Category Archive maswali na majibu

Debwani, Shali na Vifuko ni vitu gani? (Isaya 3:22)

Jibu: Labda tuanzie mstari ule wa 18, ili tupate kuelewa vizuri.

Isaya 3:18 “Siku hiyo Bwana atawaondolea uzuri wa njuga zao, na kaya zao;

19 na pete za masikio, na vikuku, na taji zao;

20 na dusumali, na mafurungu, na vitambi, na vibweta vya marashi, na matalasimu;

21 na pete, na azama,

22 na mavazi ya sikukuu, na DEBWANI; NA SHALI, NA VIFUKO”

Hayo ni aina ya mavazi waliovaa watu wa zamani, na baadhi ya hayo hata sasa yanavaliwa.. Sasa hapo yametajwa mengi, ikiwemo Dusumali, kwa urefu kuhusu Dusumali basi fungua hapa>>Dusumali ni nini katika biblia?

Lakini tutatazama hayo matatu yaliyotajwa katika huo mstari wa 22 ambayo ni “DEBWANI, SHALI, na VIFUKO”.

   1. DEBWANI.

Debwani ni vazi refu linaloanzia mabegani mpaka miguuni, vazi hili linavaliwa na wanawake, (Tazama picha chini juu).

   2. SHALI.

Shali ni vazi linalofanana na Debwani isipokuwa lenyewe linafunika kuanzia kichwa mpaka miguu, na hili linaweza kuvaliwa na jinsia zote, kwani kazi yake kubwa ni kujikinga na hali ya hewa, (baridi au mvua au upepo mkali), Shali ni Kiswahili cha “Overcoat” (Tazama picha chini).

shali

  3. VIFUKO

Vifuko si vazi bali ni mikoba inayobebwa na wanawake katika safari fupi. (Tazama picha chini)

vifuko ni nini

Je umempokea Bwana YESU?

Kama bado ni nini kinachokusubirisha? Fahamu kuwa hizi ni siku za mwisho na Bwana amekaribia sana kurudi, je ni nini kipo katika akili yako wewe kama Baba, au mama au kijana?. Je unawaza nini?.. kujenga maisha ya kimwili, kula, kunywa na kuvaa??..au unawaza nini Zaidi.

Kama unawaza kupendeza na kujifanya mzuri kwa mavazi na mitindo ya kidunia, Neno la Mungu linasema siku inakuja ambayo Mungu atawaondolea watu wote uzuri wa njuga zao  watu wote waliomwacha yeye..

Isaya 3:18 “Siku hiyo Bwana atawaondolea uzuri wa njuga zao, na kaya zao;

19 na pete za masikio, na vikuku, na taji zao;”

Achana na mapambo na fasheni za kidunia, mpokee YESU leo ukaoshwe dhambi zako.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

TWEKA MPAKA VILINDINI.

MANENO YA MUNGU YANAPINDULIWAJE?

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 12 (Kitabu cha Isaya)

Ni kwa jinsi gani Mungu anapatiliza maovu ya baba zetu sawasawa na Kutoka 20:5-6?

Rudi Nyumbani

Print this post

Biblia inasema nini kuhusu sayari, je ni kweli zipo tisa?

SWALI:  Shuleni tumefundishwa sayari zipi Tisa Lakini je maandiko yanasemaje kuhusu hili, je zipo kweli kwa idadi hiyo?


JIBU: Biblia si kitabu cha kisayansi, au cha taaluma yoyote, kwasababu lengo lake sio uvumbuzi na utafiti wa mambo ya ulimwenguni. Bali ni kumrejesha mwanadamu kwa muumba wake. Ni kitabu chenye msingi wa IMANI. Mambo yasiyothibitika kwa macho bali rohoni. Ni kitabu kielezacho njia ya ukombozi wa mwanadamu inayopatikana kupitia YESU KRISTO  mwokozi wa ulimwengu.

Ijapokuwa vipo vifungu vichache vichache vinavyoelezea uhalisia wa elimu za duniani, lakini isidhaniwe kuwa lengo lake kuu ni kutoa taarifa za kila kitu kwenye hii dunia, bali mara nyingi huwa ni kuelezea vema habari husika ya rohoni iliyokuwa inazungumziwa hapo.

Tukirudi kwenye swali linalouliza kuhusu sayari, kwamba sayansi inatuambia zipo tisa, je biblia nayo inazitaja ngapi?

Kama tulivyotangulia kusema biblia haielezi kila kitu kuhusu dunia hii, bali inaeleza kila kitu kuhusu wajibu wa mwanadamu kwa muumba wake.

kuhusu Sayari biblia inazitaja  bila shaka kwamba yeye ndio aliziumba, na magimba yote angali, ambayo yamejumuishwa katika neno jeshi la mbinguni .

Katika biblia sayari zimejatwa kwenye vifungu  hivi;

Ayubu 38:32

[32]Je! Waweza kuziongoza Sayari kwa wakati wake? Au waweza kuongoza Dubu na watoto wake?

2 Wafalme 23:5

[5]Akawaondosha wale makuhuni walioabudu sanamu, ambao wafalme wa Yuda waliwaweka ili kufukiza uvumba katika mahali pa juu, ndani ya miji ya Yuda, na katika kila mahali, pande zote za Yerusalemu; na hao pia waliomfukizia uvumba Baali, na jua, na mwezi, na sayari, na jeshi lote la mbinguni.

Lakini biblia Haijatoa idadi, kama ni tisa, au mia au elfu Mungu alizoziumba,  bila shaka ni nyingi, kwani turudipo kwenye sayansi, ndio tunathibitisha kuwa zipo mabilioni kwa mabilioni kwa mabilioni, hizi tisa walizoziona ni ambazo zipo tu kwenye mfumo wa jua letu..lakini huko angani kuna ma-jua mengi yasiyo hesabika na yote hayo yana sayari zake. Hata hivyo husema hizi nyota zote tuzionazo angani ni ma-jua kama hili letu isipokuwa tu yapo mbali sana.

Kwahiyo wanasayansi hututhbitishia zaidi uweza wa ajabu wa Mungu. Mambo yasiyoelezeka kwa ukuu na maarifa. Utukufu una yeye milele na milele. Amina.

Lakini Je! umempokea huyu Mungu aliyeumba mambo haya ya ajabu? kumbuka kumpokea yeye ni kumwamini Yesu. Kuaminije? . Ni kuamini ile kwa ile kazi yake kamilifu ya ukombozi wetu aliyotutenda sisi kwa kifo chake pale msalabani, iletao ondoleo la dhambi.

Ikiwa upo tayari leo kumpokea huyu mwokozi basi bofya hapa kwa mwongozo wa sala ya Toba  >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Mtu wa Kwanza kufika mwezini

Je! dunia Ni duara, tufe au ipo kama sahani?biblia inasemaje?

ACHENI MJUE YA KUWA MIMI NI MUNGU.

Print this post

Je! dunia Ni duara, tufe au ipo kama sahani?biblia inasemaje?

SWALI: Naomba kufahamu Je! dunia Ni duara, tufe au ipo kama sahani imefunikwa na glasi kwa juu?.


JIBU: Jambo la msingi kufahamu kuhusu biblia ni kwamba, Biblia si kitabu cha kisayansi, au cha taaluma nyingine yoyote, kana kwamba unaweza vumbua elimu ya kidunia kupitia hicho. ukitegemea biblia ikupe majibu ya kitaaluma,  kwa bahati mbaya unaweza usifikie lengo lako, kwasababu hakikuandikwa na Roho Mtakatifu kwa dhumuni hilo.

Biblia ni kitabu kinachoeleza sifa na tabia za Mungu, na jinsi mwanadamu anavyopaswa aoane nazo ili aweze tembea kama Mungu mwenyewe atakavyo. Ni kitabu kinachomrejesha mtu kwa muumba wake.  Kwa hiyo mtaala wake ni tofauti kabisa na elimu za ulimwengu huu na mavumbuzi yake.

Ni ajabu kuona mkristo analazimishia kutafuta kanuni za kibiashara kwenye biblia. Huwezi ona huko “demand and supply” au “cash flow” au masoko ya hisa. Nenda tu darasani utafundishwa vema kanuni za uwekezaji na utafanya vema.

Vivyo hivyo na kwenye sayansi, huwezi ona  aina za atomu au miamba, au mionzi, au chembe hai nyeupe za seli, au asprin huko  . Nenda tu darasani utafundishwa vema yote hayo.

Ndio, hatuwezi kukataa zipo  sehemu chache chache sana, zinazozungumzia elimu ya ulimwengu huu, lakini sio kwa lengo la kutufundisha kanuni zake, bali kwa lengo la kuelezea kwa undani jambo la kiroho katika tukio husika.

kwasababu biblia yenyewe inasema, hekima ya huu ilimwengu ni upumbavu mbele za Mungu, vilevile hekima ya Mungu ni upumbavu kwa ulimwengu. haviingiliani

1 Wakorintho 1:20

[20]Yu wapi mwenye hekima? Yu wapi mwandishi? Yu wapi mlete hoja wa zamani hizi? Je! Mungu hakuifanya hekima ya dunia kuwa ni upumbavu?

Kuhusu mapinduzi yote ya kiteknolojia ya wanadamu ambayo tunayaona  sasa, na hata yatakayokuja huwezi yapata kwenye biblia, huwezi ona facebook, internet, vikizungumziwa kwenye biblia, sio kwamba Mungu hakuyaona au kuyajua, aliyajua sana, lakini yote hayo yamejumuishwa katika neno moja kuwa “maarifa kuongezeka” (Danieli 12:4)

Sasa tukirudi kwenye swali, ambalo linauliza je dunia ni tufe, duara au kama sahani imefunikwa na glass juu. Jibu ni lile lile hakuna taarifa za kutosha kwenye biblia zinazofafanua juu ya hilo lakini haya ni maandiko machache yanayotuambia kuhusu uhalisia wa dunia..

Isaya 40:22

[22]Yeye ndiye anayeketi juu ya duara ya dunia, na hao wanaokaa ndani yake huwa kama panzi; yeye ndiye azitandazaye mbingu kama pazia na kuzikunjua kama hema ya kukaliwa;

Kwa andiko hili, tunaonyeshwa kuwa dunia ipo katika duara, aidha kama tufe au mpira. lakini ni mzunguko, na sio kama sahani yenye glasi juu.

Hivyo tukirudi katika sayansi, ukisoma huko ndio utaelewa vizuri zaidi kuwa dunia ni mfano wa tufe, na sisi tukiwa tumenata-nata juu yake sio ndani yake.

Lakini tukumbuke kuwa haya ni maarifa ya mwanadamu, aliyopewa na Mungu ya kutafiti, na maarifa yake yanatabia ya kuboreka na kupinduka. Lakini kwa upeo wao wameweza kuthibitisha hilo.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MUNGU WETU, JINSI LILIVYO TUKUFU JINA LAKO DUNIANI MWOTE!

Heshima ni nini kibiblia?

NYOTA ZIPOTEAZO.

Rudi Nyumbani

Print this post

JE KUMWAMINI BWANA YESU PEKEE INATOSHA?

Swali: Neno la Mungu linasema Katika Yohana 3:18 na 36 ..amwaminiye mwana anao uzima wa milele, asiyemwamini hana uzima? .. Je kuna haja ya kutafuta jambo lingine tena baada ya kumwamini Bwana YESU?.


Jibu: Yapo maandiko katika biblia yanayokamilishwa na maandiko mengine, yako maandiko ambayo hayahitaji kukamilishwa na mengine kwani yanakuwa yamejitosheleza lakini yapo ambayo yanaelezwa kwa ufupi hivyo ni lazima yakamilishwe na maandiko mengine…

kwamfano andiko hilo la Yohana 3:18 na 36 ni kweli maandiko yanatuonyesha kuwa “tukimwamini Bwana YESU hatutahukumiwa bali tutapata uzima wa milele”.

Yohana 3:18 “AMWAMINIYE YEYE HAHUKUMIWI; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu…..

36  Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.

Lakini tukirejea Marko 16:16 tunaona kuna jambo lingine linaongezeka..

Marko 16:16 “Aaminiye na KUBATIZWA ATAOKOKA; asiyeamini, atahukumiwa”.

Hapa kinachoongezeka ni “UBATIZO” Kwamba mtu akiamini pasipo kubatizwa bado hataurithi uzima wa milele, (ikiwa amesikia habari za ubatizo na hajataka kubatizwa).

Na ubatizo unaozungumziwa hapo sio ule wa MAJI TU, bali hata ule wa ROHO MTAKATIFU soma Luka 3:16.

Ili tuzidi kuelewe vizuri lugha hii, hebu tafakari kauli hizi mbili… “Ukipanda maharage utavuna maharage”… na kauli ya pili “Ukipanda maharage na kuyamwagilia maji utavuna maharage”.. Je kwa ni kauli ipi ipo sahihi kuliko nyingine?.. Ni wazi kuwa kauli zote zipo sahihi, isipokuwa ya pili imefafanua vizuri.. na inayofaa Zaidi ni hiyo ya pili, kwasababu ndio imekamilisha kauli ya kwanza.

Vivyo hivyo Neno linasema katika Yohana 3:18 kuwa amwaminiye YESU hatahukumiwa, lakini Marko 16:16, inakamilisha vizuri Zaidi kwamba Amwaminiye YESU na kubatizwa hatahukumiwa..Kwahiyo ya pili ni ya nzito Zaidi kwasababu imeikamilisha ile ya kwanza.

Sasa kwanini Imani pekee yake haitoshi ni lazima kubatizwa kwa maji na kwa Roho Mtakatifu??

Jibu: Kwasababu hata Mashetani yanaamini lakini bado hayana wokovu..

Yakobo 2:19 “Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda VEMA MASHETANI NAO WAAMINI NA KUTETEMEKA.

20  Lakini wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai”

Kwa hitimisho ni kwamba “IMANI YA KUMWAMINI BWANA YEESU ni LAZIMA IENDE NA MATENDO”.. Na tendo la kwanza ni hatua ya ubatizo wa Maji na nyingine ni ya Roho Mtakatifu.

Mtu anapomwamini Bwana YESU na kubatizwa kwa maji na kwa Roho anakuwa amekamilika, na kukidhi vigezo vya kuuona ufalme wa Mungu, kwani maana pia ya kuzaliwa mara ya pili ni kuzaliwa kwa maji na kwa ROHO.

Yohana 3:4 “Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?

5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, MTU ASIPOZALIWA KWA MAJI NA KWA ROHO, HAWEZI KUUINGIA UFALME WA MUNGU.

6 KILICHOZALIWA KWA MWILI NI MWILI; NA KILICHOZALIWA KWA ROHO NI ROHO.

7 Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili”.

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.


Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Wenye kubatizwa kwa ajili ya wafu ni wakina nani?

UMUHIMU WA KUBATIZWA.

TUMEPEWA, SI KUMWAMINI TU KRISTO, ILA NA KUTESWA KWA AJILI YAKE;

DHAMBI YA ULIMWENGU.

Mungu aliposema Yesu ni mwanawe pekee, alimaanisha hakuwa na wengine?

Rudi Nyumbani

Print this post

msalaba ni nini.

Msalaba ni kipande cha mti, kilichochongwa kwa kupishanishwa na kingine kwa juu. chenye lengo la kumuulia mwanadamu kwa kifo cha mateso.

Tofauti na sasa, ambapo adhabu nyingi za kifo kwa mataifa mbalimbali huwa ni kunyongwa, au kupigwa risasi, au kuwekwa kwenye kiti cha umeme, n.k.. Lakini katika falme za zamani watu waovu kupita kiasi, kwamfano wauaji, au wenye makosa ya uhaini, adhabu yao, ilikuwa ni kutundikwa au kugongelewa pale msalabani mpaka ufe. Ni mateso ambayo utataabika hapo kwa saa nyingi sana kabla ya kufa, hata siku mbili.

Hivyo kwa lugha rahisi tunaweza kusema msalaba ni chombo cha kuulia mtu.

Kwetu sisi tuliomwamini Kristo. Msalaba ni ishara kuu ya ukombozi tulioupata kwa kifo cha mwokozi wetu. Kufahamu kwa undani ni kwanini fungua link hizi; usome..

AMELAANIWA AANGIKWAYE MSALABANI.

Nini maana ya sulubu/ sulubisha?

nini maana ya kujikana nafsi na kujitwika msalaba?

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> 

https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.


Mafundisho mengine:

Neno I.N.R.I kwenye msalaba wa Yesu maana yake ni nini?

Je! msalaba kaburini una umuhimu wowote?

Print this post

Kaati na Nungu ni viumbe gani? (Isaya 34:11)

Isaya 34:11 “KAATI na NUNGU wataimiliki, bundi na kunguru watakaa huko, naye atanyosha juu yake kamba ya ukiwa na timazi ya utupu”.

Jibu: “Kaati” ni “bundi wa jangwani” (wanaoishi majangwani), na chakula chao ni jamii za panya na wadudu..Tazama picha chini.

bundi wa jangwani

“Nungu” ni aina nyingine ya bundi wanaopatikana katika misitu yenye miti iliyozeeka, yenye matundu. Aina hii ya bundi hutoa mlio mkali wakati wa usiku wanapowasiliana na jamii zao, na ndio wanaosikika katikati ya jamii za watu (Tazama picha na video chini).

nungu

Lakini swali ni je? Bundi hawa (Kaati na Nungu) ni roho za kichawi/majini?.

Jibu ni la!.. Bundi ni ndege tu kama ndege wengine walioumbwa na Bwana MUNGU, kama wakiwa katika mazingira yao ya asili, ni ndege tu kama ndege wengine, wanaohitaji pia kutunzwa.

Lakini pia ndege hawa wanaweza kutumika na wachawi katika shughuli za kichawi, kama tu vile kuku anavyoweza kutumiwa katika kafara za kichawi, na bundi ni hivyo hivyo, ila kwa mtu aliyeokoka hakuna silaha yoyote yenye uhai, au isiyo na uhai itampata.

Lakini kwa mtu aliye nje ya KRISTO, basi ni haki yake kuogopa bundi, na viumbe wengine kwani ni kweli yupo hatarini kudhuriwa na ibilisi.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Nimekuwa kama mwari nyuni wa jangwani,

IVUMBUE INJILI YA KRISTO KUTOKA KATIKA KILA JAMBO.

Je! Ni dhambi kumpiga au kumuua mnyama bila sababu yoyote?

Mjombakaka ni nani kwenye maandiko? (Walawi 11:29)

Hawa ndege katika Walawi 11:13-19 ndio ndege gani kwasasa?

Rudi Nyumbani

Print this post

Nini maana ya “Hefsiba” na “Beula” (Isaya 62:4)?

Jibu: Tuirejee.

Isaya 62:4 “ Hutaitwa tena ALIYEACHWA, wala nchi yako haitaitwa tena, UKIWA; bali utaitwa HEFSIBA; na nchi yako BEULA; kwa kuwa Bwana anakufurahia, na nchi yako itaolewa. 

5 Maana kama vile kijana amwoavyo mwanamwali, ndivyo wana wako watakavyokuoa wewe; na kama vile bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi, ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe. 

6 Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha Bwana, msiwe na kimya; 

7 wala msimwache akae kimya, mpaka atakapoufanya imara Yerusalemu, na kuufanya kuwa sifa duniani”

Hii ni habari ya tumaini la kuinuliwa tena kwa Yerusalemu na Israeli kwa ujumla, Kwamba siku ile watakapomrudia Bwana kwa mioyo yao yote basi nchi yao hiyo Bwana aliyoikataa na kuiacha na kuifanya UKIWA, basi ataibarikia tena na kuifanya kuwa FURAHA yake na ILIYOOLEWA.

Sasa tafsiri ya Hefsiba na Beula tayari imeshatolewa pale..  Hefsiba/Hefziba maana yake ni “Furaha yangu iko kwake” na Beula maana yake ni “Aliyeolewa”.. Haya ni maneno ya kiebrania yenye tafsiri hiyo. Hali kadhalika tafsiri ya “Aliyeachwa” kiebrania ni “Abuba” na “Ukiwa” ni “Shemama”..

Kwahiyo kinyume cha aliyeachwa (Abuba) ni Hefsiba (furaha yangu iko kwake)…. Na kinyume cha shemama(ukiwa) ni aliyeolewa(Beula). Ni majina ya kiebrania yaliyotumika kwa jinsia ya kike (soma 2Wafalme 21:1)

Sasa swali kwanini Mungu atumie lugha hizo za “ndoa” kuzungumza na watu wake?.

Ni kwasababu watu wa Mungu wote kiroho wanafananishwa na “mwanamke aliyeolewa/bibi arusi”

Isaya 54:4 “Usiogope; maana hutatahayarika; wala usifadhaike; maana hutaaibishwa; kwa kuwa utaisahau aibu ya ujana wako, pia mashutumu ya ujane wako hutayakumbuka tena.

5 KWA SABABU MUUMBA WAKO NI MUME WAKO; Bwana wa majeshi ndilo jina lake; na Mtakatifu wa Israeli ndiye Mkombozi wako; Yeye ataitwa Mungu wa dunia yote. 

6 Maana Bwana amekuita KAMA MKE ALIYEACHWA na kuhuzunishwa rohoni, kama mke wakati wa ujana, atupwapo, asema Mungu wako. 

7 Kwa kitambo kidogo nimekuacha; lakini kwa rehema nyingi nitakukusanya”.

Soma pia Yeremia 31:31-32, 2Wakorintho 11:2 na Ufunuo 21:9 utazidi kuliona jambo hilo..

Kwahiyo ujumbe huo haukuwa kwa Israeli peke yao, bali pia unatuhusu sisi, kwamba tumrudiapo Mungu wetu kwa mioyo yetu yote, basi tunazo ahadi za Baraka na mafanikio, na majina yetu kiroho yatabadilika na kuwa Hefsiba na Beula…Na furaha ya Bwana itakuwa juu yetu nasi tutakuwa na muunganiko wa kiroho na Bwana YESU.

Isaya 62:1 “Kwa ajili ya Sayuni sitanyamaza, na kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia, hata haki yake itakapotokea kama mwangaza, na wokovu wake kama taa iwakayo. 

2 Na mataifa wataiona haki yako, na wafalme wote watauona utukufu wako; nawe utaitwa jina jipya, litakalotajwa na kinywa cha Bwana.

3 Nawe utakuwa taji ya uzuri katika mkono wa Bwana, na kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako. 

4 Hutaitwa tena ALIYEACHWA, wala nchi yako haitaitwa tena, UKIWA; bali utaitwa HEFSIBA; na nchi yako BEULA; kwa kuwa Bwana anakufurahia, na nchi yako itaolewa. 

5 Maana kama vile kijana amwoavyo mwanamwali, ndivyo wana wako watakavyokuoa wewe; na kama vile bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi, ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe. 

6 Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha Bwana, msiwe na kimya; 

7 wala msimwache akae kimya, mpaka atakapoufanya imara Yerusalemu, na kuufanya kuwa sifa duniani”

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Yerusalemu ni nini?

Uasherati wa Kiroho maana yake nini?

HAPAKUWA NA NAFASI YA KUPITA KWA YULE MNYAMA ALIYEKUWA CHINI YANGU.

Ni kweli Paulo alipuuzia maonyo aliyopewa ya kwenda Yerusalemu?

KWANINI UNAPASWA UWE BIBI ARUSI NYAKATI HIZI ZA MAJERUHI?

Rudi Nyumbani

Print this post

Je YUDA alikuwa ni shetani kulingana na Yohana 6:70?

Swali: Je kwanini Bwana YESU aseme Yuda ni shetani, na kwanini amchague shetani kama mwanafunzi wake?


Jibu: Turejee..

Yohana 6:70 “Yesu akawajibu, Je! Mimi sikuwachagua ninyi Thenashara, NA MMOJA WENU NI SHETANI?

71  Alimnena Yuda, mwana wa Simoni Iskariote; maana huyo ndiye atakayemsaliti; naye ni mmojawapo wa wale Thenashara”.

Swali hili linafanana na lile la kwanini Bwana YESU amwite Herode “MBWEHA”.

Luka 13:31 “Saa ile ile Mafarisayo kadha wa kadha walimwendea, wakamwambia, Toka hapa, uende mahali pengine, kwa sababu Herode anataka kukuua.

32  Akawaambia, Nendeni, mkamwambie yule mbweha, Tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa, siku ya tatu nakamilika”.

Sasa kiuhalisia Herode sio “Mbweha”, wala Yuda siye “shetani”…Isipokuwa watu hao ndani yao wamebeba tabia za “Mbweha” na “shetani”.. Ni sawa na Bwana YESU anavyojulikana kama Mwanakondoo…haimaanishi Bwana YESU ni kondoo (mnyama), La!, isipokuwa ndani yake (katika roho) ipo tabia ifananayo na ya kondoo yaani ya “unyenyekevu”.

Hali kadhalika Yuda si “shetani” bali ndani yake kulikuwa na roho ya shetani ya usaliti na mauaji.

Luka 22:3 “SHETANI AKAMWINGIA YUDA, AITWAYE ISKARIOTE, naye ni mmoja wa wale Thenashara.

4  Akaondoka, akaenda akasema na wakuu wa makuhani na majemadari, jinsi atakavyoweza kumtia mikononi mwao”.

Hivyo Bwana YESU alikuwa anamaanisha roho iliyokuwemo ndani ya Yuda na si utambulisho wa YUDA, utaona pia kuna wakati alimwambia Petro kuwa ni shetani..

Mathayo 16:22 “Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, hayo hayatakupata. 23  Akageuka, akamwambia Petro, NENDA NYUMA YANGU, SHETANI; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu”.

Hapa Bwana hakuwa anaongea na Petro, wala hakuwa anamkemea Petro, bali ile roho iliyokuwa ndani ya Petro (yaani ya ibilisi) ndio aliyokuwa anaikemea.

Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba Bwana YESU hakumchagua shetani, wala Yuda hakuwa shetani bali alikuwa na roho ya shetani ndani yake.

Na hata leo kuna watu ambao ni “mashetani” katika muktadha huo, kwamba ndani yao kuna roho ya shetani.. Hivyo hatuna budi kila siku kujipambanua na kujipima na kujitakasa, ili tusiwe tusionekane kama mashetani.. na utakaso mkuu ni ule Bwana aliowaambia baadae wanafunzi wake, baada ya kumkemea Petro.

Mathayo 16:23 “Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.

24  Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.

25  Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona”.

Hapo baada ya maneno hayo kwa Petro, Bwana anaanza kusema “…Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake..”

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Je Yuda alienda wapi, ni mbinguni au jehanamu?

Ni kwa namna gani Yesu ni Simba wa Yuda?

ZIFAHAMU KAZI KUU (10) ZA SHETANI DUNIANI.

KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 3

KUMJUA YESU SI KUPATA UZIMA WA MILELE.

Rudi Nyumbani

Print this post

LAANA NI NINI KIBIBLIA?

Kibiblia  Neno laana linatafsiri kwa namna mbili.

Namna ya kwanza, ni Kupoteza sifa ya kukubaliwa na Mungu kwa jambo lolote lile. Na hii chanzo chake ni lile anguko la mwanadamu tangu mwanzo.

Namna ya pili, ni apizo alitoalo mtu kwa mwenzake au alitoalo Mungu mwenyewe, kwa mwanadamu ili wafikiwe na ubaya fulani, au wakasifikiwe na Mema waliyokusudiwa.

 

LAANA YA KWANZA:

Sasa laana hii ya kwanza, inazalika kwasababu ya  asili yetu, ambayo ilionekana tangu Adamu, kuhasi maagizo ya Mungu, ambayo hata sisi sote tuliopo leo, asili hiyo ipo ndani yetu. Ni sawa na unavyomwona mdudu kama mende, ukimtazama tu tangu akiwa mtoto, utamchukia hata kabla hajaonyesha hali yake ya kupenda uchafu, kwasababu unajua asili hiyo ipo ndani yake. Atakuja kuwa mchafu tu.

 

Ndivyo ilivyo kwetu sisi, tayari Mungu alishaona tangu tunazaliwa tutamwasi tu yeye, mfano wa baba yetu Adamu.

Na ndio maana akaandaa mpango wa kuzaliwa upya mara ya pili, kupitia Yesu Kristo. Hivyo mtu yeyote anayezaliwa mara ya pili, anaondolewa katika laana hiyo ya kukataliwa na Mungu, na anakuwa mwana wa Baraka. Laana hii haiwezi kuondoka bila damu ya Yesu.

 

Hiyo ndio sababu kwanini maandiko yanasema Yesu alifanyika laana kwa ajili yetu. Maana yake, tunapokombolewa na yeye tunafanywa kuwa watu wengine kabisa wenye asili nyingine wasio na laana, wenye kukubaliwa na kupendwa na Mungu.

 

Wagalatia 3:13  Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;

14  ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani.

 

Hivyo wewe uliyeokoka, na kupokea Roho Mtakatifu unaitwa, mbarikiwa, unaitwa mungu duniani, mtoto wa Mungu kwelikweli.

LAANA YA PILI

Lakini laana ya pili, kama tulivyoona ipo katika maapizo ambayo huyatoa Mungu au mwanadamu mwenyewe.

a) Tukianzana na zile zinazonenwa na Mungu

Mungu anaweza kukutamkia laana, hata kama utakuwa umekombolewa na yeye. Unaweza kushiriki mabaya. Laana hizi zinaweza kukufanya usipoteze wokovu wako, lakini zikakukosesha mambo mengi sana duniani.

 

Mfano wa hizi ndio zile alizowaambia wana wa Israeli, kwamba watakapoacha sheria zake, basi watatawanywa katika mataifa yote, watakuwa mikia na sio vichwa, nchi itazuliwa Baraka zake, wataondokeshewa adui zao N.k. (Kumbukumbu 28)

 

Mfano pia wa hizi, ndio kama ile aliyoilaani nchi, na nyoka pale Edeni. Akasema itatoa miiba, na nyoka atakwenda kwa tumbo (Mwanzo 3:17). Vilevile ndio ile aliyomwambia Kaini kuwa atakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani (Mwanzo 4:12).

 

Hata sasa wapo wengi wanaokutana na maapizo hayo ya Mungu kwa kufanya dhambi au makosa ya makusudi. Namna ya kueupuka laana hizi ni kutii agizo la Mungu.

Kwasababu unapozizoelea zitakufanya uangukie kabisa kwenye kundi lile la kwanza la kukataliwa kabisa..la watu ambao hawajaokoka.

 

Waebrania 6:4  Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu,5  na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo,

6  wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.

7  Maana nchi inayoinywa mvua inayoinyeshea mara kwa mara, na kuzaa mboga zenye manufaa kwa hao ambao kwa ajili yao yalimwa, hushiriki baraka zitokazo kwa Mungu; 8  bali ikitoa miiba na magugu hukataliwa na kuwa karibu na laana; ambayo mwisho wake ni kuteketezwa.

 

Kinyume cha laana ni Baraka, unapotii amri za Mungu, umejiwekea mazingira mazuri ya kupokea Baraka.

 

b) Lakini pia zipo laana  zinazonenwa na  mwanadamu.

Hizi nazo zimegawanyika katika makundi mawili.

 

i) Kundi la kwanza ni la watu wa Mungu/wenye haki.

Kwamfano Utakumbuka Hamu alipoona uchi wa baba yake. Nuhu aliulaani uzao wake, Hivyo watu wa Mungu wamepewa mamlaka hiyo, hata sasa, ndio maana Bwana Yesu alisema mtakalolifunga duniani, limefungwa mbinguni, na akatusihi pia tuwe watu wa kubariki kuliko  kulaani. (1Petro 3:9)

Unapokosewa na mwenye dhambi epuka kutoa neno la madhara kwake, kwasababu hakika jambo hilo litampata na kumwangamiza kabisa. Ndicho alichokifanya Elisha kwa wale vijana arobaini na wawili waliomdhihaki.

 

ii) Kundi la pili ni laana zitokazo kwa watu waovu.

 

Husasani wachawi, nao pia huweza kusema jambo likatokea, Utakumbuka kisa cha Balaamu mchawi, alipoajiriwa na Balaki kwenda kuwalaani Israeli wa Mungu, lakini alishindwa akajikuta anawabariki badala ya kuwalaani.

Akasema hakuna uchawi (Hesabu 23:23).

Ikiwa wewe umeokoka, huna haja ya kuogopa laana za hawa, kwasababu haziwezi kukupata, kwasababu unalindwa na nguvu za Mungu, hizi huwa zinawapata watu ambao wapo nje ya Kristo YESU.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

NUHU WA SASA.

MADHARA YA DHAMBI YA UASHERATI.

KUVUNJA MAAGANO YA UKOO.

Rudi Nyumbani

Print this post

Kututa ni nini? (Mhubiri 2:26).

Swali: Neno “Kututa” lina maana gani kama tusomavyo katika Mhubiri 2:26?


Jibu: Turejee..

Mhubiri 2:26 “Kwa sababu Mungu humpa yeye aliyemridhia hekima na maarifa na furaha; bali mkosaji humpa taabu, ili kukusanya na KUTUTA, apate kumpa huyo ambaye Mungu amridhia. Hayo nayo ni ubatili na kujilisha upepo”.

“Kututa” maana yake ni “KULIMBIKIZA”..

Kwahiyo maneno hayo tunaweza kuyaweka katika Kiswahili hiki.. “Kwa sababu Mungu humpa yeye aliyemridhia hekima na maarifa na furaha; bali mkosaji humpa taabu, ili kukusanya na KULIMBIKIZA, apate kumpa huyo ambaye Mungu amridhia. Hayo nayo ni ubatili na kujilisha upepo”.

Andiko hili linatufundisha hatari ya kukusanya mali na kulimbikiza, ikiwa tupo nje ya KRISTO. Kwa maana hapo maandiko yanasema, mali za mtu huyo (mkosaji), alizojikusanyia na kujilimbikizia, atanyang’anywa na kupewa yule Mungu aliyemridhia.

Lakini pia mstari huo unatuonyesha thawabu kuu ambazo Mungu humpa yule aliyemridhia. Na hizo si nyingine Zaidi ya HEKIMA, MAARIFA na FURAHA.

Kabla ya kumpa mtu Mali humpa Hekima, Maarifa na Furaha na hivi vitatu ndivyo vitu vya kuvitafuta kwa MUNGU kabla ya kuomba vitu vingine kama Mali. Kama Sulemani aliomba Hekima kwanza na Mungu akampa Hekima na Mali ikawa ni nyongeza.

Hali kadhalika na sisi hatuna budi kutafuta hekima, Maarifa, Ufahamu na Furaha kwa bidii kwani tukiyapata hayo basi hayo mengine tutazidishiwa, na hata tusipoyapokea, bado hekima na maarifa vitabaki kuwa utajiri mkuu.

Mithali 3:13 “Heri mtu yule aonaye hekima, Na mtu yule apataye ufahamu.

14 Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha, Na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi.

15 Yeye ana thamani kuliko marijani, Wala vyote uvitamanivyo havilingani naye.

16 Ana wingi wa siku katika mkono wake wa kuume, Utajiri na heshima katika mkono wake wa kushoto.

17 Njia zake ni njia za kupendeza sana, Na mapito yake yote ni amani.

18 Yeye ni mti wa uzima kwao wamshikao sana; Ana heri kila mtu ashikamanaye naye”

Tafuta Hekima, tafuta Maarifa, tafuta Ufahamu, Busara na Furaha..

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Tofauti kati ya Hekima, ufahamu na maarifa, ni ipi?

NI NANI ANAYEUFUNGA MLANGO WA MAARIFA?.

IFAHAMU HUZUNI NA FURAHA YA MALAIKA.

JE! NINAWEZA KUPOTEZA FURAHA YA WOKOVU?

KAMA MTUMISHI WA MUNGU, TAFUTA MAARIFA KWA BIDII.

Rudi Nyumbani

Print this post