SWALI: Ndugu zangu Huyu Mariamu MAGDALENE ni nani?”..Je! Magdene ni jina la baba yake au ni Jina la ukoo wake?.
JIBU:
Mariamu Magdalene( wengine wanamwita Magdalena) ni yule mwanamke ambaye tunamwona kwenye biblia akitolewa pepo saba na Bwana Yesu..
Luka 8:2 “na wanawake kadha wa kadha ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalene aliyetokwa na pepo saba, 3 na Yoana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana, na wengine wengi, waliokuwa wakimhudumia kwa mali zao. “
Luka 8:2 “na wanawake kadha wa kadha ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalene aliyetokwa na pepo saba,
3 na Yoana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana, na wengine wengi, waliokuwa wakimhudumia kwa mali zao. “
Ni mwanamke aliyefuata na Bwana Yesu tangu huo wakati hadi mwisho wa huduma yake ambaye yeye pamoja na wenzake, ndio waliokuwa wanamuhudumia Bwana kwa mali zao.
Mariam Magdalene tunamwona tena siku za mwisho mwisho kabisa kabla za Bwana Yesu kupaa yeye ndiye aliyeagizwa kwenda kuwaeleza wanafunzi wake juu ya kufufuka kwake.
Yohana 20:11 “Lakini Mariamu alikuwa akisimama karibu na kaburi, nje yake, analia. Basi akilia hivi, aliinama na kuchungulia ndani ya kaburi. 2 12 Akaona malaika wawili, wenye mavazi meupe, wameketi, mmoja kichwani na mmoja miguuni, hapo ulipolazwa mwili wake Yesu. 13 Nao wakamwambia, Mama, unalilia nini? Akawaambia, Kwa sababu wamemwondoa Bwana wangu, wala mimi sijui walikomweka. 14 Naye akiisha kusema hayo, akageuka nyuma, akamwona Yesu amesimama, asijue ya kuwa ni Yesu. 15 Yesu akamwambia, Mama, unalilia nini? Unamtafuta nani? Naye, huku akidhania ya kuwa ni mtunza bustani, akamwambia, Bwana, ikiwa umemchukua wewe, uniambie ulipomweka, nami nitamwondoa. 16 Yesu akamwambia, Mariamu. Yeye akageuka, akamwambia kwa Kiebrania, Raboni! (Yaani, Mwalimu wangu). 17 Yesu akamwambia. Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu. 18 Mariamu Magdalene akaenda, akawapasha wanafunzi habari ya kwamba, Nimemwona Bwana, na ya kwamba amemwambia hayo”.
Yohana 20:11 “Lakini Mariamu alikuwa akisimama karibu na kaburi, nje yake, analia. Basi akilia hivi, aliinama na kuchungulia ndani ya kaburi. 2
12 Akaona malaika wawili, wenye mavazi meupe, wameketi, mmoja kichwani na mmoja miguuni, hapo ulipolazwa mwili wake Yesu.
13 Nao wakamwambia, Mama, unalilia nini? Akawaambia, Kwa sababu wamemwondoa Bwana wangu, wala mimi sijui walikomweka.
14 Naye akiisha kusema hayo, akageuka nyuma, akamwona Yesu amesimama, asijue ya kuwa ni Yesu.
15 Yesu akamwambia, Mama, unalilia nini? Unamtafuta nani? Naye, huku akidhania ya kuwa ni mtunza bustani, akamwambia, Bwana, ikiwa umemchukua wewe, uniambie ulipomweka, nami nitamwondoa.
16 Yesu akamwambia, Mariamu. Yeye akageuka, akamwambia kwa Kiebrania, Raboni! (Yaani, Mwalimu wangu).
17 Yesu akamwambia. Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu.
18 Mariamu Magdalene akaenda, akawapasha wanafunzi habari ya kwamba, Nimemwona Bwana, na ya kwamba amemwambia hayo”.
Na kuhusu Hilo jina la Magdalene sio jina la baba yake, au la ukoo wake, Hapana aliitwa Mariamu Magdalene kuonyesha asili yake tu, ili kumtofautisha na Mariamu wengine kwenye biblia…Kumbuka hili jina Mariamu limetumika mara nyingi kwenye biblia..Hivyo ili kuwatofautisha hawa Mariam wote, huyu aliitwa mariamu Magdalene kuonyesha na Mariam aliyetokea huko mji wa MAGDALENE uliokuwa kando kando magharibi mwa bahari ya Galilaya huko Israeli. Lakini hilo sio jina la Baba yake au ukoo wake..Hapana ni jina la mji aliotokea.
Ni kama tu yule mwanamke Msamaria, hilo jina Msamaria sio jina la baba yake, hapana bali ni jina la mji anaotokea unaoitwa SAMARIA uliopo katikati ya Israeli.
Bwana akubariki.
Pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
RABONI!
JE BIKIRA MARIAMU ALIZAA WATOTO WENGINE?
Ni sahihi kumuita Mariamu mama wa Mungu?
Kwanini wanawake wengi huwa wanalipuka mapepo?
JINA LA MUNGU NI LIPI?
Je! ni vema kwa mkristo kwenda hospitali au kutumia miti shamba anapougua?
Tofauti ya kazi ya Damu ya Yesu na Jina la Yesu ni ipi?
Rudi Nyumbani:
Print this post