SALA FUPI YA UPONYAJI!
Zaburi 107:17 “Wapumbavu, kwa sababu ya ukosaji wao, Na kwa sababu ya maovu yao, hujitesa.
18 Nafsi zao zachukia kila namna ya chakula, Wameyakaribia malango ya mauti.
19 Wakamlilia Bwana katika dhiki zao, Akawaponya na shida zao.
20 Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao”.
(Uimbe wimbo huu uliotungwa na Don Moen, kufuatia Zaburi hiyo)
Mimi ni Mungu nikuponyaye,
Mimi ni Bwana mponyaji wako,
Hulituma Neno langu,
Na kukuponya magonjwa yako,
Mimi ni Bwana mponyaji wako.
Wewe ni Mungu,
Uniponyaye,
Wewe ni Bwana Mponyaji wangu,
Hulituma Neno lako,
Na kuniponya magonjwa yangu,
Wewe ni Bwana mponyaji wangu.
Urudie kwa kadri uwezavyo pale Upitiapo misiba, magonjwa na shida..mwambie “Mungu” wewe ni Bwana uniponyaye,.. wewe ni Bwana uniponyaye..wewe ni Bwana mponyaji. Na nguvu uponyaji utashuka juu yako, na kukuponya na magonjwa uliyonayo au misiba unayopitia.
“Amen”
Mada Nyinginezo:
About the author