Yapo makundi tofauti tofauti ya Malaika wa Mbinguni. Wapo Maserafi ambao ndio tutakaowazungumzia leo, wapo Makerubi (ambao ndani yake ndio alikuwa shetani), wapo wenye uhai wanne, wapo wazee ishirini na nne.. na wapo Malaika wa vita ambao ndani yake ndio wakina Mikaeli na wenzake.
Na katikati ya hayo makundi, yamegawanyika vipengele vingi!..wapo malaika wenye mbawa na wasio na mbawa, wapo wenye maumbo kama ya wanadamu lakini pia wapo wenye maumbo kama ya wanyama na ndege.
Kwa ufafanuzi kuhusu makundi hayo ya Malaika, mwisho kabisa wa somo hili utaona LINK za masomo hayo, zifungue ili uweze kuzisoma.
Sasa Maserafi ni kundi la Malaika ambao kazi yao ni kumsifu na kumtukuza Mungu mbinguni, Wamekizunguka kiti cha enzi kwa maelfu yao, wakimsifu Mungu usiku na mchana. Maserafi wana mabawa sita kila mmoja. Mawili yanakifunika kichwa kufunua kuwa KUFUNUA MAMLAKA YA MUNGU, NA UTAWALA WA KIMUNGU. Kwamba Mungu ndiye kichwa cha mambo yote. Na pia wanafunika kichwa kwasababu wanaona hata hawastahili kumtazama Mungu, wala Mungu kuwatazama wao kwajinsi yeye Mungu alivyo mtakatifu sana.
Na pia hawaishii tu! Kufunika kichwa..bali wanafunika pia Miguu, kufunua jambo kufunua kuwa hawastahili hata Mungu aliye mtakatifu kuona miguu yao.
Na mabawa mawili yaliyosalia ni kwaajili ya kuruka (yaani kupaa).
Kundi hili la malaika tunaona limetajwa katika Kitabu cha Isaya.
Isaya 1: 1 “Katika mwaka ule aliokufa mfalme Uzia nalimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu sana na kuinuliwa sana, na pindo za vazi lake zikalijaza hekalu.
2 Juu yake walisimama maserafi; kila mmoja alikuwa na mabawa sita; kwa mawili alifunika uso wake, na kwa mawili alifunika miguu yake, na kwa mawili aliruka.
3 Wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana wa majeshi, dunia yote imejaa utukufu wake”.
Bwana aliwaumba malaika hawa kwa lengo hilo la kumsifu yeye na kuufunua utakatifu wake kwa viumbe vyake vyote…ndio maana katika sifa zao wanaanza na neno.. “Mtakatifu mtakatifu”.
Na malaika hawa (maserafi) wanatufundisha na sisi jinsi ya kumsifu Mungu..Kwamba tuwapo mbele zake tujisitiri!..
Hebu tujifunze kitu hapa!..sio malaika wote wanaofunika vichwa mbele za Mungu…lakini kundi hili linafanya hivyo? kwanini?…Huoni pia katika kanisa kuna kundi la watu ambao ni lazima lifunike vichwa liwapo ibadani?..na sio tu kufunika kichwa bali hata kujisitiri mwili mzima ikiwemo na miguu.
1Wakorintho 11:5 “Bali kila mwanamke asalipo, au anapohutubu, bila kufunika kichwa, yuaaibisha kichwa chake; kwa maana ni sawasawa na yule aliyenyolewa”
Na ukiendelea kusoma mistari hiyo utaona suala la wanawake kufunika vichwa ibadani limehusishwa na “Malaika”..kasome 1Wakorintho 11:10.
Kwahiyo pia si vyema mwanamke kuingia kanisani bila kufunika kichwa wala kujisitiri mwili..Utakuta mwanamke anaingia ibadani kichwani kaweka wigi, chini kavaa kimini au suruali. Jiulize hapo unakwenda kumwabudu Mungu gani?..Maserafi wasio na dhambi wanajisitiri wewe uliye na dhambi inakupasaje?
Mwisho, Kumbuka Malaika yoyote yule sio wa kuabudiwa!..wala hatupaswi kuweka picha au sanamu ya malaika yoyote yule na kuisujudia, ni Mungu pekee ndiye anayestahili kuabudiwa na kusujudiwa.
Bwana atubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Je! mbinguni kuna malaika wa kike?. Na je! tukifika mbinguni tutafanana wote?
Naomba kutumiwa kwa email mboziwoca@gmail.com
About the author