BWANA WA MAJESHI.

BWANA WA MAJESHI.

Kwanini Mungu aitwe Bwana wa majeshi? Je! Ni kweli anayo majeshi au ni cheo tu amependa kujivika?

Watu wengi hatufahamu kuwa Mungu anayo majeshi yake…Ni kweli hili jina limekaa sana ulimini mwetu, lakini bado hatufahamu vizuri ni kiwango gani Mungu anajiita Bwana wa majeshi..Naamini siku tukilifahamu hilo vema basi tutaishi maisha yasiyo na woga na wasiwasi hata kidogo hapa ulimwenguni.

Kumbuka hajiiti Mungu wa “Jeshi” kana kwamba ni moja hapana bali anajiita Mungu wa “Majeshi” ikiwa na maana ni mengi.

Ni majeshi ambayo yaanzia mbinguni mpaka duniani. Na kama tunavyojua sikuzote majeshi kazi yake, kulinda usalama, kutunza amani, na kuupigania ufalme, kinyume na maadui zao.

Mungu alijitambulisha kama Bwana wa Majeshi, sio kwamba alitaka  sisi tumwogope, Hapana, bali alitaka sisi tujue nguvu aliyonayo katika kutupigania watu wake dhiki maadui zao (Shetani na mapepo yake). Embu Jaribu kutengeneza picha Mungu angejiita tu  majina haya, ingekuwaje?

  • Bwana wa Amani(Jehova-Shalom), au
  • Bwana mpaji wetu, (Yehova-yire), Au
  • Bwana atuponyaje(Yehova-Rafa), Au
  • Bwana atuonaye (Yehova-Shama) N.K.

Unadhani hiyo ingetosha tu?..Kwamfano tungekuwa tunapitia katika vita vikali tumezungukwa na maadui wa mwilini na rohoni, kilichobaki ni kufa na kupona, unadhani Bwana mpaji wetu(Yehova yire), tungemuhitaji wakati huo? Wakati unaona unakaribia kuchinjwa Je, utamwambia Mungu nipatie mali?..Jibu la, kinyume chake atamuita Bwana kwa nguvu  zote asimame mwenyewe akupiganie na kuwasambaratisha  maadui zako ili upone.

Hapo ndipo jina la BWANA WA MAJESHI linapoitwa (Yehova-Saboati)

Ilifika wakati Daudi alikuwa anakwenda kupigana na adui yake mkubwa Goliathi, moyoni alijua kabisa mtu kama huyu wa vita, haiwezekani kumshinda, Lakini alipogundua kuwa yupo Bwana wa Majeshi Mungu wa vita,karibu naye ndipo aliposimama kwa ujasiri na kwenda kupigana naye..tusome..

1Samweli 17:43 “Mfilisti akamwambia Daudi, Je! Mimi ni mbwa hata umenijia kwa fimbo? Mfilisti akamlaani Daudi kwa miungu yake.

44 Mfilisti akamwambia Daudi, Njoo huku kwangu; nyama yako nitawapa ndege wa angani na wanyama wa mwituni.

45 Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe KWA JINA LA BWANA WA MAJESHI, MUNGU WA MAJESHI ya Israeli uliowatukana.

46 Siku hii ya leo Bwana atakuua mkononi mwangu, nami nitakupiga, na kukuondolea kichwa chako, nami leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi mizoga ya majeshi ya Wafilisti, ili kwamba dunia nzima wajue ya kuwa yuko Mungu katika Israeli.

47 Nao jamii ya watu wote pia wajue ya kwamba Bwana haokoi kwa upanga wala kwa mkuki; maana vita ni vya Bwana, naye atawatia ninyi mikononi mwetu”.

Unaona hapo Daudi alimuita Bwana wa Majeshi, aje kumsaidia..

Ndugu fahamu kuwa, Unapokuwa mkristo, hupaswi kuwa woga wa kitu chochote, Inasikitisha kuona ni mkristo wa muda mrefu halafu bado anaogopa wachawi na washirikina, pamoja na mapepo na majini.

Shetani mwenyewe anawashaangaa, anapoona watu wa Bwana wa majeshi kama sisi, nasi tunamwogopa yeye..

Kuna wakati Elisha alikuwa anatembea na mtumishi wake Gehazi, wakafika mahali wakajikuta wamezungukwa na majeshi mengi ya maadui zao, yule mtumishi akawa anatetemeka na kuogopa sana..Lakini Elisha hakuogopa kwasababu alijua majeshi ya Mungu wa Israeli aliyo nayo ni mengi kuliko ya wale wengine..Bwana wa majeshi ndio nguvu yake.. Ndipo Elisha akamwomba Mungu amfungue macho alione hilo.

2Wafalme 6:17 “Elisha akaomba, akasema, Ee Bwana, nakusihi, mfumbue macho yake, apate kuona. Bwana akamfumbua macho yule mtumishi; naye akaona; na tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote.

18 Na walipomtelemkia Elisha akamwomba Bwana, akasema, Uwapige, nakusihi, watu hawa kwa upofu. Akawapiga kwa upofu sawasawa na neno la Elisha.

19 Elisha akawaambia, Njia hii siyo, na mji huu sio, nifuateni mimi, nami nitawapeleka kwa mtu yule mnayemtafuta. Akawapeleka Samaria”.

Hivyo hata wewe ukiwa unapitia mahali ambapo, unaona vita vikali vipo mbele ya basi mwite Bwana wa Majeshi atakusaidia,..

Lakini ikiwa wewe bado upo nje ya wokovu, nataka nikuambie hata umwite vipi Mungu katika vita vyako hawezi kukusikia wala kukusaidia, kwasababu wewe sio wa ufalme wake. Wachawi watakutesa, mapepo yatakutesa, ibilisi atakutesa,.. Lakini ukitaka leo awe upande wako, basi ni sharti kwanza umpokee YESU KRISTO katika moyo wako. Akusemehe dhambi zako, ndipo pale utakapoliita jina la Bwana wa majeshi atakusikia na kukusaidia.

Ikiwa upo tayari Kumpa YESU leo  maisha yako basi bofya hapa, kwa Sala ya toba >>> SALA YA TOBA.

Pia yapo mafundisho mengi unahitaji kujua juu ya majeshi ya mbinguni(malaika) wanavyofanya kazi na sisi(tuliookoka), hivyo nakusihi fungua na masomo mengine hapa chini, ufahamu zaidi juu ya ulimwengu wa roho wa malaika wa Bwana na utendaji kazi wao.

Zaburi 24: 10 Ni nani huyu Mfalme wa utukufu? Bwana wa majeshi, Yeye ndiye Mfalme wa utukufu.

Mungu akubariki.

Mada Nyinginezo:

HUDUMU YA MALAIKA WATAKATIFU.

 KUWAHUDUMIA MALAIKA PASIPO KUJUA.

ZIFAHAMU HUDUMA KUU (10) ZA SHETANI DUNIANI.

WAKAMCHA BWANA, NA KUITUMIKIA MIUNGU YAO WENYEWE.

JISHUSHE ILI MUNGU AKUHUDUMIE.

MADHARA YA KUKOSA MAJI YA UZIMA BAADA YA KIFO.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments