wanastahili kusaidiwa mahitaji yao. (Warumi Romans 12:13, Hebrews 13:16).
1Yohana 3:17 Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo? 18 Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli.
Hapa inalenga pia na wajane pia walio ndani ya kanisa wale walio wajane kwelikweli. (1Timotheo 5:3–5, 9–10)
iii) Maskini.
Wapo maskini wengi ulimwenguni, ambao wanashindwa kufikiwa na mahitaji yao ya msingi, wengine wanakuwa mabarabarani walemavu, wagonjwa, majirani maskini, wote hawa pia wanastahili kusaidiwa.
Wagalatia 2:10 ila neno moja tu walitutakia, tuwakumbuke maskini; nami neno lilo hilo nalikuwa na bidii kulifanya.
Hayo ndio makundi yenye haki ya kusaidiwa. Lakini wengine wanaweza kusaidiwa lakini sio haki yao, ikiwa na maana hata wasiposaidiwa hakuna shitaka lolote juu yako kwa Mungu.
Lakini Ukiendelea kusoma anagusia tena jambo la pili ambalo ni; “Ikiwa katika uwezo wa mkono wako kuyatenda”.
Akiwa na maana gani?
Mtume Paulo kwa uweza wa Roho aliandika maneno haya;
2 Wakorintho 8:12-13
[12]Maana, kama nia ipo, hukubaliwa kwa kadiri ya alivyo navyo mtu, si kwa kadiri ya asivyo navyo. [13]Maana sisemi hayo, ili wengine wapate raha nanyi mpate dhiki;
Yaani kwa jinsi moyo wako unavyoguswa, tenda mema, lakini pia kulingana na uwezo wako uliokirimiwa na Mungu, ili upande mmoja usiuache na taabu au kupungukiwa kabisa. Kwamfano umepata rizki kipimo cha watoto wako tu, ukaenda kukichukua na kuwapa maskini huku familia yako ikabaki Kulala njaa.. hapo hujafanya busara kwasababu umehamisha Tatizo sehemu moja kupeleka kwingine, hujatatua tatizo.
Tenda mema, bila kusahau pia kipimo chako ulichopimiwa cha mema.
Masomo mengine:
Elewa tafsiri ya Mithali 27:22 Hata ukimtwanga mpumbavu kwa mchi kinuni.
Elewa maana ya Mithali 18:23 Maskini hutumia maombi; Bali tajiri hujibu kwa ukali.
Nini maana ya Mithali 24:11 Uwaokoe wanaochukuliwa ili wauawe?
Swali: “Halafu ile tama ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti, (Yakobo 1:15).. je kutamani sio dhambi?”
Jibu: Kwa asili kutamani sio dhambi! Bali kunaweza kuwa ni mwanzo wa dhambi.. ni sawa na “kuongea”..kuongea si dhambi lakini kunaweza kuwa chanzo cha dhambi, kutegemea ni nini unaongea..
Na vile vile “tamaa” kwaasili ..imeumbwa ndani ya Mtu, na hata ndani ya viumbe vyote, ambayo lengo lake ni kuhamasisha jambo fulani jema au baya lifanyike katika mwili wa mtu au maisha ya mtu.
Kwamfano hatuwezi kumtafuta MUNGU kama yeye mwenyewe hajaiweka hiyo tamaa ndani yetu..hatuwezi kuomba kama yeye hatatuwekea hiyo tamaa ndani yetu n.k
Vile vile katika masuala ya mwilini, tusingependa kula wala kuhamasika kula chakula kama tusingewekewa ndani yetu tamaa ya chakula, ile tamaa iliyowekwa ndani inatuhamasisha kula chakula, na tunapokula miili yetu inapata faida, na kutimiza lengo la kuendelea kuishi.. Lakini tamaa hiyo inapozidi mipaka inazaa ulafi na ulevi ambao ni dhambi (Soma Luka 21:34, Warumi 13:13, Wagalatia 5:21, na 1Petro 4:3).
Vile vile pia mtu kawekewa tamaa ndani yake ya kimwili kwa jinsia tofauti na yake, tamaa hiyo Mungu kaiweka ndani ya mtu kwa kusudi maalumu na wakati maalumu, kwamba wakati utakapofika mtu aweze kukutana na mke/mume wake na kuzaa watoto, kutimiza Baraka alizozisema katika Mwanzo 1:28
Mwanzo 1:27 “Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. 28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi:”.
Mwanzo 1:27 “Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi:”.
Lakini tamaa hiyo inapozidi na kuvuka mipaka kiasi kwamba inampelekea mtu kushindwa kujitawala ndipo anapoanguka katika zinaa na hata zinaaa ya jinsia moja na yake.
Kwahiyo tamaa yoyote ile iwe ya chakula, au ya mwili kwaasili sio mbaya, ila inapozaa matunda mabaya ndipo inageuka kuwa dhambi..Na ndicho Biblia ilichokimaanisha hapo katika Yakobo 1:15 kuwa “tamaa ikiisha kuchukua mimba inazaa dhambi”..maana yake katika uasili wake sio dhambi!.. ila inapochochewa kwa njia isiyopaswa ndipo inapozaa dhambi.
Unatazama picha chafu mitandaoni, au unaposoma makala zenye maudhui ya zinaa, au unaposhiriki mijadala yenye maudhui ya zinaa hapo unaizalia matunda ile tamaa ya mwili ndani yako, na hiyo ni dhambi, kwasababu mwisho wa siku itakupelekea kufanya zinaa au kujichua, au mawazo yako muda wote kutawaliwa na zinaa jambo ambalo biblia imesema kuwa ni machukizo kwa Bwana, moyo uwazayo mabaya (Mithali 6:18).
Biblia inatufundisha kutoyachochea mapenzi..
Wimbo 2: 7 “Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe”.
Na tamaa nyingine zote ni hivyo hivyo, hatuna budi kuzitawala ili zisizae dhambi, maana mshahara wa dhambi ni Mauti… na tamaa zinazozaa dhambi zote zinatokana na dunia na si MUNGU..
1Yohana 2:16 kuwa tamaa ya macho na tamaa ya mwili inatokana na dunia na si Mungu
Bwana atusaidie.
NI NJIA GANI MTU AITUMIE AWEZE KUSHINDA TAMAA NA VISHAWISHI?
USIWE NA TAMAA YA CHAKULA KINGINE.
USIKATE TAMAA UNAPOPITIA MAGONJWA.
Jiepushe na tamaa ya Mali/kupenda fedha.
Roho ya kukata tamaa ni nini na inatendaje kazi?
WhatsApp
SWALI: Naomba kufahamu Warumi 7:25 ina maana gani?
Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Basi, kama ni hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi.
JIBU: Katika sura yote ya saba, mtume Paulo, anaeleza kwa kina mapambano yaliyo ndani ya mwamini. Kwamba nia yake kutoka ndani ni kuitii sheria ya Mungu, lakini mwili wake kwa nje ni kikwazo kikubwa kiasi cha kumfanya ashindwe kabisa kutimiza maadhimio yake.
Warumi 7:19 Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo. 20 Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu
Na ni kweli huo ndio uhalisia wa kila mtu. Na ndio maana mwishoni mwa sura hiyo anahitimisha kwa kueleza hali hiyo, Lakini katika vifungu hivyo, wengi wanatafsiri vibaya wakidhani Paulo anatetea udhaifu wa mwili hapana.. Kinyume chake alianza kwanza kueleza uhalisia wa kibinadamu, ili atoe suluhisho halisi la namna ya kushinda, ambalo ndio tunalisoma katika sura inayofuata ya nane (8)
Ambapo sasa kwenye sura ya nane(8) inayofuata, anaeleza namna ambayo Kristo anatusaidia kuishinda hiyo hali, kwa sheria nyingine mpya ya Roho ambayo anaiweka ndani yetu.
Warumi 8:1 Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. 2 Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti. Maana yake ni kuwa, Roho Mtakatifu, anatuweka huru katika huo utumwa wa mwili unaotupelekesha.
Warumi 8:1 Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.
2 Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti. Maana yake ni kuwa, Roho Mtakatifu, anatuweka huru katika huo utumwa wa mwili unaotupelekesha.
Inahitaji tu kutii, kwa kumfuata Roho Mtakatifu, kisha yeye mwenyewe atatupa nguvu ya kushinda mambo yote ya mwilini. Lakini sio kwa kutegemea nguvu zetu tu wenyewe.
Warumi 8: 5 Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho.6 Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani. 7 Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii. 8 Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu. 9 Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake. 10 Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki.
Warumi 8: 5 Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho.6 Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani.
7 Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii. 8 Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu.
9 Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.
10 Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki.
Hivyo ukiishi kwa kumtii Roho Mtakatifu, basi huwezi tumikishwa tena na mwili,
Wagalatia 5:16 Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. 17 Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. 18 Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria.
Wagalatia 5:16 Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.
17 Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. 18 Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria.
Warumi 7:25, Paulo analenga hasaa sababu ya sisi kushindwa kutimiza sheria ya Mungu, Ni kwasababu ipo sheria nyingine (ya dhambi iliyojificha ndani yetu) ambayo ni ngumu kutoka kwa namna ya kibinadamu, hivyo anataka hilo tulijue ili tufahamu kuwa kwa nguvu zetu wenyewe hatuwezi kuishinda, Lakini kwa Yesu Kristo atupaye Roho wake ndani yetu, tukienenda kwa kumtii huyo, basi sheria hiyo ya dhambi tutaishinda kabisa kabisa.
Ni wito wa kila mwamini kujifunza kutembea katika Roho.
Je! Unafahamu namna ya kutembea katika Roho kama sio. Basi tutumie ujumbe kwa namba uzionazo chini ya somo hili tukutumie.
NITAUVUTAJE UWEPO WA ROHO MTAKATIFU KARIBU NAMI?
MAANA ROHO HUCHUNGUZA YOTE, HATA MAFUMBO YA MUNGU.
Sadaka inayotolewa kwa mwongozo wa Neno la MUNGU ina matokeo makubwa sana kwa anayeitoa. Yapo madhara yanayoondoka kwa maombi tu peke yake, lakini yapo mengine yanahitaji sadaka pamoja na maombi.
Hebu turejee Biblia kidogo tujifunze jambo..
Wakati ambapo Nabii Samweli anataka kwenda kumpaka mafuta Daudi ili awe mfalme mahali pa Sauli..biblia inatuambia kuwa alipofikiri kwenda tu hofu ilimwingia..
Na hofu hiyo ni kwamba alimwogopa Mfalme Sauli, kwani alijua kabisa endapo Sauli akisikia mtu mwingine anaenda kupakwa mafuta ya kifalme kuchukua sehemu yake, wivu utamwingia na atataka kumwua nabii Samweli na yule atakayeenda kupakwa mafuta.
Sasa ili zoezi la Daudi kupakwa mafuta likamilike bila kuleta madhara yoyote kwa Nabii Samweli na Daudi anayeenda kupakwa mafuta ya kifalme, SADAKA ILIHUSIKA!.
Utauliza ilihusika vipi?…turejee maandiko…
1 Samweli 16:1 “BWANA akamwambia Samweli, Hata lini utamlilia Sauli, ikiwa mimi nimemkataa asiwamiliki Israeli? Ijaze pembe yako mafuta, uende, nami nitakupeleka kwa Yese, Mbethlehemi; maana nimejipatia mfalme katika wanawe. 2 Samweli akasema, Nawezaje kwenda? Sauli akipata habari, ataniua. Basi BWANA akasema, Chukua ndama pamoja nawe, ukaseme, Nimekuja ili kumtolea BWANA dhabihu. 3 Ukamwite Yese aje kwenye dhabihu, nami nitakuonyesha utakayotenda; nawe utamtia mafuta yule nitakayemtaja kwako”
1 Samweli 16:1 “BWANA akamwambia Samweli, Hata lini utamlilia Sauli, ikiwa mimi nimemkataa asiwamiliki Israeli? Ijaze pembe yako mafuta, uende, nami nitakupeleka kwa Yese, Mbethlehemi; maana nimejipatia mfalme katika wanawe.
2 Samweli akasema, Nawezaje kwenda? Sauli akipata habari, ataniua. Basi BWANA akasema, Chukua ndama pamoja nawe, ukaseme, Nimekuja ili kumtolea BWANA dhabihu.
3 Ukamwite Yese aje kwenye dhabihu, nami nitakuonyesha utakayotenda; nawe utamtia mafuta yule nitakayemtaja kwako”
Je umeiona nafasi ya sadaka katika kuyaokoa maisha ya Samweli na Daudi?.
Hapo MUNGU hakushindwa kumwambia nabii Samweli aende hivyo hivyo na kwamba atamlinda!…La! Hakufanya bali alimwambia aende na dhabihu..
Jambo hilo Bwana MUNGU wetu aliliruhusu pia ili tuelewe umuhimu wa dhabihu/sadaka.
Unapomtoleo MUNGU kwa ufunuo wa Neno, bila kushurutishwa na mtu wala uchungu, kuna mambo mengi katika ulimwengu wa roho yanafanyika, kama ni nira za mauti zinalegea na kama kuna vifungo vya dhambi pia vinaondoka.
Na kumbuka sadaka kwa BWANA inapelekwa kwa BWANA, maana yake mahali ambapo BWANA anatumikiwa (mfano kanisani au mahali panapofanyika kazi ya MUNGU ikiwemo mikutano ya injili)..hapo ndipo penye neema.
Usipeleke sadaka yako maalumu mahali pengine kama kwa marafiki, au watu au maskini wa barabarani…ni vizuri kufanya hivyo na kuna baraka zake lakini vya Bwana vinapaswa vipelekwe kwa Bwana ndivyo maandiko yanavyofundisha..
Tenga kiasi chako kingine peleka kwa maskini na wenye uhitaji, lakini hakikisha una sadaka yako maalumu kwa BWANA utakayopeleka aidha kanisani au mahali popote kazi ya MUNGU inapofanyika kwa usahihi.