MKUU WA UZIMA AKUWEKE HURU.

MKUU WA UZIMA AKUWEKE HURU.

Bwana Yesu ndiye Mkuu wa Uzima (Matendo 3:15) Kwasababu alitabiriwa kuwa atakuwa Mkuu Zaidi ya wote..(Luka 1:15)..Na kwasababu hiyo basi Mungu alimpaka Mafuta ya Ukuu kuliko wote (Waebrania 1:9)..na uweza wa ajabu aliuweka juu yake….”Uweza wa kuwaweka huru waliofungwa na uteka wa shetani.(Luka 4:18).. Na kwa jina lake ametupa sisi wote tulio mwamini, mamlaka ya kuzitenda kazi zake zote…na utukufu ule aliokuwa nao ametupa sisi (Yohana 17:22)..Hivyo tuna nguvu kama za Simba zisizokuwa na mwisho, za kufanya makubwa kama aliyoyafanya Mkuu wa Uzima Yesu.

Kwasababu alisema..

Marko 16:17 “Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;

18 watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya”.

Kwasababu hiyo basi mimi kama mmoja wa waliomwamini yeye, na kupewa mamlaka hayo…

  •  Nakuombea Bwana akupe afya katika jina la Yesu Kristo,
  •  Nakuombea Bwana akulinde na yule mwovu, katika kila kitu unachokifanya kinachompendeza yeye.
  • Nakuombea Bwana akufanikishe katika yote katika Jina la Yesu Kristo. 
  • Kama wewe ni mgonjwa, na una ugonjwa ulioshindikana, kuanzia leo ukuondoke na usikurudie tena, katika Jina la Yesu.
  • Kama umefungwa na nguvu za giza, na Kamba za mauti, na roho za mapepo, kuanzia sasa Bwana akufungue katika jina la Yesu.
  • Bwana akupe kibali kila uendako, na kila ufanyacho chenye manufaa kwako na kwa wengine kikafanikiwe wiki hii na mwezi huu unaoanza.
  • Bwana akakupatanishe na maadui zako, na kukupa furaha na amani na watu wote katika Jina la Yesu.
  • Bwana akakuondolee Mashaka yote na hofu na wasiwasi na huzuni..akakupe furaha, utulivu, raha, na akujaze Roho wake Mtakatifu katika Jina la Yesu.
  • Bwana akupe kibali katika yote uliyomwomba na ufanikiwe katika jina la Yesu.
  • Nakuombea neema ya Mungu ya kumjua yeye Zaidi, na kumfahamu na kumfuata yeye ishuke juu yako kwa wingi katika kipindi hichi katika Jina la Yesu.
  • Kila mpango wa Ibilisi uliopangwa dhidi yako, katika mwili wako na dhidi ya wale uwapendao..uondoke saa hii katika Jina la Yesu, na wala usiusikie hata dalili jaribio lolote la kishetani juu ya Maisha yako.

Amini kuwa Ameyafanya hayo yote…Na yatakuwa kama ulivyoamini.

ZABURI 18: 1 “WEWE, BWANA, NGUVU ZANGU, NAKUPENDA SANA; BWANA NI JABALI LANGU, NA BOMA LANGU, NA MWOKOZI WANGU, MUNGU WANGU, MWAMBA WANGU NINAYEMKIMBILIA, NGAO YANGU, NA PEMBE YA WOKOVU WANGU, NA NGOME YANGU”

Maran atha!

Mada Nyinginezo:

MAOMBI YA VITA

YESU MPONYAJI.

KISIMA CHA MAJI YA UZIMA NI KILE KILE CHA ZAMANI.

USITOKE NJE YA HIFADHI YA MUNGU.

WAZAZI WA YOHANA NA YAKOBO.

Je! Bwana Yesu alibatiza akiwa hapa duniani?

VITA VYA IMANI NI VITA ENDELEVU.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments