DANIELI: Mlango wa 5

DANIELI: Mlango wa 5

DANIELI 5: KUANGUKA KWA BABELI:

Tukisoma katika Historia na kwenye biblia tunapata picha jinsi mji wa Babeli ulivyokuwa mkubwa, wenye maboma yenye nguvu, na ngome Imara iliyokuwa imezungukwa na kuta ndefu zenye njia katikati pande zote, mpaka kufikia wenyeji wa mji ule kusema kuwa ni “mji udumuo milele”,

Lakini tunaona wakati mmoja Mfalme wa Taifa hilo (BELSHAZA) alipokuwa amestarehe na kujifurahisha kwa anasa katika fahari yake tunaona uharibifu ulimkuta kwa ghafla, habari hii tunaisoma katika kitabu cha Danieli mlango wa 5, pale ambapo kiganja cha mkono kilipotokea na kusimama ukutani na kundika maneno yale magumu ambayo hakuna mchawi, wala mwenye hekima aliyeweza kuyasoma na kuyatafsiri maneno yale isipokuwa Danieli peke yake kwa uwezo wa ROHO MTAKATIFU.

Danieli 5:1-8″ Belshaza, mfalme, aliwafanyia wakuu wake elfu karamu kubwa akanywa divai mbele ya elfu hao.

2 Belshaza, alipokuwa akionja ile divai, akaamuru wavilete vile VYOMBO VYA DHAHABU NA FEDHA, ambavyo baba yake, Nebukadreza, ALIVITOA KATIKA HEKALU LILILOKUWAKO YERUSALEMU; ili kwamba mfalme, na wakuu wake, na wake zake, na masuria wake, wapate kuvinywea.

3 Basi wakavileta vile vyombo vya dhahabu, vilivyotolewa katika hekalu la nyumba ya Mungu lililokuwako Yerusalemu; na mfalme na wakuu wake, na wake zake, na masuria wake, wakavinywea.

4 Wakanywa divai, wakaisifu miungu ya dhahabu, na ya fedha, na ya shaba, na ya chuma, na ya mti, na ya mawe.

5 Saa iyo hiyo vikatokea vidole vya mkono wa mwanadamu, vikaandika katika chokaa ya ukuta wa nyumba ya enzi ya mfalme, mahali palipokikabili kinara; naye mfalme akakiona kitanga cha ule mkono ulioandika.

6 Ndipo uso wa mfalme ukambadilika; fikira zake zikamfadhaisha; viungo vya viuno vyake vikalegea; magoti yake yakagongana.

7 Mfalme akalia kwa sauti kubwa, akaamuru waletwe wachawi, na Wakaldayo na wanajimu. Mfalme akanena, akawaambia wenye hekima wa Babeli, mtu awaye yote atakayesoma maandiko haya, na kunionyesha tafsiri yake, atavikwa mavazi ya rangi ya zambarau, na kuwa na mkufu wa dhahabu shingoni mwake, naye atakuwa mtu wa tatu katika ufalme.

8 Basi wakaingia wenye hekima wote wa mfalme; lakini hawakuweza kuyasoma yale maandiko, wala kumjulisha mfalme tafsiri yake.”

Kama tunavyosoma hapo Mfalme Belshaza aliona haitoshi kujifurahisha katika anasa pamoja na masuria wake tu, lakini aliongezea kwenda kuchukua vyombo vya nyumba ya Mungu ambavyo baba yake (Nebukadreza) aliona vema kuvitunza visitumiwe kwa namna yoyote kwasababu viliwekwa wakfu kwa Bwana mpaka wana wa Israeli watarejea katika nchi yao, ni vyombo vilivyotumiwa na makuhani tu katika nyumba ya Mungu kwa ajili ya ibada. Lakini ijapokuwa Belshaza ALIYAFAHAMU HAYO YOTE, na kwamba vitu vilivyowekwa wakfu kwa ajili ya nyumba ya Mungu wa Israeli havipaswi kutumiwa kwa namna yoyote. Lakini kwa kiburi chake cha kufanya moyo wake kuwa mgumu kwa kutokujali na kumdharau Mungu, alikwenda kuvitumia kwa anasa zake, tukiendelea kusoma..

Danieli 5:9-31″

9 Ndipo mfalme Belshaza akahangaika sana, uso wake ukambadilika, na wakuu wake wakaona fadhaa.

10 Basi malkia, kwa sababu ya maneno ya mfalme na ya wakuu wake, akaingia katika nyumba ya karamu; malkia akanena, akasema, Ee mfalme, uishi milele; fikira zako zisikufadhaishe; wala uso wako usibadilike.

11 Yuko mtu katika ufalme wako, ambaye roho ya miungu watakatifu inakaa ndani yake; na katika siku za baba yako nuru na ufahamu na hekima zilionekana ndani yake; na mfalme Nebukadreza, baba yako, naam, mfalme, baba yako, akamfanya kuwa mkuu wa waganga, na wachawi, na Wakaldayo, na wanajimu;

12 kwa kuwa roho njema kupita kiasi, na maarifa, na ufahamu, na uwezo wa kufasiri ndoto, na kufunua maneno ya fumbo, na kufungua mafundo, zilionekana katika Danielii huyo, ambaye mfalme alimwita Belteshaza. Basi na aitwe Danielii, naye ataionyesha tafsiri.

13 Ndipo Danieli akaletwa mbele ya mfalme. Na Mfalme akanena, akamwambia Danielii, Je! Wewe ndiwe Danieli yule, aliye mmoja wa wana wa Yuda waliohamishwa, ambao mfalme, baba yangu, aliwaleta huku toka Yerusalemu?

14 Nimesikia habari zako, kwamba roho ya miungu imo ndani yako, na kwamba nuru na ufahamu na akili bora zimeonekana kwako.

15 Basi sasa, watu wenye hekima na wachawi wameletwa mbele yangu, wapate kulisoma andiko hili, na kunijulisha tafsiri yake; lakini hawakuweza kunijulisha tafsiri ya jambo hili.

16 Lakini nimesikia habari zako, kwamba waweza kuleta tafsiri, na kufumbua mafumbo; haya! Kama ukiweza kulisoma andiko hili, na kunijulisha tafsiri yake, utavikwa mavazi ya rangi ya zambarau, na kuwa na mkufu wa dhahabu shingoni mwako, nawe utakuwa mtu wa tatu katika ufalme.

17 Ndipo Danieli akajibu, akasema mbele ya mfalme; Zawadi zako zishike wewe mwenyewe; na thawabu zako mpe mtu mwingine; walakini nitamsomea mfalme maandiko haya, na kumjulisha tafsiri yake.

18 Kwa habari zako, Ee mfalme, Mungu Aliye juu alimpa Nebukadreza, baba yako, ufalme, na ukuu, na fahari, na utukufu;

19 na kwa sababu ya ule ukuu aliompa, watu wa kabila zote, na mataifa, na lugha, wakatetemeka na kuogopa mbele yake; aliyetaka kumwua alimwua; na aliyetaka kumwacha hai, alimwacha hai; aliyetaka kumtukuza, alimtukuza; na aliyetaka kumshusha, alimshusha.

20 Lakini moyo wake ulipoinuliwa, na roho yake ilipokuwa ngumu akatenda kwa kiburi, aliuzuliwa katika kiti chake cha enzi, nao wakamwondolea utukufu wake.

21 Akafukuzwa mbali na wanadamu, moyo wake ukafanywa kuwa kama moyo wa mnyama, na makao yake yalikuwa pamoja na punda-mwitu; akalishwa majani kama ng’ombe, mwili wake ukalowa maji kwa umande wa mbinguni; hata alipojua ya kuwa Mungu Aliye juu ndiye anayetawala katika ufalme wa wanadamu, na ya kuwa humweka juu yake yeye amtakaye, awaye yote.

22 Na wewe, mwanawe, Ee Belshaza, hukujinyenyekeza moyo wako, ijapokuwa ulijua hayo yote.

23 Bali umejiinua juu ya Bwana wa mbingu; nao wamevileta vyombo vya nyumba yake mbele yako; na wewe, na wakuu wako, na wake zako, na masuria wako, mmevinywea; nawe umeisifu miungu ya fedha na ya dhahabu na ya shaba, na ya chuma, na ya mti, na ya mawe; wasioona, wala kusikia, wala kujua neno lo lote; na Mungu yule, ambaye pumzi yako i mkononi mwake, na njia zako zote ni zake, hukumtukuza.

24 Ndipo kile kitanga cha ule mkono kikaletwa kutoka mbele zake, na maandiko haya yameandikwa.

25 Na maandiko yaliyoandikwa ni haya; MENE MENE TEKELI, NA PERESI.

26 Na tafsiri ya maneno haya ni hii; MENE, Mungu ameuhesabu ufalme wako na kuukomesha.

27 TEKELI, umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka.

28 PERESI, ufalme wako umegawanyika, nao wamepewa Wamedi na Waajemi.

29 Ndipo Belshaza akatoa amri, nao wakamvika Danieli mavazi ya rangi ya zambarau, wakatia mkufu wa dhahabu shingoni mwake, wakapiga mbiu kutangaza habari zake, ya kwamba yeye ni mtu wa tatu katika ufalme.

30 Usiku uo huo Belshaza, mfalme wa Wakaldayo, AKAUAWA.

31 Na Dario, Mmedi, akaupokea ufalme, naye umri wake alikuwa na miaka sitini na miwili.

Amen.

DANIELI: Mlango wa 5, mene, tekeli, peresi

Habari hiyo imejifafanua yenyewe, huo ndio ulikuwa mwisho wa Babeli, historia inasema usiku ule ule Danieli alipokuwa anawapa tafsiri ya maneno yale, kumbe jeshi la waamedi na waajemi lilikuwa limeshauzingira mji kwa mbali, hao hawakujua lolote kwasababu walishajitumainisha katika ulinzi wa kuta zao ndefu zinazouzunguka mji huku geti kubwa la kuingilia njia za miji ukiwa umefungwa,

Hivyo walijua hakuna namna yoyote taifa lolote lingeweza kuwavamia kwa njia yoyote ile, lakini hawakufahamu jambo moja, kwamba kwa Mungu hakuna lolote linaloshindikana, akisema mji huu utaanguka, ni kweli utaanguka! Hivyo Danieli alipomwambia maneno yale: “ufalme wako umeanguka na wamepewa waamedi na wajemi”, Mfalme alichukulia kama ni jambo ambalo ni gumu kutokea kwa wakati ule hivyo pengine ifikiria kichwani kwake kwamba kuta zake ndefu na majeshi yake imara yanayokesha usiku kucha kuulinda mji hayawezi kuvamiwa, na hakuna taifa lolote duniani lingeweza kupigana nalo , hivyo akastarehe tena na kutaka kumtukuza Danieli pasipo kujali maneno yale kwa kuanguka na kutubu saa ile ile.

Pia tazama..

1 Tofauti kati ya mbinguni, peponi, Kuzimu, Jehanamu, na Paradiso ni ipi?
2 Jehanamu ni nini?
3 Kisiwa cha Patmo kipo nchi gani?.
4 Kabila la Benyamini.
5 Watu wenye ulemavu wa akili, wataenda mbinguni?
6 Moabu ni nchi gani kwasasa?
7 VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1
8 Ashuru ni nchi gani kwa sasa?
9 Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma.
10 Umedi na uajemi, zilitawalaje?

Lakini hakujua maabaya yatakayomkuta muda mfupi baadaye, kulikuwa na mto mkubwa uliokuwa unaingiza maji katika mji ule, na tunafahamu siku zote hauwezi kuziba njia ya maji kupita, lazima kuachwe tundu kuruhusu maji kupita yaingie mjini, na ndivyo ilivyokuwa Babeli.

Palikuwa na mto mkubwa (FRATI) uliokatiza mji ule hivyo maadui zao walipokuja (Waamedi na waajemi) hawakupita kwa njia ya mageti au kubomoa kuta za miji, kwasababu kule zilikuwa zinalindwa na maaskari wengi waliomakini, Hivyo njia waliyoitumia waamedi na wajemi ni kwenda kukausha maji ya ule mto kwa kuyaundia mchipuko mwingine, hivyo yakaanza kupungua kidogo kidogo pasipo wao kujua, na mwisho kufikia kiwango cha watu kuweza kupita kwa miguu, jeshi kubwa la waamedi na wajemi liliweza kuingia kiurahisi kuuteka mji, na usiku ule ule Mfalme Belshaza aliuliwa bila kujua watu wameingilia wapi? na ufalme wake ukachukuliwa. Na Babeli kuishia hapo.

Wengi wanasema unabii wa Mungu huwa unachelewa kutimia, lakini si kweli ukichelewa ni kukufanya wewe utubu, kumbuka hapa tunaona mara tu baada ya Danieli kumtabiria Belshaza kuanguka kwake pengine alidhani ingekuwa kama ya Baba yake, kwamba yatatimia baada ya miezi au miaka kadhaa, lakini haikuwa hivyo kwake yeye ilitimia usiku ule ule.

Vivyo hivyo na BABELI ya rohoni (Utawala wa dini ya RUMI -UKATOLIKI ) iliyopo sasa, ambayo inapeleka mamilioni ya watu kuzimu, kama biblia inavyomwita katika

Ufunuo 17,“BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI”. NAYO PIA uharibifu wake utakuja ndani ya siku moja Biblia inasema 

Ufunuo 18:6-8″ Mlipeni kama yeye alivyolipa, mkamlipe mara mbili kwa kadiri ya matendo yake. Katika kikombe kile alichokichanganyisha, mchanganyishieni maradufu.

7 Kwa kadiri alivyojitukuza na kufanya anasa, mpeni maumivu na huzuni kadiri iyo hiyo. Kwa kuwa husema moyoni mwake, Nimeketi malkia, wala si mjane, wala sitaona huzuni kamwe.

8 KWASABABU HIYO MAPIGO YAKE YATAKUJA KATIKA SIKU MOJA, mauti, na huzuni, na njaa, naye atateketezwa kabisa kwa moto. Kwa maana Bwana Mungu aliyemhukumu ni mwenye nguvu. ” AMEN.

Kumbuka pia jambo lingine lilolosababisha Mungu kuihukumu Babeli ni pale VYOMBO VYA NYUMBA YA MUNGU vilipochanganywa na SANAMU na kusababisha CHUKIZO kubwa lililoleta UHARIBIFU, Vivyo hivyo pia katika Babeli ya rohoni itakuja pale yule mtawala wake yaani mpinga-kristo (PAPA wa wakati huo) atakapojiinua na kuingia katika hekalu la Mungu kule YERUSALEMU na kutaka kuabudiwa kama Mungu, litakuwa ni chukizo kubwa kwa Mungu ambalo litapelekea uharibifu wake moja kwa moja hilo ndilo CHUKIZO LA UHARIBIFU.

Habari zake zinazungumziwa hapa na mtume Paulo;

2 Wathesalonike 2:1-4″ Basi, ndugu, tunakusihini, kwa habari ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na kukusanyika kwetu mbele zake,

2 kwamba msifadhaishwe upesi hata kuiacha nia yenu, wala msisitushwe, kwa roho, wala kwa neno, wala kwa waraka unaodhaniwa kuwa ni wetu, kana kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwapo.

3 Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa YULE MTU WA KUASI, mwana wa uharibifu;

4 yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe KUKETI KATIKA HEKALU LA MUNGU, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.”

Vivyo hivyo kuutumia MWILI wako kwa uasherati, au fashion (vimini, suruali, hereni, wigy,) au ulevi, au wizi, au anasa, au rushwa,ulanguzi, NI SAWA NA KUVICHUKUA VYOMBO VYA NYUMBA YA MUNGU NA KWENDA KUVITUMIA KWA ANASA, haya yote ni machukizo yatakayokuletea uharibifu wa ghafla, Kwasababu Bwana alisema katika 1Wakoritho 6 kuwa “mwili ni kwa BWANA na BWANA ni kwa mwili na atakayeliharibu hekalu la hilo, Mungu atamuharibu mtu huyo.”

Au unapotumia Karama za Mungu kwa ajili ya faida zako mwenyewe, kwamfano unajiita mchungaji/nabii/mwinjilisti na bado ni unazini na washirika wako, au unatumia karama/vipawa hivyo kuwachukulia watu fedha,au kuwalaghai, huko ni SAWA NA KUVICHUKUA NA KUVITUMIA VYOMBO VYA NYUMBA YA MUNGU KWA ANASA, kama alivyofanya Belshaza hayo yote ni machukizo makubwa ambayo yatakupelekea kuanguka kwako haraka sana.

Hivyo ujumbe tulionao kwa kizaazi hiki cha mwisho ni huu:

2 Wakorintho 6:14 -18″ Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?

15 Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini?

16 TENA PANA MAPATANO GANI KATI YA HEKALU LA MUNGU NA SANAMU? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.

17 Kwa hiyo, TOKENI KATI YAO, MKATENGWE NAO, ASEMA BWANA, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha.

18 Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike,

Ukisoma tena Ufunuo 18:4 inasema;

4 Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, TOKENI KWAKE, ENYI WATU WANGU, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.

5 Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake. “

Hivyo Jitenge na DINI za uongo, na pia jitenge na mienendo ya watu watendao dhambi.

Ubarikiwe na Bwana.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Kwa mwendelezo >>> Mlango wa 6


Mada Nyinginezo:

MNARA WA BABELI.

JINSI MWISHO ULIVYOKARIBIA.

KITABU CHA YASHARI KINACHOZUNGUMZIWA KATIKA 2SAMWELI 1:17-18, NI KITABU GANI?

KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 1

NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE.


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments