Category Archive maswali na majibu

Msingi wa imani ya kikristo ni upi?

Msingi ni chimbuko, au mwanzo au kiini cha kitu fulani.

Ni wazi kuwa kila jambo lina msingi wake. taifa lina msingi wake, taasisi ina msingi wake, kabila lina msingi wake vilevile pia imani ina msingi wake.

Hivyo tukirudi katika ukristo. Msingi wa imani yake ni upi?

Msingi wa ukristo ni YESU KRISTO mwenyewe, na kazi yake aliyoikamilisha ya kufa na kufufuka kwake. Na sio kanisa, au dhehebu, au mapokeo fulani, au kikundi fulani cha wanaharakati.

Pasipo Yesu hakuna ukristo.

Yeye anafananishwa na lile jiwe kuu la pembeni, ambalo hakuna mjenzi aliyeweza kusimamisha jengo bila kuliweka hilo.

1 Petro 2:6

[6]Kwa kuwa imeandikwa katika maandiko Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika. 

Habari kamili za Yesu, na kazi yake aliyokuja kuifanya duniani unaipata katika kitabu kimoja tu kiitwacho BIBLIA. Hivyo huwezi kutenganisha biblia na Yesu Kristo.

Ili mtu ashawishwe kuipokea imani, ni sharti, aisikie kwanza injili yake ambayo hiyo utaipata katika Neno la Mungu yaani biblia..(Warumi 10:17)

Mpaka mtu aitwe mkristo ni lazima amtambue kwanza Kristo ni nani, na nini amekileta duniani, vinginevyo hawezi kuwa mkristo, hata kama atajiunga na kanisa, au dhehebu na kuyashika mapokeo yote aliyoyakuta huko, au kuisoma biblia yote, huyo bado hajawa mkristo.

Ni muhimu sana kumtambua Yesu ni nani kwetu. Kumtambua Yesu kama mwana wa Mungu bado inaweza isikupe wokovu, hata kumtambua Yesu kama Mungu bado inaweza isikupe wokovu (ijapokuwa vyote hivyo ni vyeo vyake). Lakini vyeo hivyo sio kiini cha ukristo.

Yesu ni nani na ni nini alikileta duniani?

Yesu ni MKOMBOZI, kama tafsiri ya jina lake linavyojieleza( Mathayo 1:21)

mkombozi wa nini?

Alikuja kutukomboa roho zetu, nafsi zetu na miili yetu, Na kama ilivyo kanuni ya kiroho ili jambo hilo liweze kukamilika ilipasa itolewe kafara isiyo na kasoro yoyote(yaani dhambi). Na aliyeweza kukidhi vigezo hivyo ni Yesu pekee.

Ndio maana ilimgharimu afe, kama fidia ili sisi tupokee ondoleo la dhambi na msamaha wa dhambi kwa kifo chake. Hivyo yoyote anayeamini(yaani anayeupokea wokovu huo aliouleta).

kwa toba ya kweli na ubatizo, Basi anakuwa ameokoka, hivyo ile ghadhabu ya Mungu kwa wenye dhambi wote haiwi tena juu yake, tangu huo wakati anaitwa mbarikiwa, au mkristo, kwasababu dhambi zake zinakuwa zimefutwa kabisa.

Na zaidi ya hayo mtu huyu moja kwa moja anapewa zawadi ya Roho Mtakatifu, ambaye tangu huo wakati na kuendelea anakuwa ndani yake kama msaidizi, kumsaidia madhaifu yake, katika kuomba, kuijua kweli, kumkumbusha aliyoyasema Yesu, kumpasha habari ya mambo yajayo, na kumtia nguvu ya kumtumikia Mungu, pamoja na kumpa nguvu ya kushinda dhambi.

Huyu ndiye mkristo.

Swali ni je! umemwamini ipasavyo? au umempokea kwa namna ile ya kidini?

Usifikiri kuhama dini, wewe ni Kristo, au kuzaliwa kwenye familia ya kikristo wewe ndio mkristo, au kusomea theolojia, hapana hizo ni kampeni tu, ukristo halisi huja kwa kumwelewa Kristo ni nani na ni nini amekifanya kwako.

Ikiwa bado hujaokoka na unataka kumpokea leo ili upate ondoleo la dhambi zako. Basi uamuzi huo ni bora sana kwako. Fungua hapa kwa mwongozo wa sala ya toba.>>

KUONGOZWA SALA YA TOBA

Ubarikiwe.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

JE! UKRISTO UNAMPA MTU DHAMANA YA KUWA TAJIRI?

Dini ni nini, na Imani ya kweli ni ipi?

Nini maana ya “Tumejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii”?

Rudi Nyumbani

Print this post

Je imani ya Shincheonji ni imani ya kweli?

Je Kanisa la Sayuni (au Shincheonji) ni la kweli?


Kanisa la Kristo la Shincheonji (Shincheonji Church of Jesus kwa kifupi (SCJ)).  Ni Imani iliyoanzia nchini Korea Kusini na ilianzishwa na mtu ajulikanaye kama Lee-Man-Hee

Shincheonji ni lugha ya kikorea yenye maana ya “Mbingu mpya na Nchi Mpya” …Imani ya Shincheonji inafundisha kuwa muasisi wa Imani hiyo yaani Lee-Man-Hee ndiye Mchungaji aliyeahidiwa wa Agano jipya, na yeye pekee ndiye mwenye uwezo wa kukielewa kitabu cha Ufunuo na kukifunua mafumbo yake.

Lee-Man-Hee anafundisha kuwa mtu yeyote ambaye hatakuwa katika Imani yake basi siku ya mwisho hatapokea msamaha, bali atahukumiwa milele.

Imani ya Shincheonji inafundisha pia kuwa… Majina ya makabila kumi na mawili ya wana wa Israeli yamechukuliwa kutoka kwa majina ya wanafunzi kumi na wawili wa Yesu, na inafundisha pia ile idadi ya waliotiwa muhuri katika Ufunuo 7:4  (wale 144,000) ni washirika wa makabila 12 ya Shincheonji jambo ambalo si kweli, kwani biblia imesema wazi kuwa ni makabila 12 na tena imetaja majina yake.

Lakini pia Imani ya Shincheonji inafundisha kuwa Malaika wote ni wanadamu, jambo ambalo pia si kweli kwani biblia imeweka wazi kuwa kuna Malaika na pia wapo wanadamu, 1Wakorintho 4:9, 1Wakorintho 13:1 na Ufunuo 9:15 inaelezea Zaidi

Imani ya Shincheonji inazidi kufundisha kuwa Ufunuo 7:2 inaelezea Taifa la Korea (Mashariki ) na Lee-Man-Hee ndiye malaika yule wa kwanza, Zaidi sana inamtaja Lee-Man-Hee kwamba ndiye Yohana mpya ambaye amechukuliwa juu mbinguni na kuonyeshwa yaliyopo kule sawasawa na Ufunuo 4:1, Imani ya namna hii pia ilizuka kwa baadhi ya watu nchini Nigeria akiwemo Amos Segun na baadhi ya watu Ulaya katika karne ya 20 mwanzoni na 21 mwishoni, wakidai kuwa wao ni Yohana, kama anavyodai sasa Lee-Man-Hee, na Imani zao zikakomba idadi kubwa ya watu lakini wote hawakufanikiwa katika uongo huo.

Sayuni Christian Mission Center ni mkono wa elimu wa Kanisa la Shincheonji ambao Juhudi zake za  kimsingi za imani ya chuo hicho ni kuwaalika watu kuhudhuria madarasa katika vituo vyao mbalimbali,.

Na Wasomaji wanapohitimu, wanasemekana kuwa “wametiwa muhuri” kama washiriki wa 144,000, na hivyo mwisho wa siku wataokolewa, jambo ambalo si kweli kibiblia kwani idadi ya 144, 000 biblia imeweka wazi kuwa ni wayahudi ambao watatiwa Muhuri wakati wa kipindi cha dhiki kuu, wakati ambapo injili itarudi Israeli.

Chuo cha Sayuni Christian Mission Center inatoa viwango vitatu vya masomo ya kozi.

Katika kozi ya ngazi ya mwanzo (Maarifa ya Kweli ya Siri za Ufalme wa Mbinguni)

wanafunzi wanafundishwa “maana ya kweli ya mifano iliyoandikwa katika Biblia.” Ikiwa wanafunzi hawaelewi mafumbo kwa usahihi, anadai Lee Man-hee, “hawawezi kusamehewa wala hawataokolewa.”

Kozi ya ngazi ya pili inatoa muhtasari wa Biblia ambao, kulingana na Lee Man-hee, utasaidia wanafunzi “kufahamu muktadha wa jumla wa Biblia” ili kuwasaidia katika kujifunza na wokovu wao wa mwisho.

Ngazi ya tatu na ya mwisho inashughulikia Kitabu kizima cha Ufunuo.

Kufikia mapema Agosti 2024, kulingana na Shincheonji, makanisa 1,352 katika nchi 41 yamebadilisha ishara zao na Imani zao na kuzifuata zile za Kanisa la Shincheonji Church of Jesus na Zaidi wanatuma maombi ya kuomba kutumiwa wakufunzi na elimu hiyo.

Zaidi walengwa wa kwanza wa elimu ya Shincheonji ni wachungaji wenye makanisa tayari, kwani wanaamini kwa njia hiyo itakuwa rahisi kuifikisha Imani mbali Zaidi.

Shincheonji amekuwa akitumia “kutabiri”  kama njia za uinjilisti kwa baadhi ya makundi. Wanawakaribia vijana na wataalamu kupitia shughuli za klabu zilizojificha, uwekaji kazi, na tathmini za kisaikolojia. Kwa wazee, hutoa bahati nasibu bila malipo mitaani ili kukusanya habari za kibinafsi. Mbinu zao zinahusisha namna mbalimbali za kujificha na kudanganya, wakijihusisha katika utendaji unaonyonya dini ili kufuata masilahi ya kikundi.

Zaidi ya hayo yapo mambo mengine ndani ya Shincheonji yaliyo kinyume na biblia, lakini kwa hayo machache itoshe kusema kuwa Imani hii, si ya KRISTO YESU, imebeba upotoshaji ambao unao msingi wa mafundisho ya Uongo, na pia msingi wake ni IMANI katika MTU, Zaidi ya katika KRISTO  YESU.

Bwana akubariki.

Maran atha.

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

ORODHA YA IMANI POTOFU- Sehemu ya 1.

IMANI “MAMA” NI IPI?

IMANI YENYE MATENDO;

Je maombi ya mlimani yana ulazima wowote kwa mkristo?

MAMBO (2) YATAKAYOKUTENGA NA IMANI SIKU HIZI ZA MWISHO.

Rudi Nyumbani

Print this post

Je Mungu anaua?

Swali: Je Mungu anaua kama watu wanavyoua?


Jibu: Ndio Mungu pia anaua, maandiko yanasema hivyo..

Mathayo 10:28  “Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; AFADHALI MWOGOPENI YULE AWEZAYE KUANGAMIZA MWILI NA ROHO PIA KATIKA JEHANUM”

Sasa anayeweza kuua mwili na kuungamiza kwenye jehanamu ya moto ni MUNGU peke yake, mwanadamu anaweza tu kumuua mtu, lakini asiweze kuiona roho ya mtu wala asijue inakokwenda, lakini Bwana MUNGU anaweza kufanya yote (kuua mwili na kuangamiza roho vile vile)

Na maangamizi ya MUNGU ni makubwa na mabaya sana kwani hasira yake iwakapo haangalii wingi, ndicho kilichotokea wakati wa gharika ya Nuhu, dunia nzima iliuawa isipokuwa watu nane (8) tu ndio waliosalimika, na aliyewaua si shetani bali ni MUNGU mwenyewe.

1Petro 3: 20  “watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji”.

Na Bwana MUNGU anaua mtu/watu pale maovu/maasi yanapozidi sana, kiasi kwamba watu hao hata maonyo hawataki kusikia tena..

Kutoka 22: 22 “Usimtese mjane ye yote aliyefiwa na mumewe, wala mtoto yatima.

23 Ukiwatesa watu hao katika neno lo lote, nao wakanililia mimi, hakika yangu nitasikia kilio chao,

24 na hasira yangu itawaka moto, NAMI NITAWAUA NINYI KWA UPANGA; na wake wenu watakuwa wajane, na watoto wenu mayatima”

Maandiko mengine yanayoonyesha kuwa Mungu anaweza kuua ni pamoja na Amosi 2:3 na Ufunuo 2:23.

Lakini pamoja na kwamba Mungu ni mwingi wa hasira na pia anaua, na maangamizi yake ni makubwa na mabaya kuliko ya wanadamu, lakini bado yeye NI MWINGI WA REHEMA WALA SI MWEPESI WA HASIRA.

Nahumu 1:3 “Bwana si mwepesi wa hasira, ana uweza mwingi,…”

Hasira yake ipo mbali sana, na iko hivyo ili tupate nafasi ya kutubu kabla ya hasira yake kumwagwa.

2Petro 3:9 “Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.

10  Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea”

Je umempokea Bwana YESU au bado unajitumainisha na mambo ya mwilini, yaletayo hasira ya Mungu?..

Warumi 8: 13 “kwa maana kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi”

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

SIKU YA HASIRA YA BWANA.

MWE NA HASIRA, ILA MSITENDE DHAMBI.

NIFANYE NINI NIWEZE KUDHIBITI HASIRA?

Wivu ni nini na kuna aina ngapi za Wivu?

UFANYE MOYO WA MUNGU UWAELEKEE WATU WAKE.

Rudi Nyumbani

Print this post

Je Mungu ana jinsia?

Swali: Je Bwana Mungu anayo jinsia kama wanadamu tulivyo na jinsia?


Jibu: Biblia inasema Mungu alimwumba “MTU” kwa mfano wake, na si “WATU” kwa mfano wake.

Na Mtu wa kwanza kuumbwa alikuwa ni ADAMU mwenye jinsia ya KIUME, na baadaye ndipo Hawa akaumbwa kutoka katika ule ubavu uliotwaliwa kwa Adamu.

Kwahiyo Mtu wa kwanza kuumbwa aliyekamilika ndio TASWIRA kamili ya MUNGU. Na Mtu huyo ni Adamu, aliye na jinsia ya kiume,

Sasa maadamu MUNGU si mwanadamu, hivyo yeye hana jinsia ya kiume, bali anao Utu wa KIUME, Kwasababu jinsia inahusisha mambo mengi ya kibinadamu ikiwemo mifumo  ya uzazi. Lakini Mungu yeye sio kama sisi wanadamu, hivyo yeye anao utu wa KIUME na sio wa KIKE, na utu huo wa Kiume alionao ulianza kwake ndipo tukapewa sisi, na haukuanza kwetu kisha yeye akaiga baadae hapana!.

Hivyo kwa hitimisho ni kwamba utu wa MUNGU ni wa kiume, na ndio sababu anajitambulisha yeye kama BABA kwetu, (Soma Mathayo 6:9) na sehemu nyingine anajitambulisha  kama MUME (Soma Isaya 54:5), na hakuna mahali popote katika biblia panapoonyesha Bwana MUNGU akuchukua uhusika wa kike, au utu wa kike.

Na la mwisho pia kufahamu ni kuwa, Mungu ni Roho, na tunamwabudu katika Roho na kweli.

Yohana 4:23 “Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu

24  Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.”

Je umeokoka?, kama bado unangoja nini?..Hizi ni siku za mwisho na YESU yupo mlangoni, wakati wowote parapanda ya mwisho italia, je utakuwa wapi?

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Anaposema mwanamume mmoja katika elfu nimemwona anamaana gani?

NI KIPI MUNGU ANACHOKITAZAMA ZAIDI, MOYO AU MWILI?

Je shetani ana uwezo wa kujua mawazo ya mtu?

VIJANA NA MAHUSIANO.

Je suruali ni vazi la kiume tu?

Rudi Nyumbani

Print this post

Je mtu anaweza kupoteza wokovu?

Jibu: Ipo elimu isemayo  kuwa “Mtu akiokolewa, ameokolewa na hivyo hawezi kupoteza wokovu”.. (Once saved, always saved).

Ni kweli msemo huo ni kama unataka kuleta maana kwamba mtu akiupokea wokovu hawezi tena kuupoteza…

Lakini maandiko yapo wazi yanayoonyesha kuwa mtu anaweza kuupoteza Wokovu.

Ufunuo 3:11 “Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, ASIJE MTU AKAITWAA TAJI YAKO

Sasa jiulize, kama mtu hawezi kupoteza wokovu alionao, kwanini Bwana YESU asisite kushika kile tulicho nacho.

Lakini pia, bado maandiko yanazidi kutufundisha kupitia safari ya wana wa Israeli, kwamba kweli walipata WOKOVU kutoka katika utumwa wa FARAO, lakini walipokuwa katika safari yao ya kuelekea KANAANI njiani waliupoteza ule wokovu, na Mtume Paulo kwa ufunuo wa Roho aliliona hilo pia na kulisema huku akulifananisha na Wokovu tuupatao, kwa njia ya kumwamini Bwana YESU na kuokoka kwamba tusipouthamini basi hatutapona kama wana wa Israeli walivyopotea.

Waebrania 2:1  “Kwa hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi hayo yaliyosikiwa tusije tukayakosa.

2  Kwa maana, ikiwa lile neno lililonenwa na malaika lilikuwa imara, na kila kosa na uasi ulipata ujira wa haki,

SISI JE! TUTAPATAJE KUPONA, TUSIPOJALI WOKOVU MKUU NAMNA HII? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia”

Sasa kiswahili chepesi cha maandiko hayo ni hiki… “SISI JE TUTASALIMIKAJE TUSIPOUJALI NA KUUSHIKILIA ULE WOKOVU TULIOUPOKEA???” Na kumbuka hapo Mtume Paulo alikuwa haongei na watu ambao hawajaokoka, LA! Bali alikuwa anaongea na watu ambao tayari wanao wokovu, lakini huenda wanasuasua, hivyo anatoa hiyo tahadhari.

Wengi tusomapo mstari huo, tunawalenga wale wanaosikia injili lakini wanaifanya mioyo yao kuwa migumu kutii, lakini andiko hilo, halikuwa kwaajili ya watu walio nje ya Imani, bali kwa watu ambao tayari wanao WOKOVU.

Maana yake ni kwamba wokovu mtu anaweza kuupoteza kabisa kama hatakuwa makini, kama atakuwa sio mtu wa kujali.

Wanaoshikilia kuwa “Mtu akiokolewa ameokolewa hawezi kupoteza tena wokovu” wanasimamia mfano ule wa Baba na mtoto, kwamba mtoto akishazaliwa katika familia, hakuna kitakachoweza kumfanya asiwe mtoto wa baba yake.

Ni kweli kibinadamu hilo haliwezekani, aliyezaliwa katika familia ni lazima damu yake itabaki kuwa ya Baba yake hawezi kamwe kuupoteza ule wana (hiyo ni kweli kabisa)… Lakini kimaandiko sisi hatupokei uwezo wa kuwa wana kibinadamu, bali ni katika roho.. na kama uwezo huo unafanyika katika roho, basi pia katika roho unaweza kutanguka.

Ndicho kilichomtokea Esau, ni kweli alikuwa mwana wa kwanza wa Isaka, lakini alipoidharau nafasi yake ile ya uzaliwa wa kwanza ilihamia kwa ndugu yake Yakobo, yeye Esau aliendelea kuwa mzaliwa wa kwanza kwa tarehe za damu na nyama, lakini katika roho tayari ni mzaliwa wa pili, sasa kama mambo hayo yanaweza kubadilika hivyo, kwanini mtu asipoteze UWANA pale ambapo anaupuuzia wokovu wake? (Waebrani 12:16-17).

Ni wazi kuwa atapoteza ile hali ya kuwa Mwana wa Mungu, na atakuwa mwana wa Ibilisi katika roho, endapo asipouthamini wokovu wake.

2Petro 2:20  “Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza.

21  Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa.

22  Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaa-gaa matopeni”

Hivyo kwa hitimisho ni kwamba Mtu anaweza kupoteza Wokovu endapo hataushikilia ipasavyo na hataujali, na kumbuka siku hizi za mwisho mafundisho haya yanamea kwa kasi sana, ambayo yanawafundisha watu kuwa ukishamwamini BWANA YESU inatosha, ishi uishivyo, fanya ufanyalo, wewe mbinguni utaenda.

Ndugu usidanganyike, maandiko yameweka wazi kabisa kuwa pasipo Utakatifu! Hakuna mtu atakayemwona MUNGU, iwe Mchungaji, iwe nabii, iwe Raisi wa nchi, iwe Mtume, iwe Papa, iwe mwanaume iwe mwanamke, iwe mtu yoyote ule. PASIPO UTAKATIFU, HAKUNA MBINGU!!!

Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, NA HUO UTAKATIFU, AMBAO HAPANA MTU ATAKAYEMWONA BWANA ASIPOKUWA NAO”

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

JE! SISI KAMA WAKRISTO NI DHAMBI KUSHEHEREKEA KRISMASI?.

Nini tofauti ya haya maneno. 1) KUOKOKA, 2) WOKOVU, 3) KUONGOKA.?

Kama tunaokolewa kwa neema kwanini wokovu tuupate kwa nguvu?

DHAMBI YA ULIMWENGU.

ESTA: Mlango wa 4

Rudi Nyumbani

Print this post

Patasi ni nini? (Kutoka 32:4)

Swali: Patasi ni nini kama tunavyosoma katika kitabu cha Kutoka 32:4?

Jibu: Turejee..

Kutoka  32:4 “Akaipokea mikononi mwao akaitengeneza kwa PATASI, akaifanya iwe sanamu ya ndama kwa kuiyeyusha; nao wakasema, Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri.”

“Patasi” ni zana inayotumika kuchonga vitu vya jamii ya mbao au chuma. Kifaa hiki mara nyingi kinatumiwa na mafundi seremala, katika kuchonga mbao, na kuzitia urembo mbalimbali, au maandishi (Tazama picha chini).

patasi ni kifaa gani

Katika biblia neno hili limeonekana mara moja tu, pale ambapo wana wa Israeli walipojitengenezea sanamu ya ndama ili iwarudishe Misri walikotoka. Na waliifanya kwa kuyeyusha dhahabu zao na kisha kuzichonga kwa mfano wa ndama kupitia patasi.

Kutoka 32:1 “Hata watu walipoona ya kuwa Musa amekawia kushuka katika mlima, wakakusanyana wakamwendea Haruni, wakamwambia, Haya! Katufanyizie miungu itakayokwenda mbele yetu, kwa maana Musa huyo aliyetutoa katika nchi ya Misri hatujui yaliyompata.

2 Haruni akawaambia, Zivunjeni pete za dhahabu zilizo katika masikio ya wake zenu, na wana wenu, na binti zenu, mkaniletee.

3 Watu wote wakazivunja pete za dhahabu zilizo katika masikio yao, wakamletea Haruni.

4 Akaipokea mikononi mwao akaitengeneza kwa patasi, akaifanya iwe sanamu ya ndama kwa kuiyeyusha; nao wakasema, Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri.

5 Naye Haruni alipoona jambo hili, akajenga madhabahu mbele yake; Haruni akatangaza akasema, Kesho itakuwa sikukuu kwa Bwana.

6 Wakaondoka asubuhi na mapema, wakatoa dhabihu, wakaleta sadaka za amani, watu wakaketi kula na kunywa, wakaondoka wacheze.

7 Bwana akamwambia Musa, Haya! Shuka; kwa maana watu wako uliowatoa katika nchi ya Misri wamejiharibu nafsi zao”.

Kiroho jambo hili linaendelea hata sasa, sanamu zinaendelea kuchongwa hata sasa,..matendo  yasiyofaa tuyafanyayo ndio ibada ya sanamu (soma Wakolosai 3:5) na tamaa zetu ndio “Patasi”.

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

JINSI WATU WANAVYOIUNDA SANAMU YA NDAMA MIOYONI MWAO.

HARUNI

FIMBO YA HARUNI!

USIABUDU SANAMU.

Kwanini ndugu wanaokaa pamoja wawe kama mafuta ya Haruni?

Rudi Nyumbani

Print this post

Kunafisisha ni kufanyaje? (Mwanzo 9:27)

Jibu: Turejee..

Mwanzo 9:27 “Mungu AKAMNAFISISHE Yafethi, Na akae katika hema za Shemu; Na kaanani awe mtumwa wake”

Kunafisisha ni “KUTOA NAFASI  au KUTANUA” .. Kwani mzizi wa neno hilo ni “Nafasi”…hivyo andiko hilo tunaweza kuliweka hivi… “Mungu akamtanue Yafethi, Na akae katika hema za Shemu; Na kanaani awe mtumwa wake”

Kwanini Mungu amtanue Yafethi na kumlaani Kanaani?.

Ni kwasababu Hamu alifanya dhambi ya kuutazama uchi wa baba yake.

Mwanzo 9:20 “Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu;

21 akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake.

22 Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje.  23 Shemu na Yafethi wakatwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; na nyuso zao zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao.

24 Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea.

25 Akasema, Na alaaniwe Kaanani; Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake”.

Je umempokea YESU?.. Kama bado basi wakati uliokubalika ni sasa, fanya maamuzi kabla kabla hazijaja siku za hatari.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Kanaani ililaaniwa (Mwanzo 9:20-25,) kwanini Mungu awapeleke wana wa Israeli katika nchi iliyolaaniwa?

Hema ya kukutania ni nini, na ilikuwaje?

KWANINI NABII ISAYA ALIAGIZWA KUHUBIRI UCHI?

KUOTA UPO UCHI.

Je shauri la kuipepeleza Kanaani lilitoka kwa wana wa Israeli au kwa BWANA?

Rudi Nyumbani

Print this post

Debwani, Shali na Vifuko ni vitu gani? (Isaya 3:22)

Jibu: Labda tuanzie mstari ule wa 18, ili tupate kuelewa vizuri.

Isaya 3:18 “Siku hiyo Bwana atawaondolea uzuri wa njuga zao, na kaya zao;

19 na pete za masikio, na vikuku, na taji zao;

20 na dusumali, na mafurungu, na vitambi, na vibweta vya marashi, na matalasimu;

21 na pete, na azama,

22 na mavazi ya sikukuu, na DEBWANI; NA SHALI, NA VIFUKO”

Hayo ni aina ya mavazi waliovaa watu wa zamani, na baadhi ya hayo hata sasa yanavaliwa.. Sasa hapo yametajwa mengi, ikiwemo Dusumali, kwa urefu kuhusu Dusumali basi fungua hapa>>Dusumali ni nini katika biblia?

Lakini tutatazama hayo matatu yaliyotajwa katika huo mstari wa 22 ambayo ni “DEBWANI, SHALI, na VIFUKO”.

   1. DEBWANI.

Debwani ni vazi refu linaloanzia mabegani mpaka miguuni, vazi hili linavaliwa na wanawake, (Tazama picha chini juu).

   2. SHALI.

Shali ni vazi linalofanana na Debwani isipokuwa lenyewe linafunika kuanzia kichwa mpaka miguu, na hili linaweza kuvaliwa na jinsia zote, kwani kazi yake kubwa ni kujikinga na hali ya hewa, (baridi au mvua au upepo mkali), Shali ni Kiswahili cha “Overcoat” (Tazama picha chini).

shali

  3. VIFUKO

Vifuko si vazi bali ni mikoba inayobebwa na wanawake katika safari fupi. (Tazama picha chini)

vifuko ni nini

Je umempokea Bwana YESU?

Kama bado ni nini kinachokusubirisha? Fahamu kuwa hizi ni siku za mwisho na Bwana amekaribia sana kurudi, je ni nini kipo katika akili yako wewe kama Baba, au mama au kijana?. Je unawaza nini?.. kujenga maisha ya kimwili, kula, kunywa na kuvaa??..au unawaza nini Zaidi.

Kama unawaza kupendeza na kujifanya mzuri kwa mavazi na mitindo ya kidunia, Neno la Mungu linasema siku inakuja ambayo Mungu atawaondolea watu wote uzuri wa njuga zao  watu wote waliomwacha yeye..

Isaya 3:18 “Siku hiyo Bwana atawaondolea uzuri wa njuga zao, na kaya zao;

19 na pete za masikio, na vikuku, na taji zao;”

Achana na mapambo na fasheni za kidunia, mpokee YESU leo ukaoshwe dhambi zako.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

TWEKA MPAKA VILINDINI.

MANENO YA MUNGU YANAPINDULIWAJE?

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 12 (Kitabu cha Isaya)

Ni kwa jinsi gani Mungu anapatiliza maovu ya baba zetu sawasawa na Kutoka 20:5-6?

Rudi Nyumbani

Print this post

Biblia inasema nini kuhusu sayari, je ni kweli zipo tisa?

SWALI:  Shuleni tumefundishwa sayari zipi Tisa Lakini je maandiko yanasemaje kuhusu hili, je zipo kweli kwa idadi hiyo?


JIBU: Biblia si kitabu cha kisayansi, au cha taaluma yoyote, kwasababu lengo lake sio uvumbuzi na utafiti wa mambo ya ulimwenguni. Bali ni kumrejesha mwanadamu kwa muumba wake. Ni kitabu chenye msingi wa IMANI. Mambo yasiyothibitika kwa macho bali rohoni. Ni kitabu kielezacho njia ya ukombozi wa mwanadamu inayopatikana kupitia YESU KRISTO  mwokozi wa ulimwengu.

Ijapokuwa vipo vifungu vichache vichache vinavyoelezea uhalisia wa elimu za duniani, lakini isidhaniwe kuwa lengo lake kuu ni kutoa taarifa za kila kitu kwenye hii dunia, bali mara nyingi huwa ni kuelezea vema habari husika ya rohoni iliyokuwa inazungumziwa hapo.

Tukirudi kwenye swali linalouliza kuhusu sayari, kwamba sayansi inatuambia zipo tisa, je biblia nayo inazitaja ngapi?

Kama tulivyotangulia kusema biblia haielezi kila kitu kuhusu dunia hii, bali inaeleza kila kitu kuhusu wajibu wa mwanadamu kwa muumba wake.

kuhusu Sayari biblia inazitaja  bila shaka kwamba yeye ndio aliziumba, na magimba yote angali, ambayo yamejumuishwa katika neno jeshi la mbinguni .

Katika biblia sayari zimejatwa kwenye vifungu  hivi;

Ayubu 38:32

[32]Je! Waweza kuziongoza Sayari kwa wakati wake? Au waweza kuongoza Dubu na watoto wake?

2 Wafalme 23:5

[5]Akawaondosha wale makuhuni walioabudu sanamu, ambao wafalme wa Yuda waliwaweka ili kufukiza uvumba katika mahali pa juu, ndani ya miji ya Yuda, na katika kila mahali, pande zote za Yerusalemu; na hao pia waliomfukizia uvumba Baali, na jua, na mwezi, na sayari, na jeshi lote la mbinguni.

Lakini biblia Haijatoa idadi, kama ni tisa, au mia au elfu Mungu alizoziumba,  bila shaka ni nyingi, kwani turudipo kwenye sayansi, ndio tunathibitisha kuwa zipo mabilioni kwa mabilioni kwa mabilioni, hizi tisa walizoziona ni ambazo zipo tu kwenye mfumo wa jua letu..lakini huko angani kuna ma-jua mengi yasiyo hesabika na yote hayo yana sayari zake. Hata hivyo husema hizi nyota zote tuzionazo angani ni ma-jua kama hili letu isipokuwa tu yapo mbali sana.

Kwahiyo wanasayansi hututhbitishia zaidi uweza wa ajabu wa Mungu. Mambo yasiyoelezeka kwa ukuu na maarifa. Utukufu una yeye milele na milele. Amina.

Lakini Je! umempokea huyu Mungu aliyeumba mambo haya ya ajabu? kumbuka kumpokea yeye ni kumwamini Yesu. Kuaminije? . Ni kuamini ile kwa ile kazi yake kamilifu ya ukombozi wetu aliyotutenda sisi kwa kifo chake pale msalabani, iletao ondoleo la dhambi.

Ikiwa upo tayari leo kumpokea huyu mwokozi basi bofya hapa kwa mwongozo wa sala ya Toba  >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Mtu wa Kwanza kufika mwezini

Je! dunia Ni duara, tufe au ipo kama sahani?biblia inasemaje?

ACHENI MJUE YA KUWA MIMI NI MUNGU.

Print this post

Je! dunia Ni duara, tufe au ipo kama sahani?biblia inasemaje?

SWALI: Naomba kufahamu Je! dunia Ni duara, tufe au ipo kama sahani imefunikwa na glasi kwa juu?.


JIBU: Jambo la msingi kufahamu kuhusu biblia ni kwamba, Biblia si kitabu cha kisayansi, au cha taaluma nyingine yoyote, kana kwamba unaweza vumbua elimu ya kidunia kupitia hicho. ukitegemea biblia ikupe majibu ya kitaaluma,  kwa bahati mbaya unaweza usifikie lengo lako, kwasababu hakikuandikwa na Roho Mtakatifu kwa dhumuni hilo.

Biblia ni kitabu kinachoeleza sifa na tabia za Mungu, na jinsi mwanadamu anavyopaswa aoane nazo ili aweze tembea kama Mungu mwenyewe atakavyo. Ni kitabu kinachomrejesha mtu kwa muumba wake.  Kwa hiyo mtaala wake ni tofauti kabisa na elimu za ulimwengu huu na mavumbuzi yake.

Ni ajabu kuona mkristo analazimishia kutafuta kanuni za kibiashara kwenye biblia. Huwezi ona huko “demand and supply” au “cash flow” au masoko ya hisa. Nenda tu darasani utafundishwa vema kanuni za uwekezaji na utafanya vema.

Vivyo hivyo na kwenye sayansi, huwezi ona  aina za atomu au miamba, au mionzi, au chembe hai nyeupe za seli, au asprin huko  . Nenda tu darasani utafundishwa vema yote hayo.

Ndio, hatuwezi kukataa zipo  sehemu chache chache sana, zinazozungumzia elimu ya ulimwengu huu, lakini sio kwa lengo la kutufundisha kanuni zake, bali kwa lengo la kuelezea kwa undani jambo la kiroho katika tukio husika.

kwasababu biblia yenyewe inasema, hekima ya huu ilimwengu ni upumbavu mbele za Mungu, vilevile hekima ya Mungu ni upumbavu kwa ulimwengu. haviingiliani

1 Wakorintho 1:20

[20]Yu wapi mwenye hekima? Yu wapi mwandishi? Yu wapi mlete hoja wa zamani hizi? Je! Mungu hakuifanya hekima ya dunia kuwa ni upumbavu?

Kuhusu mapinduzi yote ya kiteknolojia ya wanadamu ambayo tunayaona  sasa, na hata yatakayokuja huwezi yapata kwenye biblia, huwezi ona facebook, internet, vikizungumziwa kwenye biblia, sio kwamba Mungu hakuyaona au kuyajua, aliyajua sana, lakini yote hayo yamejumuishwa katika neno moja kuwa “maarifa kuongezeka” (Danieli 12:4)

Sasa tukirudi kwenye swali, ambalo linauliza je dunia ni tufe, duara au kama sahani imefunikwa na glass juu. Jibu ni lile lile hakuna taarifa za kutosha kwenye biblia zinazofafanua juu ya hilo lakini haya ni maandiko machache yanayotuambia kuhusu uhalisia wa dunia..

Isaya 40:22

[22]Yeye ndiye anayeketi juu ya duara ya dunia, na hao wanaokaa ndani yake huwa kama panzi; yeye ndiye azitandazaye mbingu kama pazia na kuzikunjua kama hema ya kukaliwa;

Kwa andiko hili, tunaonyeshwa kuwa dunia ipo katika duara, aidha kama tufe au mpira. lakini ni mzunguko, na sio kama sahani yenye glasi juu.

Hivyo tukirudi katika sayansi, ukisoma huko ndio utaelewa vizuri zaidi kuwa dunia ni mfano wa tufe, na sisi tukiwa tumenata-nata juu yake sio ndani yake.

Lakini tukumbuke kuwa haya ni maarifa ya mwanadamu, aliyopewa na Mungu ya kutafiti, na maarifa yake yanatabia ya kuboreka na kupinduka. Lakini kwa upeo wao wameweza kuthibitisha hilo.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MUNGU WETU, JINSI LILIVYO TUKUFU JINA LAKO DUNIANI MWOTE!

Heshima ni nini kibiblia?

NYOTA ZIPOTEAZO.

Rudi Nyumbani

Print this post